Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Mh. Deodorous Kamala (kulia) akizindua rasmi ubia kati ya kampuni ya Serengeti Breweriers Ltd na East African Breweriers Ltd/DIAGEO ya Kenya katika kusambaza vinyaji vikali vinavyotengenezwa na EABL/DIAGEO hapa nchini.
Uzinduzi huo ulifanyika usiku kuamkia leo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, ambapo kampuni ya Serengeti sasa inazo haki za kusambaza vinyaji vikali kutoka kampuni hiyo ya kenya hapa nchini kama vile Smirnoff, Johnnie Walker range of whiskies, Richot Brand na Bond 7.
Ijumaa iliyopita nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilitia saini makubaliano ya soko la pamoja (East Africa Community Common Market Protocol) ambapo kampuni hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania zinaashiria mwanzo wa utekelezaji wa makubaliano hayo ya soko la pamoja. Shoto pichani ni mwenyekiti wa Serengeti Breweriers Ltd Jaji Mark Bomani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu Mzee Mark Bomani ni kati ya watu ambao wametoa mchango mkubwa sana kwa taifa letu. Pia ni mchango ambao ameutoa kwa miaka mingi sana.

    Naweza kusema kuwa ame-devote maisha yake kulitumikia taifa kwa namna mbali-mbali.

    Hata hivyo, Jaji Bomani na waheshimiwa wengine wote wa umri wake nadhani umefika wakati wa kupumzika. Wasisubiri mpaka wajukuu wanastaafu ndipo wao wafuatie.

    Ni vizuri kukabidhi usukani kwa vijana ili wazee nao wapate wakati wa kuwaona vijana wakitumikia taifa na kutumia wakati huu kwa uzoefu pia taaluma walizonazo kuwashauri (vijana) na kuwaelekeza.

    Lakini kama watasubi mpaka wachoke kabisa, nadhani hawataweza kutoa ushauri mzuri wakati huo.

    Ni maoni yangu na nimemtaja Mheshimiwa Jaji Bomani kama kiwakilishi tu lakini wapo wengi.

    Kama nilivyosema haya ni maoni yangu inawezekana wengine wakawa na maoni tofauti.

    Nawasilisha.

    Mdau
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  2. SERENGETI BREWERIES KUWENI MAKINI NA HIYO NDOA NA HAO EABL ISIJE IKAWA WANAINGIA ILI KUILINDA TBL KATIKA SOKO KWANI HAO NI DAMUDAMU, KUMBUKENI TBL ILIVYOIUA KIBO! hii ni ndoa ya mashaka msilale chumba kimoja asije akachinjwa mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...