Didier Drogba wa Chelsea na Ivory Coast ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika 2010. Mshambuliaji huyo amepata kura zaidi kuliko Samuel Eto'o, Michael Essien, Yaya Toure, na Tresor Mputu Mabi kushinda taji hilo.
Matokeo ya kura - zilizopigwa na mashabiki kote Afrika yalitangazwa moja kwa moja kutoka Angola kupitia kipindi cha Fast Track katika Idhaa ya Kiingereza ya BBC.
Drogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.
Baada ya kuanza mwaka vibaya, Drogba aliimarisha kiwango chake cha soka na kuwa mmoja wa washambuliaji tishio duniani.
Baada ya kuwekwa kando kucheza kikosi cha kwanza na kocha Luis Felipe Scolari kutoka Brazil, mshambuliaji huyo alifunga goli moja tu katika mechi 10 ilipofika Februari.

hizo ndio media za uingereza, hata lampard yupo ktk 1st 11 ya best players of the decade.!
ReplyDeletedidier for what 2008/2009 zaidi ya eto'o na mda mrefu alikuwa injury
kombe la mbuzi FA??
ukiwaachia tuzo ya mchezaji bora atashinda rooney akifuatiwa na lampard,owen,messi,cr7
Mithupu nawewe unapoandika uwe unarudia kusoma bwana! mala unaipa umaalufu sana hii timu ya Drogba ,,,Badae unakuja kuandika eti hii timu ya Drogba inapewa nafasi kubwa ya kushindwa????Au umeshazoea kuandika habali za timu za Tanzania,,kwasababu wao ni kupewa nafasi kubwa za kushindwa tuuu.
ReplyDeleteDu naona inatakiwa utoe W katika kipengele hiki hapa chini:
ReplyDeleteDrogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.
Naona kama wana nafasi kubwa ya kushinda.
Nimjitolea kuwa Editor na nilipata A katika kiswahili form four mwaka 1992.
Ni hayo tu, ni mimi
Editor aliyejitolea
Anonym. wa 01.06 PM kiswahili chako kinachefua, sehemu ya "R" unaweka "L". "MALA, UMAALUFU"!!!!!
ReplyDeletewewe umeedit kazi yako kweli kabla ya kuituma? Usijitie mkosoaji wakati lugha inapiga chenga. Mwone vile.