Wadau wakiwa mbele ya duka la wabongo lililopo 0xford road mji wa Kusoma liitwalo Bongo Flavour. Toka shoto ni mdau Gardol, mkurugenzi wa duka hilo Dixon, Mahamudu na Mdau Banduka. Hii inadhihirisha kwamba si kweli kwamba wadau wote huku ughaibuni ni wabeba maboxi. wengi wao ni wajasiriamali wa nguvu...
baadhi ya bidhaa ndani ya Bongo Flavour
ndondozzzzz kama kawa
hapa unapata tui la nazi ndani ya boxi
Bongo Flavour kwa ndani





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. brother michuzi usituharibie lugha yetu. mbeba boksi ni mtu yeyote alieko huku na kujipatia riziki yake kwa kufanya kazi yeyote ile iwe nurse, warehouse, muuza duka, mfagiaji na kazi nyenginezo woote hawa kwa lugha yetu sanifu wanaitwa wabeba boksi.

    ReplyDelete
  2. Bab kubwa kazi nzuri sana

    ReplyDelete
  3. ingawa sina budi kuwapa hongera kwa jitihada mlizopitisha kuanzisha mradi huu, lakini naona mnafanya utani na vyeo sasa, yaani kadika lenu hilo lina mkurugenzi? are you joking me? sio manager wa duka?

    ReplyDelete
  4. UTOKE TANZANIA UJE UFUNGUE KADUKA UK, KWELI UMASIKINI NI AGHALI, KIHINDIHINDI SIO, YOTE HIYO AMTAKI KWENU. SHIDA NINI NAISHI ULAYA, MMM MWEEEEEE. MSHUKURUNI LABOUR KWA KUWAPA MAKARATASI CONSERVATIVE HUYO ANAKUJA MTAKOMA UBISHI, MTASHANGAA KAMA MKO FERRY HIVI

    ReplyDelete
  5. hongereni sana waafrica wezangu. wezentu wachina wana maduka yao huku ugaibuni na wengi wao wanafanya vizuri sana kwa sababu ya support kutoka kwa wachinese wengine. hao watu mara nyingi wana nunua chakula au vitu vingine kwenye maduka yao tu hata kama hayo maduka yako mbali na wanapoishi. didi wakenya tumeanza kufanya hivyo. hii itafanya tuwe successful.

    ReplyDelete
  6. Wale wapenda majungu endeleeni tu majungu ila Kumbukeni Marekani imejengwa na wa Jewish na wataliano hivihivi wamejipatia riziki ambazo zimewapa jina nchini kwao na nchini marekani wacheni wenzenu wapate pakula. japo hao niliowataja wapo juu sana ila Watanzania mungu anawasaidia wakuwapinga ni wauza unga tu.

    ReplyDelete
  7. wewe acha wivu - kwani mtu akijiita Mkurugenzi/ Rais/Meneja wa Duka kuna tatizo gani? Haya basi, tukuite wewe Rais basi kama unataka? Wabongo bwana! Roho za Korosho

    ReplyDelete
  8. Yaani Michu kama tulikua tunawaza sawa leo!! Na mimi leo kwa mara ya kwanza nimeenda huko East London, yaani kule si London, ni Dar-Kampala-Nairobi manake mtaani ni Kiswahili na Kiganda ndio unakisikia kwa sana.

    Sasa jamaa zangu wa kiGanda wakanipeleka kwenye duka la vitu vya Afrika Mashariki, linaitwa Pascheal's shop (sijakosea spelling, ndivyo linavyoitwa) Hili duka ni la Mganda. Humo ndani sikuamini macho yangu, kuna Unga wa aina mbali mbali wa Azam, bia za Serengeti, Tusker, malapa ya Umoja, Royco, Blue band, dagaa wakavu, magimbi, maparachichi ya ukweli (si huu utani wao wa huku Ulaya) yaani bidhaa kibao za nyumbani.

    Hongereni sana waTanzania mnaofanya bidii katika shughuli zenu popote mlipo

    ReplyDelete
  9. KILICHOHARIBU HAPO NI ULEVI TU.

    ReplyDelete
  10. wamejitahidi saaaana hongera sana mzee dixon bado unakopesha?

    ReplyDelete
  11. mimi ningekuwa mpiga box uko nisingekubali kupoigwa picha na kuwekwa humu!! kweli shule muhimu

    ReplyDelete
  12. AGH mimi nilizania mbeba box ni diaspora yeyote yule. Sikujua shurti ubebe box kupewa jina hilo. I was so out of the class

    Next time ukija USA uje ututembelee nasisi. Ila wengi wetu tuko low key ...whatever u see iwe off record.

    ReplyDelete
  13. Mimi huwa naenda hapo Bongo Flavour kununua bidhaa mbalimbali na pia kutuma Paundi ££££ zangu mara kwa mara Tanzania tena kwa gharama nafuu sana na ni waaminifu sana, huwa pia nakutana na ndugu zetu wa Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda wengi wanatumia duka hili kutuma Paundi ££££ zao katika nchi zao. Mbali ya yote Bongo Flavour wako karibu sana na Watanzania katika kushiriki katika mambo mbalimbali ya Kijamii. WELL DONE MAMA NA BABA BONGO FLAVOUR - READING NA WAJASILIAMALI WENGINE HAPA UK

    ReplyDelete
  14. Weka bidhaa za Tanzania wewe...

    ReplyDelete
  15. Kama ameanzisha duka ni yeye na ujue huyo ana makaratasi ndo mana anatafuta riziki yake! Hao wanaoponda mara uswazi ni sawa tu lakini wanatamani kufika huko na hawajafanikiwa kupata viza! Acheni kuponda vitu msivyovijua...

    ReplyDelete
  16. NAONA UNGA WA IWISA TOKA KWA MADIBA KWELI NGOMA IMEKAA KIBANTU

    ReplyDelete
  17. jamani hata mtu akijiita mkurugenzi roho inakuuma kwa nini? mtaji wake, biashara yake, bills analipa mwenyewe hajafungiwa wewe unafikiri kuran business uk ni lelemama.anza yako basi tuone.kazi kukimbia bills kwenye nyumba everyday sasa majungu tu umebakiza

    ReplyDelete
  18. Hongera mama dicky na mzee dicky yote hayo hapo juu yatawatia moyo na soon mtaongeza nyingine.naamini penye mchaga hapawezi kuharibika kitu sawa msee wangu tupo proud kusikia mchaga ana duka ulaya. well done both of you. mkija moshi nitafuteni niwape kitochi.

    ReplyDelete
  19. watanzania ndio maana watu wanawaogopa kwa ajili ya maneno, this is 2010 going 2011 you need to change, mambo manyoongea yamepitwa na wakati, huu ni wakati wa kumtafuta mungu kwa sababu hujui kesho utakuwa wapi, andaa mazingira utakayoenda kuishi mungu akiamua kuchukua roho yako leo, ukiona mwenzio amefanikiwa mshukuru mungu na be proud ndio maisha yanavyoenda wapendwa, angalieni wahindi kila sehemu duniani wako nawamesimama kwa miguu yao siyo kwa midomo mbarikiwe

    ReplyDelete
  20. Punguzeni bei ya hiyo nazi ya 2.99 kwani TESCO hawapo mbali na bei yao ni 1.99. Michuzi usibane hii plz

    ReplyDelete
  21. Duka Bomba na Bidhaa zipo. Tatizo nyie watu wa Bongo hamtengenezi bidhaa zenye viwango vya kimataifa. Sasa basi, tunawaomba wasomi wetu ambao hambebi maboksi kama sisi muanze kutengeneza vitu venye kiwango sio kusema tu weka bidhaa za bongo - aweke nini? Maharage ya mbeya kwenye gunia? Huku ulaya bwana vitu vinapimwa sio mambo ya kutandika gunia ukaanza kuuza nyanya. hongera Mdau wa Reading keep it up!

    ReplyDelete
  22. mungu hakuwaweka uk kwa bahati mbaya anamakusudi, mguu wako utakapokuwa ndio liziki yako ipo, wewe unafikiri ambao wanamaduka hawajaenda shule? i feel sorry for you, be your own boss. I'm proud of you bro keep it up! we love you guys and don't let anyone put you down, work hard as you always do, but usisahu kusali may be iko siku utafungua supermarket

    ReplyDelete
  23. mungu hakuwaweka uk kwa bahati mbaya anamakusudi, mguu wako utakapokuwa ndio liziki yako ipo, wewe unafikiri ambao wanamaduka hawajaenda shule? i feel sorry for you, be your own boss. I'm proud of you bro keep it up! we love you guys and don't let anyone put you down, work hard as you always do, but usisahu kusali may be iko siku utafungua supermarket

    ReplyDelete
  24. mungu hakuwaweka uk kwa bahati mbaya anamakusudi, mguu wako utakapokuwa ndio liziki yako ipo, wewe unafikiri ambao wanamaduka hawajaenda shule? i feel sorry for you, be your own boss. I'm proud of you bro keep it up! we love you guys and don't let anyone put you down, work hard as you always do, but usisahu kusali may be iko siku utafungua supermarket

    ReplyDelete
  25. Hongereni sana.Safari huanza na hatua moja. Hata Mbuyu ilianza kama mchicha

    Mpiganaji mzalendo- Tabora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...