marehemu Bona Max ni wa kwanza kushoto waliochuchumaa.
HABARI ZINASEMA WINGA MACHACHARI WA YANGA ENZI HIZO, BONA MAX, AMEFARIKI DUNIA IJUMAA USIKU HUKO AFRIKA KUSINI. CHANZO CHA KIFO CHAKE HAKIJATHIBITISHWA, ILA DADA WA MKE WAKE MAMA GERE AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO NA KUELEZA ALIKUWA AKIUMWA.
MAMA MAGERE AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII SASA HIVI KWA SIMU KWAMBA MIPANGO INAFANYWA KUULETA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI SIKU YA IJUMAA IJAYO NA KWAMBA MSIBA UKO TANDIKA SOWETO.
MAREHEMU BONA MAX ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI WAKE WA KUCHEZA WINGA YA KULIA KWA UHODARI NA KASI YA AJABU, PAMOJA NA MAJALO ZILIZOZAA MAGOLI MENGI YA YANGA ENZI HIZO.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI - AMIN


nimepokea habari za kaka Max kwa msituko mkubwa sana kaka yetu mpendwa Max tutakumbuka naima ulala mahali mapema amen,
ReplyDeletemdogo wako Manchester.
WATOTO WA VICTOR HAO.
ReplyDeleteRIP BONA MAX . NAAMINI HII LILIKUWA MIAKA YA 70, HASA 1974/75
ReplyDeleteRIP Bona Max.
ReplyDeleteThat is the Young Africans I used to love.
The years should read 1970s and not 1980s.
Anyway, again RIP Bona Max.
RIP my friend Bona Max. Mimi nilikuwa rafiki yake Bona na classmate wake 1968 -1971 at St Joseph's Forodhani Sec School. The funny thing is back then tukicheza ndiki(soccer pickup game) Bona alikuwa Simba halisi like me so we always played on the same side
ReplyDeleteAzania Bitoz
Huyu Sio Baba yake Oscar BomaMax kweli? Mtoto wa Temeke?
ReplyDeleteRip Bona max imekuwa pigo kubwa hapa cape Town wiki iliopita wamefariki watanzania 7 kwa ajali wengine na mmoja kachomwa kisu na Baba mwenye nyumba wake na mmoja kafa kwa stroke basi balaa tu lakini mungu atajalia tutawarudisha wote tz
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteHiyo picha Yanga ilikuwa Brazil 1974 ilienda kwa kujiandaa na mashindano ya Klabu bingwa Tanzania wakati huo ilikuwa ni knock out si ligi kama ilivyo sasa na ilikutana na Simba kwenye fainali uwanja wa Nyamagana Mwanza na yanga walichukua hilo kombe kwa kuwafunga Simba goli 2-1 na katika mchezo huo nafikiri Marehemu Bona max alikuwa ndiye mchezaji aliyekuwa na umri mdogo zaidi ya wote waliocheza mchezo huo na aling'ara vizuri mechi hiyo kiasi ambacho Mohamedi kajole "machela" beki mkali alikuwa uchochoro hata kufikia kumvuta bukta hiyo ndio hasa mechi iliyomfanya ajulikane na akumbukwe hata leo kwenye fikra za wapenda soka hasa kwa wakati ule wa mwanzoni mwa miaka ya 70.
Kama kumbukumbu yangu imepinda sehemu wadau mnaweza kuionyosha.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - AMIN