Naitwa Damian nimeoa na tuna watoto watatu. Ndoa yetu imedumu miaka 15 na imekuwa ya furaha siku zote hadi wiki mbili zilizopita. Mimi na mke wangu huwa hatuchangii simu na tupo kwenye mitandao tofauti.
Wiki mbili zilizopita mtandao wa simu yake ulikuwa na matatizo aliniomba simu yangu ili amtumie mdogo wake message ya muhimu sana. Nilimpa simu yangu alipoenda kwenye sehemu ya kutumia message akakuta message niliyotuma hapo kabla bado ipo.
Simu yangu huwa haindoi message iliyotumwa kwenye sehemu ya kuandikia message mpya. Message iliyokuwepo ilikuwa inasomeka “Hello honey, leo sitafika kwako mtoto anaumwa inabidi nibaki kufuatilia maendeleo ya hali yake, sorry dear”. Hii message nilikuwa nimeituma muda mfupi kabla hajaniomba simu na ni ya kweli.
Mke wangu aliisoma halafu akaendelea kuandika ya kwake. Wakati akiwa anaandika message yake, ile message niliyotuma ikajibiwa. Basi akamaliza kutuma ya kwake halafu aka-exit. Ile message mpya ikaonekana, simu yangu unaweza kusoma message bila kuifungua. Message
ikawa inasomeka hivi “Mpz siwezi kuelezea ni kwa kiasi gani nitakumiss leo plz muuguze mtoto tutaonana kesho mungu akipenda”.
Mke wangu aliisoma halafu akaendelea kuandika ya kwake. Wakati akiwa anaandika message yake, ile message niliyotuma ikajibiwa. Basi akamaliza kutuma ya kwake halafu aka-exit. Ile message mpya ikaonekana, simu yangu unaweza kusoma message bila kuifungua. Message
ikawa inasomeka hivi “Mpz siwezi kuelezea ni kwa kiasi gani nitakumiss leo plz muuguze mtoto tutaonana kesho mungu akipenda”.
Mke wangu akathibitisha kwamba nina uhusiano na mtu mwingine wa nje. Hakunirudishia simu yangu kwa siku nzima ili kuangalia messages zingine za nyuma. Amekuwa akilia sana na muda wote akilalamika kwamba nimemsaliti kwenye ndoa.
Ni kweli nimekuwa na uhusiano na msichana mmoja kwa muda kama miezi minne hivi sasa. Ni msichana mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu. Ni yeye aliyenianza tulipokutana nje ya Dar kikazi. Kwa kweli mwanzo nilisita sana kuwa na uhusiano naye. Nilimweleza kwamba nimeoa na nina watoto lakini bado hakuweza kurudi nyuma.
Ni kweli nimekuwa na uhusiano na msichana mmoja kwa muda kama miezi minne hivi sasa. Ni msichana mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu. Ni yeye aliyenianza tulipokutana nje ya Dar kikazi. Kwa kweli mwanzo nilisita sana kuwa na uhusiano naye. Nilimweleza kwamba nimeoa na nina watoto lakini bado hakuweza kurudi nyuma.
Nikawa na hofu kwamba labda ni mgonjwa fulani anataka kunimaliza tu na mimi. Basi nikapendekeza tupimwe kwanza tena sehemu tatu tofauti. Na hapa bado tena hakurudi nyuma. Na pressure ikawa inazidi kadri siku zilivyosonga. Hatimaye tukapima sehemu tatu tofauti kwa interval ya wiki mbili mbili. Matokeo yakawa ni mazuri kwa wote wawili na nikawa nimekosa kisingizio kingine kilichofuata baada ya hapo ni mapenzi mazito sana.
Nimempenda sana na ana vitu vingi sana tofauti wengine wengi ambao nimewahi kuwa nao kabla sijaoa. Na yeye pia huwa ananiambia kwamba hili ndilo penzi lake kubwa la kwanza amepata. Tunapendana sana na suala hapa si pesa, hajawahi kuniomba pesa wala kunimbia kama ana tatizo linahusiana na pesa. Wakati fulani huwa naona kama anahitaji pesa vile lakini niki-offer kumpa anakataa. Ni mapenzi tu na mama yake anaelewa mahusiano yetu na huwa tunawasiliana naye wakati fulani fulani.
Bado nampenda sana mke wangu na kila nilipokuwa nikitoka huko nyumba ndogo bado niliweza kumpitia pia mke wangu tena “with the same rythms” copy and paste. Ndoa yangu inatikisika sana. Nimekiri makosa yangu kwake na nimemwomba sana radhi. Nimekuwa nikifanya hivi karibu kila siku tangu matatizo yajitokeze lakini bado hajarudi kwenye mood yake.
Bado nampenda sana mke wangu na kila nilipokuwa nikitoka huko nyumba ndogo bado niliweza kumpitia pia mke wangu tena “with the same rythms” copy and paste. Ndoa yangu inatikisika sana. Nimekiri makosa yangu kwake na nimemwomba sana radhi. Nimekuwa nikifanya hivi karibu kila siku tangu matatizo yajitokeze lakini bado hajarudi kwenye mood yake.
Unaweza kukuta tumelala mke wangu ananikumbatia lakini mara anashtuka kunisukuma ghafula kutoka kwake. Kuna siku nikiwa nimelala nasikia, nikidhani naota, kama vile naumwa na nyuki sehemu za kifuani na tumboni. Niliposhtuka nikamkuta amenikalia huku ameshika kisu kwa mikono yote miwili nadhani akitafakari anichome wapi kifuani au tumboni. Lakini alitupa kisu chini na kuanza kulia sana huku akinikumbatia.
Nilimweleza yule msichana wangu wa nyumba ndogo matatizo ninayoyapata naye akawa ameguswa sana. Nikamuomba anipe break at least a month ili niweze kufix tatizo la nyumbani. Najua ananipenda sana na naelewa ni kwa kiasi gani atakuwa anaumia kwa mimi kumueleza hayo maneno.
Niko kwenye dillema kubwa sana. Wiki ya kwanza ikapita salama. Last week nimeambiwa yuko hoi amelazwa hospitali na akawa amemwambia mama yake kupona kwake ni yeye kuniona mimi. Mama yake alinipigia simu akaniomba na kunisihi sana niende. Nimekwenda na kweli hali ilibadilika na akaruhusiwa kutoka hospitali. Nilimpeleka kwake nikakaa naye hadi jioni then nikarudi nyumbani kwangu. Leo asubuhi mama yake amenipigia simu kaniambia kwamba lile tatizo limemrudia na safari hii hali ni serious sana.
Ndugu zangu naomba ushauri wenu nifanyeje?
Ndugu zangu naomba ushauri wenu nifanyeje?
She is a very different girl, really!!
Mdau Damian
Mdau Damian


Misupu,
ReplyDeleteUnayopenda sana haya, habithi kweli kweli, shenzy taipu!
Kuna watu na viatu wewe kiatu, mimi ndio mke wake, kwa hiyo wewe unakusudia nini kutuma ujumbe wake kama huu....
Tamaa zako zitakupeleka kuzimu ww.Waha hustahili ushauri maana kote kuna maji....sijui utakanyaga wapi.
ReplyDeleteDaah mzee DAMMY nakuhisi upo katika position gani,hapo ni pagumu sana,eeh bana kuwa nganagri hapo,kwani kumpoteza mke nako si kuzuri,mzuge tu MY WIFE wako kwa muda,then unaliendeleza kule kama kawa,badilisha simu,tafuta simu yenye MAUJANJA kibao sasa,kwani umesha kua CHEATER sasa,na ukiwa hivyo lazima uwe na TOOLS za kazi ka hizo simu zenye akili zake,uwezo wa kuwa muongo wa ghafla etc.
ReplyDeleteDamian,pole sana na dilema,
ReplyDeletefrom a man's point of view,inabidia umuoe tu kupunguza stress za mapenzi,
Je uko tayari kuoa mke wa pili,in other words wakutanishe wajuane muwe wote marafiki,
mfano kama Mr.Maulid Kitenge,yeye ana wake wawili na wote wanaelewana vizuri,kuoa mke mmoja ni dhana ya kizungu,sisi waafrika bwana,
wish u all the best
mdau
upuuzi huu.
ReplyDeletewe unaweza kuwa mwendawazimu..huwez penda watu wawili at same tym huo no uongo..and haijawah tokea lazima kuna mja ni chaguo lako la ukweli na mwingine ni wakuzugia si kihivyo..unamfurahia bt u don hv true love sa sijui ni mkeo o nyumba ndogo..and soon utaharibu ndoa yako na huyo mwanamke unaweza jikuta yalikuwa ni mapenz ya mda..acha ubwege kaka.and ipo siku na yeye atakusaliti coz atakuwa ameshakutoa maanan trust me and unaweza usijue milele
ReplyDeleteWewe bwana Damiani unafanya mambo yako ya gizani na mkeo anaekushikia kisu anaweza kuwa anapangilia mauaji yako,nafikiri wotee watatu na huyo changudoa wako inabidi muende mukamuone dakitari bingwa wa mambo ya akili,sijaua hospitali za watu wa akili ziko wapi Tanzania ila niliyokuwa naisikia maarufu sana ni ile ya mirembe.Na mkipewa dawa mfuate dozi vizuri manake mnaweza kurudia hali ile ile ya utahahira .Nafikiri huu ushauri utakufaa wewe na mkeo.
ReplyDeletemhangaza wa kanazi Ngara
http://duniayetukubwa.blogspot.com/
Mwehu wewe nani kakwambia kuwa ukipima Ukimwi baada ya wiki mbili mbili unakuwa huna? Unajua taratibu za kupima Ukimwi wewe? Unatakiwa upime kwanza kisha upime tena baada ya window period kupita, na hiyo window period ni miezi 3. Umeshaukwaa huyo mwanamke hana ugonjwa wa mapenzi wala nini ni huo huo Ukimwi tu. Siku hizi watu wanakula dawa na virusi vinajificha kwenye uti wa mgongo kwa hiyo havionekani kwa urahisi.
ReplyDeleteKaa kitako utulize boli, nenda mkapime tena wewe na mkeo kama umekwishamuambika basi tumieni ARVs, na maisha yataendelea kama kawaida baada ya ARVs. Unajiaminisha na hivyo vi lab vyetu vya Dar??
Hayo kwanza si mapenzi wala nini ni infauation na tamaa tu, akija mwanamke mwingine akakutaka na yeya mkienda kupima huko vichochoroni mkakuta hamna, basi naye utakula naye uroda, akikumwagia vimbwanga kwa kuwa wewe ni bwege mtozeni limbukeni wa mapenzi utafalls tena heads over heels in love kama unavyojinadi. Kumbe ni ukware tu uroda. Utakufa vibaya Chunga sana ndugu yangu!! Ulisoma boys boarding nini?? Maana wengi wanaotoka huko ni malimbukeni wa wanawake!!
You are more than stupid
ReplyDeleteWewe ni dini gani? Mkeo naye dini yake? Ndoa mliyofunga ni ya kiserikali au ya kidini?
ReplyDeleteKama both of you ni wakristu basi umeharamisha ndoa yako. Mkeo anaweza dai talaka. Lakini naye anapaswa akusamehe kwa vile umekiri. Anaweza kusamehe lakini kusahau siyo rahisi ataifanyia nongwa sana na especially kama yeye ni mwaminifu.
Otherwise achana na nyumba ndogo na uijenge upya nyumba yako kubwa.
pole kaka.nami i was in the same situation a couple of months ago,it take time to handle it and to return things mend but do not give up u are men.
ReplyDeleteDuh kaka Damian lakini huyo ni mkeo wa ndoa mind u. Huyo msichana asikuharibie ndoa na mapenzi yako ya miaka 15. Plz achana na huyo dada tulia na familia yako.
ReplyDeletepole kaka na matatizo yaliyokupata.mm binafsi siwezi nikakulaumu maana wewe ni binadamu kukosea kupo kaka yangu.nachowesha kukushauri rudisha moyo wako na mapenzi yako kwa mke wako,sahau kabisa huyo dada mwingine.nakwambia hivyo kwa maana hii je kama mke wako angekuwa na mtu nje ungejisikiaje?nadhani ingekuuma sana kama yeye mkeo ilivyomuuma.kwa kuwa ulimuoa mke wako basi yeye ndiyo mwenye haki
ReplyDeleteInaonyesha huyo mwanamke wa nje unampenda na mke wako unampenda. Mshika mawili moja humponyoka,ingawa huyo wa nje anakupenda bora uachane nae mara moja.kwani huna future nae yoyote ile zaidi ya kuzichezea feelings zake tu.Utamtesa mtoto wa watu bure wakati wewe tayari una responsibility zako.ulijiona kama tiger wood ulihisi mke wako asingejua.Jenga ndoa yako na huyo wa pembeni ipo siku na yeye atapata wake na sio wa kushare,jee na wewe ukisikia mke wako ana mwanamme wa pembeni utajisikiaje?kuachana na wa nje ni ngumu lakini jitahidi,punguza nae mawasiliano kidogokidogo ataumwa mwisho atapona huyo.Trust me nimeshawahi kuwa katika position kama yako kwa hivyo naelewa hali halisi na ilinichukuwa muda mrefu kuunga.
ReplyDeleteKaka, wewe ni mwanamme.. Cha kufanya kata mawasiliano na nyumba ndogo, haitakufaa kabisa.. Ni kweli huwa inatokea. Ila utafanyaje?? Achana kabisa na nyumba ndogo, ingawa inakupenda.. Unless, familia yako utaiweka matatani!!! Rudi , achana na huyo mdogo, anakupenda ila achana nae..
ReplyDeleteHuwezi kupanda farasi wawili ndugu, ukifika njia panda na kila farasi akaelekea njia yake utabaki na yupi? ukiweza kujibu ni yupi utabaki nae basi amua sasa angali mapema ili yasikukute hayo yanayokaribia kukufika muda mfupi ujao.
ReplyDeletewewe ni kiazi kweli kweli
ReplyDeletendo utatia akili unajifanya tiger woo sio ehh?? utashaa!! merry christmas
ReplyDeleteTUNAOA KWA MAPENZI SIO KWA KUDUMU MIAKA MINGI. KAMA MAPENZI YANAISHA UNAMOVE ON SIO MNAKAA KAMA NDUGU.
ReplyDeleteUSIPOKUWA NA RAHA HATA NDOA YENYEWE HAINA RAHA.
watu wengine bana, wewe damian kwanini uliendelea kusikilizia kwa nyumba ndogo? ungekula mara 2-3 halafu ungeishia mbali. sasa unaona yanayo kutokea? achana na nyumba ndogo. next time ukipata demu mwingine kula mara 2/3 halafu ishia mbali. usibaki kusikilizia kwa sana matokeo yake ndio haya sasa unayaona..
ReplyDeletewewe ni taahira, huelewi unafanya nini, miaka 15 ya ndoa unasema unapenda nyumba ndogo? huku ukisema pia unampenda mkeo?. Ushauri wa bure, mbembeleze mkeo muwe kitu kimoja mlee hao watoto wenu, achana na hiyo nyumba ndogo utaangukia pua.
ReplyDeleteHuyo nyumba ndogo pamoja na mama yake they are all birds of the same feathers, hakuna mama mwenye akili timamu anafurahia mwanae kuchukua bwana wa mtu tena ni uzinifu na bado anakupigia na simu, hawana lolote wasanii tu hao hebu usiende tuone kama atakufa! haumwi wala nini zuga tu zakukuteka. Jali familia yako
ReplyDeleteMimi ninashindwa kukupa pole kwa sababu yaliyotokea sio yametokea kwa bahati mbaya umechukua muda mrefu kuyatekeleza hayo uliyoyafanya. Sisi Wislamu tumeamrishwa kuoa kuanzia wawili
ReplyDeletehadi wanne na hata ukifanya nini
NDOA yako imeshaingia DOA, sasa
hivi mkeo anachopanga ni kulipiza kisasi MAWAZO kibao yanamjia na IBILISI ndie kiongozi wake ukiona
ametulia ujue AMESHAGAWA TUNDA kwa
muuza nyanya gengeni au msukuma
mkokoteni.Kama ungeomba ushauri kabla haujaanza na huyo MSICHANA tungejua nini cha kukushauri,sasa umeshafika katikati ya BAHARI unataka tukufundishe jinsi ya KUOGELEA itakua vigumu.Chakufanya tenda vile AKILI yako inavyokutuma,KISHWA ya shini ikisimama KISHWA ya JUU HAFANYIKAZI.UTAJIJU>
Naomba niongeze msaada hapo..maana ninatatizo kama hilo ila mm sijaoa binti ndo hivyo anakuja speed lakini nahisi sijampenda kiasi anachonipenda yeye na ningependelea kuwa na mwingine, lakini still anakomaa nami...pls
ReplyDeleteKwanza napenda kutoa ushauri wangu wa dhati - sina ubaya wala nini, umeomba ushauriwe basi naomba fuata ushauri wa wengi. Tunakuombeani wote ili kuishie vyema. Bongo tunapoteza watu kila leo kwa sababu ya makosa - na ikiwa tutashauriana bila kukomoana basi naona tutaokoana na matatizo ya kujitakia au ya kutojitakia.
ReplyDeleteEe bwana, nakushauri uachane na nyumba ndogo. Kama umepata muda wa kusoma mtandao leo wengi tunashauri uendelee ya ndoa yako.
Wewe unaresponsibility ya kulea watoto wako - ichukulie kuwa ni responsibility muhimu. Bado unampenda mke wako endelea kumpenda, ila usishangae kuona yeye amebadilika, kwani umemuumiza yeye na watoto. Japo umesema kuwa nyumba ndogo alikuwa anakufuatilia sana wewe ungeweza kukataa kutoka kumwonyesha kuwa haupo interested. Nadhani ulikuwa interested nae... wether una kiri hivyo au laa... ujue kuwa wakati kama huo ndio ungemuhusisha mke wako ili kama nguzo akupe nguvu ya kuto kujikwaa. Nakiri kungekuwa hakukaliki lakini, ukilinganisha na jamba jamba la sasa .... matokeo yake yangekuwa bora zaidi. Kubali kwa kiasi kuwa wewe pia ulitaka uwe na huo uhusiano wa nyumbani ndogo - acha kusingizia.
Most important bwana ni hivi virusi vingine vinachukua muda kujitokeza, vingine kwa wale wagonjwa vinachificha... kwa hiyo nnenda tena kapime, kwa maana nyingine kupima kwenu haithibitishi kuwa yeye au wewe ni wazima. Mnashauriwa wote mpime kila miezi mitatu... and then stop this dangerous living.... ikiwa haujaupata shukuru Mungu!! Wewe hunanjia ya kujua kama huyu binti wa nyumba ndogo hana wengine...unaelewa lakini ?
Mungu akusaidie kwa kweli - fuata ushauri wa wengi stick to your your married familia.
Wengine tumesoma na tunakuombea, kwa sababu inaonekana kuwa kuna uwezekano wa kuokoa familia yako... na wewe usali sana!
Huu kweli ni uendawazimu,mambo unayoyafanya ni ya aibu, unadhania labda ni sifa ku post utumbo kama huu kwenye public website kama hii. Nenda mirembe kwanza ukatibiwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteAchana na huyo dada wewe!Kwani kabla hajakufahamu alikuwa anaishije?Achana nae,akifa ujue siku zake ndo zimefika.Make up with your wife na jenga familia yako.Kumbuka ulikotoka na mkeo.Muache huyo dada.Atapona na Mungu atampa wa kwake.
ReplyDeleteAina ya shenzi (shenzi type) wewe, usitafute umaarufu kwa story ya Tiger Woods. Yaani hapo lipi gumu, inaonyesha ulioa bila kujua umeingia mkataba gani. Kutaja nyumba ndogo/ kimada,ooh ananipenda mpaka amelazwa si sifa ila inaonyesha huijui ndoa na nakwambia omba Mungu akuepushe kwani huyo mkeo nae akipitiwa na shetani ndo utajua farasi yupi alikufaa (rejea anony mmoja hapo juu). Umekwisha vunjika mguu wewe rudi zizini kwa bidii na muagize mkeo akununulie line nyingine. Ooh, tulipima kwenda zako huko wanaopima na kuzijali afya zao wanabaki na wake zao siyo wewe. Period
ReplyDeleteKwanza kabisa,nadhani unajidanganya kumwomba msamaha mke wako wakati unakiri kuwa huyo nyumba ndogo ni mzuri,n.k!It is very strange kuwa unatafuta suluhisho wakati utamuumiza tena mkeo(remember umemwomba huyo nyumba ndogo mwezi mmoja urekebishe mambo nyumbani-kwa faida ya nani??)Kumbuka kuwa mshika mawili moja humponyoka au yote kabisa.You are going to lose all,my friend!Mimi nadhani wote sisi tunavuna kile tulichopanda.Wewe umepanda haya na sasa ndio wakati wa mavuno.
ReplyDeleteKumbuka vile vile uzuri wa mwanamke sio umbo.Mkeo kwa sasa amejawa na roho ya mauti na usipoangalia ndugu yangu,atakutia kisu wakose wote.Na akijua zaidi unamwomba msamaha na wakati bado una mawasiliano na huyo wa nyumba ndogo,the game is all over!I would suggest that ukae na mkeo na uachane na huyo nyumba ndogo.Mkeo ni mkeo tu,iweje leo utake kumuumiza kihivyo?Kwani yeye hana moyo kama wewe?Imagine ni wewe ndio unafanyiwa haya yote!Nitashangaa sana kama kuna mtu atakushauri uendelee na huyo mwanamke mwingine.Muombe Mungu sana kwa sababu,mengine yanakuja usipoangalia sasa hivi.
jibu unalo mwenyewe, je kama wewe ndo ungekuwa umefanyiwa hivyo na mkeo ungechukuwa hatua gani?! au kama ukigundua mkeo anatoka nje ya ndoa ungefanyaje?? mbona kabla hujafanya huo upuuzi ukuomba ushauri? si uliona unayaweza? sasa unataka tukushari nini tukuambie umwache mkeo kisa hawara yako anaumwa sana!!!! wewe huna msimamo katika maisha ndo maana unashindwa kujua nani ni nani. acha kutupotezea muda kwa mambo ya kipuuzi
ReplyDeletewhat goes around,camez around so get prepared!!!!!!
ReplyDeletemuulize mkeo akuambie uchukue hatua gani sababu yeye ndo anajua umemuumiza kiasi gani na nivipi atapenda u make over!!!!!!!!!!
ReplyDeletegudluck!!!!!!!!!!!
Annon wa Fri Dec 25, 02:53:00 PM, umenifurahisha sana meku wangu...ila sidhani kama tiger ni mnyama muharibifu!! huyu Daminani anajifanya CHEATER WOOD!!!
ReplyDeleteDani kama utasoma hizi comments zote, ninaamini ukiisoma hii utakuwa umepata suluhisho la kweli, kama kweli una nia ya kutafuta ushauri.
Kaka Dani, ni nini unakosa kwa mkeo ambacho huyo changudoa anacho? inaonekana dhahiri humpendi mkeo!! na unachohitaji kiushauri katika mawazo yako unataka mawazo ya kukusaidia ili uendelee na wote wawili..POLE SANA..ingawa wengi wamekupa ushauri (mzuri kwa mbaya) kama kweli unampenda mkeo kwa dhati, haihitaji uwe na degree kuamua, rudi kwa mkeo muite kaa naye, tena ikiwezekana waite na washenga wenu uwaeleze kwa uwazi ulichokuwa unafanya na umuombe msamaha mkeo mbele yao na pia kuonehsa kuwa umejirudi mpigie huyo kimada wako mbele yao (na uweke loud speaker) umweleze kuwa kuanzia siku hiyo uhusiano na yeye basi...na kama ikiwezekana badili namba ya simu..ili uendelee kuishi kwa amani, furaha na upendo na mkeo na watoto wenu, lasivyo.. unajichimbia kaburi ndugu yangu. Unawapa picha gani watoto wako..kuwa wewe ni kiwembe ama CHEATER?? na wao wakija kufanya hivyo utakuwa wa kwanza kusema watoto wamekuwa wahuni na wamekosa adabu...YOU ARE STUPID (hili sio tusi kwa maana mjinga anaweza kujirudi)..nani alikufundisha kuwa ukimwi unapimwa kwa interval ya wiki mbili?? au kwakuwa ulikuwa na hamu ya kuonya kifaa kipya ukaamua kupunga siku. Again YOU ARE STUPID DAMIAN.
Tafakari,
DJ
ha ha ha ha, MBWA KALA MBWA. Hizi ni kazi za watu, pambaf.
ReplyDeleteWenzio tunafanya haya kabla hatujaoa, anyway ujue na wewe mkeo sasa wenzio watamtafuna.
Ngoma droo, usije rusha ngumi tu atakapoanza kuwaonyeshe wanaume wengine kalufundi kake.
Pambaf!! Tutawazika sasa hivi
Huyu bwana anahitaji maombi ili kumtoa pepo alilonalo kwanza nafikiri amezoea kuombwa pesa na mkewe sasa alipopata mwanamke asiyemwomba hela akaona kafika paradiso kaka yangu mkeo wa miaka kumi na tano umwache kwa ajili ya mpita njia nyoooooo umepotea imagine kama wewe ndo ungekuwa wa kwanza kukutana na msg za mkeo anacheat ungejisikiaje jiweke kwenye nafasi yake inauma jaribu kufikiri kama binadamu mwenye moyo mkeo anadeserve better than this imposter .ukitaka kujua umepotea fikiri kuna mzazi gani anaekubali na kufurahia mwanae kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzie kama sio wazimu na ni mwanamke gani anaefurahia kuona ndoa ya mwanamke mwingine inayumbayumba kwa ajili yake wote hawa ni wauwaji!kaka hapa umepatikana mama na mwana wote ni type ile ile huyo binti anaejidai kuumwa ni kuzuga tuu ni ugonjwa gani huo anapona ghafla akikuona wewe kwani wewe metakelfini chukua tahadhari huyo ni ibilisi keshaingia kwako kama hutasafisha nyumba yako kwa maombi ni hakika ibilisi keshahamia mwache nyumba ndogo mungu ndie mponyaji hata akiumwa mungu atamuangalia umemkuta akiwa ameshakuwa mtu mzima na kazi yake mwache usijipe nafasi ya mungu mungu atamlinda pale anapoona anahitaji ulinzi wake.
ReplyDeletemrudie mkeo na uombe msamaha ukiwa na maana yakuacha ufirauni wako na sio kuomba likizo maana usipoacha machozi ya mwanadamu hayaendi bure iko siku utalipwa hapa hapa
Mama mpenda amani
wewe babu unachotakiwa kufanya ni ...uchukue wanao kama unao halafu anza..huyo mke atakuua tu siku moja umelala...huyo mpenzi achana nae badilisha simu anza maisha mapya..maana mkeo hatakuja kurudi katika mudi unayotaka...so it ova bwoy!!
ReplyDeleteAnony wa kwanza kabisa umenikuna kwa salamu zako, na ingawa si kawaida yangu kuja huku uwanjani kwa wadau naona heri nikufahamishe kwamba hii ni Globu ya Jamii haijalishi napenda ama sipendi vitu au mada. Chochote kile mradi hakichafui hali ya hewa na kinagusa jamii mie hukitumia bila matatizo. Pia kumbuka Tarishi hauwawi....
ReplyDeleteasante kwa matusi yako
Unaleta story za KUTUNGA hapa,ebu acha uongo huo wa kwenye Filamu za Bongo..X-mass yote hii na Yanga imechinja mnyama...daaa Yanga Oyeeeeeeee
ReplyDeleteHivi nikuulize huyo nyumba ndogo mulipotakana hukumueleza kuwa wewe una mke?/na kama alijua kuwa wewe una mke mbona hakufikiria kuwa kama yeye akiingilia mapenzi yenu atakuwa amemuumiza mkeo,unamind nini kumkataa achana nae kama yeye alivokuwa hakumfikiria mkeo,upo tayari kumkosa mkeo wa miaka 15 na furaha ya nyumba yenu ambao ni watoto wenu unataka nini mwenzetu?Mimi nna watoto watatu kama wewe na nnaona raha kuwaona wakipita wakifukazana wala sihitaji nyumba ndogo mke wangu na watoto wangu ni kila kitu changu na wala sitaki masihara na familia yangu,ushauri wangu kwako muommbe radhi mkeo kwa uliyomtendea maana mkeo na watoto wako hawa deserve unayowafanyia na muda ambao uliokuwa unaupoteza huko nyumba ndogo uutumie kwa ku spend na mkeo na watoto wako maana ndoa kama hiyo sio healthy ya kuendeana kinyume,haki ya Mungu unasikitisha unajitafutia matatizo ya kujitakia wakati unajua jinsi ya kuyatatua,achana na nyumba ndogo hio for the sake of your children,grow up.
ReplyDeleteWatoto wa zinaa hawatakwisha mitaani mpaka wakwale kama nyie mtulie
ReplyDeletehebu tuondolee upuuzi wako wewe acha kutunga hadithi ambazo huwezi
ReplyDeleteKazi ndogo hiyo, badili dini halalisha kwisha. ya nini taabu?
ReplyDeletemi naona uufuate moyo wako, lakini kabla ya hilo kitu gani unachopata huko mke wako hana kama ni manjonjo ya mapenzi ni swala la kuongea na mke wako kumwambia kuwa mi nataka vitu fulani kwenye mapenzi ,na hilo ndo tatizo la wanaume wengi hamuongei na wake zenu kuhusiana na swala zima la mapenzi. then unatakiwa uwe mwangalifu sana kwenye maamuzi yako inaweza kuwa uyo kimada wako anataka tu kukuaribia tu familia yako, kwani si anajua kama ulikuwa na mke so kwanini now ajifanye ndo anastrong feelings tuseme yeye hana mwanaume mwingine nje, au unafikili uko peke yako kwako, be smart
ReplyDeleteSisi waislamu unaoa wote wawili unapojiona unaweza kuingia katika uhusiano usio halali-kila mmoja ana win.
ReplyDeleteThe 2 ladies wote wanakuwa na mume.
Kiislamu tatizo lina jibu.
Kikristo hamuruhusiwi kuoa zaidi ya mmoja kwa hiyo chagua moja na mwanamke mmoja awe loser.
Mshamba wa mapenzi huyo ndugu yetu. Inasikitisha maana sote tuna wake na vimada na hatuchanganyi mada hata dakika moja.
ReplyDeleteKimada kipo pale unapohitaji shughuli ambayo mke wako wakutosholezi. Lakini si wakumpenda mpaka ukajisahau kiasi hicho. Kama tatizo simu haifuti msg unayo andika si ungenunua simu bora ili siku ka hii isngetokea??. Mimi na kuona BWEGE TU wala huitaji ushauri. Mdudu kasoro mkia.
DAMIAN NIMEKUWEKEA TOPIC YAKO KWENYE BLOG YA HARUSI YANGU, TAFADHALI TEMBELEA HUKO, HUKO NDIO KWENYE MAJIBU YOTE,NENDA HARUSI YANGU UONE WALIVYOCHANGIA, WAMAMA KULE HAWATAKI MCHEZO.
ReplyDeleteHabari Damiani,
ReplyDeleteaisee pole muzee kwa hiyo drama ilokukuta, ni kawaida sana kwa wanaume kukutwa na mikasa kama hiyo..so from now on you are player you love the game, u have to follow the rules, let me tell you brother...u r not alone in this game..so many men out there are playing also..there are so many rules one of them is to try to be fare on the home grounds and put first priority..in that way u will blind them and..she wont see what u r doing out there...also try to make sure u give enough love to the chicky as she might not be satisfied and have some substitutes also..then BE WARNED; ...womens are not the kind u can trust easly..they are great liars, great pretenders, and they are born professionally with this..they are many rules bro..find out.....
Inawezekana kaka Damian kuna kitu umeonjeshwa kwenye nyumba ndogo ambacho labda hukipati nyumba kubwa, hivyo umepagawa lakini kumbuka penzi huchuja, kumbuka siku za mwanzo ulipokutana na mkeo utapata jibu!
ReplyDelete"WHEN BITCH GOT HORNY,NIGGA DIE" KWA HIYO WE SUBIRI MKEO AKUCHINJE AU VIDUDU VIKUNYEVUE
ReplyDeleteWEWE UNALETA STORY ZA KWENYE RADIO...UMEDATA NINI MSHIKAJI
ReplyDeleteMIE SINA MENGI ILA USHAURI KWAKO WEWE KAKA NA WENGINEO WENYE TABIA KAMA HIYO NI HUU
ReplyDelete"UTAMALIZA MABUCHA, LAKINI NYAMA NI ILE ILE"
Kama hii drama siyo ya kutunga, Damian wanaume wengi wana tabia kama yako ila zote hizo ni tabia mbaya kwa wake zenu, haipendezi hata kidogo. Kuhusu uzuri wanawake wazuri walianza kuwepo tangu zamani na kila siku wanazaliwa na wana vitu kama hivyo unavyovipata ila brother ukishaoa na hukuwahi kuvipata na mkeo hana, basi ndugu mchezo umeshaisha lea ndoa kaa na mkeo achana kabisa na nyumba ndogo. Matokeo yake one day utajuta na itakuwa imeshatoka. Najua ni kaprocess mpaka mkeo akuelewe sababu ni doa hilo but i believe kama utajirekebisha ataona tu mme wangu amechenji. Kiri kosa kwa kumaanisha na ikiwezekana umpigie huyo kimada umpe live mbele yake kwamba its over.
ReplyDeleteMtu mzima ovyooooo!
ReplyDeleteDamian,wewe unajiona shujaa lakini wewe ndie bwege...utapoteza ndoa yako nzuri kwa kitu cha kijinga!achana na huyo msichana angalia familia yako..!hiyo ni muhimu kuliko huyo anyejipa stress zisizo na msingi.Ulishamwambia umeoa..sasa hilo penzi linalomsumbua kwako linatoka wapi..?
ReplyDeletepole sana ndugu mheshimiwa ushauri wangu naomba uuzingatie,kama unaweza badili dini ikiwa wewe ni mkristu pia wabadilishe dini wote huyo mkeo na hawara yako wawe waislamu pia halafu mnitafute niwafungishe ndoa ya kheri iliyojaa shari ndogo ndogo pia muishi nyumba moja ili usisumbuke nauli kwani nafikiri huna gari.
ReplyDeleteikiwa hutaki kubadili dini basi muowe kikabila huyo hawara uhuru huo unao kwani mila zetu zipo la muhimu ni kuwaweka pamoja ili wasaidiane kazi.jitahidi usitafute watatu kwani mambo haya hayaonjwi.kama huna dini basi njoo ofosi zetu za chama tukufungishe ndo kikatiba kwani matatizo kama yako tunayo karibu kila siku katika CCM.
AHSANTE.
MUNGU yupo mzima kabisa..... ulifikiriaje wewe... kenge bluu kabisa
ReplyDeleteSIMU GANI HIYO? MSHINDI? NUNUA SIMU YA KISASA, KAMA UNAWEZA NGONO UNASHINDWAJE SIMU YENYE AKILI, WEWE DUME BWANA, KUFUMANIWA NDO UANAUME HUO, SI UOE TU WATU BE, INARYHUSIWA HIYO. KULA KAM KAWA, KWA MBELE USIANGALIE MAKUNYANZI. NKOME NYANI GILEDI, NI PARE KWA MBELE.
ReplyDeleteBest Pole sana najaribu kuvaa viatu vyako najua unavoumia,mapenzi kitu kigumu sana lakini kaza mwendo.Uzungu mwingi unatuponza kwakuwa umemweleza ukweli kuwa una mtu mwingine tulia kwanza na chukua hatua asije akakuua baadaye atatulia.Vuta subira lazima ataumia ila elewa mke mmoja siyo utamaduni wetu waafrika,cha msingi jali familia watoto wale waende shule mambo yatatulia usizae kwanza na mke huyo mpya its too early.
ReplyDeleteWEWE DAMIAN MIMI SIKUJA HAPA KUKUTUKANA ILA NITAKUPAKA TU KWANZA UNATAKA JINA AMA VIPI? UNAONEKANA WEWE UMECHANGANYIKIWA KIUKWELIKWELI SIYO KWA MAPENZI LAKINI HAKIRI YAKO NI KAMA YA WATOTO AMA IQ YAKO NI NDOGO KAMA YA KUKU. HUU UCHAFU UNATAKA NANI AKUSHAURI? NENDA KAMUULIZE TIGER WOODS LABUDA ATAKUWA NA JAMBO LA KUKUAMBIYA. HUYO MAMA UNAYEMUPA URODA ANGEKUCHOMA HICHO KISU KIUKWELIKWELI NA KUONDOKA NA HIZO SEHEMU ZA SIRI ILI HUSIJE KUONGEZA MAGONJWA KWA WATOTO WETU WA TAIFA LA KESHO ASUBUHI, HUNA HATA HAIBU KUTOA MAUCHAFU YAKO KWENYE PUBLIC? UNATAFUTA USHAURI GANI HUMU NDANI? HAYA NGOJA NIKUPE HUSHAURI MUNONO KUNA MIARABU INAPENDA SANA VIJANA WADOGOWADOGO KAMA WEWE TENA MAPETITI VIPI NIKUPE NUMBER ZA SIMU ZAO? MIDA YOTE HAO WAALABU HUVAA KANZU TU PILA CHINI (UNDER)WEAR WANASHAURI SANA WATU KAMA WEWE UWAWONE ILI WAKUPE DOZE. MICHUZI POLE KWA KUPEWA MITUSI KWENYE BULOG LAKINI HIYU DAMIAN NAONA ANA AKILI KAMA YA MUTOTO MWENYE KUTAMBAA, UTAWEZAJE KUMUANIKA MUKE WAKO HUMU NDANI YA BULOG BILA HAIBU WALA FEZEHA? ANGALIYA MUTOTO DAMIANI BE CAREFULLY HUSIJE KUPATA MUTUNGO WA BURE CHUNGA TABIYA YAKO KABISA. HACHA KUUMIZA WAREMBO WA KESHO.
ReplyDeleteAnon wa 26/12/200 saa 08:04:00 tabia yako inaonyesha haina tofauti kabisa na anaetafuta ushauri humu. Yaani bila aibu unasema kufumaniwa ndo uanaume. mpuuzi sana wewe na ukome kushauri ujinga. by the way wewe bwana rudi kwa mkeo acha ngono zembe. umri wa ndoa yako hauhitaji kutafuta ushauri kwa misupu. cha msingi achana na huyo nungayembe na endesha familia yako. Jina lako ka ni la kikwelii unaonyesha ni mkristo so huna haja ya kuongeza mke kutokana na maadili ya dini ya wakristo.
ReplyDeleteInaonyesha hukuwahi kufanya haya mambo ujanani mwako halafu ni kama vile mke uliye nae ulichaguliwa na wazazi wako. Kwa kutojihusisha kikamilifu na haya mambo ujanani mwako pengine kwa sababu ya shule kumepelekea wewe kukosa technic na kudeal na haya mambo kama ulivyokiri mwenyewe kwamba huyo hawara yako ni yeye aliyekutongoza na ndio maana unafikia hatua ya kumsifu kwamba hajakuomba chochote (fedha)wakati mwenzio anakutega kama ungekuwa mzoefu ungelielewa hilo kwa sababu hakuna mwanamke anaweza kumpenda mwanaume tena aliye oa hivi hivi tu. Kwa kutokushiriki kwako kwenye haya mambo kwenye umri muafaka kumepelekea vile vile kutijua mbinu za kina dada wanapotaka kukuingiza mkenge ikiwemo kupewa nyama ya bata ambayo si rahisi kuipata nyumbani na vikorombwezo vingine, yote kwa yote hii nadhani inachangiwa na kukuosa elimu ya JANDO.
ReplyDeleteUHAURI:
1.Achana na nyumba ndogo hana lolote ana mpango wa kukumaliza tu, kama unaona ndo umefika kigoma basi
2.Sheria ya nchi ya ndoa inaruhusu kuoa hata wake sita,changamkia
Bwana Damiani eee,utamu wa bigijii umeshaisha baada ya miaka 15 na taya linaanza kuleta matatizo. hapo ni kumshitaki mkeo kwa attempted murder yako kwani alipremeditate mpaka akakutisha usingizini.mdondoshe,alafu anza na bigijii mpya kwa miaka kadhaa tena.watoto,nyumba na mali zote utakeep alafu mkeo atarudi kwa wazazi wake na kupata mwengine.ndio maisha hayo kijana.move on otherwise mkeo atakudondosha.si ulitaka ushauri haya huo hapo very radical hahaaaa
ReplyDeletemdau uk
hivi Damiani una akili kweli unatuletea huu utumbo wako kwenye blog hii ya jamii huna aibu huu ni utahaira kabisa eti unasema unawapenda wote uongo mtupu halafu huo ni ushamba inaelekea una matatizo,kwanza inaelekea umeshamchoka mkeo huna lolote achana na huyo malaya kaa na mkeo mtunze watoto , hicho kimalaya kinajifanya kinaumwa uongo mtupu mwache afe.
ReplyDeleteKaka Damian pole sana kwa masahibu uliyonayo.
ReplyDeleteUmefanya vizuri kuweka wazi tatizo lako lakini kusema ule ukweli hiyo ndiyo dilemma ya wanaume wengi sana siku hizi.
Usione kwamba wengi nao wanajaribu kukupotezea lakini kimoyo moyo umewagusa kweli kweli kwenye maeneo yao sumbufu.
Yaonekana kwamba mamaa hayuko tayari kukuacha vinginevyo angekuwa ameondoka. Fanya maombi kaka yangu Mungu atakusaidia.
msijifanye kumrushia mwenzenu mawe humu ndani na hakika asilimia 99.99 wote wenye ndoa na msokuwa nazo mnacheat kwa kwenda mbele hapa mnajidai wakali kama mmekunywa maji ya betri wachangiaji wengine hata leo wamebanjua amri ya sita nje ya ndoa zao acheni hizo mpeni ushauri na sio kumnanga kama vile na nyinyi mko perfect bill clinton denzil washington lionel richie rambo swaziniga tiger woo jlo jay z brad pitt van dame wote hawa ni masupa staa lakini wameshabanjuka nje ya mahusiano yao hivyo ni poa tu mtu afanye kwa siri hakuna mbaya ila ukibambwa tu ndo inakula kwako wanabanjuka masista mapadre wachungaji ndo itakuwa huyu??? hiyo kitu ina raha yake jamani otherwise watu wangetulia na ndoa zao takatifu kuna burdani flani tuu huko nje ni full kujiachia! huko nje unaitwa baby honey full masaji hm mambo kimgambomgambo he he heee acheni tuu. sasa we anko siri ishafichuka achana tu na huyo demu mchukue mamaa nenda naye vekesheni huko sychell ukampoze iwe kama honeymoon flani muanze upya mkirudi shwariiii
ReplyDeletehizi comments siyo reflection ya moral values za majority ya tanzanians kizazi cha sasa.
ReplyDeletekama ni comments za ushauri fine, lakini kama comments kulingana na maisha yetyu, hapa tunadanganyana.
katika ndoa 100, zisizokuwa na aina hii ya madudu nadhan ni 10. most of these comments ni unafiki, sina maana mdau aendelee, lakini tujikague wenyewe kwanza.
kama siyo kuandikwa na press, leo ningewambia tiger woods ana vimada wote mngepinga. mambo magumu haya ya kuvuana nguo.
Damian, i will give the most honesty and practical advice, not like all these people who have just been pretending as good guys so they try to give an advice that make them look so...Ni hivi ndugu yangu, wewe unampenda nyumba ndogo kuliko unavompenda mkeo, ..nna uhakika hata ukireconcile na mkeo lakini hautaacha kutoka na hiyo nyumba ndogo hapo baadae, kitu ambacho kikigundulika matatizo yake yatakuwa makubwa kuliko haya ya sasa. Huyo mwanamke wa nje na mkeo wana tabia tofauti kabisa, ndo mana unachanganyikiwa,lakini wote wanakupenda. sasa either way utakavoamua utaenda kumuumiza mmojawapo, so ushauri wangu ni kwamba fuata moyo wako ulipo,,ambayo katika hii case naona wewe moyo wako upo kwa nyumba ndogo, mpe talaka mkeo kwa amani na uendelee na nyumba ndogo yako, muoane muendelee na mapenzi yenu
ReplyDeletethis is stupid.
ReplyDeletejust imagine mkeo ndo kafanya hivyo.anyway yu men we can say your selfish.mwanamke akicheat its so hard kwenu to forgive bt nyie mnaespect msamehewe.
All decision will be up to u.hamna kitu mtu akikwambia yu will hear o listen so choose,wat do yu want?
nimekasirika natamani nikutukana bt c vyema.
Mtukane msitukane-Kosa lilishafanyika haya zoeni hayo maji mtumie, au rudisha hiyo nyama iwe ng'ombe tuone kweli mmekasirika. Iwe hadhi yakutunga au yakweli yafaa kwa mafundisho kuwaonya watu na kuwasaidia.Sasa kaka sikiza ndugu yangu mimi nakushauri kaa chini ufikiri nini unataka ...
ReplyDeleteOne of the principle to success I like the most is DECIDE WHAT YOU WANT.
Ukisha amua unalo taka ndipo uchukue hatua za kijasiri kutekeleza utakalo...
Hajalishi ni baya kwa watu wengine au jema kama moyo wako, akili na roho yako vimeamua...You will make it in happiness...Watu tunatafuta kwajuhudi zetu zote happiness..
Usione mtu anitwa fisadi lengo ni kuwa happy..
Usikubali watu wakachezea happiness yako acha uwe mshamba lakini tii kile kinachokupa furaha do not loose your happiness no mata wat..
Kuchonga kawaida yetu..
Uiogope kisu kama umepangiwa kufa kwa kisu utakufa kama si hivyo haitakuwa .
Sisemi umuache mkeo au ummuumize lakini nakushauri tafuta na fanyamaamuzi yatakayo kupa furaha yako...
Natamani kuandika makala bt naomba nishie hapo kakangu..
Hope itafaa.
Pole take simple though, simple is not always easy...
Byeeeeeeeeeeeeeeee!
Baki na ujinga wako peke yako. Sasa unatundika upuuzi huu kwenye net ili iweje!? Tukuonee huruma au!? Mpuuzi kabisa wewe! Mwanaume wa kweli huheshimu ndoa yake kwa nguvu zote. Inaelekea ulioa kama fasion wewe!
ReplyDeletenahisi hii ni story tu haina ukweli wowote ila pia sikatai kuna matukio kama haya mengi tu..sasa namshauri yeyote aliyekumbwa na mashauri kama haya basi aelewe kuwa ukiamua kuwa mvuvi basi elewa kuwa kuna kuliwa na samaki wakali na kufa maji,na ukiwa dereva wa mbio za magari basi uwe tayari kufa kwa ajari ama gari kukuharibikia porini sasa kwa kuwa wewe umeamua kuwa player basi kubaliana na concequences zake,kuvunjika kwa ndoa yako ama kufa kwa ukimwi
ReplyDeleteMIMI NIMEKWISHA SEMA KAMA WEWE DAMIAN HUTAFUTI JINA BASI UNATAFUTA KUKANDAMIZWA NA MIARABU YA PEMBA/ZANZIBAR. MUTU MWENYE IQ YA KUKU AMA BATA NDIYO PEKEE ANAWEZA KUONDOA HII TABIA YAKO YA UCHAFU. NENDA KATAWAZE ILI UKAAE NA WATOTO WENZAKO, MARIA, NA SASHA OBAMA.KAMA HAO WANAWAKE WAPO BASI WATAKUWA WABOVU SANA, WEWE JIPE MOYO TU ETI UMEPIMA VIRUSI, SIKU ZINAYOYOMA UNATIA HURUMA NA KICHEFUCHEFU KWA KWELI UNAHITAJI KUKANDAMIZWA TENA SANA TU NA MIARABU ILI USIKIYE UTAMU WAKE....!
ReplyDeletemimi nadhani huyo damian na huyo binti walikuwa na mahusiano before ya watoto kuzaliwa labda huyo dada alimzingua mwenzake ndio maana damian aliamua kuoa mwanamke mwingine , sasa inaonekana huyo dada kaachwa na jamaa yake ndio maana alimtongoza damianai, hapo kosa linaonekana ni la huyo msichana kwa kuwa mpofu wa kuona mbali kitu ambachao kitamsumbua sana katika maisha yake!!!
ReplyDeleteMdau nawakilisha!!
Mdau wa Jumapili tarehe 27 December 06:44 pm, Hueleweki. Tumia alama za michoro, ikibidi hata ya barabarani kufafanua.
ReplyDeleteKenge Bluu wewe.
soma hapa 8020 rule
ReplyDelete"Interesting quote from the movie 'Why did I get married?'
In most cases, especially in relationships, you will only get 80% of what you NEED and you will hardly get the other 20% that you WANT in your relationship. There is always another person (man or women) that you will meet and that will offer you the other 20% which is lacking in your relationship that you WANT And believe me, 20% looks really good when you are not getting it at all in your current relationship.
But the problem is that you will always be tempted to leave that good 80% that you know you have, thinking that you will get something better with the other 20% that you WANT
But as reality has proven, in most cases, you will always end up with having the 20% that you WANT and loosing the 80% that you really NEED and that you already had.
Be careful in deciding between what you WANT and NEED in your life.
Adultery happens when you start looking for what you don't have. 'Wow, this girl in my office is a real looker. But it's not her Wynona Rider features that got me. I'm crazy about her because she's also understanding, intelligent, tender - so many things that my spouse is not'
Somewhere along the way, you'll find a woman or a man who will be more charming or sensitive. More alluring. More thoughtful. Richer. Have greater appeal. And you will find a woman or man who will need you and pursue you and go loco over you more than your spouse ever did.
Because no wife or husband is perfect. Because a spouse will only have 80% of what you're looking for. So adultery takes place when a husband or wife looks for the missing 20%. Let's say your wife is melancholic by nature.
You may find yourself drawn to the pretty clerk who has a cherry laugh no matter what she says: 'I broke my arm yesterday, Hahahaha . . ..'
Or because your wife is a homebody in slippers and pajamas, smelling of garlic and fish oil, you may fall for a fresh-smelling young sales representative that visits your office in a sharp black blazer, high heels, and a red pencil-cut skirt Or because your husband is the quiet
type, your heart may skip a beat when you meet an old college flame who has the makings of a talk show host.
But wait! That's only 20% of what you don't have.
Don't throw away the 80% that you already have! "
Reginald (Morogoro)
yaani mimi nashangaa, wewe damian!!! fanya kitu roho yako inapenda sio kuwauliza watu wakufanyie uhamuzi, mimi ningekushauri uhamue kuwa na huyo kimada lakini sasa umesema unampenda na mkeo!! hapo tu ndio umeniacha njia panda na mimi, ungesema imetokea umempenda huyo dada wa nje kuliko mkeo ningesema basi fanya maamuzi maana roho yako inampenda huyo dada na si mkeo, kama ungesema mkeo humpendi unampenda huyo dada, basi ningekwambia hachana na mkeo na umpende huyo dada, sasa ndio umenichanganya kuwa wote unawapenda, sasa kaka hiyo ni tamaa maana huwezi kuwapenda wote wawili, mapenzi ni kumpenda mtu mmoja tu na si wawili, basi mimi nakushauri endelea kumpenda tu mkeo na jitahidi umusahau huyo dada wa nje, acha mawasiliano nae na utaona unamsahau tu taratibu ingawa inauma kwa mtu ukishampenda kumsahau sio kirahisi, ila itabidi ufanye hivyo tu umusahau.
ReplyDeleteHuyo nyumba ndogo akisikia Damian yupo na mwanamke mwingine tena na yeye atakisikiaje?? Aache umalaya mbona wanaume single wapo wengi???
ReplyDeleteDamian ww unaonekana unawangonoa sana wanawake haiwezekani nyumba ndogo ipagawe na penzi la mume wa mtu namna hiyo watu tumezoe mume wa mtu ndo anayepagawa anapeleka matumuzi yote ya nyumbani kwa nyumba ndogo ila wewe mh! tofauti, halafu bi mkubwa naye asikie uchungu wa kutaka kuamua tukose wote mh!, ila ninacho kwambia hao wanawake watakuua achana na umalaya rudi kwa mkeo na ninaamini siyo huyo tu peke una wanawake wengine wengi wa nje acha hiyo tabia hiyo angalia maendeleo ya familia yako.tena usiombe ushauri kama huu tena! kwa sababu inaonekana huna huruma hata na familia yako, watoto wako bado wadogo we ulishaanza kurukakuruka vipi eenh!!!huu muda na gharama unaohangaika kutafuta vimada ungeutumia kufanya jambo la maendeleo ridhika na mkeo wazuri hawaishi wanazidi kuzaliwa kila siku utazini na wangapi!?.Unajua siku zote chura huona umuhimu wa maji yakishaanza kukauka sasa ww utamuona mkeo muhimu pale utakapoukwaa na kimada wako ukimbie huna mtu wa kukusaidia kwahiyo mpe thamani yake.Badilika!!!!Huyo mwanamke mwambe atafute wanaume single wapo wengi, yeye anajua kabisaa huwezi kumuoa anang'ang'ania nn!?huko kujitia gundu
ReplyDeleteYanishangaza mtu mzima mwenye mvii zake anawezaje kupigana na watu aliyo wapita umri kwa kiasi kikubwa sana kisa mwanamke.Mwanamke aliye ni mdogo sana kwake anayeweza kuwa ni mtoto wake tena wa mwisho.Hata hao vijana waweza kuwa wadogo zake au hata wanae.
ReplyDeleteUkiachilia mbali mwanamke huyo ana mpenzi na inajulikana na mzee mzima ni mume mwenye familia ya kutunza nyumbani...
Heshima imepotelea wapi na unidhamu je? Mtu mzima washikana mashati wanaoweza kukupiga na kukuvunja viungo kisa tamaa...Heshima ya ndoa na mwanamke imepotelea wapi? Maana hapa amedhalilishwa yule mke aliyoko nyumbani, yule mke aliyemzaliya watoto, yule mke anayempikia na kumjali.
Na je huyo mwanamke aliyepiganiwa?Heshima yake iko wapi?Imepotea. Hiyo aibu aliyoachiwa, sura yake aipitishe wapi. Jina limeshachafuliwa.
Kweli mtu mzima na elimu yake, heshima zake anaweza kufanya vituko kama mtoto aliyebalehe juzi kisa tamaa ya mwanamke?
Ni kwanini baba zetu hawaheshimu ndoa zao, mama zetu na dada zetu?Unidhamu uko wapi? Maadili yako wapi?