mdau mkongwe katika tansia ya muziki Felician Mutta akiwasili Kunduchi Beach hotel jijini Dar na kausafiri kake asubuhi leo akiwa kama mmoja wa wana Kili Tanzania Music Awards Academy ambayo wikiendi hii imefunga kambi hotelini hapo katika mchakato wa kupata wateuliwa (nominees) wa wasanii bora wa mwaka 2009.
Felician Mutta hivi sasa anaendesha libeneke la usambazaji wa kazi ya muziki na filamu kupitia kampuni ya FMWASAMBAZAJI yenye kupatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Hv ni macho yangu au nakosea, hii si hammer kweli? Duh naona FM kazi ya si ya kitoto! Ngoja nisubiri waosha vinywa...thnx

    ReplyDelete
  2. kweli wafanyabiashara wa kitanzania tabu kweli kweli mtu anaendesha hammer anafanya biashara ya usambazaji anatumia email ya yahoo, hana hata website mmhhh.... kazi ipo

    ReplyDelete
  3. he!kila kitu kinawezekana,ukisikia mtu mzima maana yake ni vitendo,sio kulalamikia maisha tuuu kila siku,big up mtu mzima.

    ReplyDelete
  4. sasa wewe unashangaa nini,mbona hammer bongo ni kitu cha kawaida

    ReplyDelete
  5. NI HIVI HUYU PAPAA MUTTA ALIKANUNUA KAHAMMER KADOGO AKAKAPA DOZI YA KICHINA ILE YA MAHIPSI NDO KAMETOKEA HIVI.

    ReplyDelete
  6. Hammer la kichina!

    ReplyDelete
  7. ...........Benitez oyeee

    ReplyDelete
  8. Duuh KWELI BONGO KILIMO KWANZA,WAMAREKANI WAMESHINDWA GHARAMA ZA UWENDESHAJI WA HAMMER BONGO WATU WANAPETA KWA KUHUZA BONGO FLAVA

    ReplyDelete
  9. wewe nawe wa wapi?nini cha ajabu hapo?ndio mara yako ya kwanza kuona hummer(sio hammer)??uko wapi kijijini ndanindani au?acha ushamba tembea uone.eti usubiri waosha vinywa ili iweje??wenzio washazizoea hizo hapo tz,by the way hio model ya zamani kuna latest zaidi ya hio hapohapo bongo

    ReplyDelete
  10. Hammer sio kitu cha kawaida hapo Bongo mbona likipita watu wanalikodolea kama wameona nn vile, wakati hizo Corlla zikipita watu wanaendelea na shughuli zao, acha hizo ww shahidi wa maisha !!

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi,
    Mimi sina wasiwasi wala kinyongo na wanaoendesha Hizo sijua "hama"wala nini. Mimi ninakubali kuwa biashara ni sehemu kubwa ya ujenzi wa taifa. Sasa ninapenda kushaurio hawa wafanyabiasghara wetu wawekeze pia katika sekta ya mitandao/Internet katika biashara zao. Mimi Kaka michuzi sioni kama biashara za Tanzania ziko serious katika kutanganza biashara zao kwa internet. Mfano sasa hivi tuna hii kitu mnaaita Kilimo Kwanza...sijaona internet hata moja ya Kampuni inayosambaza viofaa vya kilimo..majenmbe, nk.nk Sasa utasemaje Kilimo kwanza wakati taarifa zake hazipatikani. Mimi nazipa sekta za fedha mfano Bima na Mabenki BIG UP maana wanaongoza kuwa hewani...wengine naomba waige

    ReplyDelete
  12. Michuzi,
    Mbona hiyo picha inaonekana kama kaka Muta alishawasili kwa huo mkutano akapata kitambulisho chake kisha akaenda kwenye hammer lake kufotoa...kama alipewa kitambulisho kabla ya kufika Kunduchi sawa kama sivyo hiyo maelezo ha hiyo picha yana ka-ufix fulani..
    Ni ufuatiliaji wa kizushi tuu....

    ReplyDelete
  13. Duh, hay ni matokeo ya 'dozi ya kimatumbi' kuzidi. Eti HAMA, jamanie mbavuu zanguuuuu! Eeeee nipe mbavu zangueeee! Yaan mtu anaangalia na majicho yote mambili alafu anaandika 'HAMMER'! Ni HUMMER jamaniiii!

    ReplyDelete
  14. hao wanaoshangaa labda washamba wenzio na watoto wanaoshangaa how big and ugly it is!!!

    ReplyDelete
  15. WIZI MTUPU!! KWA MAISHA YA MSTARI HAMMER INAWEZEKANA. SWALI NI? KUNA MAISHA YA MSTARI MINAZI?

    ReplyDelete
  16. Anon. wa Tarehe Sun Mar 21, 07:57:00 PM, na wewe unalo nini?Je likipita pembeni yako (kama huna), utafunga macho? Maana unaongea kama unalo vile? nyie ndo wale wale. Kumbuka; "Ushamba si mzigo kila mtu anao"

    ReplyDelete
  17. Kwa Bongo
    Ishu ya magari ya kifahari au nyumba siyo dili kabisa..Humer siyo ishu zipo kibao..na watu hawazifagilii kabisa...kama ilivyo kwa Lamboghini,Vogue etc...nyie wabeba box ndio mnashangaa mtu kumiliki hayo madude..sisi huku tunanunua kwa Cash bila matatizo yeyote..wala hatuhitaji ma internet/website yenu..tunapiga kavukavu kiutu uzima na mambo yanakwenda fresh...

    Mazee

    ReplyDelete
  18. hahahaaaa ebu nicheke mimi!!

    aya

    ReplyDelete
  19. ......Hilo linaitwa "HAMMA" nyie wooooooooote mmekosea rudini shule kwanza.

    ReplyDelete
  20. Ninyi wote mnao toa maoni ya watu kutumia internet, je mnajua biashara ya huyu na jamaa inavyofanyika? Je nmajua mazingira ya Tanzania ya leo?

    Huyu jamaa biashara yake ni kusambaza miziki na maigizo. Hivyo watu wake wa karibu ni wamachinga ambao ndio wanapeleka hizi kazi za wanasanii kwa wateja, sasa wamachinga na internet kuna uhusiono gani?

    Pili hata kama kuna watu wengine anafanya nao kazi, watu wangapi Tanzania wanatumia computer? Je issue ya umeme kukatika hovyo itamwezesha mtu kutegemea internet kufanya biashara Tanzania?.

    Mtu kama anaona biashara yake ipo safi hana haja na internet.

    Internet ni kwa watu wa Ulaya na Marekani, bongo bado sana.

    ReplyDelete
  21. KionambaliMarch 22, 2010

    hajui ku-park gari,angalia tairi la mbele kushoto limepinda. Lesseni Class Z.

    mdau,
    Kionambali.

    ReplyDelete
  22. Ankal naona wadau tunaondoka kwenye mada husika.Fikra zangu hapa zinaniacha na swali kuwa ni nani anafadi kati ya mtunzi na msambazaji wa kazi za wasanii wa muziki?

    ReplyDelete
  23. mchina oyee walau na sisi tunapamba HAMMA(kimatumbi)kizhungu nafikiri HUMMER.

    ReplyDelete
  24. Hivi yule dada Saida Karoli, wa mwenye wifu ajinyonge huko wapi leo? Jibu lake litakupa kama wasanii wanafaidi kwa kazi zao?

    ReplyDelete
  25. wewe unaesema hammer ya kichina we hapo ulipo huna hata hiyo bito ya kichina unasema vya wenzako,fight upate na wewe japo bito ya kichina,sio unabaki unachooonga.

    ReplyDelete
  26. Naona hoja imehamia kwenye gari. What makes this car so special?

    ReplyDelete
  27. wacheni wivu wa kitoto

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  28. Mafuta yatatoka katika jasho la wasanii...wajinga ndio waliwao!
    MZAZI.

    ReplyDelete
  29. watu wanadiscuss kuhusu hummer,dah kazi ipo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...