Naibu waziri wa Ulinzi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia) akikunjua bendera ya taifa kabla ya kumkabidhi nahodha wa timu ya taifa ya bara 'Kilimanjaro stars;, Salum Sued( pili shoto) wakati wa kuiaga timu hiyo leo ofisi za TFF tayari kwa kushiriki michuano ya chalenji Kenya kuanzia Nov.28. shoto ni kocha Marcio Maximo, Makamu wa Rais wa TFF Mh. Nyamlani na katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela
Naibu waziri wa Ulinzi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akimkabidhi bendera ya taifa nahodha wa timu ya taifa ya Kilimanjaro stars, Salum Sued wakati wa kuiaga timu hiyo inayokwenda kushiriki michuano ya chalenji Kenya kuanzia Nov.28. wengine toka shoto ni kocha wa timu ya taifa ya vijana, kocha wa taifa stars Marcio Maximo, Makamu wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani
Meneja uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika akikabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa katibu mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebele leo asubuhi kwa ajili ya timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Twiga stars inayojiandaa na michuano ya kimataifa. vifaa hivyo vina thamani ya sh. milioni 14.5. Kushoto mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake, Lina Mhando.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kifimbo ChezaNovember 25, 2009

    """"
    kilimanjaro stars yakabidhiwa bendere, twiga stars yapewa vifaa"""""


    Imekabidhiwa bendere??????

    ReplyDelete
  2. MAXIMO UPO JUU!!!!

    hakuna kitu ninachokipenda kama nidhamu katika timu, hilo umefanikiwa... HEKO MAXIMO! wapuuzi wengi wanauchukia msimamo wako juu ya "WAVUTA BANGE"... hivo hivo endelea kuwabania hao wavuta bangi hata kama wana uwezo wa kudaka kama alivyokuwa OLIVER KHAN au ni viungo machachari kama ZIZZOU au BOBAN au washambuliaji hatari kama MESSI... WANYIME NAFASI HAO! hii itatusaidia kuwajengenga kisaikolojia na kinidhama watoto/vijana wadogo ambao wanatamani siku moja wacheze timu ya taifa wajue BANGI,MADAWA YA KULEVYA, UTOVU WA NIDHAMU au ULEVI ULIOPINDUKIA havina nafasi ktk timu ya taifa...

    bora uwe na magolikipa mia wabovu kama Mustafa Bartez au Dihile lakini wenye nidhamu kuliko kuwa na wazuri kama Buffon wakati nidhamu hawana vilevile ni model wabaya kwa KIZAZI KIJACHO

    USHAURI:
    watanzania waache kumuiga DIOUF hata kama ni skipper wa N/Team kwani historia inaonyesha walioijenga misingi ya soka la Senegal walikuwa na nidhamu ya hali ya juu ndio maana wao sasa ni rahisi hata kucheza ulaya wakati hapa bongo ni kituko na sasa ndio wakati wa kuweka misingi bora ili wale copa cocacola waje kucheza soka ulaya na kuinua kiwangom chetu

    "IN MAXIMO WE TRUST"

    ReplyDelete
  3. Jamani fedha zote hizo zinatumika lakini mbona hakuna matokeo ya kuridhisha.

    Kitu muhimu, Tanzania mpaka sasa hivi haina first eleven ya Taifa. Kila kukicha timu mpya, kocha anajaribu kila mchezaji. Hii ni dalili ya matatizo kwani hata wahenga walisema mfa maji haachi kutapatapa.

    Na kwa kawaida mtu asiyejua afanyalo kila mara hatashika kila kitu, kwani hajui pa kuanzia wala pa kumalizia. Mfano mzuri ni fundi uchwara wa redio. Redio kama imeharibika basi atakugusa waya huu mara ule, transitor hii mara ile, hoo betri zina kutu, mara weka nyingine, ili mradi tu kubahatisha hakuishi. Na ikitokea kabahatisha basi atajisifu kuwa yeye ni fundi kweli kweli. Hasipo weza mara utasikia basi inabidi uje kesho kuna waya, transitor n.k inabidi nikatafute nyumbani au dukani. Ukija kesho hoo unajua zile spea hazipatini sasa, hii yote mwisho wake unakuja kugundua kumbe tatizo sio redio, tatizo ni fundi. Fundi hana hata kifaa cha kupima kama systems za redio zinafanya kazi?? Fundi gani huyu.

    Fundi Maximo bwana.

    ReplyDelete
  4. WATANZANIA MSITEGEMEE MATOKEO MAZURI KIRAHISI.MATOKEO MAZURI YANAKUJA MUDA MREFU BAADA YA KAZI KUBWA KUFANYIKA.KAZI ANAYOFANYA MAXIMO INARIDHISHA SANA NA HATUA TANZANIA ILIYOPIGA KISOKA BAADA YA YEYE MAXIMO KUSHIKA TIMU, MSITEGEMEE MAFANIKIO YAJE KIRAHISI INACHUKUA MUDA NA ITAWEZEKANA TU IWAPO WACHEZAJI WETU WAKIWA NA NIDHAMU UWANJANI NA MAZOEZINI.MAXIMO AMETUTOA MBALI SANA NA ANAJARIBU KADIRI YA UWEZO WAKE LAKINI BADO KUNA MAMBO MENGI YANAMKWAMISHA HASA NIDHAMU NA WACHEZAJI KUJITUMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...