Mkuu wa kaya.. naomba usiibanie na hii..

Salaam,

Kwanza naomba niwatulize mioyo wale ambao kwa namna moja au nyingine wanajisikia kukwazika na kile kilichoendelea Bungeni leo hii na hasa suala la Richmond. Ninafahamu watu wengi wangependa kuona mambo makubwa yanatokea tena na watu wanatimuana na hata ikibidi kupeana mipasho ya papo kwa papo. Wengine wangetamani kuona wale ambao walijitangaza kuwa ni wapiganaji wanachukua msimamo mkali zaidi na kutokubali kwa namna yoyote ile kulimaliza suala hili kimya kimya.

Hata mimi ningependa hivyo.

Hata hivyo, inaposemwa kuwa "siasa ni mchezo mchafu" siyo suala la utani ni suala la ukweli. Wakati wowote unaposhughulika na wanasiasa ni lazima utarajie mambo kama haya kama gharama ya wanasiasa. Lakini zaidi pia ni lazima tuzingatie kuwa wanasiasa wote (na hapa naamanisha wote duniani) wanafanya mambo wakiongozwa na kanuni kubwa tatu duniani:

a. Watafanya jambo lolote ili wachaguliwe kushika madaraka
b. Wanataka wachaguliwe tena kushika madaraka (re-election)
c. Endapo kuna uwezekano wa wao kutochaguliwa, angalia kanuni "a".

Hivyo, yaliyotokea Bungenii leo na yatakayotokea kwenye suala la Kamati ya Mwinyi na hata baadaye kabla ya kuvunjwa kwa Bunge katikati ya mwaka huu ni LAZIMA yaangaliwe kwa mwanga huo.

Kwa maneno mengine msipate matumaini ya uongo kusikia wanasiasa wanaanza kujitokeza kuwa wapiganaji ufisadi kweli kweli baadaye mwaka huu huku miongoni mwao wakiwa ni wale waliokuwa mawaziri.

Hawa mtawasikia wakijitetea kuwa wakiwa mawaziri wanatakiwa kusimamia maamuzi ya serikali n.k na wengine watasema walichukua maamuzi mbalimbali ili kuonesha umoja ndani ya chama na siyo kwa sababu walikuwa ni dhaifu! Yote ni katika kufanya kazi kwa kanuni "a".

Ninachosema ni kuwa tusiwaangalie wanasiasa kama chanzo cha matumaini yetu ya kulibadilisha taifa letu! Tusiweke imani yetu yote kwa wanaotaka madaraka kwa namna yoyote ile kwani uwezekano wa wao kutuangusha ni mkubwa mno kama tulivyoona. Wakati umefika sisi wananchi wenyewe tuamue kumshika ng'ombe mapembe yake na kumuongoza tunakotaka.

Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba bila ya sisi wananchi kusimama pamoja na kusema nini tunachotaka (siyo kukubali kile ambacho wao wanasema nini tunataka" basi hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyataka.

Naomba niwatie shime enyi wana na mabinti wa taifa langu; msikate tamaa kwa kukatishwa tamaa na wanasiasa! Msiinamishe vichwa vyenu kwa masikitiko kwa sababu hawajakidhi mahitaji yenu! La hasha! Tuinue vichwa vyetu juu na kusema "tunawaelewa" na kwa sababu hiyo hatuwataki tena.

Muda unakuja ambapo Watanzania wataitwa wachukue msimamo dhidi ya wanasiasa wao; msimamo ambao utalitikisa taifa letu. Tumeanza kuona dalili zake toka mbali (CCJ na sasa "Tamko").. kama Moshi uliofichwa nyuma ya kilima tunaweza kusema kwa uhakika mahali fulani kuna moto; kama mwangaza wa jua linavyopambazuka tunaona nuru yake kabla hata halijatoka, lakini tuna uhakika kuwa nyuma yake lipo jua!

Mwaka huu ni mwaka wa Uamuzi wetu; ni mwaka wa uchaguzi wetu. Tusiwaache wanasiasa watuamulie tunachotaka ili tuwachague; tuwaamulie kile tunachotaka ili wakikubali tuwachague!!

Ni mimi ndugu yenu,
Mwenzenu,
rafiki yenu,
Na wengine adui yenu wa kudumu

Mpaka msalimu amri!!

M. M. Mwanakijiji

NB: Tutaanza matangazo yangu ya audio wiki ijayo inshallah.. mwendo mdundo mpaka kampeni.. zikiiva..tutaonana majukwaani!!

Wenye uwezo wa kurekodi CDs (downloads) tutakuwa na option ya kudownload episodes za "kijijini leo hii" na mnaruhusiwa kuzicheza na kuzisambaza mahali popote!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. kaka masikitiko niliyonayo hayaelezeki leo kutwa sina raha, mimi nipo ughaibuni nimeona tu hizo clip 3 kupitia global leo japokuwa hazijakamilika ljn maadhimio kama 20 yalikuwa yameshatajwa na yote ni kamati imeridhia....kamati imeridhia
    yaani tunageuzana watoto sasa,

    uwe mwanzo na mwisho wa hizi kamati, sina imani tena na nchi yangu

    ReplyDelete
  2. Ni rahisi kupiga soga kwenye mtandao, lakini tunayoyataka ni vigumu kufanyika. Njoo mtaani mkuu MM tupambane, si kuandika tu huko uliko.

    ReplyDelete
  3. Mgombea Binafsi- Shasi)February 10, 2010

    Mwanakijiji wewe ni:
    1. Mwandishi uliyebobea
    2. Mhamasishaji makini
    3. Mchambuzi mzamivu
    4. Mdadisi mzoefu
    5. Mwanasiasa Mchumi
    6. Mtaalam mwenye fikra pana
    7. Msanii wa sanaa endelevu
    8. Mchochezi wa mada adimu za kimaendeleo
    9. Mhabarishaji mzalendo
    1o.Mkarimu na Mkaribishaji uliye tayari kusaidia wenye shida & taabu mbalimbali


    Pamoja na sifa hizo zenye watu wachache sana, mimi nakushauri kuwa:

    UJITAMBULISHE RASMI NA KUWEKA AGENDA YAKO WAZI ILI WANANCHI TUKUFAHAMU MAANA SIFA NO.7 HAPO JUU INAWEZA KUKUFANYA TUSIKUELEWE AU KUKUTAFSIRI VYEMA WAKATI FULANI.

    NAJUA KUNA WATU WATASEMA UTAJITAMBULISHA WAKATI UKITIMU, LAKINI BINAFSI NAONA KWA MANENO ULIYOYASEMA HAPA LEO WAKATI NI HUU VINGINEVYO

    PENGINE UTAKAPOAMUA KUJITAMBULISHA, UGONJWA ULIO KATIKA MOYO NA AKILI YANGU UTAKUWA HAUWEZI KUTIBIKA TENA.

    ReplyDelete
  4. hii scnadal la richmond jamani tusidanganyike....yote ni drama..wanajuana...kama uchafu wote wanaucheza ila ni bahati mbaya idondokee kwako uaonekane..bado mnaamini kuna serekali tz...? mimi naaamini kuna ..the organised mafia...ndio mana si rahiki kukamatwa.utakamatwa wewe uliyekuwa kivyakovyako...

    ReplyDelete
  5. we mwanakijiji usilete siasa zako huku za chadema,kama umeona mtandao wako hakuna watu unatuletea nzi huku kwa ankal,ukome,viongozi wote wa africa ni wabovu,kweli lakini wa chadema wameova,bora kuchagua ccm kuliko chadema,maaana chadema ni ngos sio chama.kwenda

    ReplyDelete
  6. upuuzu mtupu.huna sera wewe

    ReplyDelete
  7. misupu usiweke mijadala ya huyu jamaa huku,analeta kampeni kwenye blog ya jamii,alipie basi

    ReplyDelete
  8. haibiwi mtu hapa.tumeshtuka dogo

    ReplyDelete
  9. Ninakubaliana na MM. Dawa pekee ni kuimarisha na kupanua siasa za upinzani. Angalia Marekani waDemocrats na waRepublicans wanavyoviziana. Upinzani imara unaweza kutuwezesha kuwabadilisha hao mamuluki kila baada ya miaka mitano na wakitoka hapo wanashika adabu. Miaka mitano CCM, mingine mitano CCJ, mingine mitano CHADEMA. CCM akija kurejea baada ya miaka 15 anakuwa ameishashika adabu ya kukaa kijiweni!!!

    ReplyDelete
  10. Wewe unajua leo? Beba box mzee wangu usaidie ndugu zako siyo kulialia tu na kutegemea mambo ambayo hayapo.

    ReplyDelete
  11. Naanza kuamini huyu jamaa ni Mzee kweli. Mtu kama kijana yuko Marekani nashindwa kupiga masaa aweze kusaidia ndugu zake huko nyumbani anaanza kuangaika za siasa za bongo. Ndiyo maana hapeni kutaja jina lake maana ndugu zake watamng'ang'ania. Wewe utaongea weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee kama hutoi hela hakuna mtu atakayekuchagua. Ni upuuzi tu. Ukienda kule kwenye forum yao utaona jinsi watu walivyo na ndoto na wanavyojua kupoteza muda. Mimi hapa naandika naviangalia vizee mwendo mdundo. $$$$$$$$$$$$$$$$. Hiyo Richmond haikulipwa hata senti moja sasa sijui tatizo liko wapi.

    ReplyDelete
  12. Jeshi lishike madaraka ya uongozi Tanzania. Ili hawa "viongozi" wa sasa watiwe adabu.

    Nyie mnaosema sijui Mzee Mwanakijiji analeta sera za CHADEMA humu ndani acheni ujinga. Sasa hivi hakuna cha CHADEMA, CCM wala nini. Tunatakiwa tuweke Utanzania mbele, la sivyo tutafika pabaya. Si busara kupinga tu kijumla jumla bila kupima mada,wabunge na kamati zao wamechemsha leo full stop. Ni wajibu wetu kama waTanzania kuamka na kuchukua hatua sasa.

    ReplyDelete
  13. Mwanakijiji,

    Ulichosema ni cha maana sana lakini kumbuka kwamba concept ya sisi wananchi ndio tuna uwezo wa kuamua na iko nje ya uwezo wa Mtanzania wa kawaida kuelewa. Wewe unaishi marekani na ndio maana unaelewa vizuri nguvu ya kura ya mpiga kura amabayo huzlazimisha Serikali kusalimu amri.

    Bongo viongozi bado ni kama wafalme, hata wakiboronga wanadunda tu.

    Ninaamini una uwezo wa pekee kuelemisha na kuhamasisha. nakushauri kwanza uwaelimishe wananchi kwamba mabadiliko yako ndani ya uwezo wao na kwamba hakuna manabii wataoshuka kutoka mbinguni kuja kuongoza nchi hii.

    It will take a few thousand years for Jesus to come back and rule the world with justice, so in the meantime lazima sisi wenyewe tukubali kwamba kukubali kudhulumiwa ni dhambi.

    Good luck comrade, mimi niko nawe.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  14. Big up Mwanakijiji

    ReplyDelete
  15. @Shasi.. naomba nikutoe shaka wewe na watu wengine; mimi siyo mwanasiasa. Sitamani na wala sitaki madaraka yoyote yale na kutokana na hilo natosheka kweli jinsi nilivyo.

    Ajenda yangu mimi ni moja tu; kusababisha mabadiliko ya fikra ambayo mara zote hutangulia mabadiliko ya kura. Ni mpaka tutakapoweza kubadilisha fikra zetu ndipo hapo tutakapoweza kuchagua viongozi na watawala ambao kwa kweli wanatufaa na hatutasita kuwawajibisha kila inapobidi.

    Katika hili nadhani inatosha kuangalia hoja zangu, kuzipima, kuzipangua na kuzikataa. Na wakati mwingine kuzipuuzia kama anons kadhaa walivyofanya. Ndiyo uzuri wa demokrasia.

    shukrani.

    ReplyDelete
  16. Napendekeza ule wimbo wa mr Politician wa kiswahili uwe unapigwa mara kwa mara ilikuwakumbusha watu kuwa wanarudi tena na kauli zile zile!

    ReplyDelete
  17. KAMA HIVYOVIVYO ULIVYOSEMA WATAFANYA LOLOTE ILI WASHINDE NA WEWE UNAANZA KUFANYA VYOVYOTE KWA KUPIGA KAMPENI ZA KUWAPONDA ILI NA WEWE USHINDE...HIVYO NA WEWE NI MWANASIASA.....KWANI WADAU MMESAHAU YULE JAMAA ALIYEWAZIKA MAITI NA MAJERUHI THEN POLISI WALIVYOKUJA WAKAMUULIZA ILIKUWAJE? AKAWAJIBU "MAJERUHI WALIKUWA NI WANASIASA NA WALIKUWA WANALALAMIKA HAWAJAFA LAKINI SI UNAJUA WANASIASA WALIVYO WAONGO? NIKAJUA WANADANGANYA HIVYO NIKAWAZIKA WOTE" .....M.M ACHANA NA SIASA...JISHUGHULISHE NA MAENDELEO YA FAMILIA NA NCHI YAKO.

    ReplyDelete
  18. Michuzi asante sana kwa kutuhabarisha. Mwanakijiji tunakuoungeza kwa kuandika mara kwa mara. Nadhani sitachafua hali ya hewa hivyo usiniminyie maana hatya ni mawazo yangu na ninaweza kuwa Wrongo kama binadamu.

    Mwanakijiji, inakuaje mwanzo aiponde CCJ halafu hapa anainyanyua?

    Jamani kuna mtu mmoja sijui nani, sikumbuki aliwahi kuandika hapa kuhusu huyu Mwanakijiji na kazi zake anazofanya hasa, nami sikutilia maanani maana niliona kuwa ni mzushi fulani mwenye wivu lakini sasa ninaanza kupata picha.

    Na ukweli ukiona yale maandishi ya Katiba ya CCJ & hilo analoita 'Tamko' ni utunzi wa staili ya Mwanakijiji. Siku zinakuja na mtathibitisha maneno yangu.

    Atudanganyiki tena!

    ReplyDelete
  19. Inasikitisha kuona watanzania wanatoa maoni yao kwa kuwa tu ni wanazi wa chama fulani cha siasa, ndio maana hatutaendelea kwa kuwa wengi wetu ni mawazo finyu, huyo mwanakijiji kaongea ya maana sana kwa watu wenye akili timamu, ni kujiuliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili hasa uadilifu, ila ona maoni ya watz, inasikitisha sana tumedumaa kimawazo na fikra, ndio maana tupo hapa tulipo

    ReplyDelete
  20. nadhani watu wengi wamekurupuka kutoa maoni bila kusoma taarifa, ni wachache sana ambao tumeisoma hii habari yote na kuielewa, mwanakijiji hakubase upande wowote wa siasa au chama, nchi hii ni ngumu sana kuendelea na hapa wengi wameweka personal emotions mbele..

    kamwe tusitegemee wanasiasa waje kutukomboa. imetulia.

    ReplyDelete
  21. Mnaoponda wote ni wale mnaishi na kupata ugali wenu kwa fedha ama zinazo au zilizotokana na wazazi au ndugu zenu kuwa serikalini tanzani. kama wewe ni mtanzania mwenye uchungu hakika lazima utamsapoti huyu bwana. he is simply brilliant!!! hakuna kingine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...