Mara kadhaa watu wamekuwa wakitoa maoni kuhusiana na vyanzo vya ajali, ikiwemo vyombo vibovu vya usafiri, barabara mbaya, kukosa umakini kwa dereva na kauli chochezi za abiria.

Hili la baadhi ya abiria kuwa ni chanzo cha ajali za barabarani limedhihirika katika ajali iliyotokea mkoani Tanga ambapo wanafunzi wapatao kumi na wanane (18) walipoteza uhai na wengine mia moja, ishirini na watano (125) kujeruhiwa.

Wanafunzi wa chuo Cha Shamsil-Maarif, Dunga - Tanga walikuwa wamepakia lori aina ya Fuso wakitoka katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyokuwa katika kijiji cha Kibafuta.

Inasemekana abiria hao walikuwa wakimshawishi dereva kuongeza mwendo na walipofika sehemu ya kipita-shoto walimtaka dereva kurudia kuzunguka mzunguko huo na ndipo tairi ilipogonga katika kiambaza na kusababisha ajali katika eneo hilo.

Mtembelee SUBI kwa habari zaidi

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. This happens all the time. Nilishapotza cousin wangu kwenye ajali alipokua shule moja hivi huko kwenye milima ua Ugweno au Usangi...Walikua naoa wanatoka kwenye mashindano Moshi Mjini wakamwambia dereva ongeza mwendo na dereva akawasikiliza wakafa sijui ni wanafunzi wengi tu.

    Sijui ni kwanini madereva wanakua hivi au ni kwa vile hawaendi shule ya kujifunza kuendesha. Au hawaheshimu kazi zao.

    Inasikitisha sana.

    lakini hii yote ni kwajili serikali haiwashikilii watu wanaoajiri madereva ushuzi..Ingetakiwa watu wenye mabiashara wanakua liable na kulipa watu au familia za watu

    Halafu hilo lori ni kubwa kiasi gani kubeba watu wote hao?

    ReplyDelete
  2. Ina lilahi wainailaihi Raajiuun,

    I have said it before, and I WONT GET TIRED OF REPEATING MYSELF AGAIN ON THIS.

    FACT!

    In Tanzania you have more chance of dying on a horiffic accident than MALARIA, may be i will stretch it further of dying of AIDS..because you know why? we are so damn smart on these ILLNESSES, WE KNOW THEM INSIDE OUT, THE EFFECTS, THE DRAMA AND EVERYTHING! AND WE ARE MORE CONSCIOUSLY AWARE OF THE DANGER AND THE TRAGIC OF THESE ILLNESSES, WE CAN ALMOST BREATH AND FEEL THEM, RIGHT AT THIS MOMENT, WE ARE TOO DAMN PRETTY GOOD CONSCIOUS OF THEM. BUT ROAD ACCIDENT IT IS A NO! NO! WHO CARES WONT HAPPEN TO US, IT IS ALWAYS WILL BE SOME ELSE IN REMOTE PLACES.

    BUT TO BE HONEST IT(ROAD ACCIDENT) LIKE LION IN A JUNGLE WAITING FOR A PRAY, AND I AM PRETTY SURE WE ARE THE ONE.

    MICHUZI AND GOOD PEOPLE OF THESE BLOG DO TAKE CARE OF YOURSELF. I CANN'T STOP THINKING ABOUT MY FAMILY, BROTHER, SISTERS, RELATIVES, FRIENDS AND THE WHOLE COUNTRY ABOUT THIS. IT MAKE ME LOOSE SLEEP SOMETIME.

    MAY GOD BLESS US! AMEN IF WE DON'T ACT NOW, IT WILL BE TOO LATE BEFORE THE FAMILIES ARE BROKEN, THE DISABLES LEFT ON THEIR OWN, THE ORPHANS BECOME DESPERATE, MAY BE THEN, WE CAN START LIP SERVICE OF MAY BE THEN WE DRUG OURSELF WITH SLOW MOTIONS PUT A LITTLE ADVERTS ON OUR COUNTRY ROAD AND CITIES JUST SIMPY SAYING "AJALI INAUA KULIKO MALARIA!! ENDESHA GARI KWA UANGALIFU", "HAPA CORNER HII WAMESHAKUFA WATU 100 KWA UZEMBE WA BARA BARA" DAMN IS THAT NOT SIMPLE AND COST EFFECTIVE MEANS OF JUST VALUING OUR LIFE, I AM SURE I CAN DO AND WE CAN DO IT. SO DO THE GOVERNMENT, A WARNING AD. COULD SAVE LIFE!

    MUNGU TUBARIKI YA RABI! AMEN ATUPE MAISHA YA SALAMA AMANI, UTULIVU WA MOYO NA AMANI, NA ATUPE UWEZO WA KUFANYA KWA VITENDO KILE KILICHO NA UWEZO NACHO, MUNGU ATUJAALIE TUWE WENYE KUJALI MAISHA YA JIRANI ZETU, YA RAFIKI, NDUGU NA WANANCHI, KITUUME SISI HICHI KAMA NI NDUGU WA DAMU ZETU, AWAPE VIONGOZI WETU, UWEZO WA KUTAMBUA UMUHIMU WA USALAMA BARA BARANI, KAMA UJIRANI WA MIOYO YAO NA VIFUA VYAO.

    ReplyDelete
  3. poleni ndugu wafiwa mungu arehemu wote waliopeteza maisha
    mimi ni mgeni niko kwa wadosi ila nimezunguka kwa barabara zaidi ya states sita huku bwana wata wanajua kukanyaga mafuta yaani spidi mpaka naogopa ila wako makini hakuna dereva anayeruhusu ajali. wanaheshimu si pikipiki si baiskeli si watembea kwa miguu si bajaji wala maloli wote sawa hakuna ubabe na barabarini ni spidi mtindo mmoja na ajabu huwa magari yao hayana side mirror unaovateki kokote (zigzag)wanatumia honi tu infact huwa nafikiri labda wana akili za ziada barabara hazina tofauti saana na zetu
    yaani huwa nasema ingekuwa bongo wangeuana kichizi

    ReplyDelete
  4. ama kumbe waliomba wenyewe??

    afu ilo lori likoje kubeba watu wote hao 143??

    idadi ya watoto wa kiume inapungua jameni!!

    mh

    ReplyDelete
  5. ni jana tu nimepata habari za msiba wa shemeji yangu kutokana na ajali ya barabarani, wahusika sijui wanalichukuliaje hili hali imekuwa mbaya sana tena sana sijui ni ajali ngapi zimetokea kipindi cha wiki mbili,
    si lazima kung'ang'ana na cheo pia kujiuzuru ni jambo jema.AJALI ZIMEZIDI....Mungu awalaze mahala pema peponi.AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...