Kaka balozi wa nanihii,
Tafadhali kwa heshima na taadhima nisaidie kuhusu uhalali wa kikosi
cha zimamoto kusimamisha magari barabarani na kuulizia stika za fire.
Uhalali huu wameutoa wapi?
Hivi karibuni nilikuwa moshi wakati naelekea Arusha nikaona jamaa wa fire wametanda barabarani kuuliza je una fire extiguisher? ukisema unayo wanataka stika....je, moto unazimwa na extinguisher au stika? mnaosafiri nchi mbalimbali kuna mambo kama haya?
imefika mahali kila anayetaka kuchuma
atuonee wananchi.hali hii mpaka lini?
Halafu hao jamaa wa faya wanataka kulkazimisha tuwafanyie kazi zao. wao wanalipwa kuwa matrafiki ama kuzima moto...????
Sheria ziko wazi mtu akinunua property yake anatakiwa afanye nini. Kwa mfano gari,una register,unapata road licence,na insurance. hivyo ni vitu vya lazima. stika ya fire na ya nenda kwa usalama ni za nini?
balozi tusaidie sana katika mambo haya ili ifike mahali viongozi wajue walalahoi tunaonewa sana.
Mdau Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Yaani ndugu yangu umenena! Maana hizi sheria zingine sijui zinapitishwa wapi?! sijui chini ya mwembe au baa! Sasa Dar town ndio mshikemshike kishenzi na hao jamaa! Halafu hapa sasa, wanakuwa na trafiki wawili na FFU! Lazima wakunase tu. Twafa! Kuwa na gari, sasa ni sheshe.

    ReplyDelete
  2. KATIKA UTAALAMU WA UZIMAJI MOTO STIKA NDICHO KITU MUHIMU SANA KULIKO MAJI KWANI STIKA INAPUNGUZA KASI YA CHOMBO KUUNGUA NA SI EKSITINGWISHA KAMA UNAVYODHANI. SASA PESA NI KWA AJILI YA KUJIKIMU TU SI UNAJUA VIKOSI VYA ZIMAMOTO HAVINA BAJETI KUBWA NA NDIYO CHANZO CHA VIFAA DUNI VYA KUZIMIA MOTO, TUSAIDIE TUKUSAIDIE.

    ReplyDelete
  3. Si kila idara imetakiwa ichangie ipendekeze jinsi ya kufyatua visenti kwa huu..naniihhii.. unaokuja. Na wakubwa wao wamependekeza stika za fire!!Sekta ya Afya nasikia imependekeza Stika za Je Umepimaa??

    ReplyDelete
  4. Kwani mlipoambiwa maisha bora kwa kila Mtanzania hakuelewa? Hii ni njia ya kuwapatia maisha bora Matrafiki.

    Njia yao ya mwanzo ya kujificha nyuma ya miti imepitwa na wakati kwa vile wakijibanza nyuma ya mti vitambi vinatokeza kwa hiyo madereva wanashtukia dili.

    Hebu hao Traffic Police watupe statistics za magari yanayokwenda kukaguliwa kila mwaka na idadi ya Sticker zinazotolewa. Sidhani kama magari yanayokaguliwa yanavuka 5% ya magari yanayotembea lakini kila gari utakuta lina sticker na fomu ya kuonyesha kuwa limekaguliwa.

    Tanzania nchi yangu, nakupenda kwa moyo wote.

    ReplyDelete
  5. Anko mithupu hii ni dili kubwa tena jamaa(Wazima mioto) nao wanapewa hesabu wapeleke kila jioni kwa wakubwa, nami mdau nipo hapa miundombinu nilikua namshauri mkuu wangu tuanzishe sheshe la stika za Tanroad maana nasi jua linawaka kidogo, waswahili wanasema kula nami nikule!

    ReplyDelete
  6. Tatizo hapa sio sheria. Sheria ni mzuri kabisa ila utekelezaji wa sheria hii unaruhusu vitendo vya rushwa. Kimsingi ni tatizo la watanzania wengi kutozingatia maadili ya kazi zao pamoja na kushindwa kuheshimu kazi zenyewe.

    Kiutarabitu sticker ya fire ina maana yake. Gari inatakiwa imepelekwe sehemu maalum ikakaguliwe kuhakikisha ina kila kitu kwa ajili ya usalama wa moto. Endapo mtu anayekagua atajirisha basi anatoa sticker. Pia na stikers za usalama barabarani gari inatakiwa kukaguliwa.

    Tatizo liloko Bongo huo utaratibu haufuatwi kabisa. Kwani stickers zinauzwa tu mitaani bila hata kuona gari. Kibaya zaidi hela zenyewe haziendi serikalini.

    Wenye magari pamoja na askari wanachangia kuwepo mchezo huu mchafu.

    Mimi nadhani serikali ingeondoa huu utaratibu kwani hauna maana yeyote zaidi ya kuwanufaisha askari barabarani na wezi wengine ambao wanatengeneza sticker feki.

    Hizo ni kero ndogo ndogo na zipo nyingine nyingi tu hapo Bongo. Kuondoa hizi kunahitaji viongozi makini ambao wanafuatilia mambo yanayowahusu wananchi kwa karibu sana. Kwa bahati mbaya sana viongozi hao Tanzania hakuna kwa sasa.Mpaka viongozi hawa watakapopatikana watanzania wataendelea tu kuishi na kero mbalimbali.

    Kura yako mtanzania ndiyo ukombozi wako. Embu jaribu kumchagua kiongozi wa serikali ya mtaa, diwani, mbunge na hata rais ambaye hana mahusiono na wale walioko maradarakani ambao wameshindwa kuondoa kero halafu muone kama hakutakuwa na mabadiliko.

    Vyombo vya habari navyo vina nafasi kubwa sana ya kupigania wananchi katika kutatua kero hizi ndogo ndogo, embu tumieni nguvu yenu ya kupeleka habari na kushawishi kupiga vita kero hizo. Habari sio tu EPA, Richmond, na malumbano ya CCM. Hizi habari za kero ndogo ndogo ni muhimu sana kwani zinahusu maisha ya kila siku ya mtanzania wa kawaida pamoja na nyie wenyewe waandishi. Andikeni, hulizeni maswali kwa wahusika wakuu na mhakikishe mnapata majibu sahihi na yenye tija. Kama hakuna mabadiliko endeleni kuandika na kuwashawishi wananchi wachukue hatua zinazofaa, kama vile kuwakataa viongozi wabovu.

    Wako
    MG

    ReplyDelete
  7. Poleni na nchi yenu.Huko ndiko kusukuma gurudumu la maendelea mpaka lifike huko kusikofikika.Na next thing utasikia WIZARA YA AFYA, nao wanataka kila kwenye gari kuwe na BOX LA CONDOMS ,maana kasi ya ukimwi inatisha.Kutokuwa na box hilo ni kisa kwa mujibu wa watawala, sio kwa mujibu wa sheria.

    ReplyDelete
  8. Watanzani wizi mtupu,vitu vya mhimu kwenye gari ni road lisence,insurance na TRA-mapato hivi vingine ni wizi mtupu,issue ya fire extinguisher ni dili za wakubwa kama ilivyokuwa speed gervanor zililetwa na waziri mtaafu -Sumaye,ziko wapi sasa,hakuna anafuatilia hivyo vinguza mwendo

    Hili hata mimi limenigusa,utakuta unaulizwa una fire extinguisher,una stika,mtungi wa kilo ngapi? ukiwaambia unayo,kama hujanunua kwao wanakuambia gas uliyoweka ni feki na mtungi hauna viwango vya TBS,kwa hy wanakulazimisha ununue kwao kila kitu,mbaya zaidi wanalazimisha hata gari za watu binafsi,kuna baadhi ya gari zinakuwa-imported zikiwa na f,extinguisher,lakini wao hawataki mitungi hiyo,
    -je moto wa TZ na Ulaya una tofauti?
    At least inaleta maana katika public transport ,mfano mabasi,lakini private naona haina maana.
    -Hivi gari yangu ikiungua wao wanapata hasara gani?
    -Je kama umenunua kwao vitu vyote,gari likawaka,nimejaribu kutumia gas yao imeshindwa,je nitasaidiwaje?
    -Je kuna mafunzo yoyote ya fire marshal-utaalam yanatolewa kwa waendesha magari? mimi ninavyojua kila aina moto ina utaalam wake wa kuzima,
    -Wanakukagua kama umelipia stika wakati hawajafanya ukaguzi,does it make sense,its None sense!

    Jamani wapi tupeleke malalamiko yetu,kila taasisi/wizara wanatafuta jinsi ya kutukamua,

    Watanzani inabidi tuwe aggressive kudai haki zetu,Tanzania is no longer a peaceful country,raia tunanyanyasika sana,AMANI haipo ila wa TZ waoga kudai haki zetu,i think nchi za Ulaya hawana ujinga kama huu,mafisadi wanatunyonya jamani!

    ReplyDelete
  9. tanzania nchi yetu lakini kuna vitu vinakera mpaka unachukia nchi yako,barabarani unasimamishwa na kila aina ya mtu mwanajeshi,ffu,mgambo na sasa zimamoto,hivi hii nchi inaenda wapi?kweli ni kichwa cha mwendawazimu,hayo magari tujiulize yalikotengenezwa hawakufikiria FIRE HAZARD?hakika walijua kuna fire hazard lakini tishio lake sio kubwa kiasi cha kuweka fire extinguisher especially in private light goods vehicles...nimeendesha gari nchi chache duniani ikiwemo zilizotengeneza hayo magari lakini sijaendesha gari lenye fire extinguisher au kusimamishwa na kuulizwa gari ina fire extinguisher au la.nafikiri ingekuwa busara hawa wanazimamoto wangehimiza watu wawe na fire extinguishers nyumbani sababu naamini ndani ya nyumba ndio kuna fire hazards nyingi kuliko gari.muda mwingine unajiuliza hawa viongozi wetu wamekwenda shule au vipi,lakini utasikia wote wanaitwa profesa au dokta fulani,kweli kusoma sio kuelimika.

    ReplyDelete
  10. Ebaeeh bongo lazima uwe na Jina ndo utaishi kwa upole au mjomba wako awe fulani ubabeubabe tu kila mtu anatunga sheria unakumbuka early 90s ilitokea sheria ya kutoweka tinted ktk gari chanzo waziri mmoja nyumba ndogo yake ilifichwa ndani ya gari lenye tinted chochote kikimuathiri kiongozi itakua sheria wakati huohuo mtanyanyaswa mpaka mfe ntarudi likizo tu mie simo hapa kwangu hata insurance ni option

    ReplyDelete
  11. Kuna haja ya kuhoji huu uonevu Wabunge hawtozwi hizi kodi, na ni asilimia chache sana ya wa Tanzania ndiyo wanaumia hivyo swala hili litaendelea kuumiza watu. Na sidhani kama utalisikia bungeni. Wanaharakati wapo wapi? Non-citizens hawatozwi. Huu ni uonevu unatofauti gani na kodi ya kichwa? Kodi ya maendeleo? Hizi double taxations zilishafutwa....

    ReplyDelete
  12. Nyie nyie nyie, hii ndio Tanznia bwana ukisikia nyingine ni ya kuchonga. Kila kitu kinakwenda kinyumenyume. Mimi niliwahi kuuliza Je stika inazima moto au ndio ujasiriamali wenyewe kila idara inabuni miradi? sikupata jibu. Tuyaache haya yana wenyewe. wewe nunua tu ukuze uchumi wa nchi yetu kama ni kweli. Hata hizo fire extinguisher wenye nazo hawajui kuzitumia, moto ukiwaka itajitumia yenyewe. Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake.

    ReplyDelete
  13. ubaya wake walioamuru hii ujangili wa mchanga kweupe peee wanajua kuwa tunajua kuwa wanajua namna ya kutafuta hela kwa ajili ya uchaguzi. tulikiletewa kanga na kofia mwakani tunadhani zimetoka kwa obama pasi na kufahamu kuwa ni hela tulizoporwa mchana mchana zinafanya kazi ya kuwaweka watu madarakani

    ReplyDelete
  14. ninakoma na hili gari nilonunua kwa mkopo yalabi!!!

    one day yes...sijui lini ila one day

    ReplyDelete
  15. hiyo ni sehemu tu ya ushahidi wa jinsi wafanyakazi wa serikali walivyo wavivu, wanataka malipo bila kufanya kazi, wapo wengine waliolipishwa wanafanya kazi wizara hiyohiyo lakini wanaona uvivu hata kuiuliza wizara yake uhalali wake. pia ni uweledi wetu hatuujui, mfano iwapo si halali na mwanasheria akiamua kuliulizia hili mahakamani je litakuwepo? wewe mithupu hapo unapofanyia kazi si ni karibu sana na hao wakina nanihii? kwanini usitusaidie kuwauliza halafu ukatueleza. pengine umewauliza lakini kwasababu ni wavivu na hawajui kazi yao (ya kusema tu SI HALALI NA IKOME MARA MOJA) wamekaa kimya. mithupu samahani kwa kuwaambia ukweli ninyi mnaofanya kazi serikalini, ninyi ni wavivu na serikali ni mnyang'anyi wa mali na maendeleo ya wananchi kuliko mtu yeyote. lakini sentensi hii haiwahusu wale wachache wanaofanyakazi serikalini wanaojitahidi kufanyakazi kwa bidii na uadilifu kwa wananchi ingawa wanapikiwa majungu na mivivu hiyo mingi.

    the brain.

    ReplyDelete
  16. wabongo acheni kulalamika sana na kufikiri idara za serikali ndio za kupeleka matatizo yenu,its time sasa kutumia mahakama zetu vizuri kupinga sheria za kishenzi kama hizi ambazo hata kwenye katiba yetu hakuna..nendeni mahakamani mkashtaki uhalali wa hii sheria nina uhakika hakuna sheria kama hii zaidi ya wakurupukaji wachache wasiojua katiba wameamua kutumia vyeo vyao kuweka visheria visivyo na maana yeyote na wala havijulikani na bunge ili kuhalalisha ulaji wao,hii nina uhakika wananchi wakienda mahakamani watashinda

    ReplyDelete
  17. nilisoma ile habari ya mashaka,japo kuwa simjui huyo mashaka ndio nani,na leo nimesoma habari hii ya stika,machozi yananilenga,donge limenibana kooni.
    kama mnakumbuka,kuna kipindi umeme ulikua unakatwa saaana,lile lilikua dili,kuna mkubwa alianzisha biashara ya majenereta.sasa hivi kuna mkubwa mwengine ameleta biashara ya fire extinguisher,kwahiyo moto utawaka bongo mpaka arudishe hela yake aliyonunulia na apate faida.
    hope baada ya miaka mitano ijayo nitakapoamua kurudi bongo itakua imeisha,but believe me,lazima kuna kero nyengine itakuwepo kushinda hiyo.

    ReplyDelete
  18. mmechagua wenyewe CCM sasa mnalia nini na sheria za kipuuzi zinazotungwa kwenye mabaa.

    ReplyDelete
  19. Nilpokuwa Dar mwanzoni mwa mwezi huu, nilikuwa kwenye daladala ambayo ilisimamishwa na wanafaya kuulizia hiyo sticker na kama wana extinguisher huko Bagamoyo Road. Nadhani ni wazo zuri kwa kila gari, daladala kuwa na extinguisher. Lakini nachoshangaa ni utekelezaji wa kuhahikisha kuwa magari wanasticker/extinguisher. Si, ingekuwa kazi ya trafiki? Kwa kweli nilishangaa kuona wanafaya wameacha kituo chao cha zimamoto kwenda kusimama barabarani kusimamisha magari na daladala. Kama wangehitajika kuzima moto wangefanyeje? Kwa kweli haifai.

    ReplyDelete
  20. Sasa hii ni njaa kali hivi zimamoto ndo kazi yao hiyo? SAID MWEMA NDIYE MWENYE MAKOSA HAPA, HAYA MAMBO ANAYASIKIWA LAKINI HAYAKEMEI, NA WABUNGE PIA WANAYAONA HAYA LAKINI HAWAYAZUNGUMZI KWA VILE HAYAUSU KWA VILE HAWASIMAMISHWI, JAMANI WANANCHI WAKATI UMEFIKA WA KUCHAGUWA VIONGOZI WANAOTUJALI SISI WALALA HOI, IKIBIDI NA HII CCM NZEE TUIPIGE CHINI TUTAFUTA CHAMA KIJANA CHENYE UCHUNGU NA SISI, TUSIANGALIE MAKUNYANZI, TUMTWENGE NYANI TUKIWA TUMEFUMBA MACHO, MWAKANI CCM CHINI, NA WABUNGE WOTE WA SASA CHINI, MWISHO SAID MWEMA NA WAZIRI WAKO TUNATAKA MAELEZO JUU YA UPUUZI HUU.

    ReplyDelete
  21. Sasa umefikia wakati kwa serikali kuu kutoa power za sheria ndogo ndogo za mijini kama hizi fire extinguisher,speed governor ama kutumia ear piece wakati ukiongea na simu huku ukiendesha gari kupitishwa na mabaraza ya madiwani kwenye kila mkoa na kuwa sheria.Nimeweza kushuhudia kuna viji sheria vinaubuka kama kiongozi furani yuko ofisini akija mwingine inakuwa historia.

    ReplyDelete
  22. Mwaka ule uchaguzi ulipokaribia jamaa akatangaza spidi gavana ziliwasaidia sana katika uchaguzi. Mwaka huu mafisadi wamebanwa na kuna uhasama umejengeka baada ya kutajana na wengine kufikishwa mahakamani hivyo wafadhili wa uchaguzi ujao wamepungua au wanaelekea kususa kufuatia kashfa zinazoendelea. Sasa vyanzo vya fedha za uchaguzi zitatoka wapi? FIRE!!!!!!!

    Sheria imeshatungwa na imeshapitishwa na wabunge wenu mliowachagua na sasa fire wanafanya tu kutekeleza hiyo sheria wala msiwalaumu sana. Unachotakiwa kufanya ni kulipa na kama una malalamiko uendelee nayo kwenye vyombo husika. Ila niwakumbushe kwamba mwisho wa kulipa ni tarehe 31 December 2009 na kama akikukamata mtu yoyote kabla ya muda huo asikubabaishe mwambie deadline bado. Kuanzia January mwakani unatakiwa uwe na sticker sii chini ya nne kwenye gari yako including TRA, Insurance, Fire na usalama barabarani. Naombeni jamani idara nyingine msituletee kodi nyingi (AFYA - UMEPIMA?;

    ReplyDelete
  23. Msiumize vichwa sana jamani kuhusu hili jambo. Kwani hapa mtu unashindwa kuelewa kama hili ni deal la watu kula pesa!!!?? Sisi watz tumekuwa wajinga sana ndio maana tunaburuzwa hadi na mambo kama haya. Hapa ni watu wamekaa wakapanga ni namna gani wale pesa za watu ndo wakaja na idea hiyo. Wanaona magari yanaingia kwa kasi hapa nchini na watu wana pesa sasa cha kufanya ni kuzifaidi hizi pesa zao ndo wakaja na hiyo project. Walishawahi kula pesa kwa kuchora mikanda ya daladala na kuandika ubavuni! Eti VETA peke yao ndo walikuwa na uwezo wa kufanya hiyo kazi!! Wakichukua 20,000/ kwa kila daladala ni kiasi gani cha pesa? Wakati kama ni kuandika hata mimi tu naweza nunua rangi na nikaprint "nauli Tsh 250/" lkn unaambiwa upeleke VETA!! Wajinga ndio waliwao...tujiandaeni hadi mgambo watatusimamisha.

    ReplyDelete
  24. USHAURI WA BURE KWA WALE WAAENDAO NYUMBANI (TZ) KWA AJILI YA X-MAS!!
    1. Kabla ujaendesha gari hakikisha lina fire extingusher.
    2. Elfu Mbili Mbili za Kutosha kama huna Leseni ya gari
    3. Hakikisha gari lina stika ya week ya kwenda kwa usalama.
    4. Stika ya fire
    5. Insurance
    6. Vitaulo vidogo na WHITE-T za kutosha maana kuna joto la kufa mtu.

    7. Mipira sio lazima sana....maana watoto wakibongo wazuri mnoo..halafu ngoma sio vile dont belive the statistics......
    8. Cologne za kutosha.
    9. Hakikisha unakojoa na kunya nyumbani kabla ujaenda bar maana vyoo vya bar zetu unaweza ukatapika badala ya kunya au kukojoa.( They are nasty! in short.)
    10.Kuanzia mwenge mpaka morocco ukiwa unaenda/unarudi mjini please! please usiendeshe kwenye LANE YA KATIKATI maana utakufa.
    12.Kama utakuwa na mpango wa ku-hang na washiukaji au ndugu zako wa karibu please wape cologne/deodorant/mouthwash kabla hamjaingia mtaania maana unaweza ukawachoka mapema.
    12. Usinywe HEINEKEN maana unaweza kunywa maji ya mtaro.(Ziko feki za kumwaga).
    13. Usinunue kitu chochote cha Electronic maana vitakuwakia moto.
    14. Beba extra charger ya vitu vyako vyote vya electronic maana umeme ni wa mgao.
    15. Usisahau kubeba Lotion yako, shampoo, Body wash, after shave na bar soap za kukutosha maana hata za Mlimani City ni feki.
    Aza zani zati nawatakia likizo njema.
    Mdau, Likizo Dar.

    ReplyDelete
  25. uwanja wa fisiNovember 28, 2009

    nunueni baiskeli kuondokana na usumbufu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...