Isha Maushauzi - Jahazi Modern Taarab
Khadija Omar Kopa - ToT
Mwanahawa Ally - Jahazi Modern Taarab
Zuhura Shabani - Zanzibar Stars
Ule Mpambano wa "Nani mwanamke mkali wa Taarab Tanzania" utakao fanyika ktk Ukumbi wa Traventine Hotel Magomeni siku ya tarehe 28 March mwaka huu umepeta baraka kutoka kampuni ya simu za mkononi Tanzania VODACOM ambao watatoa zawadi kwa washindi na kudhamini Tamasha hilo.

Mtanange huo utakaokutanisha wanawake wanaong'ara sana na kutambiana ktk miondoko ya Taarab wataonyeshana nani zaidi huku mashabiki waki-jaji, usiku huo wa tarehe 28 ya mwezi March mwaka huu, Traventine Hotel Magomeni.

Huku bendi ya Jahaz Morden Taarab chini ya Mfalme Mzee Yusuph ikisindikiza mpambano huo wa aina yake, baadhi ya wanawake watakaoshiriki ktk show hio ni pamoja na malkia wa Taarab Khadija Kopa (TOT), Mwanahawa Ally (Jahaz), Zuhura Shaban (Znz), Isha 'Mashauzi' (Jahaz) na wengine.

Tamasha hili la Mpambano wa mwanamke mkali wa Taarab limedhaminiwa na VODACOM TANZANIA na kuandaliwa na DIDA CLASSIC BOUTIQUE iliyopo Kinondoni Vijana.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. MwanaHawa Ally na Zuhura Shaabani... Waliobaki kwisha kazi!!

    ReplyDelete
  2. Kuna tofauti kati ya wanaoimba taarabu na mipasho. Mbona mmewachanganya kwenye hili?

    ReplyDelete
  3. Mh!!Zuhura nguo yako nzuri

    ReplyDelete
  4. Wapi mwanadada mwenye sauti ya kutoa nyoka pangoni-Bi Sabah Muchacho?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. MWANAHAWA ALLIY MKALI ZAIDI

    ReplyDelete
  6. mipasho vs taarab=vitu 2 tafauti

    kuna wale wanakata mauno/vibrate adi unaona hee jehenam imeamia duniani

    kazi kweli

    ReplyDelete
  7. Zuhura Shaaban Mashaalah..Sauti nyororo, Kuanzia akiwa melody alikotamba na Siadhiriki,Watakerekwa sana,Nani Zaidi,Hakuna Tenda Hakuna buzi na nyingine nyingi..Mpaka Zanzibar stars anapotamba na Sichagui Sibabui, Sina Kinyongo,Akutukanaye,Sifedheheki, Kamawema Unauzwa, na huu unaotamba sasa hivi wa Hasara Zenu..Zuhura Yuko Juu sana, ila kumuweka ligi moja na Isha Mashauzi, wanakosea hapo wamekosekana, Rukia Ramadhani, Sabah Salum na Khadija Yusuph..

    ReplyDelete
  8. jamani hii taarabu yetu ya siku hizi kulikoni?naona jahazi wamekuwa na wanenguaji vipi? sio ile taarabu tuijuayo

    ReplyDelete
  9. I heard some nice Swahili Taarab music https://bit.ly/2wwhGg6 . If you are planning to travel to one of the East African beaches, They have nice music called the taarab that is little bit like Arabic but with some nice tune. https://bit.ly/2KR8NRw.Enjoy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...