ankal akiwa north london kwa mdau mjasiriamali Pompy alieachana na boxi ili kujiajiri katika duka lake la P&P Collections lililopo 447 Eastham, High Street North, ambapo ni mmatumbi pekee anayefanya biashara hii. Namba yake ya simu ni 07990 873392 wakati email ni pnpcollection@gmail.com
mdau pompy akiwa golini kwake
ankal anaambulia kiwalo cha ze fulanazzzzz ikiwa ni asante P&P collection
viatu na moka na vya kuchumpa kibao
viwalo mbalimbali

majaketi ya kufa mtu...





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. safi sana, big UP brother!

    ReplyDelete
  2. hayo majaketi ya KUFA M2 ndo ukivaa unakufa au?...hahahahhaa

    ReplyDelete
  3. Hongera Pompy, and all the best. Mwenyezi Mungu akuzidishie baraka ili ufanikiwe na biashara yako.

    ReplyDelete
  4. duke kama la pailonga kabisa

    ReplyDelete
  5. mbona wewe pompy ndio unakwenda front-Pailonga yuko wapi?

    ReplyDelete
  6. ankal hilo duka mwambie jamaa aje kufungua bongo, mbona kama hayo mwenge yapo mengi tu. aache kasumba kuwa ulaya ndo kuna maisha mazuri. kwa hilo duka na life style ya huku hapo ni kama chinga tu. alete mtaji afungue huku ili achangie pato la taifa na kutoa ajira kwa ndugu zake. WEWE KAMA MBAU WA DIASPORA 2 UNAWASHAURI NINI VIJANA KAMA HAO AU UNAISHIA TU KUPIGA KONOOOOOOOOOOOOOOOZ.

    ReplyDelete
  7. hongera Ahmed.

    ReplyDelete
  8. POMPY: Hii ze fulanazzz ninayokupa ndiyo malipo yenyewe ya kunirusha kwenye blog ya jamii

    ANKAL: OK mkuu, lakini hata usingesema ndiyo maana yake na wadau wameshajua ni hivyo.......

    ReplyDelete
  9. Mkuu unastahili Hongera sana, Hongera sana Mungu akuzidishie uzidi kupeperusha bendera ya Bongo vema. ‘’Keep it Up Mkubwa”.

    ReplyDelete
  10. Ankal usitake kupotosha maana ya msamiati wetu: kubeba box ni kubeba box - kila unachofanyia ughaibuni hata kama ni urais (kama alivyo ndugu yetu bo)vyote ni kubeba box! Wadau mnasemaje?

    ReplyDelete
  11. Kweli kazi za nje hata Obama ni Mbeba Box la Marekani. Na huku kwetu ni wala vumbi ila jamani wacheni wivu Huyo anapata pesa zaidi hapo kuliko wivu wako unaosema machinga machinga ndio yeye machinga wewe utabaki tu kutype hapo huna moja unasubiri Kukaa kwa Wazazi wako mpaka miaka 40 sasa inakupita hapohapo, Kazi yako kunungunika.

    Ndosi.

    ReplyDelete
  12. Mbona vitu vyenyewe kaa vya kwetu Kariakoo yaani made China..Bora urudi ufungue bongo tu!

    ReplyDelete
  13. Ambacho wamatumbi wala vumbi wa Bongo wanashindwa kuelewa ni kuwa m'beba box hupata kipato halali. hakuna kupunjwa wala kukwepa ushuru au kodi. Ni hakki bin hakki! Hakuna wiiz! Hata kama unauza products za China Ughaibuni ndugu yangu, bado ukweli unabaki palepale kuwa bila wiiz au kufahamiana (au kula pamoja) na watu wa mapato mtu hawezi kufanikiwa hiyo nchi ya vumbi. Jamaa keshakupiga gepu huyoo, mtabaki kulalama tu. Kodi ya hiyo kabine ya mwezi m1 tu inalingana na kipato chako cha miaka mitatu kudadeekk!!

    Dayaspora

    ReplyDelete
  14. Hongereni sana, lakini mbona kibao kimeandikwa "unisex" halafu ndani nguo za kiume tu?

    Halfau we mdau hapo juu, hujui kuwa siku hizi dunia nzima bidhaa zinatoka China? Kwani uliambiwa huku Ulaya/ Magharibi ni Mbinguni? Ni watu wa kawaida kama wewe, wala si kwa ajabu

    ReplyDelete
  15. Bwa Michu, East Ham iko East London; sio North London. Labda umechanganya na jina la mtaa wenyewe duka lilipo; High Street North (of East Ham).

    ReplyDelete
  16. na mke ndo keshaacha!

    ReplyDelete
  17. Rocawear Nyekundu ya Kike hapo mbele yako imetundikwa huioni?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...