TANGAZO KWA KINA MAMA WOTE WAISHIO JIRANI NA MJI WA SLOUGH; KAMA, READING, HOUNSLOW, SOUTHALL NA KWENGINEKO.

ASSALAAMU ALAYKUM.

TUKIJAALIWA JUMAMOSI HII YA TAREHE 13/2/2010
SAA 9 MCHANA KATIKA MSIKITI WA DIAMOND ROAD

KUTATOLEWA MAWAIDHA NA BI MARYAM WA LONDON, NADHANI WENGI WETU TUMEWAHI KUMSIKIA AMA KUMUONA NA TUNAJUA NI JINSI GANI ALIVYOJAALIWA NA MWENYEZI MUNGU KATIKA KUTOA DAAWA.
HIVYO BASI TUNAKUOMBENI KINA MAMA TUJITOKEZE KWA WINGI ILI TUPATE MANENO YA MWENYEZI MUNGU. NA PIA TUNAWAOMBA KUZINGATIA MUDA, NA UKIJAALIWA KUSOMA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO.

ADDRESS NI,
Diamond Road Slough
SL1 1RT

AHSANTENI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Inshalah tukijaaliwa

    ReplyDelete
  2. Sisi tuliombali na UK tungependa kuyasiia mawaidha ya SHEIKHATY,kwahiyo tunawaomba muyaweke kwenye MTANDAO, OLA atawajazi INSHAALLAH.

    ReplyDelete
  3. sawaaaa lakini fanyenifanyeni mrudi nyumbani..........

    ReplyDelete
  4. ASANTE SANA KAKA YANGU KWA KUTUTOLEA TANGAZO LETU, TUNASHUKURU SANA NA MOLA AKUJAALIYE KILA LA KHERI KATIKA SHUGHULI ZAKO ZA KILA SIKU, NA AKUFUNGULIYE MILANGO YA KHERI. INSHAALLAH. mdogo wako,nusrat.

    ReplyDelete
  5. Michuzi ahsante kwa kuwatolea kinamama hao tangazo lao, ombi langu ni kwa kinamama wa Leeds iwapo mtajaaliwa kuandaa kongamano kama hili tafadhalini mlitangaze ili na sie wageni hapa Leeds tuje.

    ReplyDelete
  6. Nauliza hivi je nasisi wasomali wa kibajuni tunaruhusiwa kuja?,maana kama mawaidha yatakuwa yakitolewa kwa kiswahili basi hata sisi wabajuni tunajua kiswahili tunaweza kuja naomba jibu jamani,maana wasomali tunaojua kiswahili tuko wengi sana hapa Miltonkeynes
    Asanteni

    ReplyDelete
  7. MWANAMAMA YOYOTE ALIYEMUISLAMU, AWE MZUNGU, MHINDI, MBAJUNI NK, MRADI TU UNAFAHAMU KISWAHILI, BASI MNAKARIBISHWA NYOTE. waandaaji, Slough.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...