Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makita Wilayani Mbinga baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara ya Shule hiyo leo ambapo ameahidi kuchangia jumla ya kompyuta mbili. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi na Wakulima wa kijiji cha Kitai Wilayani Mbinga aliposimama kwa muda kwa ajili ya kusalimiana na Wananchi hao, alipokuwa akielekea katika kijiji cha Makita kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Makita leo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa Miradi ya maendeleo. Juu na chini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein katikati, akitembelea Shamba la Uzalishaji wa Mbegu bora za Mahindi linalomilikiwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT katika kijiji cha Mlale Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Mlale Wilayani Mbinga, mara baada ya kuwahutubia kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika kijiji hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa Miradi ya Maendeleo.
Juu na chini anaonekana Mbunge wa Jimbo la Peramiho CCM Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma Mhe. Jenista Muhagama, akijumuika na wasanii wa ngoma ya Wazee wa jimbo hilo ambayo ni ngoma ya asili ya kukaribisha wageni Mashughuri, wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili Wilayani Mbinga kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani hum leo. Picha na Amour Nassor








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Candid ScopeFebruary 21, 2010

    Mbunge wa CCM jimbo la Peramiho wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma Mhe. Jenista Mhagama.
    Mwandishi jaribu kuwa makini na mipaka ya maeneo unayotembelea vinginevyo unatukoroga vichwa
    Jimbo la uchaguzi la Peramiho liko wilaya ya Songea vijijini na wala si wilaya ya Minga. Hivyo Mheshimiewa Jenista Mhagama ni Mbunge wa jimbo la Peramiho wilaya ya songea vijiji si Mbinga.

    ReplyDelete
  2. Candid Scope, hebu pata tano (5). Usijali sana, hiyo ndo ILIMU dunia waliyo nayo waandishi wetu wa reo reo! Madesa kibao waingia nayo kwenye vyumba vya mtihani. Vyeti feki kibao vyauzwa kule Balaza la Mitihani Bongo.

    Wala sishangai kabisa. Eti Mlale pia iko Wilaya ya Mbinga, mweeeeh! Dunia nzima. Je huyo mwandishi akiripoti habari za nchi nyingine si atakoroga zaidi? Fye fyeee!

    ReplyDelete
  3. CCM JARIBUNI KWENDA NA WAKATI KUJUA TOFAUTI YA CHAMA NA SERIKALI, KATIKA JAMBO LOLOTE LA KISERIKALI LINAHUSISHA WAFUASI WA VYAMA VYOTE, NA VINGOZI WALIOKO MADARAKANI NI VIONGOZI WA WATU WOTE, KATIKA JAMBO LA KISERIKALI MKIWEKA BEDERA NEMBO ZA CCM NI KUWANYIMA WALE WASIO CCM HAKI ZAO KIFIKRA, TUSIEW NA MABO YA KIZAMANI TWENDE NA WAKATI AU TWENDE.

    ReplyDelete
  4. per dm ndogo hiyo..na wewe anza kula flight za kwenda europe na usa ili na wewe uwe unakula per dm kubwa kama boss wako!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...