Mustafa Hassanali na mamodo wake kwenye shoo ya huko siku za nyuma. Cheki alivyokuwa bwanyeye. Hivi sasa ameslimu na hataki kutaja siri ya mafanikio yake. anasema siri hiyo ataitoa wakati wa Swahili Fashion Week mwezi ujao....
Mustafa Hassanali akiwa amekula suti kali. Hii ni mara ya kwanza kula pamba namna hii toka azaliwe. na jinsi alivislimu pamba imemtoa kweli

mustafa akipozi na stella na adil wa kampuni ya infinity ambayo
pia inafadhili Swahili Fashion week mwezi ujao

SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA RASMI

Kwa mara ya pili mfululizo wiki ya mitindo –Swahili Fashion Week (SFW) - itafanyika tena jijini Dar Es Salaam na kuwapa wapenda mitindo siku tatu zilizojaa shoo za mitindo za aina mbali mbali.


Swahili Fashion week ni siku chache za mitindo ya kisasa yenye mahadhi ya uswahili na vile vile hujumuisha wabunifu wa mavazi wenye vipaji kutoka sehemu mbali mbali nchini, nchi zinazozungumza Kiswahili na nchi nyinginezo. Katika onyesho hilo wabunifu huonyesha kazi za kipekee zenye mahadhi ya kiafrika zikijumuisha, nguo, viatu, mapochi na urembo mwengine.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa onyesho hilo la mavazi mwanzilishi wa SFW Mustafa Hassanali ambaye ni mmoja wa wabunifu maarufu nchini alisema mwaka huu Swahili Fashion Week inahamasisha ‘Mitindo kama biashara.’

“Swahili Fashion Week mwaka huu ni mwanzo wa ari mpya; tunaandaa onyesho litakalohamasisha mitindo kama biashara. Tunataka kukuza shughuli za mitindo nchini ili isiwe inachukuliwa kama fani ya burudani bali mojawapo ya njia za kukuza kipato.


Ulimwenguni kote fani ya mitindo ni moja kati ya fani zinazochangia katika uchumi wa nchi, hivyo basi na sisi tungependa kusisitiza umuhimu wa fani hii nchini ili watu waipe umuhimu unaotakiwa kama njia mojawapo ya kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa ujumla,” alielezea Hassanali.

Wiki ya Mitindo ya mwaka huu itajumuisha wabunifu mavazi 14 kutoka mikoa mbali mbali nchini na wabunifu 6 kutoka nje ya nchi na maonyesho hayo ya mavazi yatafanyika tarehe 4 hadi 6 novemba mwaka huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam.

“Swahili Fashion week inatoa nafasi kwa wabunifu wanaoibuka na waliobobea kuonyesha kazi zao ndani ya paa moja na hivyo kuwapatia nafasi wabunifu wakongwe kuwapa ushauri wale wachanga.


British Council inashiriki katika hili kwa kuaanda tuzo ya mbunifu asiyejulikana mwenye kipaji inayoitwa ‘Emerging Designer Award.’ SFW pia inatoa nafasi ya kipekee kwa wabunifu kukutana pamoja kubadilishana mawazo na pia kupata ujuzi zaidi kupitia warsha mbali mbali zitakazoandaliwa na Goethe Institute,” aliongeza Hassanali.

Kama ilivyokuwa SFW ya 2008, mwaka huu pia washiriki wa fainali za shindano la kisura wa Afrika maarufu kama ‘M-net Face of Africa’ watashiriki katika maonyesho hayo ya mitindo kama sehemu ya shindani hilo kwa kuonyesha mavazi.

Wabunifu wanaoshiriki katika SFW wanachaguliwa na bodi ya wana mitindo inayoitwa ‘Fashion Advisory Board (FAB)’ ambayo wajumbe wake ni pamoja na Emelda Mwamanga Mkurugenzi Mkuu wa Jarida la Bang, Mwanasheria Matukio Chuma, Mkurugenzi wa sanaa na promosheni wa BASATA Nsia Shalua, na mmiliki wa klabu maarufu ya starehe jijini Dar es Salaam Abigail Plaatjees.


Maonyesho ya Swahili Fashion Week mwaka huu yanaletwa kwa ushirikiano na kampuni za Vodacom Tanzania na ZTE.

Vile vile wadhamini wngine ni, Infinity Communications Ltd, REDDS, Southern Sun, Goethe Institute, British Council na BASATA.

Pia wadhamini wengine ni Ultimate Security, Primetime Promotions, Vayle Springs, ZG Designs & Films, Jan Malan Umzingeli, Choice Fm & Clouds fm, Mwananchi Communications Ltd, Brooklyn Media, 1&1 Internet solutions, Channel Ten, Imaging Smart, IMAN Cosmetics, Darling, Runway Lounge, Perfect Machinery na African Life Assuarance.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. ...kuslimu siyo kuingia dini ya uislamu...au mimi tu?

    ReplyDelete
  2. You don't have to be a rocket scientist to know the secret behind Hassanali's weight loss, I am certain he went under the knife (Liposuction).

    ReplyDelete
  3. Hey folks...its called weight loss surgery....Lmao

    ReplyDelete
  4. .... aisee hata mie pia nataka kujua siri ya mafanikio mustafa toka bwanyenye hadi model kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  5. Safi sana! Keep it up nasubiria siku hiyo ili nijue siri ya mafanikio

    ReplyDelete
  6. anon wa kwanza uko nje ya topic kabisaa hapo ni jinsi mustafa hasanali alivyopungua tukirudi kwa ishu ya mustafa hilo sio tizi wala mazoezi wala vidonge vya kukonda hiyo ni surgery alifanyia south africa asidanganye watu ati ni diet lol diet miezi miwili unakuwa kipotapo namna hiyo aah wapiiiii na jinsi alivyokuwaga ithili ya pepekale hata angefanya diet mwaka mzima asingekuwa jinsi alivyo sasa hiyo ni SURGERY TUUU FULL STOP!! tena wakati yuko south kwenye wall ya facebook akawa anadai amelazwa kule ati anaumwa malaria isshh kumbe alikukwa anakula kisu kupunguza mamichelini hongera kwa kupungua si useme ukweli tuu kwani utakufa mbona ni vitu vya kawaida sana??

    ReplyDelete
  7. SIRI YA MAFANIKIO NI NGOMAA

    ReplyDelete
  8. mh! ok,basi ameloose weight.

    ReplyDelete
  9. Njia rahisi ya kuslimu ni kupata ngoma tu, unachuja mwenyewe bila kujishughulisha.

    ReplyDelete
  10. Kuslimu ni kubadili dini kuwa Mwislamu iwapo unatumia lugha ya Kiarabu kutengeneza msamiati wa Kiswahili, yaani kutoka "kuwa Mwislamu" kuwa kuslimu, jambo ambalo ni sahihi kwa mantiki na muundo wa Kiswahili.

    Kuslimu inaweza kuwa kujikondosha au kupunguza uzito iwapo unatumia lugha ya Kiingereza kutengeneza msamiati wa Kiswahili, unakumbuka watu husema amevaa "slimu fiti" ambayo ni Kiingereza kamili katika matamshi ya Kibantu.

    Kwa hiyo maana zote mbili ruksa.

    Mwenyekiti Mtarajiwa BAKITA.

    ReplyDelete
  11. Mwanaume rijaliutakaaje umekunja nne ya kufumba hivyo!
    Katoa siri ya kukonda kwenye gazeti la udaku la Shigongo. Na pia ni mchumba/mume wa Jacklin Ntuyabaliwe.

    ReplyDelete
  12. nimesoma udaku wanadai amefanyiwa operation ya kupunguza minyama sauzi aflika na special tritmenti alivyokwenda india.

    Thu Oct 15, 03:58:00 PM
    slim= practise to become thinner in attractive way

    ReplyDelete
  13. lol @al musoma

    ReplyDelete
  14. Ame "slim" ndio kuchanganya swahili -english huko...

    May be amefanya gastric by pass surgery....not sure labda diet tu.

    ReplyDelete
  15. nin kimempata huyu jamaa?alikuaga mnene sana sio ugonjwa umempitia kwel?manake wakat wote yuko na vimodo.du kali hiyo.

    ReplyDelete
  16. GASTRIC BYPASS SURGERY! Is that right?

    ReplyDelete
  17. Nna hakika 100% huyu sio Mustafa original, huyu ni pacha wake ambae alikuwa yuko kwao huko india, sasa huenda huyo mustafa mwenyewe kaenda kwao vacation, then huyu pacha kaja kutuzingua, na hiyo siku ya swahili show ndo atakuja mustafa original (bwamnyenye), yuko vile vile kitambi maji!

    ReplyDelete
  18. PETER NALITOLELAOctober 16, 2009

    NYINYI WATU HAMNAGA HAKILI NDIO MAANA MNAROPOKA OVYO.HUYU AMEKULA PILIPILI ZA KIINDI NDO MAANA AKIPITAGA NAMUONA KAMA VILE ANADENGUA NA MIKONO YAKE. SISI WATU WASOMI KUTOKA MUZUMBE CHUKO CHA UNIVESITY HAYA YOTE TUNAYAJUA LAKINI YUNANYAMAZA TU KWA SABABU WE ARE EDUCATE PEOPLE LIKE ROGER MTAGWA NA MR. BLUE

    ReplyDelete
  19. He got to be on crack.You can loose weight fast on crack and thats real.

    ReplyDelete
  20. excellent bwana...however, mbona wakati umeslimu there are no beautiful girls in the pictures and and when you ere heavy weight, you were sorrounded by beatiful GIRLS all around you...can some explain me that?

    ReplyDelete
  21. Hebu na yeye mustafa aache roho mbaya.Kuna watu kibao wenye unene kama aliokuwa nao yeye na wanahitaji msaada ili nao wapungue. Lakini yeye kila siku akiulizwa kafanya vipi hadi kupungua ili angalau na hao wengine walio wanene wafuate nyao zake yeye anabaki kutoa majibu ya kubabaisha tu. Kama si roho mbaya ni nini? Acha hizo wewe.

    ReplyDelete
  22. Mustafa ana eating disorder, inaitwa anorexic, This guy barely eats na akila anakua na hasira, Mustafa ni anaogopa chakula sana na akijiona amekula sana, he feels guilty, hana siri ya mafanikio zaidi ya kua na mental disorder which is related to eating disorder.

    ReplyDelete
  23. HAYA NYIE WATU WA LEEEBOOZIII KWENYE MAKOTI TOENI HIZO LEBO SI MNAONA SUTI INAVYOKUWA.

    ReplyDelete
  24. "Tarehe Fri Oct 16, 02:57:00 AM, Mtoa Maoni: PETER NALITOLELA

    NYINYI WATU HAMNAGA HAKILI NDIO MAANA MNAROPOKA OVYO.HUYU AMEKULA PILIPILI ZA KIINDI NDO MAANA AKIPITAGA NAMUONA KAMA VILE ANADENGUA NA MIKONO YAKE. SISI WATU WASOMI KUTOKA MUZUMBE CHUKO CHA UNIVESITY HAYA YOTE TUNAYAJUA LAKINI YUNANYAMAZA TU KWA SABABU WE ARE EDUCATE PEOPLE LIKE ROGER MTAGWA NA MR. BLUE"

    Ndo maana nchi haiendelei, kama wasomi mnakaa kimya huku mambo mkiyajua je yule mbongo asiyefahamu mnamsaidia vipi, au hiyo elimu unataka ikusaidie peke yako.... Mtaendelea kufa maskini kama elimu mliyopata haitawasaidia PUMBAVU ZENU!!!

    ReplyDelete
  25. Michuzi mimi moyo wangu umemdondokea dada Stella...kwa kweli kanivutia sana...kwa kifupi nimempenda..naomba nipe data zake zaidi..huyo jamaa wa pembeni ndo mdau wake nini...email yangu rashmaki@gmail.com

    ReplyDelete
  26. HAKUNA KISWAHILI CHA KUSLIMU UKIMAANISHA KUPUNGUA UNENE, UNAWACHANGANYA WATU KUINGIA DINI YA KI-ISLAMU NDO KUSILIMU

    ReplyDelete
  27. Wewe mdau unayejiita Peter Nalitolela nadhani unamuharibia jina mshkaji tu..Peter nnayemjua mimi hawezi kuongea pumba namna hii..don't do that, jiite anony tu, tutakusoma..

    ReplyDelete
  28. huyo anayejiita Peter Nalitolela ni Nshimimana aka Dumisane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...