Video ya Martina akiwa jukwaani Italia
kwenye sherehe ya Kinamama

Martina anavyoonekana leo akiwa na umri
wa miaka 19 akiwa na Tuzo yake ya Zeze
aliyokabidhiwa na mfuko wa utamaduni Tanzania
Martina wakati huo akiwa na umri wa miaka 4 akiongoza wenzie kuimba wimbo wa 'Tanzania eeee' katika tamasha maalum la watoto liliofahamika kama ZECCHINO D’ORO katika mji wa Bolognia nchini Italia mwaka 1995

"....Tanzania eee,
Nchi yangu eeeeee,
yapendeza eeeeee,
karibu muioneeee,
Sura yake yavutiaaa,
kila konaaaaaaa,
kwa maziwa na bahari,
nchi kavu na mipakaa….."

Hii ni sehemu ya wimbo maarufu sana ambao ulitokea kupendwa na watu wengi ndani na nje ya nchi katika miaka 1994 na 1995, wakiwemo zaidi watoto, vijana na hata watu wazima.


Nyakati hizo vituo mbalimbali vya Televisheni na Radio vilikuwa vikiupiga wimbo huo na vipo ambavyo vilikuwa vikiutumia wimbo huo kuwavutia watoto ambao walikuwa wakialikwa kushiriki katika vipindi vyao vya redio na Televisheni ambavyo moja kwa moja vilikuwa vikishirikisha watoto.

Martina na wanafunzi wenzie shule ya chekechea ya Clara Kawe, Dar
Na Ripota wetu

Sababu kubwa ambazo zilichangia watu kuupenda wimbo huo ni mbili.
Mojawapo ni kwamba wimbo huo unasifia kwa uhalisia wake rasilimali zilizopo nchini ambazo pindi watu wakitembelea wanaweza kunufaika kuziona, pamoja na uzuri wa Taifa la Tanzania ambalo limejaaliwa duniani kuwa na vivutio vya kila aina vikiwemo mbuga za wanyama, ardhi zenye rutuba, maliasili kama madini ya thamani na kadhalika.

Sababu nyingine ya pili ambayo iliwafanya watu kuupenda sana wimbo huo ni kutokana na ukweli kuwa uliimbwa na mtoto mdogo wa miaka minne kutoka barani Afrika tena nchini Tanzania ambapo pia alilenga kuisifia nchi yake.
Hapa namzungumzia Martina Chambiri ambaye miongoni mwa watanzania wengi jina hili siyo geni, Martina aliimba wimbo huo katika tamasha maalumu la watoto liliofahamika kama ZECCHINO D’ORO ambalo lilifanyika nchini Italia katika mji wa Bolognia mwaka 1995.

Tamasha hilo liliwashirikisha watoto wa umri wake kutoka nchi mbalimbali duniani na wimbo huo wa Tanzania ambao yeye alifanikiwa kuuimba ukaingia tano bora na kushika nafasi ya tatu.
Martina akipongezwa na Profesa Philemon Sarungi, Waziri wa Elimu wakati huo ambapo alikwenda kukabidhiwa bendera ya Taifa akiwa mwakilishi wetu katika tamasha la watoto. Hii ndiyo ilikuwa safari yake ya kwanza kati ya tatu alizofanya.
Martina Chambiri alizaliwa Januari 1990 katika hospitali ya Aghakan jijini Dar es salaam, wakati akiwa na umri wa miaka minne alianza chekechea katika shule ya Masista ya Clara Nursery School, iliyoko Kawe ambako ndiko nyumbani kwao.

‘’nakumbuka tulikuwa shuleni Sista akasema kuna mashindano ya kuimba, hivyo tukashindanishwa wote na mimi pale shuleni nikawa mshindi na hivyo kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo’ Anasema.

Anasema anachokumbuka zaidi ni kwamba wimbo huo ulitungwa na mwalimu wa muziki katika shule hiyo aliyekuwa akifahamika kama mwalimu Julius Kapinga, na hatimaye yeye kufanikiwa kuuimba kwa ufasaha.

Anasema wimbo huo aliweza kuuimba kwa lugha mbili yaani Kiitaliano na Kiswahili, ambapo sehemu ya kiitaliano ilitungwa na waandaaji wa shindano hilo wakiongozwa na mama mmoja kwa jina la Mariella ambaye kwa sasa ni Marehemu.

Martina katika mahafali ya kidato cha sita Shule ya sekondari Loyola na mdogo wake Lilian Chambiri (shoto) na ndugu yao. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza pointi 14 na anasema wakati huu akisubiri majibu ya kidato cha sita anategemea kufanya vyema.

Anasema kabla ya kufanyika kwa tamasha hilo ilibidi aende Italia kwa ajili ya kujifunza na kuchanganyika na washiriki wenzake ikiwa ni pamoja na kuimba kwa kupokezana kwa kuwa alikuwa akiimba Verse na wenzake wakiimba Chorus.
Anasema pia katika safari hiyo ya kwanza alikuwa akifundishwa jinsi ya kulitawala jukwaa wakati anaimba , ikiwa ni pamoja na kuzoea kuimba kwenye umati mkubwa wa watu.

Martina anabainisha kuwa alitakiwa tena kurudi Italia mwaka huo huo kwa ajili ya Tamasha lenyewe ambapo Tanzania ilishika nafasi ya Tatu, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Pedro(Costa Rica), na mshindi wa kwanza akiwa Eugenia(Russia).

Aidha anasema alitakiwa tena kurudi tena Italia kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la wanawake lililofahamika kama Women’s Festival ambapo alialikwa kutumbuiza na kwa mara nyingine akafanikiwa kukonga nyoyo za watu wengi.
Martina na wenzie huko Italia
‘Baada ya kumalizika kwa matamasha hayo nchini Italia, niliporudi hapa nyumbani bado nilikuwa na shauku kubwa ya kuimba na hatimaye kutaka kuendeleza kipaji changu kwa sababu ninaweza kuimba na ninapenda sana”. Anasema.

Anasema alikutanishwa na baba mmoja anayemkumbuka kwa jina la Gideon ambaye alimtungia nyimbo 6 zote zikihusu mazingira na zote zikarekodiwa na kisha kutengeneza album moja.
‘sababu kubwa ya kutungwa kwa nyimbo hizo zikiwa na mada kuhusu mazingira ni kutokana na kutaka kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa faida ya vivazi na vizazi’. Anasema.
Baada ya kuimba nyimbo hizo za mazingira, sauti ya Martina ikawa haisikiki, mpaka mashabiki wake wakawa wanajiuliza kulikoni, maana wengi walikuwa na shauku ya kufahamu hatima yake katika tasnia hii ya uimbaji na hasa kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha katika matamasha yaliyofanyika nje ya nchi.

Kilichogundulika baadaye ni kwamba ulikuwa ni wakati ambao alitakiwa kuanza shule, hivyo mawazo yake mengi ikabidi yahamie shuleni zaidi kuliko kuimba hivyo akaanza shule ya St. Constantine iliyoko Arusha, na kujikuta alipoanza darasa la kwanza akarushwa darasa hadi darasa la tatu.

Martina akiwa na wazazi na mdogo wake Lilian
Aidha baada ya hapo wazazi wake wakaamua kumhamisha shule hiyo na kumuandikisha shule ya St. Mary’s Tabata, na kisha kumalizia darasa la saba katika shule hiyo hiyo eneo la Mbezi Beach.Anasema pamoja na kufaulu vizuri kujiunga na shule za serikali, lakini wazazi wake waliamua afanye usaili katika shule za Marian, Kifungilo na St. Francis, alifanikiwa kupata nafasi katika shule ya Marian na kisha kuanza kidato cha kwanza na kufanikiwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2007.
‘nilipenda sana masomo ya biashara, nilipomaliza kidato cha nne nikafaulu kwa kupata daraja la kwanza pointi 14 na masomo ya Hesabu, Commerce na Book-keeping nilifaulu vizuri , na kwa kuwa niliyapenda nikaamua kusomea masomo hayo kidato cha tano’. Anasema.

Binti huyo anasema anafurahia kuwa wazazi wake walikuwa hawamlazimishi kusomea masomo ambayo hataki isipokuwa hawakusita kumpa ushauri kwa kile ambacho yeye alikuwa anachagua kukifanya.

‘baba yangu alikuwa akipenda sana niimbe na pia nishiriki kwenye michezo, na mimi napenda sana michezo na hasa kuogelea, ila mama alikuwa akiuliza ni kwa nini nisisome masomo ya Sayansi, ila masomo ambayo nilichagua walikubaliana na mimi kisha wakaniambia niyasome kwa bidii ili niyafaulu vizuri’Anafafanua.

Anasema alipomaliza kidato cha nne akafanya usaili Loyola Sekondari na kufanikiwa kupata nafasi kwa ajili ya kujiunga na kidato cha tano ambapo mwezi uliopita alifanya sherehe na wenzake kwa ajili ya kumaliza kidato cha sita.

Aidha mhitimu huyo wa kidato cha sita anasema kuna tofauti kubwa kati ya shule ya bweni na kutwa kama alivyojionea Marian na Loyola kwa kuwa Marian ilikuwa ni wasichana watupu na Loyola ilikuwa mchanganyiko, lakini jambo la msingi ilikuwa ni kuhakikisha anasoma kwa bidii.

Martina anasema jambo muhimu ambalo anamshukuru mungu ni kumpatia wazazi ambao walishirikiana kumpatia malezi mema, na pia walimjengea misingi ya kumpenda mungu na hivyo kumuwezesha angalau kufikia sehemu ya malengo yake.

Lakini anasema katika maisha yake aliwahi kupatwa na mshituko mkubwa sana alipopata taarifa ya kifo cha baba yake mzazi mwaka jana kilichotokana na ajali ya gari huko Lindi.

‘ulikuwa ni mshituko ambao siwezi kuuelezea, baba yangu alipenda sana maendeleo yangu, na alikuwa anaeleza ni jinsi gani anajisikia fahari kuwa na mtoto kama mimi, lakini hakuna jinsi ni mipango ya mungu. Namuombea mungu ampumzish kwa amani” Anasema.

Ukifanikiwa kukutana na Martina Chambiri hutaweza kuamini kuwa ni yeye alililetea sifa kubwa taifa hili kwa kufanikiwa kupeperusha bendera ya Tanzania nchini Italia na pia alikuwa ni mshiriki pekee kutoka bara la Afrika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. du hongera dada umetoka mbali, all the best for the future and sorry about your Dad, may he RIP.

    ReplyDelete
  2. uwiiii jaman huyu mtoto ndo amekua hivyo?aisee miaka inakimbia kweli nshazeeka!anyways baangaa she can still do it.

    ReplyDelete
  3. Aise ankal, ungetutaftia kijiclip kaule wimbo bwana utuwekeee kidgo. Tanzania eeeee, totomela aaaaa, akupnda fwaiiiii, sijui nininini...

    ReplyDelete
  4. Ankal, naomba uwasiliane na mama Chmabiri (mama yake Martina), ikiwezekana watoe CD na DVD ya nyimbo za Martina.. maana nimewahi kuzisikia zikipigwa katika radio..lakini kwa sehemu ndogo tu.. nadhani vema ziwe zinapigwa au kurushwa katika Tv ili watu wajue kipaji cha binti huyu.. nimeona wimbo wa "Tanzania Eh!" katika you tube.. hebu down load na ubandike watu wauangalie..

    ReplyDelete
  5. Hongera Mungu akulinde akuzidishie, uendelee na juhudi zako.Ila Michuzi inaonekana story yote amesimulia mwenyewe kitu ambacho siamini kama anaweza kukumbuka yote hayo katika umri wa miaka minne, pili hajatumabia Kidato cha sita amefauru kwa kiwango gani. Otherwise kila la kheri dada.

    ReplyDelete
  6. Wadau,kiukweli ni hivi karibuni tu nilikuwa najiuliza ni wapi alipo huyu binti? na yule kijana aliewahi kushinda tuzo ya muziki marekani? alitunga wimbo kwa jina la My passion.Vibaji vimepotea,je Martina alikuwa na kibaji au zali la kitoto tu?

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Martina ulifanya kazi nzuri sana. Je bado unakumbuka kiitaliano? mana kuna perfomance moja ulikuwa unahojiwa kiitaliano, na ulijibu vizuri mpaka nilishangaa.

    ReplyDelete
  8. Mmh!huyu sio mdogo wake Elizabeth Chambili kweli?

    ReplyDelete
  9. DUH TANZANIA WALAHII, SIJUI CHA KUSEMA, SOMETIMES UNAZALIWA SEHEMU KAMA USINGEZALIWA HAPO, MUNGU BADO YUPO NAWE DADA, KEEP IT UP.

    ReplyDelete
  10. kingwendu jr.March 15, 2010

    Haya hiyo ndiyo tanzania, vijana kama hawa ndiyo serikali ingeweza kuwasaidia na kuwaendeleza vipaji vyao, lakini serikali wala haishtuki na chochote, juu ya kwamba aliiwakilisha nchi na kuiletea sifa, sasa mnategemea kutakuwa na uzalendo wa mtu kuipenda nchi yake?
    hiyo ndiyo Tanzania, fadhila ya punda .......

    ReplyDelete
  11. sujaelewa kashinda tena? au ndo mnamrusha tuu?

    ReplyDelete
  12. LMAO...Hahaha!!! Anonymous wa tatu 02:07pm you had me rollin' buoy!!. Automatically siku zote mtu akisikia Jina Martina Chambiri unasikia that song playing in your head!! Amazing!. Tanzania eeeeh!! Tanzania aaaaah!.

    That's a special young lady right there....I see a very bright future ahead of you, young lady. I see her winning presidency of Tanzania, if she wants to run for it.

    Kitu kingine nakumbuka Mike Mhagama, kwenye DJ Show....Ah Ah A D, Ah D, Ah Dj, Ah DJ Show!!!!

    ReplyDelete
  13. wanaotaka kuangalia video ya wimbo huu hii hapa!! http://www.wavuti.com/19/post/2009/12/tanzania-eeh-tanzania-aah.html

    mdau
    Nkya
    A town

    ReplyDelete
  14. Ama kweli kamichuzi umeniliza.

    wimbo huu umenikumbusha mengi yaliyonikuta kwenye maisha yangu, wakati huu mwimbo ndio umevuma sana nyumbani mie nilikuwa na matatizo makubwa sana ambayo nikitizama nyuma nacheka na kufurahi hapa nilipo.

    wakati wa mwimbo huu bwana ambae aliniambia atanioa ndio alienda kuoa bibi mwingine bila ya kuniambia (kisa anadai eti mie wazazi wake wasingenikubali sababu mie mkristo) nikashtukiziwa tu wakati niko kazini na mwenzangu "hivi unajua?" "B/F wako anaoa wikiendi" nilitamani kuruka kilimanjaro hoteli ila nililia sana, mpaka niliokuwa nao jirani walidhani nitajiua.
    mwaka ukapita nikampata mwenzangu mwingine ambae niko nae mpaka sasa lakini mwimbo huu umenitolesha machozi tena.
    Afu jamaa mwenyewe hata hawakudumu na mkewe waliachana baada ya muda akarudi kwangu eti tuoane sasa, mie mmmmh saa hizi jioni ndio unaniona??

    ReplyDelete
  15. YAANI BAADA YA KUONA HIZO VIDEO, MACHOZI YAMENITOKA MTU MZIMA, INAUMA SAANA JAMANI, TANZANIA EEEEH, TUNAPIGWA CHINI SAAANA!!!! WHY JAMANI???? KIPI MUHIMU BASI NCHINI KWETU KAMA SIO KUWAENDELEZA TAIFA LA KESHO? KIKO WAPI SASA?!

    ReplyDelete
  16. Mmmmh!

    Jamani watoto wa siku hizi- wa dot com wanakua haraka!

    Khaa!

    ReplyDelete
  17. Hongera sana dada.
    Mungu akubariki sana.Vipi kanisani huwa unaimba kwaya?
    Ukifanya hivyo Mungu atakubariki zaidi na zaidi.

    Hongereni baba na mama wa Martina,inaonyesha malezi yenu ni safi.

    ReplyDelete
  18. Martina, Mungu akubariki uzidi kukuwa katika kimo na hekima umpendezaye yeye na wanadamu wote wakupende ingawaje ni vigumu, nakutakia heri katika maisha yako. pole kuhusu baba yako.hii dunia ni njia ya kupita tu. uwe na maisha mema.

    ReplyDelete
  19. Safi sana! Ni vizuri kuona Martina anaendelea vizuri. Hapa USA wanamwita 'CHILD STAR'.

    ReplyDelete
  20. Mwaya wasikudanganye dadangu, lile lilikuwa zali la utotoni, bukua mwanetu upate nondo ndo uanze sijui bongo fuleva, so far bado mdogo, ukumbuke hukusoma darasa la II na hata hilo la I ulirushwa tu, usije rudi utotoni kwa kuruka staji moja muhimu. Nasema hivi, soma. Wakware weshakuona, mate nje nje. Utaishia kuuza magazeti ya Udaku sasa hivi.


    Mpg Bx

    ReplyDelete
  21. TeQuann

    Ama kweli wewe ni mswahili sana manake mtu kama Martina Chambiri hata hakukaribishwa na raisi kwa mlo wa ain yoyote lakini alifanya kututangaza sana mie binafsi namshukuru sana.
    Haya kaja Hashim hata ushindi hajaleta nyumbani lakini mikiki yote mlimfanyia, sasa ona. Yote hayo ninakushangaa wewe Tequanne kuandika mambo kama hayo wakati Martina alifanya yote haya kwa mapenzi yake sio kutaka kuwa celebrity wala nini.
    Go crawl under a rock or something mstzzzzzz shukrani huna.
    Martina keep your head up wewe ndio watu tunaokupenda manake unatutangaza bila ya kudai chochote.

    Go Martina go

    Mdau California.

    ReplyDelete
  22. Kingwedu Jr

    Maneno yako ni ya kweli kabisa manake watu huku wanataka mtu kama vile Hashim, hata kombe hajaleta ila vishindo hivyo mmmh wakati martina anatangaza tu jina bila ya kutaka chochote.

    ReplyDelete
  23. Jamani wadau wenzangu andikeni kwa lugha ya taifa viingereza vyenu havieleweki. Hata kama mnaishi ulaya inayonyesha wazi bado mnahitaji kupolish lugha za wenzetu.

    ReplyDelete
  24. huyo mtoto ni talent sana hakuna asiyejua kama alitanga sana tanzania na kusimama kwake jukwani kulichangia kushawishi watalii kuja tanzania kuviona hivyo vivutio,lakini mambo ya TZ jitoe wengine waneemeke, kimtazamo zawadi kubwa ambayo serikali wangempa huyo binti ni offer ya kumsomesha bure tena katika shule yoyote aitakayo any way ndiyo nchi yetu na sijua hata kama mwalimu aliyewashiwishi watoto kuingia katika shindano hilo kama alipewa motisha yoyote au ndiyo iliishia hapo,jamani serikali oneni aibu in my memory huyu mtoto alichangia kushawishi watoto wengi kuonesha vipaji vyao hususani vya uwimbaji,nguzo yake moja imeondoka msaidieni asome.

    ReplyDelete
  25. she was so cute ohhhhhhhhh my Lord look at her now i cant beleave, she is so big and still cute God bless u ma lil sister keep it up and dont give up,sorry about ur dad keep on praying for him its all about god ndio mambo ya dunia alilo panga mungu haliwezi kupanguka but dont give haters chance 2 come near u

    ReplyDelete
  26. Huu wimbo sikuujua ...kipindi hicho ndio niliondoka kuja kuanza masomo huku. Hivyo nikapitwa nao...Ila tuwe Simon cowell. Mimi kwa kuusikiliza huu wimbo nimeona mtotot huyu alikua hana haibu na hilo ndio lilimsaidia lakini sauti ya kuimba nyimbo kweli hana. Afadhali uliamua kusoma na huwezi jua hizo nyimbo zingine zilizotungwa na sauti yake kupotelea somewhere ni kwavile huyo producer aliona quality haikua kama alivyotegemea.

    Kazana na elimu na ujasiri wako utakufikisha mbali...Mimi ningekuambia uwe lawyer...Unaonekana kama unaweza kusimama mbele ya watu na kuongea saana

    Pole kwa matatizo ya yaliyokukuta. Hata mimi nilipoteza baba yangu miaka michache iliyopita na kila nikiwa nafanya tukio muhimu natamani angekua hapa aone mafanikio yangu. Lakini nahisi ndio yeye anawork upstairs for me....

    ReplyDelete
  27. Mdau wa California

    Kha! we vipi, mbona kunishambulia bila sababu ati?. Hebu rudi juu ukasome comment yangu tena kwanza. That was all praise!. I started with LMAO niki refer comment iliyotolewa mwanzo. Where did Hashim get into this? LOL

    Again I say, and I quote what I wrote earlier:

    "That's a special young lady right there....I see a very bright future ahead of you, young lady. I see her winning presidency of Tanzania, if she wants to run for it.
    "
    Nothing but LOVE.

    ReplyDelete
  28. jamani nimekumbuka mbali wakati huo nakula bure kwa baba na mama mambo super cjui kutafuta hata hela. niko shule leo najitafutia maisha mtihani natamani kurudi nyuma kuwa kama mtoto tena nile bure nivae bure nikiumwa nilie baba anikumbatie yaani mpaka nimelia.kip it up martina

    ReplyDelete
  29. Jamani kweli huyo mtoto ni cku nyingi sana, ila nimepotezana na Aunt yake long time anaitwa Gati Chambiri, ningependa sana nipate namba zake za simu kama itawezekana, mi ni rafiki yake wa cku nyingi sana sema tu tulipotezana....

    Mdau

    ReplyDelete
  30. Kaka michuzi umenikumbusha mbali sana,nilikuwa nataka kujua kwa muda mrefu sasa habari za Martina,wakati huo huu wimbo ukivuma sana nilikuwa form 3 naenda form 4.Nilikuwa naupenda sana.
    Nimefurahikufaham habari za Martina Chambiri tena na jinsi anavyoendelea.Nafikiri kama inawezekana tumwone tena kwenye tv atusalimie watanzania pia atupe au atukumbushe kipaji chake,hata wale ambao hawakumwona wapate kumwona.
    Umenikumbusha sana mbali Kaka Michuzi.
    Itabidi niwatafute wadau wa FORM4C1 1997 JITEGEMEE SECONDARY tukumbukie zile enzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...