siku za ubabe wa kukwangua anga iliyokuwa nayo jengo la Parastatal Pensions Funf a.k.a PPF la PPF Tower jijini dar zinahesabika kwani ubavuni pake panamea kikwangua anga kingine mali ya mfuko wa pensheni kwa wafanyakazi wa watumishi wa umma - Public Service Pensions Fund a.k.a PSPF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MAENDELEO KITU CHA AJABU SANA LEO HII NCHIFULANI ILIYOENDELEA ILIJENGA HICHO KIKWANGUO MIAKA 1925SASA WANAUMIZA KICHWA WATABOMOAJE SISI NDIO TUNAANZA.

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi naomba nitolee hewani.

    Ni jambo la kushangaza sana kwa wasomi wetu wa Tanzani pale wanapopewa nafasi za kazi kubwa maofisini na kuzitumia vibaya kwa manufaa yao. Maafisa mipango miji na mainjinia wao tunashindwa kuwaelewa pale wanapo ruhusu majumba marefu, makukubwa na mazuri kuota kwenye miji yetu wakati hatusikii mipango ya kuondokana na kuzagaa kwa maji machafu mitaani. Niaibu kuwa na majengo kama hayo huku miundo mbinu ya taka ikiwa mibovu. Baada ya muda maafisa hao wanaishauri serikali kuvunja nyumba za walala hoi ili waweke miundombinu ya maji taka. Ni vigumu kuamini kuwa hivyo ndivyo walivyofundishwa wasomi hao. Kama hiyo haitoshi, watanza kuhujumu mradi walioupendekeza wao wenyewe na kuwaacha waliobomolewa nyumba zao wakihangaika na kuishia kulipwa pesa kidogo ambayo haitoshi kujenga nyumba nyingine. Kwa makusudi hupendekeza kwa serikali gharama kidogo itakayo tumika kuwalipa wananchi watakaobomolewa nyumba na wao Kuomba pesa nyingi kwa ajiiri ya mradi huo. Hizi ni njama wanazofanya kwakushilikiana na maafisa wengine serikalini ilikijinufaisha na kuchota pesa za serikali. Umefika wakati wa serikali kuambiwa kuwa raia tumechoshwa na vitendo hivyo.

    ReplyDelete
  3. HIYO NDIO FAIDA YA WASOMI WETU TUNAYOJIVUNIA SASA TUTAPELEKA WAPI HAYO MABUA(HUSK) YANAYOVUNWA NA WANANCHI WAKATI WASOMI WANANYONYA KWA MRIJA MAHUNDI(CORN) YA WENYE NCHI. CHONDE CHONDE JAMANI KURA NI SIRI ILA TUSIOGOPE KULA. PIA MAJENGO HAYA NI USHAMBA ASILIA KWAMBA LABDA TUFANANE KAMA MAHALI FULANI WANANCHI WANATAKIWA WATATULIWE MATATIZO YA UCHUMI SIO BENKI KUU YENYE MINARA PACHA

    ReplyDelete
  4. wasomi wetu hawasomi ili waweze kutatua matatizo yetu, na kuyatatua kitaalamu. Wanasoma ili wapate "ulaji". sasa ulaji ukishapatikana basi tena kazi ni wizi, unyonyaji, pombe na ngono nzembe.

    ReplyDelete
  5. ingekua vizuri kikosi cha zima moto kikatueleza mapemaaa mikakati gani imeweka kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika vikwangua anga hivi isije baadae janga lishatokea tukaanza kupeana sound ya 'mikakati kabambe' maana Dodoma tumeshaona hamna hata gari la kuzimia moto na msifikiri lile gari lenu moja lenye ngazi ndefu ndio suluhisho. Janga likitokea mtahitaji kuzima moto sambamba na kuokoa watu na kuwa na maji ya ziada karibu na tukio pamoja na fire hydrants zinazofanya kazi, helicopter za kuokoa watu including trained pilots anaeweza kumanuva katikati ya jengo na jengo, elimu kwa watumiaji jengo, assembly points etc.

    ReplyDelete
  6. Hata waziri Wa wizara husika alisema magorofa yatapunguza uhaba Wa nyumba. Ni kiongozi Wa juu ndani ya ccm tena ni dr

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...