Mzee wa libeneke mambo yanakwendaje?
Nimeamua kushiriki kwenye blog kwa kutuma picha na ukiona zinafaa basi utaziweka ili wadau wapate kuziona.Nilikuwa na safari ya toka tunduru hadi masasi na kisha masasi mpaka dar.Nilitoka tunduru ijumaa na kulala masasi wiki iliyopita.
Nimetoka masasi jana j3 kuja dar.Wiki iliyopita watu wamelala sana njiani kati ya Somanga na Muhoro ila jana tumepita bila tabu sana sehemu hiyo ila kuna baaadhi ya matukio ambayo nimeona niyatume baada ya kupiga picha kadhaa.
KAKA KULE KUSINI KWETU MWENZIO AKINASA KWENYE TOPE JARIBU KUSAIDIA ILI ATOKE.UKIJIFANYA UJANJA UANZISHE NJIA YAKO BASI LAZIMA UKAE TENA VIBAYA ZAIDI KULIKO YULE MWENZAKO.
Picha za njia ya Tunduru hadi Masasi zinahusisha basi nililopanda mimi na hizi nyingine zinahusisha malori yaloyoziba njia katika kipande cha kutoka Somanga hadi Muhoro kuelekea nyamwage na hatimaye ikwriri.
Ni hayo tu kaka.
Ni mimi mdau wa Blog ya jamii "Joseph"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Asante MAISHA MAZURI KWA KILA MTANZANIA.

    ReplyDelete
  2. Bongo tambararezzzzzz!

    Mdau wa Mwenge

    ReplyDelete
  3. zile dola viongozi walizochoma kwenda London kuhudhuria diaspora 2zingetumika kukarabati hizi barabara.
    Mimi nikiwaambia wananchi kuwa Tanzania haina vipaumbele hamnielewi. hii ni moja ya mifano...tunaendelea..!

    ReplyDelete
  4. Tunataka flyovers!

    ReplyDelete
  5. HIVI BARABARA YA DAR --- LINDI HAIJAISHA JAMANI???????? TUONEENI HURUMA WENZENU WA KUSINI TOKA UHURU MIAKA KARIBU HAMSINI SASA HATUNA BARABARA JAMANI, TUWENA NA PLANS NA UTARATIBU MZURI TUMALIZE BARABARA MOJA KWANZA THEN TUENDE KWA NYINGINE SIYO MNATAKA KUJENGA BARABARA ZOTE KWA WAKATI MMOJA KWA KUTAFUTA SIFA RAHISI ZA KISIASA NA UMASIKINI HUU, HII BARABARA MKAPA ANGEIMALIZA KWA VILE ALIKUWA NA UTARATIBU MZURI NA MWANANA, JAMANI SISI WATU WA KUSINI TUMEKOSA NINI KWENU NA KWA MUNGU JAMANI HII SI SAWA KABISA KABISA TUNAOMBA TUMALIZIENI HII BARABARA NA UCHAGUZI HUO UNAKUJA ITATUWIA VIGUMU KUWACHAGUWENI TENA JAMANI HIVI MTATULAUMU!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Kama alivyosema mdau hapo juu. Pesa zinaliwa na akina ankal na wenzake huko london na mji wa kusoma wa Tanzania wanachimba mahandaki kukwamua magari yaliyotumbukia ndani
    !!!!!!

    ReplyDelete
  7. ina mkapa hakujenga barabara kwao kusini?aliishia kununua RADAR

    ReplyDelete
  8. Yani inakatisha tamaa jamani mjue kusini mwa tz ni bado kuko nyuma uwezi kuamini ni tz yetu iliopata uhuru miaka rukuki iliotaka kujitawara ili ijipatie maendeleo yake yenyewe sasa sijuwi tulifanya kosa kuwafukuza wazungu yani jibu sipati tuliamua kuwafukuza ili tujitaware tufaidike na mali asili yetu ilio kuwa inaibiwa na wangu mda mwingine huwa nafikilia rabda viongozi wetu wa mwanzo walitumia ule mwanya wazungu kutuibia wakatushauli ili tuwafukuze ili watutaware wao bira kufikilia faida za watu wote ambao sasahivi ndio wana ma kaunti uraya na kua na majumba ya samani. mungu tusaidie waja wako tume kosa nini sisi wa tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...