UBUNIFU ZAIDI UNAHITAJIKA
UWAVUTIA WATALII WA KIMAREKANI
Na Ripota wetu, New York
Na Ripota wetu, New York
Kila mwaka katika jiji la New York hufanyika onesho la utalii la kimataifa maarufu kama ‘ The New York Times Travel Show”. Kwa mwaka huu onesho hilo ambalo ni la saba lilifanyika mwishoni mwa wezi wa February na kushirisha Mawakala wa Makampuni ya Utalii na Usafirishaji zaidi ya 500 kutoka nchi 150.
Nchi hizo zinawakilisa mabara ya Afrika, Asia, Australia, Pasifiki ya Kusinim Kanada, Visiwa vya Karibian, Ulaya, Mexico, America ya Kati na Marekani na yalifanyika katika Ukumbi maarufu wa mikutano na Maonesho wa Jacob K. Javits.
Baadhi ya mawakala walioshiriki onesho hiyo kutoka Afrika, walikuw ani kutoka mashirika ya Umma kwa maana ya Tanzania Tourist Board na TANAPA kwa upande wa sekta binafsi walikuwa kampuni ya BONGO Tours and Safari ambayo Meneja wake Mkuu ni Bi Fortunata Temu. Halikadhalika kulikuwa na wakala kutoka Zanzibar Bw. John Malongo.
Wakitoa maeoni yao kuhusu onyesho hilo na ushiriki wa Tanzania, mawakala ho kutoka Tanzania waliezea kuridhishwa kwao na kwa jinsi walivyotembelewa na wateja wengi walionyesha hamu ya Tanzania Bara na Visiwani kujionea na kufaidi utajili wa mali asili na pwani za kuvutia ambazo Tanzania imejaliwa.
Mmoja wa washiriki wa onesho hilo ambaye ni wakala wa kujitegemea katika masula ya Utalii, kutoka Zanzibar Bw. John Malongo , amemweleza mwandishi wa taarifa hizi kwamba, tofauti na mwaka jana, mwaka huu wateja wengi wametembelea meza ya Tanzania na wameonyesha hamu kubwa ya kuja nchini mwakani.
“ Hii ni mara yangu ya pili kushiriki maonesho haya, ninachoweza kusema, mwamko wa mwaka huu ni mkubwa sana, watu ni wengi na wakiingia tu wanauliza Meza ya Tanzania iko wapi na wamefika kupata taarifa na wameonyesha nia kubwa ya kuja kutembelea vivutio vyetu vya utalii hasa kuanzia mwaka ujao, na hii ni faraja kubwa sana” akasema Bw, Malongo
Akasema kuwapo kwa uwingi wa watu waliojitokeza alijikuta yeye na wenzake wakipungukiwa vipeperushi na majarida yaliyokuwa na taarifa mbalimbali viliko vitutio vya utalii, aina ya huduma na namna ya kufika huko.
Akijibu swali ni taarifa za namna gani ambazo watalii watarajiwa walikuwa wakizitaka. Bw. Malongo anasema kwamba wateja wengi walikuwa wakitaka kujua taarifa kuhusu Serengeti, Ngorogoro, Mlima Kilimanjaro, kwa upande wa Zanzibar walikuwa wakiuliza majengo ya kihistoria na Beaches na walitaka kujua kama tuna Hoteli za Nyota Nne na Tano.
“ Kwa kweli kuna mwamko mkubwa kwa watalii wa Marekani kuja nchini mwetu, na cha kufurahisha zaidi hivi sasa ukiwaambia Mlima Kilimanjaro uko Tanzania hakuna anayebisha tofauti na miaka ya nyuma ambapo wengi walikuwa wakiamini kwamba milima uko nchni Kenya.”
Naye Bi Fortunata Temba, kutoka kampuni ya Utalii ya Bongo Tours and Safaris.yeye pamoja na kuunga mkono maoni ya Bw. Malongo kuhusu kujitokeza kwa wageni wengi katika meza ya Tanzania, yeye amesema bado Tanzania inayo nafasi kubwa ya kuwavutia watalii wa kimarekani ilimradi juhudi na ubunifu zaidi ufanyike.
“Ni kweli tumepata watu wengi walioitembelea meza yetu, lakini nimejifunza kitu kimoja, bado tunasafari ndefu ya kuvuna soko hili la Marekani ambalo linaushindani mkubwa sana. Angalia washiriki waliojaa hapa kutoka mataifa mbalimbali. Tutakuwa tunajidanganya kama hatujajitahidi kubuni mbinu zaidi za kuvutia watalii kuja Tanzani” anasema Bi Temu.
Na Kuongeza, tunahitaji kushiriki kwa wingi hasa sisi sekta binafsi, kama unavyoona hapa tupo wawili wa kutoka Tanzania ukiacha hawa wa mashirika ya umma na wengine wawili ambao ni wa hapa hapa Marekani.
Anaongeza kuwa kama kweli Tanzania inadhamira kubwa ya kunufaika na soko la Marekani, Tanzania inatakiwa kuwa na Banda lake ni si meza . “ hapa tulipo kwa kweli si Banda la Tanzania, tumekaa kama sehemu ya mawakala kutoka Afrika. Tulihitaji kubwa na Banda maalum kama lile la Afrika ya Kusini. Bado tuna safari ndefu”
Akasema eneo jingine ambalo mawakawala wa utalii wanatakiwa kujifunza ili kupanua wigo wa soko ni pamoja na aina ya vipeperushi na majarida ya utalii wanayoyaanda na vitu kama mavazi yanayomtambulisha kuwa yeye ni niwakala kutoka Tanzania.
“ Tunajitaji kuwa wabunifu zaidi , angalia hata mavazi yetu hayatutambulishi tunatoka wapi, wengine wamevaa suti, na aina nyingine ya mavazi ambayo si kielelezo cha utaifa wetu wala kile tunachokitangaza. Kama si haya mabango si rahisi kwa mgeni kubaini kwamba sisi tunatoka Tanzania. Tofauti na wenzetu wa Kenya au hata Afrika ya Kusini wanamavazi yao ambayo ukiona tu unajua hawa wanatoka wapi” anasema Bi Temba.
Eneo jingine ambalo anasema linahitaji kuendelezwa na kutiliwa mkazo ni utoaji wa huduma ( Hospitality). Anasema bado eneo hili halijaendelezwa vya kutoka, kwani namna unavyomkaribisha mgeni, unavyozungumza naye, unavyojibu maswali yake, unavyojichukua wewe mwenye ni sehemu muhimu sana katika sekta ya utalii.

kwa wale vijana enzi hizo tunatafuta wazungu dar tunapiga sink pale kisutu,mzee mamko wa ponya mzee pwele mzee wa totozzzz,hapo a-town mzee noman kwa mashele huuuuu hiyo mzee victor tom koks,adili,hahahha sitaki kumalizia pwele utamalizia maisha ni story ndefu,
ReplyDeletemdau hollwood,TKS 56
Hii habari nimeipanda lakini imenisikitisha.
ReplyDeleteYani Tanzania na ukubwa wake na utitiri wa makampuni ya utalii ni mawakala wawili tu walituwakilisha? na bado tunasikia soko la Marekani ndilo linaloongoza kwa kutoa watalii duniani; au niseme wamarekani ndio wanaoongoza kwa kusafiri.
Ninadhani TTB na TANAPA wanahitaji kuwahamasisha wadau wa utalii (hasa sekta binafsi)k.v. Mahoteli, Makampuni ya utalii, makampuni ya ndege, wamiliki wa vivutio binafsi n.k.
Pia washiriki wanaotuwakilisha huko wajue hawaendi kutembea, wala hawaendi ili wapate posho kutoka maofisini kwao ili wakirejea nchini waje kununua nyumba au gari jipya; wanatakiwa watambue wanaenda vitani, au kwenye michuano mikali. Wanaenda kugombea soko. kila mtu anayekwenda huko kwenye maonesho huwa amejipanga.
Kwa mfano kwenda bila ya vipeperushi vya kutosha ni uzembe. Sawa hawakujua kama watu wangeonesha mwamko na meza ya TZ. Lakini mnapobeba vipeperushi vichache ni lazima muwe na mpangilio wa dharura - pesa ya dharura na nakala laini(soft copy) ili mkiishiwa mtu mmoja anachomoka maramoja na kwenda kuchapisha vingine, hata kwa mkopo. Biashara italipa tu. matokeo ya Maonesho ya mwaka huu yanaweza yakaonekana baada ya mwaka mmoja au miwili, sio mwa huu huu.
Pia wanaoenda huko wawe na uelewa mkubwa wa bidhaa wanayoenda kuitangaza. Na hao wanaowateua watu wa kutuwakilisha huko wateue kutokana na uelewa wa mtu na bidhaa inayoenda kutangazwa, na SIO WATEUE KIUPENDELEO.
Mtu hajui A wala B kuhusu destination TZ halafu anakurupuliwa kwenda kuitangaza TZ. Akifika huko wateja wakimwuliza "haya ndugu umekuja na bidhaa gani mpya mwaka huu?" mtu anabaki anajiuma-uma!
Au mtu anaulizwa... "unafikiri kwanini mtu aje kutalii TZ na sio Kenya? au kwanini mtu aje ZNZ na asiende Sheli Sheli?" Mtu hawezi kujenga hoja!
Jamani, swala la kuitangaza TZ sio kuwa na Vipeperushi, vijarida, banda badala ya meza, au kuvaa nguo ya aina fulani. Kutangaza bidhaa yoyote kunahitaji uhodari, uelewa wa bidhaa yenyewe, na umahiri wa kupiga domo. Hivyo vingine vinafuata baadae.
Pia wahusika wasiishie kwenye meza/banda tu. Wawafuate hao mawakala wakubwa kwenye vilabu na migahawa, wachape nao porojo, wawafanye kuwa marafiki, kisha waombe apointimenti nao baada ya maonesho - hata miezi miwili au mitatu baada ya maonesho. Sio mtu unatoka kwene maonesho halafu husafiri tena kwenda kufuatilia ma-supplier uliowapata.
Anyways, mimi sio mtoa mada ni mchangiaji tu.
Na Huyo Ndio Bw John Malongo kutoka Zanzibar eyee?
ReplyDelete