JK leo amewaapisha Katibu Mtendaji wa tume ya Mipango na manaibu katibu watendaji wanne wa Tume hiyo Ikulu jijini Dar. JK amemwapisha Dk. Philip Isdor Mpango kuwa katibu Mtendaji wa tume hiyo na manaibu wake wanne akiwamo Bwana Maduka Paul Kessy, Bi.Happiness Mgalula, Bi.Florence Maridadi Mwanri na Bwana Klifford Katondo Tandari.Pichani Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dr.Philip Mpango akila kiapo. Kati ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Philemon Luhanjo
JK akimkabidhi zana za kazi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dr.Philip Isdor Mpango wakati wa sherehe za kumwapisha leo Ikulu jijini Dar

JK akimkabidhi zana za kazi Naibu Katibu Mtendaji wa
Tume ya Mipango, Clifford Tandari mara baada ya kumwapisha Ikulu
JK akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wapya wa Tume ya Mipango baada ya kuwaapisha leo. Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Clifford Tandari akipongezwa na familia yake baada ya kuapishwa












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera Engineer Happiness Mgalula,Mungu akutangulie katika kazi yako.

    ReplyDelete
  2. Mbona manaibu wengi? au ndio kupeana ulaji.

    ReplyDelete
  3. Ukiteuliwa unakaribishwa na nduguzo kwenye kuapishwa. Ukitimuliwa pia unakaribishwa na nduguzo?

    ReplyDelete
  4. Sijui haya maua ni ya nini. Umeteuliwa manake umepewa kazi hivyo kafanye kazi sasa maua ya nini au ndio kushangilia ulaji??!!
    Hii ni kazi wakimaliza muda wao wakiwa wamefanya vizuri ndio wanastahili maua kwa kazi nzuri....
    Hapa wangetuambia watafanya nini katika kazi hiyo sio kuanza kukaa mkao wa kula.
    Mdau

    ReplyDelete
  5. Hongera sana! Hongera sana mr Tandari Mungu awe nawe katika kazi yako.yesu mnazareti akutangulie kwa kila hatua utakayopitia.your the best!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2012

    Hongera sana bwana clifford tandari mungu akutangulie katika kazi yako you deserve the best be blessed

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2012

    Maua ni jambo la kheri kupewa mwanzoni na mwishoni ni sawa,hiyo ni ishara ya kumtakia kila la kheri katika kazi yake

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2012

    Maua ni jambo la kheri kupewa mwanzoni na mwishoni ni sawa,hiyo ni ishara ya kumtakia kila la kheri katika kazi yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...