Mwandaaji wa ZABURI GOSPEL SEARCH Flora Lauwo

Kampuni ya Flora Promotions ya jijini Mwanza imeaandaa shindano la kutafuta, kukuza na kuwezesha vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili liitwalo ZABURI GOSPEL SEARCH 2009, ili kueneza neno la mungu kupitia nyimbo.

Akizungumza mapema leo asubuhi na vyombo vya habari jijini Mwanza ndani ya ukumbi wa Nyumbani Hotel,Bi Flora Lauwo amesema kuwa kipindi hicho amekibuni yeye mwenyewe na amefuata taratibu zote za uendeshaji wa shindano hilo kupitia taasisi za sanaa hapa nchini.

“ Suala la zawadi liko wazi kabisa, ni kwamba mshindi wa kwanza atajinyakulia gari aina ya Vistar yenye thamani ya milioni nane,mshindi wa pili ataibuka na seti ya vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Samila Mobile Sound,mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi laki moja,lakini pia mshindi wa kwanza mpaka tano watarekodiwa albamu moja moja na studio za Habari Maalum” alisema Flora.

Flora ambaye ndiye mkurugenzi wa kampuni ya Frola Promotions amesema kuwa,kwa mara ya kwanza mwaka 2009, kipindi cha ZABURI GOSPEL SEARCH kitaanzia kanda ya Ziwa kwa kutafuta washiriki kila mkoa na kuchukua waimbaji watano ambapo jumla watakuwa 20, “ washiriki hawa wataingia kambini kwanza,ili kuanza michuano itakayo rushwa kupitia tv na wananchi kuwapigia kura wakisaidiana na majaji kutafuta mwimbaji bora.”alisema Flora.

“ ZABURI GOSPEL SEARCH 2009 itakuwa na matamasha makubwa matatu moja litakuwa ni robo fainal litakalofanyika mkoani Shinyanga tar,25/12/2009 na nusu fainali itakuwa Musoma mkoani Mara tar,27.12.2009, na fainali yenyewe itafanyikia jijini Mwanza Januari 1 2010, siku ya mwaka mpya”alieleza Bi Flora..

Bi Flora alimaliza kwa kusema kuwa lengo lao ni kukuza na kuwezesha waimbaji wa muziki wa injili na kuwatangaza Kitaifa na Kimataifa, ili waweze kijipatia kipato na kufaidika kwa namna moja ama nyingine kama wasanii wengingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. mbona huyu mdada anaonekana mtemi sana?

    ReplyDelete
  2. ni full mtemi

    ReplyDelete
  3. Kwanza kwa nini anatuwekea picha kama anahisi KICHEFUCHEFU?

    ReplyDelete
  4. Ina maana hana picha nyingine nzuri??

    Alafu anapenda sifa sana, sio wote wanaodhamini wako kama yeye, wengi wao no wazuri wa roho. yeye anataka watu wamuone anachofanya.

    ReplyDelete
  5. Uyu biashara kwanza Mungu baadae na hapo kwanza akamate pesa ndio amjue Mungu kwanza angalia yake sio nzuri, bora angeingia kwenye bantu star search

    ReplyDelete
  6. Mtoto wa CoastDecember 02, 2009

    Wazo zuri na linalowezekana kufanyiwa kazi na likafanikiwa sana dada.
    Hata hivyo unapoiga au ibia basi uwe mbunufu kidogo hata kwa jina tu.

    Huu mradi wako ungeuita kitu kama MPANZI 2009 AU TARANTA INAYOZAA/INAYOONGEZEKA 2009 (rejea ya hadithi katika injili) n.k.

    Zaburi(kiswahili) na Gospel Search(kiingereza) ni mkorogo na kuiga-ruduvisha Bongo search!

    ReplyDelete
  7. kwa muonekano pia anaonekana anazarau.Ameolewa kwel?

    ReplyDelete
  8. kwanza nakupongeza sana kwa wazo lako hilo la kuinua vipaji kwa njia ya injili lakini nina mawazo au maoni yafuatayo
    1. ninamashaka kama majaji wako wanaujua mziki kweli kwani tukiangalia mfano wa B.S.S. majaji wako kamili kuna mzee wetu Kitine pale tunamfahamu sana kuhusu mziki nakama nimfuatiliaji wa BSS utagundua kuwa madame Ritta sisana msemaji wa majaji isipokuwa anakuwepo kuongeza challange lakini kazi kubwa inafanywa nawatu wanao jua mziki si kwakusikiliza mdundo tu bali hata noti za mziki wenyewe nimejaribu kufuatilia kipindi chako sioni kama unajaji anaye elewa wewe mwenyewe ndo hivyotena tunajua shughuli zako si za mziki hivyo basi swala hili lisiwe la manufaa yako tu bali lisaidie kweli kama ulivyo panga.kwani hata maswli mnayo wauliza wanaenjili utadhani ni usahili wa maisha plus niuchokozi tu.

    ReplyDelete
  9. dada angu wewe ni mrembo na unapendeza na siku nyingine ukipiga picha hakikisha unatabasamu ..utatokea vizuri zaidi ya hap. asante

    ReplyDelete
  10. hii blog ya jamii ina mabachela kibao kina lord US blogger na wengine kibao sasa wewe kununa namna hiyo kwenye photo halafu ati unaileta huku blog ya jamii ha ha haa ni sawa na kutia kidole kwenye nyumba ya siafu ni kung'atwa tuu kwa kwenda mbele pole kwa madongo lakini ni moja ya changamoto next time unajipanga kabla hujaingia humu ndani ya blog ya jamii michu mwenye anajua humu ndani ukiingia ovyo tu unasulubiwa hadi ujiju kweli hapo kwa photo umetokea kibaunsa sana mtoto wa kike smile bwana alah!!

    ReplyDelete
  11. kumbe tuko wengi...

    u look so baunsa dada khaaa smile mweee

    ReplyDelete
  12. Flora hongera dada kwa utafutaji wa pesa, umeamua hadi kuingia kwenye INJILI!!! upromota umekushinda tena? utamuweza wapi Rita dada?? ila nakuaminia mama kwa kutafuta pesa hongera kwa hilo,, ila jaribu kutafuta majaji kama kina mzee kitime hao sio ni wazugaji tuu, mimi kwa ushauri wangu ni kwamba jaribu kutulia na biashara yako ya salon inakuingizia kipato kikubwa, unayeuliza kuwa ameolewa? au bado? huyu mdada kaolewa bwana na mume wake ni mdogo wa mwenye star TV hapa kwetu mza. picha inatisha mama japo ndivyo ulivyo lakini ungechekapo kidogo mayo wajameni. Msalimie Dave

    ReplyDelete
  13. duu ungecheka kidogo japo ndivyo ulivyoumbwa dada, kaolewa huyu jamani. ni bonge la mtafutaji mwz.

    ReplyDelete
  14. pole kwa madongo, ila kweli ungechekapo kidogo, japo ndivyo sura yako ilivyo, komaa mama kwa kutafuta pesa hujambo, wewe ni mchaga wa ukweli aminia mamake.

    ReplyDelete
  15. Waswahili bana utawajua tu, hawanaga zuri hasa kama kinachofanyika sio chao. Nyie mnaotaka huyu dada ambaye ni mke wa mtu atabasamu ili iweje? kwani anauza sura au kaawambia ni mcheza sinema au mwanamitindo? Dada yangu songesha hao wanakuponda eti umekopi kwa Ritha wasikutishe kwani hata Chadema, CUF, NCCR na wengineo wamekopi kwa CCM na wako kwenye gemu vilevile.

    ReplyDelete
  16. ana sura nzitoo lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...