Can your partner be with your phone
for a day and things remain the same?

One Friday morning, John woke up hurriedly and prepared for work. He worked in a busy institution and was expected early at work. His wife worked a distance from where her husband's office was.

As a result of doing things in a hurry, John unknowingly, carried his wife's mobile phone leaving behind his own. After he had gone his wife Jane noticed the mix-up but it was too late for her to do anything about it. She thought for a while and decided to carry her husband's phone in case he came back for it.

On arriving at his place of work John noticed that he had confused his wife's phone for his but decided not to go back for it. He sighed deeply because he knew his wife could access romantic messages sent by his many mistresses.
His wife too was disgusted because she had several toy boys.

Drama began to unfold when John received an SMS intended for his wife sent by somebody saved as 'Peter-Taxi', which read,
"Hi sweetie, ope yo monin' is fine, 4 me am okay just mad! My love 4 you kills me. I couldn't stop dreaming about you even after we met last evening coz you hold the password to ma heart." John was shocked to see this and thought he understood why his wife had come home late the previous evening. He decided to stay mum to see what more would come.

After one hour he received another SMS from somebody saved as 'Susan-Salon' which read, "Monin darling, ope ur fine, am also fine but not so fine without seeing you next to me coz you control every part of ma heart. Nice day sweetie, see you at lunch."

The third SMS ticked in from somebody saved as 'Winnie-Handbags' which read, "Monin ma beautiful queen, I wish you were a gum, I would chew you every time, you make me feel young like I was born yesterday, you without whom I would go on a hunger strike. Have a bright day ma dear."

John was deeply shocked by these messages but knew that on the other side his wife might be seeing drama too.
Meanwhile, Jane had seen even more than her husband. She had received three messages from three women that clearly showed they were his mistresses. The first SMS was from a woman saved as 'Ochieng-Car wash' which read, "Hi deah how's ur monin? 4 me am okay with ur son here, he says he loves you so much n you should come n stay with us. gday."

Jane almost fainted on seeing this because she could not believe that her husband had a son outside marriage.

Before her anger was over, she received a second SMS from' 'Omosh-Kinyozi' which read, "Monin ma deah, ope ur enjoyin ur day. Mine can't be complete without you. Every time I sleep in this house you bought 4 me I dream 2 love u always. The BM u bought me is perfect on road. Thanks, g'day."

The last message came from 'Karanja-Electician' and read, "Sasa honey? Ope u r fine. pls i am not happy wit u. u promised to send me money since last week,But i have not seen it. honey pls send me the 40k for the project. Hav a nice day, love you big."

Jane had found the answer to why her husband was always penniless!
When evening came John and Jane met at home. They could hardly talk but only stared at one another with suspicion.

Now, If they called you to intervene,
sincerely how would you solve their problem?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. HAPO BWANA NI NGUMI TUU AMA WASAMEHEANE LOL... THEY ARE NOT FAITHFULL TO EACH OTHER NA HAINA MAANA YA KUINTEVENE IN BTN LET THEM SOLVE THEMSELVES..

    ReplyDelete
  2. Duh! hapo nilikuwa naona ni kama mimi vile??? naona ndiyo imenitokea mimi sasa!!! duh!!!

    ReplyDelete
  3. hapo hamna ndoa tena, kila mtu achukue chake, wawe wanakutana kwenye issue za watoto tu! it is clear they r both not marriage material, maana mtu anweza kuteleza kwa mmoja, sasa huku vimada watatu kule watatu si ina maana wameshindikana hao???

    ReplyDelete
  4. jamani!!kwani cha kushangaza hapo kitu gani?? si ngoma imeshakuwa droo, .no more intervene.50/50 .

    ReplyDelete
  5. Mbona hiyo kazi rahisi sana wazee? kutafuta solution haimaanishi eti lazima uwapatanishe! Hata kuwasaidia kat separation yao ikawa peaceful, basi utakuwa ume-play good party.

    Mimi nitakachokifanya, nitasoma messeji za wote wawili kwa sauti ili kila mmoja asikie , then nitaanza kumuuliza mwanaume, umesikia messeji ulizotumiwa wakati simu yako anayo mkeo, na pia nitamweleza mke same way kama nilivyommuliza mume, then nitawaambia, hizi meseji nisababu tosha kwa nyie kuachana, mimi basi naomba muachane kwa amani ili kila mtu ashike hamsini zake. Kwa kuanza hivyo, ndio nitamuuliza mme kwanza, je unadhani una sasbabu ya maana ya kutomuacha mkeo ukizingatia haya yoye ameyajua? kwa navyowafaham madume, litaangalia pembeni kwa noma,ukilinganisha na uchafu wake ktk zile messeji so hatojibu then nitamgeukia mke kumuuliza,hivi mama fulani unadhani kuna sababu ya wewe kuendelea na huyu mwanaume?? Najua mwanamke ataanza kulia na kupandisha mzuka.......mimi nadhani huu ndio utakuwa mwisho wa ndoa yao ingawa dume atalazimisha hapo baadae kudonyoa!

    k'dume.

    ReplyDelete
  6. ni upuuzi. ukichukua cmu ya mtu cha kwanza ump-igie umwambie unayo. la sivyo izime hadi akija ichukua mwenyewe.

    lakini kina mama no sasa hivi wamejanjaruka. mie wa kwangu saa kumi na mbili asbuhi unakuta yuko nayo mezani ukimuuliza anasema ananiwekea cheka taimu!!!!! kazi kweli kweliii

    ReplyDelete
  7. ladies and gentlement, hapo mfumbuke macho kwamba sio kila jina linalokuwa saved kwenye simu ndivyo lilivyo! utakuta Jane-salon anapiga kumbe ni John, au Hassan-car wash kumbe ni Hamisa. watch out cheaters coz you are next!

    ReplyDelete
  8. mimi ushauri wangu ni kwamba wasifuate maneno ya watu kwenda kupima afya

    ReplyDelete
  9. Mbuzi wa bwana kheri, akiingia shambani kwa bwana kheri, akala kisanvu cha bwana kheri...yote kheri tu!!!

    Hao wakapeane 'haki' and all will be good. They are a perfect match. Hakuna wa kumnyooshea mwezake kidole. Uongo Jiang?

    Suluja

    ReplyDelete
  10. Mwanabidii FulaniNovember 26, 2009

    Huyo mwanaume hana tofauti na mimi ila mimi mwenzie hayajanikuta tu. Inawezekana na mke wangu nae akawa kama huyo demu. Aah!! Yote maisha tu ila tatizo ni kuondoka kwa ngoma na kuwatesa watoto.

    ReplyDelete
  11. Ya akhii Michuzi
    Daima wanifurahisha kwa ujuzi wako wa kutuelimisha. Maafa yaliyowasibu hawa jamaa yafaa kuwekwa kama juzuu mpya kwenye Hadithi na mikasa ya Esopo
    Nakubali jamaa wameenda sare, three own goals each,they should sit down and reassess their relationship and define their future,for the rest of us,thanks for the hidden message
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  12. Duuuu!!! Hiyo jamani haina mjadala manake ngoma droo!! Kila mmoja amemjua mwenzie so waendelee tu na maisha yao ya kizinzi or wakae wayamalize kwa kuamua kutulia wote wawili!

    ReplyDelete
  13. Wote si waaminifu na ndio maana kila mmoja alikuwa na wasiwasi kuhusu simu yake iliyo kwa mwenzie. na kwa kuwa ngoma ni droo hakuna wa kumlaumu mwenzie cha mhimu kama wanataka kuendelea na ndoa yao hawana budi kusameheana. ila Yote tisa mwanaume kazidi

    ReplyDelete
  14. mimi nilishakuta msg za namna hiyo kwa mke wangu, mara ya kwanza akaniambia ni mtu hamfahamu ila wanachat tu huyu ni mtu mmoja, siku nyingine nikakuta msg nyiningine ya mtu mwingine nikachukua hiyo namba yake bila yeye kujua nikapiga hiyo namba sauti kiume akijabu halfu simu ikakatwa nikamuuliza ni nani akanijibu ni rafikie yake wa kike, nikamtupia simu nikamuambia ukweli nilionge na huyo jamma jibu likawa ni rafiki yake huko kwa maeneo ya mikocheni, halfu mke ni mlokole kila jioni yuko kasini.bado sijaamini hayo majibu yake, kwa kweli simu zinaleta matatizo mengi kwe ulimwengu wa mahusiano

    ReplyDelete
  15. Yote hii inaonyesha kuwa uasherati haulipi chochote. Chungeni ndoa zenu!

    ReplyDelete
  16. Hizi mechi za AWAY GAMES siku hizi ni hatari sana.Zamani ukifumaniwa wapigwa kwa ngumi na bakora ua wachomwa kisu matakoni, siku hizi ukifumaniwa,huenda ukapigwa na virusi
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  17. kusema ukweli wote hawana uaminifu ila mwanaume KAZIDI jamani eenh!!!! Kaonga gari, hela za project sijui anamjengea nyumba na kuzaa juu!!!!!
    Afadhali mwanamke yeye vibuzi vya hapa na pale vya kumuondolea stress, lakini mumewe kiboko!

    ReplyDelete
  18. Kama ingekua mimi yote hayo yasingetokea,ingetokea kwa mwanamke tu manake mim bwana simu yangu kuiaccess ni ngumu nimeencrypt nimeweka mapassword kibao hiyo tunafanyaga kwa ajili ya confidentiality na pia unazuia conflict,kama huyo mwanaume/mwanamke wangekua wamelock simu zao kwa password or pincodes kusingekuwa na mambo ya kutengana.

    ReplyDelete
  19. Hayo ndio maisha tunayoishi sema zamani kulikuwa hakuna vilongalonga. Hapo ni kila mmoja kukabidhi simu ya mwenzie na kwenda kupima afya. Zaidi wanaweza kukaa na kuongea ni kipi ambacho kimepungua kwenye uhusiano wao kinachowafanya waende nje. Inawezekana kwa mfano jamaa haendi uchumvini au mwenzie halambi koni au kuna mwenye tabia za kwenda kinyume cha maumbile. Wakiongea watajua kama wajaribishe vitu vipya au watupiane virago. Hakuna haja ya msuluhishi hapo.

    ReplyDelete
  20. shughuli nzito ni kuuchuna tu kama hakuna kilichoharibika manake sijui nani atalianzisha

    ReplyDelete
  21. WOTE WAWILI SIO WAAMINIFU KWENYE NDOA KAMA WANAWEZA KUVUMILIANA NDOA IENDELEE.

    LAKINI KUNA KOSA KUBWA LIMEFANYIKA. KAMA MTU ANACHUKUA SIMU AMBAYO SI YAKE KULIKUWA HAKUNA HAJA YA KUENDELEA KUITUMIA.

    KAMA ALIVYOSEMA MDAU MMOJA HAPO JUU WALITAKIWA KUTAARIFIANA AND THEN AMA WAZIME SIMU AU WABADILISHE PROFILE ZISIPIGE KELELE ILI KUONDOA BUGHUDHA KWAO.

    NDOA INAWEZA KUENDELEA LAKINI HUYO BWANA ANONEKANA KIMWAGA SANA ITAKUWA NGUMU KUTUNZA FEDHA KWA AJILI YA FAMILIA.

    ReplyDelete
  22. simu huleta mambo mengi sana,ndoa kuvunjika,marafiki kugombana ,wengine kutukanwa nk.
    Rafiki yangu mmoja mumewe huficha simu ndani ya mto wake ,na kulalia.Kisa mke asiiguse.
    wengine ndo wana save majina call 1,withheld,unknown ,ukiiona unaambiwa ni int.call.
    kikubwa ni uaminifu,ikishindikana weka pswd mchezo kwisha.Ila kuna kazi ya ziada kwenye mambo ya simu !!!

    ReplyDelete
  23. Wabongo tuache umalaya jamani...tumezidi...

    ReplyDelete
  24. (Mwanabii) Nov 26 Thur 03.27pm, kaka kama unatambua tatizo kwa nini huamui kubadilika? Maana kama umejilinganisha na huyo jamaa walie muelezea hapo kweli fikiria tena mwenendo wako. Nimecomment hivi kwa kuwa umesema mwenyewe kuwa uko kama huyo jamaa.

    Huwa inaumiza sana kuona watoto waliokuwa ktk matunzo mazuri wakiachwa na kurandaranda mitaani bila mbele wala nyuma. Ukiangalia faida waliopata wazazi kwa kuwa na mahusiano ya nje wala huioni bali ni matatizo matupu!! Tamaa haisaidii, inapoteza amani na uhuru na kutesa watoto tu.

    ReplyDelete
  25. Hivyo ndio ndoa karibia zote za kitanzania zilivyo ,mie ni mtarajiwa na najua kabisaa kuwa wanaume siku hizi ni kama wanawake wa kabila fulani ambao wanahusudu mafiga matatu na zaidi. Hivyo ndivyo wanaume wa siku hizi walivyo kama mie yakinikuta sitashangaa cos ni khali halisi.......

    ReplyDelete
  26. Friday, 27 November 2009
    HAKUNA SABABU YA KUWA NA MABWANA AU MABIBI WA NJE YA NYUMBA YENU. JAMBO LA MSINGI NI KUWA WAAMINIFU KATI YENU WAWILI. IKIWA MTACHAGUA MAISHA YA AINA HII YA UAMINIFU, HATA MUME AU MKE AKICHUKUA SIMU YA MWENZAKE HAKUNA YATAKAYOJILI KAMA HAWA WAWILI YALIVYOJITOKEZA. MAISHA NI JINSI MNAVYOPENDA KUISHI. PESA ZOTE ZENU ZITUMIENI KUENDELEZA FAMILIA YENU KATIKA ELIMU, MAISHA BORA NA YENYE FURAHA KATI YENU NA MTAKAOJALIWA KUWA NAO. JENGENI NYUMBA YENU KWA MIKONO YENU NA AKILI ZENU PAMOJA.HUO NDIO USHAURI WANGU.
    Mshauri wa Kujitolea

    ReplyDelete
  27. Binti MremboNovember 27, 2009

    Jamani msimwone mwanaume kama ni hatari zaidi eti kwa sababu kapata mtoto. No. Ni tabia ya nyumba ndogo ambazo hazijaolewa na ambazo hazitarajii kuolewa kupenda kupata mtoto hata kama ni mume wa mtu. Hapo ni kuwa wanaume hufanyiziwa na kupata watoto bila wao kutaka. Na muelewe wazi kuwa hakuna anayependa kupata mtoto na nyumba ndogo si wanaume wala mwanamke. Ila ikishatokea na hali unajua ume-do naye basi hakuna jinsi.
    Tunajua kwa wanawake ni hatari sana wakipata watoto nje. So wamekuwa makini sana kwa hili, na hata wengine wamekuwa wakitoa mimba ili tu asimpate mtoto.
    Na kama ni mambo ya kutoa mali, mwanamume apewaye na mwanamke huwa anatabia ya kutopenda aonekane kapewa na mwanamke na huwa hanyenyekei na huwa hapendi kutaja mali ile kila mara kwa mwanamke na ni ile dhana ya kuwa mwanamume kapendwa na mwanamke. Lakini kwa mwanamke aliyepewa huwa mara kwa mara anataja zile mali kwa mwanamume ili kuonyesha anavyothamini na kujali kwa upendo aliofanyiwa. Lakini wanawake nao pia wanatoa vitu vingi tu, hata gari wanatoa. Unamkuta muuza duka mtaji unaongezeka tuu.. au kijana wa saloon mambo yananyooka. Inasemekana wanawake ni hatari zaidi wanapoamua kujiachia.
    Kwa hiyo hapo ngoma ni droo, hata kama mmoja ingekuwa zaidi ya mwenzie. Mtu anaweza akawa na mmoja akawa balaa zaidi ya mtu mwenye wawili au watatu. Maana yake ni mtu akishaenda nje tu basi ni hatari.
    Tuache tabia mbaya tuyalinde maisha yetu, tujenge maisha yenye furaha na kutumia mali zetu vizuri. Tusibaniane pia, tupeane kila kitu turidhishane.
    Kumbuka, unavyovipata nje mbona kwako vipo. Just know how to get them.

    Binti Mrembo kiboko kwa vibuti.

    ReplyDelete
  28. karibuni sana jamen ARVs hazina wateja kabisa zimejaa sana hospitalini kwetu na kwengine.

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  29. okkk wawe wapole tu,wasameheane na kuaza life ,km vipi kila mtu ale kona

    ila izi familia zinatesa watoto jaman???

    ReplyDelete
  30. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  31. tunachosema hi hiviiiiii nenda mbele rudi nyuma hii yote shida ya kung'ang'ania ndoa ya mke mmoja haina tija wala nini!!!!!!!

    ndoa ya mke mmoja haina tija kwa wote...si mwanaume wala mwanamke.....
    hasara zake ni kwamba mwanaume anakuwa zezeta....hana tija ya kazi wala haoni umuhimu wa mafanikio......na anazeeka kabla ya siku zake....

    mwanaume anakosa apetait ya kula hata vitu vya ndani....kumbuka kupanda mtungi si mchezo....

    mwanaume anakuwa na hasira zisizokuwa na kichwa wala miguu... hasara kwa familia.....

    mke akizidi ukali mzee asiwe anapita vijiweni ndo mbaya zaidi mzee anamgeukia yule housegirl anayeangalia vyema watoto na familia na kujirindima... housegirl anaanzishiwa mji wake na hasara inarudi kwa nyumba kubwa....

    mwanamke akiwa mtu mzima na anaona hiyo mambo ni usumbufu baba kama hana bi mdogo anaanza kupata magonjwa ya njia za mikojo na kujikojoleakojolea kwani mishipa inakosa zoezi saaaa miiingiiii

    kwa ufupi haya mambo ya vichungwaa yako zaidi kwenye nyumba za watu wa kisasa one man one woman....tunasahau kuwa wazungu hufanya hivyo kwa sababu talaka kwao ni mwendo mdundo...unakukla kitu miaka miwili mfululizo ukiacha unarukia nyingine...kwetu huku talaka ni failure...ni vema ukawa na wake wawili hakuna kuacha hakuna kutoka nje.....mnadhani ni kwanini uarabuni ukimwi ni wa kutafuta sana???

    chao!

    ReplyDelete
  32. A similar thing happened to a friend of my and I must say that their loving relationship is not the same.

    ReplyDelete
  33. Hapo hakuna ujanja kila mtu ashike njia yake tu....Wataendelea kuwekana sawa mpaka lini??Hakuna mapenzi wala imani hapo.

    ReplyDelete
  34. Yote hiyo inaonyesha UKIMWI hautakaa uishe hapa kwetu TZ, yaani mtu anazaa nje, hapo kuna matumizi ya Kondom kweli? Si mwendo wa ngozi kwa ngozi. Kama mie ningekuwa msuluhishi kabla ya kuongelea ishu yao ningewaomba waende wakapime afya zao kwanza! Hilo suala la kupima afya peke yake ni mtihani tosha wa kujua kama hawa watu kweli wako serious au ni mazagazaga ya dunia tu! eeh ndio maana kuna watu na mazagazaga yamemwagwa duniani hata uyaambie nini wao kwao ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

    Sasa wakishakubali kupima Ukimwi bila kelele wala Mikwarizo inabidi tuje kwenye suala la wao na ndoa yao ambayo kimsingi kutokana na hizo sms ni kama haipo ni mabecholor wawili wanaozini wao kwa wao na watu wengine wa nje. Vile vile kabla hatujaanza mjadala lazima niwaulize kama kuna ukweli wowote kwenye hizo msgs, nakwambia baada ya kupima UKIMWI confessions zitakuja kilaini, asikwambie mtu suala la UKIMWI mlisome hivyo hivyo kwenye magazeti na mlisikie redioni lakini usikutane naloface to face confo yote inakuondoka mwana wane. Kama wanao au hawana baada ya confession tunaanza program ya kuishi kwa matumaini na kutunzana pamoja na kulea watoto wao. Kama hawana na wameconfess tunatafuta njia mbadala ya kutatua tatizo lao kwani inaonekana hawataki kuishi maisha ya ndoa, ama hawakuwa tayari au walilazimishwa kuishi pamoja, na kwa kuwa wameamua kuishi katika hizo risky behaviur na ushauri nasaha watakaoupata huko Angaza au Muhimbili utawawezesha kuamua kuishi maisha wanayotaka kuishi.

    Utaweza tu kumpeleka punda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa majii.

    Vile viel imeandikwa katika maandiko matakatifu kuwa "MZINIFU KWA MZINIFU MWENZIWE!" Kwa hiyo ukiona tu kapepo ka uzinifu kamekujia au unaanza kuzini basi ujue haitachukua muda mkeo au mumeo pia naye atazini utake usitake kwa sababu imeandikwa. Ukiona unaweza kujichunga na vishawishi basi ujue na upande wa pili ni hivyo hivyo.

    Mswahili

    ReplyDelete
  35. Mungu atuhurumie! kwa kweli si jambo la kuchekelea hili, Mungu na atuhurumie, tha's what i can say for now.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...