mashabiki wakimpapatikia Drogba alipokuwa Dar
Didier Drogba wa Chelsea na Ivory Coast ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika 2010. Mshambuliaji huyo amepata kura zaidi kuliko Samuel Eto'o, Michael Essien, Yaya Toure, na Tresor Mputu Mabi kushinda taji hilo.

Matokeo ya kura - zilizopigwa na mashabiki kote Afrika yalitangazwa moja kwa moja kutoka Angola kupitia kipindi cha Fast Track katika Idhaa ya Kiingereza ya BBC.

Drogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.

Baada ya kuanza mwaka vibaya, Drogba aliimarisha kiwango chake cha soka na kuwa mmoja wa washambuliaji tishio duniani.

Baada ya kuwekwa kando kucheza kikosi cha kwanza na kocha Luis Felipe Scolari kutoka Brazil, mshambuliaji huyo alifunga goli moja tu katika mechi 10 ilipofika Februari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hizo ndio media za uingereza, hata lampard yupo ktk 1st 11 ya best players of the decade.!
    didier for what 2008/2009 zaidi ya eto'o na mda mrefu alikuwa injury
    kombe la mbuzi FA??

    ukiwaachia tuzo ya mchezaji bora atashinda rooney akifuatiwa na lampard,owen,messi,cr7

    ReplyDelete
  2. Mithupu nawewe unapoandika uwe unarudia kusoma bwana! mala unaipa umaalufu sana hii timu ya Drogba ,,,Badae unakuja kuandika eti hii timu ya Drogba inapewa nafasi kubwa ya kushindwa????Au umeshazoea kuandika habali za timu za Tanzania,,kwasababu wao ni kupewa nafasi kubwa za kushindwa tuuu.

    ReplyDelete
  3. Du naona inatakiwa utoe W katika kipengele hiki hapa chini:


    Drogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.

    Naona kama wana nafasi kubwa ya kushinda.

    Nimjitolea kuwa Editor na nilipata A katika kiswahili form four mwaka 1992.

    Ni hayo tu, ni mimi
    Editor aliyejitolea

    ReplyDelete
  4. Anonym. wa 01.06 PM kiswahili chako kinachefua, sehemu ya "R" unaweka "L". "MALA, UMAALUFU"!!!!!
    wewe umeedit kazi yako kweli kabla ya kuituma? Usijitie mkosoaji wakati lugha inapiga chenga. Mwone vile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...