Tunatoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mazishi ya Baba yetu Mpendwa Mzee Samike wa Samike aliyefariki dunia Februari 15, mwaka huu.
Tumefarijika sana kwani wengi walitufariji (kwa kutupa maneno ya faraja) na tulikuwa nao pamoja katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na baba yetu kipenzi.

Tunamshukuru Mungu kwani shughuli zote za mazishi zilikwenda salama hadi tulipompunzisha baba yetu katika nyumba yake ya milele. Bwana ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe.
Amina

Leah Samike

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. poleni sana leah,mwambie esther classmate wangu anicheki kwenye mail hii,docmsaf@gmail.com

    ReplyDelete
  2. poleni sana familia ya samike.
    nilisoma ihanja na vijana wake wawili, mojawapo anaitwa esther

    ReplyDelete
  3. poleni sana kwa msiba huu mkubwa! mungu ametoa na mungu amtwaa, nyinyi mlimpenda lakini mungu alimpenda zaidi. R.I.P baba. mimi ni classmate wa esther mwambie aweza kuwasiliana nami kwa email brohm77@yahoo.com.

    ReplyDelete
  4. Pole sana Leah, you are a strong lady, the one and only female chief photographer of a reputable newspaper.

    You will get through,
    RIP Mzee Samike.

    Pasco.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana familia ya Mzee Samike!Rest in peace Mzee Samike!

    ReplyDelete
  6. Mimi nawapa pole sana katika msiba huo mzito na mkubwa kwa kuondokewa na Baba yetu Naomba mwenyezi mungu alaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi na pia uwape Nguvu familia ya Samike. Iwe mwenyezi mungu sisi tulimpenda ila wewe umempenda zaidi baba yetu. Amen

    ReplyDelete
  7. Poleni sana Leah, Minza mungu atawapa nguvu, Kwani mimi Binafsi nilishtuka sana kusikia taarifa hizi. mimi nipo mbali nikirudi Inshallah nitakuja nyumbani kuwapa pole. R.I.P Baba. masqtz@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...