mojawapo ya viota vilivyotamba sana enzi za mwalimu ni hiki cha motel agip barabara ya pamba rodi jijini dar. hata disco la clouds liliibukia hapo na ma DJ Emperor, Jesse Malongo, Bonny Luv na wengine. wadau wenye data zaidi msaada tutani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Bonny luv hakuwa hapo, alikuwa New africa,enzi hizo Dj Joseph kusaga mwenyewe! wajanja ndio walicheza enzi hizo. kama hujacheza hapo basi wewe sio janja. watu walikuwa wanajuana hapo.

    ReplyDelete
  2. umemsahau jessy..kabla ya hapo walikuwa wanapiga kwenye ma pary tu..bon wakati uwo alikuwa mtoto mdogo tu upanga

    ReplyDelete
  3. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...hizo ni enzi za mwinyi.

    ReplyDelete
  4. hata hivyo bado wajanja tulicheza disco bilibi kaka wakati huo tunawahama akina chris fabi na madj wa rungwe na sliver haa haaa i kaka michuzi nakukumbuka enzi ya RSVP. yule michuzi kibonge yuwapi? wakati huo tunakalia sementi pembeni banda la bati kwa huduma za supu. asante.

    ReplyDelete
  5. Data zaidi ni kwamba Hotel hiyo kwasasa ni gofu kama Embassy Hotel. Kwa maana haitumiki.. mamilioni yamelala hapo.

    ReplyDelete
  6. WATU WANAOKUMBUKA MIAKA YA MWISHO YA 1960s(1968-1969), 1970s HADI 1980s DISCO, SINEMA BAR ZA KILEVI VILIKUWA VITU VYA FURAHA YA AINA FULANI HIVI HUWEZI KUIELEZEA, DISCO LA SEA VIEW, YMCA, KUNDUCHI, MBOWE NA KWINGINEKO. UKIENDA HUKO WEEKENS BUS NI UJIKO NA MTAANI NI GUMZO TU HASA WATU AKINA SISI TOKA USWAHILI, KINONDONI, ILALA, MAGOMENI, MAMBO YALIKUWA SAFI NA UTAMU WA AINA FULANI HIVI, WAKATI HUWA JIJI HALIKUWA LIMEJAA KAMA LILIVYO SASA. NA KULIKUWA NA KAHEWA FULANI HIVI NZURI SI JOTO LILIKO HIVI SASA. WAKATI HUO UKIENDA MITAA YA POSTA, IKULU, OCEAN ROAD KULIKUWA KUMETULIA TULI, AND YOU FEEL AS IF YOU WERE IN ANOTHER WORLD.

    ReplyDelete
  7. Ni Pamba Road au Barabara ya Pamba? Ipi ndio Ipi. sio wa Morogoro tunataka kujuwa tu.

    ReplyDelete
  8. hizo zilikuwa enzi za bigmark codrai na jeanz babake na superga hii kiatu ilikuwa buku mbili usipime totoz tulikuwa tunachukuwa kwa majina hahahah these time will never gonna come back hakuna mawaja wala nini enzi hizo kipala tu pekuuuu lol

    ReplyDelete
  9. LOO!KAKA MICHUZI WAKATI HUO PALE MASASI MTWARA WAJANJA WALIKUWA NAO WANAJICHANGANYA KIWANJA CHA MASASI HOTEL,NAMKUMBUKA JAMAA YANGU KALAMULA NA MAMBO YA BREAKDANCE,KIOTA HICHO NACHO KIMEBAKI MAJENGO TU...

    ReplyDelete
  10. Nyie watoto wadogo mnajiona wajanja kwa disco la Motel Agip.
    Kwa wale wenzangu wa late 1940s, mpaka 1950s mnakumbuka mambo yetu tulivokuwa tukiselebuka kwa miondoko ya swing dance na twisti katika sehemu zetu zile kama Hotel Gossage, Tanganyika Rifles Club na King George's bar. Ahhh zile ndio enzi bwana, wenzangu akina Andanenga, Mwalubena, Sir John Sweetman mpo? Hawa watoto wanataka kutueleza nini bwana?

    ReplyDelete
  11. MtatifikoloOctober 14, 2009

    we anony wa Wed Oct 14, 02:49:00 PM acha uongo. Okay umesema ulikuwa unajirusha in 40s and 50s sio. I am going to make very conservative estimations and say ulianza kujirusha at 15 and that was right at the end of the 50s, so the youngest you could possibly be is 75 (born in 1944).

    Now I highly doubt mzee wa miaka 75 atakuwa anakaa online kuandika message kama yako hapo juu katika blog.

    ReplyDelete
  12. Ama kweli blog ya jamii ni burudisho tosha la jamii! Ukiwa umechoka na mihangaiko ya hapa na pale ya kutafuta riziki, ingia kwenye intaneti, fungua blog ya jamii nenda kwenye maoni ya wanablog, huko lazima utaburudika tu kwa kucheka kutokana na maoni mbalimbali yanayotolewa! Angalia kama hapo juu mtu anasifia muziki wa miaka ya 40 na 50, si ajabu huyo mtu alikuwa hata kuzaliwa bado, hii nadhani ni burudani vilevile. Ahsante Michuzi kwa blog yetu hii ya jamii!!!

    ReplyDelete
  13. hapo umesema kweli, tena with 15years you were not allowed to go near any club, huyu kibabu atakua anafanya nini kwenye blogu????

    ReplyDelete
  14. Hahaaha jamaa kapatikana Mzushi tu huyo Tena Kipindi hiko mtu ukiwa na 15 miaka ya kuzaliwa ata siku moja hawakukubalii si miaka ya ufisadi. Labda alikuwa Wazee wake wafanyakazi anaenda kuchukuwa vitu ndani akasafishe. muwe mnasema ukweli jamani. Mambo disco Rungwe Beach, Bahari Beach 1985.

    ReplyDelete
  15. MtatifikoloOctober 15, 2009

    my bad... I meant so say ulianza kujirusha right at the end of the 40's (i.e 1949) and you were 15 then (i.e. you were born in 1934)...

    ReplyDelete
  16. Sie tulijirusha Forodhani, Anatoglu, Kibarua bar wakati huo Chibuku ilikuwa tamu kama nini kwani hata wakurugenzi pia walipuliza povu la Chibuku na kuinywa.

    Mdau
    Kakamiye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...