RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEUA BW WILSON MUKAMA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAGAZETI YA SERIKALI (DAILY NEWS NA HABARI LEO CHINI YA TANZANIA STANDARD NEWSPAPERS LTD - TSN) KUANZIA FEBRUARY 26, 2010.
BW. MUKAMA ALIWAHI KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA AMESTAAFU HIVI KARIBUNI AKIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI. ALIWAHI PIA KUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA JIONI HII, KUFUATIA UTEUZI HUO WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO MH. GEORGE MKUCHIKA AMEWATEUWA WAJUMBE WANNE KUUNDA BODI YA TSN KAMA IFUATAVYO:
1. BI. HIJJAT HAWA MMANGA AMBAYE NI MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)
2. BW. KALUA SIMBA (MCHUMI WA KUJITEGEMEA KUTOKA SEKTA BINAFSI
3. BW. CLEMENT MSHANA (MKURUGENZI IDARA YA HABARI - MAELEZO)
4. BW. CHARLES RAJABU (AFISA HABARI MKUU DARAJA LA KWANZA, WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.
Asante kwa nyuuuz.Mzee Mukama ni mtu swaafi. Sasa tusubiri Managing Editor. Sijui utakuwa wewe Michuzi??? Hapo tuombee dua kwani nafasi hiyo ni nyeti sana.
ReplyDeleteE bwana hivi na mi nikitaka kupata ulaji wa kwenye bodi nifanyeje?
ReplyDeleteHongera Bw. Mukama, tafadhali wacha legacy hapo TSN manake tumechoka kuwa na Wenyevyiti wasio na vision, watu wanakuja na kuondoka bila ya kuweka new direction.
ReplyDeleteMkurugenzi nambari 4, hapo ni aliyekuwa Managig Editor wa Daily News ama mwingine?
(US Blogger)
charles rajabu arudishwe ukurugenzi.
ReplyDeleteIGP Mwema apangua tena maofisa wa polisi
ReplyDeleteNa Mohammed Mhina
10th March 2010
Kombe wa usalama barabarani astaafu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Saidi Mwema, amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye jeshi hilo kwa kumteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Mohammed Mpinga, kuwa Kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na James Kombe ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.
Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo, Abdallah Mssika, alisema jana kuwa nafasi ya Kamanda Mpinga, inachukuliwa na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Johansen Kahatano.
Kabla ya uteuzi huo, Kamanda Mpinga alikuwa ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama barabarani .
IGP Mwema amemteua pia Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Advera Senso, kuwa Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi, badala ya Mrakibu Suzan Kaganda, ambaye amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa msaidizi wa kitengo cha masuala ya operesheni.
Wengine waliohamishwa ni Ofisa Mnadhimu mkoa wa Tanga, ACP Simon Mgawe, kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Kigoma, SSP Salehe Mbaga, kwenda kuwa Mkuu mpya wa Usalama barabarani Mkoa wa Pwani.
Kamanda Mssika alisema Mkuu wa Upelelezi wa Kikosi cha Reli, Mrakibu wa Polisi Adolphina Kapufi, sasa anakuwa Ofisa Mnadhimu wa Mkoa wa Tanga ambapo nafasi yake inachukuliwa na SP Sebastian Mbutta, kutoka Upelelezi Singida.
Alisema SP Robert Masanja, ambaye ni Mkufunzi Chuo cha Polisi CCP Moshi sasa anakuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na ASP Marco Joshua, ambaye sasa anahamishiwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma.
Kamanda Mssika aliwataja maofisa wengine waliohamishwa kuwa ni ASP Anthony Masonzu kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu jijini Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Polisi William Mkonda ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kigoma.
Alisema kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga zaidi katika kuboresha ufanisi katika kutoa huduma za Polisi kwa Jamii.
Hivi karibuni IGP Mwema aliteua makamanda wapya wa mikoa wa polisi, uteuzi uliogusa RPC wanne.