Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Iringa, akimvisha Skafu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo, kuanza ziara ya siku sita ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Iringa. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Watoto wa kijiji cha Mgera Wilayani Iringa alipowasili katika kijiji hicho kwa ajili ya kuzinduwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa Wanachi wa kijiji hicho leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo ya Wananchi Mkoa huo. kulia Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Mohamed Abdulazizi katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ismani ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. William Lukuvi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, akiondosha kitambaa kuzinduwa rasmi mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa wananchi wa kijiji cha Mgera Wilayani Iringa leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa Miradi ya maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Mihayo Fundi kushoto, kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya hiyo akimkabidhi kilo mia moja za mchele pamoja na mbuzi kwa ajili ya kitoweo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Ali Mohamed Shein ikiwa kama zawadi kutoka kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuweza kuwatembelea na kuwazindulia miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo leo. wa pili kulia Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Mohamed Abdulazizi na wa pili kushoto Mbunge wa Jimbo la Isimani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. William Lukuvi. Picha na mdau Amour Nassor (VPO)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...