
Mkuu wa Usalama barabarani James Kombe (pichani) akizungumza leo jijini Dar kuhusu utoaji huduma ya usafiri kupitia kampuni ya Majembe Auction Mart.
SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
Yaania Kuanzia Desemba 1, 2009 Kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART imekasimiwa kazi ya kusimamia, kufuatilia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni ya kusafirisha abiria katika jiji la Dar na kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo.
Mbli na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.
Wenye vyombo vya Usafiri, wafanyakazi wao, abiria na wananchi kwa ujumla wanaombwa kutoa ushirikianao wa hali ya juu ili kuleta maboresho yenye manufaa kwa umma.
Mbli na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.
Wenye vyombo vya Usafiri, wafanyakazi wao, abiria na wananchi kwa ujumla wanaombwa kutoa ushirikianao wa hali ya juu ili kuleta maboresho yenye manufaa kwa umma.
SUMATRA NA TRAFIKI WATUELEZE KWANZA UJUZI WALIONAO MAJEMBE KATIKA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI, NA KAMA WAO WANAUWEZO MKUBWA ZAIDI YA SUMATRA BASI HAKUNA HAJA YA KUWA NA SUMATRA ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UTENDAJI. INAELEKEA KUNA WATU WAMEAMUA KUPEANA ULAJI KUTOA UDALALI MPAKA KUSIMAMIA KANUNI ZA USAFIRISHAJI NI VITU VIWILI VISIVYOOANA.
ReplyDeleteHII NI DALILI NYINGINE KWA VYOMBO VYA SERIKALI KUSHINDWA KUFANYA KAZI AMBAZO WAMEPEWA KISHERIA.
ReplyDeleteHAPA KUTAKUWA TU NA HARUFU MBAYA YA KIFISADI.JE TENDA HII ILIFUATA KANUNI ZA MANUNUZI YA UMMA? KAMA KANUNI ZALIFUATWA JE MASHARTI MAALUM YALIKUWEPO? KAMA KULIKUWA NA MASHARTI JE SHARTI LA MKANDARASI LAZIMA AWE NA UWEZO NA UJUZI WAKUFANYA KAZI HASWA YA KUSIMAMIA MASUALA YA USAFIRI LILIKUWEPO? JE MAJEMBO WANA UJUZI WOWOTE KATIKA FANI YA USAFIRISHAJI?
KAMA HAKUNA MAJIBU SAHIHI KWA MASWALI HAYA MARAHISI TU BASI MPANGO HUO NI HAUNA MANUFAA KWA JIJI. HII NI KUIBIA SERIKALI NA KULETA USUMBUFU KWA WANANCHI.
KWA NINI SUMATRA NA POLISI USALAMA BARABARANI WASIAJIRI VIJANA NA KUWAPA MAFUNZO YA KUSIMAMIA MASUALA YA USAFIRI KITU AMBACHO KINGEKUWA UENDELEVU ZAIDI BADALA YA KUINGIA MKATABA NA KAMPUNI BINAFSI AMBAO INAONEKANA HAINA UJUZI KATIKA HII KAZI.
WAFANYAKAZI WA MAJEMBE AUCTION HAWATAFANYA LOLOTE LA MAANA ZAIDI YA KUENDELEZA KUPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA MADEREVA WAZEMBE.
MHESHIMIWA WAZIRI MKUU PINDA FUATILIA HILI JAMBO MAPEMA KABLA HAWA JAMAA HAWAJAANZA KAZI KUZUIA HASARA KWA SERIKALI. JE HII INA TOFAUTI NA ILE DILI YA WASIMAMISI WA KITUO CHA MABASI UBUNGO AMBAO IMEONEKANA ILIINGIZIA SERIKALI HASARA YA MABILIONI YA FEDHA?
ReplyDeletemmmmh wabongo kwa kupeana michongo basi tena! jamaa tayari ashakatiwa posho hapo!!
ReplyDeleteSUMATRA imeshindwa kazi; tunaipa kampuni Binafsi kazi ya kusimamia sheria za nchi...!!!
ReplyDeleteHaya tafuteni hela za uchaguzi kwa nguvu zote.
MAJEMBE SASA KUKABIDHIWA VIWANJA VYA NDEGE NA KUKAGUA LESENI ZA MARUBANI....!SUMATRA IVUNJWE BAADA YA KUKUBALI KUWA IMESHINDWA KAZI NA HAINA UJUZI KATIKA UCHUKUZI KAMA ILIVYO MAJEMBE.
ReplyDeletesitaki kuamini...majembe tena???
ReplyDeletetuvunje vyombo vyote vinavokura pesa ya serikali kwa kushindwa simamia kazi hizi za umma (SUMATRA)
Kweli Bongo tambarare, tangulini Auction Mart inakuwa trafic law enforcer??? kama serikali imeunda chombo cha kuhakikisha sheria zinafuatwa, kwanini majukumu yake yanakuwa out-sourced? kuna haja gani ya kuwalipa Sumatra na Traffic Police au kuendelea kuwa nao kama kazi hiyo imewashinda?? Kodi ya wavujajasho sasa inawalipa Majembe na inaendelea kuwalipa watumishi wa Sumatra na Jeshi la Polisi!!!! Muda mtasikia jeshi la polisi linawapa Majembe au kampuni binafsi tenda ya kufanya kazi za ki-Police...
ReplyDeleteMdau Uncle Tom, Dallas-USA
Bongo Tambarareeeeeeeeeeeeee!
ReplyDeleteNa bado watatafuna nchi mpaka ibaki mifupa. Kwikwikwikwi
TRA SASA SUMATRA(DALADALA)
ReplyDelete1.HEBU SUMATRA NA AFANDE K WATUELEZE HII MAJEMBE NI YA NANI?WAMILIKI WAKE
2.JE TARATIBU ZA KUMTAFUTA HUYU MAJEMBE ZILIFUATWA?
3.KAMA ZILIFUATWA JE AUCTION MART NA USAFIRISHAJI MBONA HAVIFANANI?
4.NAONA TRL NA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI TUWAPE MAJEMBE
MDAU MAKUSARO
Hivi hii nchi inaelekea wapi ? Kweli jamani kampuni ambayo imespecialize kwenye masula ya auction wanapewa kazi ya kuenforce sheria za barabarani kweli ? Sasa lengo la kuwa na Sumatra ni nini? Halafu mnasema Bongo tambarare , bongo ya vikwangua anga ..wakati mwananchi kila siku anabanwa ? sasa nimeelewa kwa nini watu wanatafuta jinsi ya kukimbia hiyo nchi !
ReplyDeleteMim ninavyoijua majembe kwa miaka mingi wanausika na mambo ya auction au yaa sale au minada,sasa nimejaribu kutafuta connection ya kaz yao ya minada na ukaguaji wa magari nimeshindwa kuelewa.
ReplyDeleteSasa itabidi Kombe atujibu sis wananchi
1)Kwanza majembe wanaleseni ya Kusimamia,Kufuatilia na kufanya ukaguzi wa mabasi?
2)Ni kipengele gani cha sheria kilichotumika kuruhusu kampuni binafsi kufanya kazi ya Kusimamia,Kufuatilia na kufanya ukaguzi wa mabasi?
3)Hao wafanyakaz wa majembe wamepata mafunzo wapi ya kufanya hizo kaz?
4)Je inapowekwa kampuni binafsi kufanya kaz ambazo ni za polis na SUMATRA sis wananchi tueleweje kuwa polis na SUMATRA wameshindwa kazi?