soko kuu la mji wa tokyo
stendi kuu ya mabasi tokyo
uwanja wa mji wa tokyo
kitongoji cha bagamoyo, tokyo
demokrasia imetawala tokyo
ankal na limo la babu ambalo bado linadunda
ankal na mdau chale rajabu walipogongana tokyo
ufugaji wa kisasa upo tokyo
ankal na wanafamilia baada ya kuzuru makaburi tokyo
hapa tokyo miwa nje nje tu..
ankal moses wa sweden akichuma muwa tokyo
ankal moses akijipendelea
ankal tony na moses wakiangalia mandhari ya mji wa tokyo
ankal tony akitoka kuritachi kwa obama hapa tokyo















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. Ama kweli Waafrika tuna utamaduni wa kupenda vitu vibaya. Yaani hata uwanja wa mpira unatushinda kuutengeneza vizuri! Bongo tambarare!

    ReplyDelete
  2. Ankal mi katika vyote naomba tu mniletee " IMYUBHA- MIWA, na MABIFU- NDIZI KISUKARI" Ndagha musyilile (Poleni na kuzika nyanya yenu)

    ReplyDelete
  3. TULETEE PICHA YA KABURI LA JOHN NA WANAKIJIJI WENZEKE WALIOKUWA WAKIIBA MAFUTA KUTOKA KWENYE LORI LILILOPINGUKA. WENYE NDOO HAYA WENYE VIDUMU HAYA

    ReplyDelete
  4. tokyo tokyo nini jamani huko tukuyu usipaparike na maJINA YA sehemu za watu

    ReplyDelete
  5. Nimeamini kweli ankal Moses anaishi Sweden. Jamani miwa haing'olewi, inakatwa!!!!
    Vinginvyo nimependa mandhari ya uoto na hali ya hewa ya Tokyo, muonekano ni kama wa kwetu Katerelo.

    ReplyDelete
  6. Thanks for nice pictures of Tukuyu. We hail them for eating well balaced diet. Picha ya wanafamilia inaendana na mlo kamili wanaokula. Hongera sana nasi tuige!
    Hata hivyo nawatadharisha watanzania wenzangu kuhusu mila potofu za kudhuru makaburi ya wafu. Hasa Wahehe, Wachagga (Rombo na Kibosho) na Wanyakyusa. Acheni wafu wapumzike tukutane peponi. Mmesikia yaliyotoke Poland uongozi wote umefutika sababu ya kuabudu wafu. Wachagga wengi hufa wakienda au kutoka kujengea makaburi jamani. Wanashehereki kwa bia na nyama hata kama ni vijana wamekufa. Someni maandiko vizuri. Iweje leo huko Mazombe Iringa Makaburi ni mazuri kuliko nyumba za watu. Yanajengwa mithili ya nyumba?? Watu wanalala kwenye Mapagale , za nayasi lakini Makaburi ni ya matofali na tiles. Leave deads to rest in their graves, they are not part of us anymore. Ankal sorry ila tuwe wazi.

    ReplyDelete
  7. mdau 11:00
    umenena wachaga wa rombo wana mila mbaya kuliko watu wote duniani na hata mtu akifa haawogi hadi wazike nahoji je mwanamke akiwa katika siku zake?? hizi mila zinaleta hadi magonjwa !! pumbavu sana!

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa Apr 13, 02:11
    We ndio unaefuata mila usizozijua, si wengine tunafuata jadi yetu na kutambika na kujali makaburi ya waliotutangulia. Hayo maandiko yalitumika kutukandamiza na kutunyanyasa na yanaendelea hadi leo, fungua macho uone. Mwafrika nae ana dini yake ya jadi na mizimu yetu ni sehemu ya dini zetu za jadi...Usipotoke na dini za waarabu na wazungu!!
    Big up dini zetu

    ReplyDelete
  9. yaani ankal umenikumbusha kwetu kabisa .. Bagamoyo nimefurahi sana..... umenikumbusha mama yangu mama Zara ....I miss you mum...,nimemuona ankal wangu chale ,nimemuona sheikh Shida ....namkumbuka sana sana aunt stumai sijui yupo wapi sasa,...ametulea sana,umenikumbusha mwisho wa mji....yaani I cant stand...nimefurahi sana...nimeona soko lililotukuza,nimeona kiwira wakati ule tulikuwa tunapaita mia zoteee...thanks my dear..nimefurahi mnooo.......

    ReplyDelete
  10. Brother Michuzi asante kwa kuchapisha maoni yangu kuhusu Mila potofu za kuzuru makaburi ya wafu japokuwa zimekinzana/negative na yale unayoamini. Kweli blogu yako ni ya ukweli na uwazi kwa kila mtu. Nakutakieni safari njema ya kurudi DAR ES SALAAM wewe na rafiki zako na PIA maisha memma kwa familia yako.
    Wako mwanamtandao Richard Mazingira
    richardmazingira@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  11. Ankal...nimefurahi sana sana kuona kwetu kabisa......umenikumbusha mtaani kwetu nilikokulia Bagamoyo ,umenikumbusha sana mama yangu Mama Zara,...I miss you mom...nimemuona uncle Chale umepiga nae picha,nimemuona Sheikh Shida,nimemuona aunt Situmai ametulea sana sijui yupo wapi siku hizi...umenikumbusha mwisho wa mji...kiwira mia zoote wakati ule...I cant stand ...nimefurahi mno....Thanks a lot ankal...

    ReplyDelete
  12. ANKO MBONA ZE FULANAZZ BADO IPO! AU ILIKOSA MTEJA?

    ReplyDelete
  13. Ankal,, i thought ze Fulanaz went for ze mnada.. natafuta fulana kama hiyo,, nitaipata wapi
    Mdau,, Costrori

    ReplyDelete
  14. jamani tukuyu ,naona hapo maankal wako landmark hotel kwenye cannopy,opp na laxmi hotel

    uncle ndizi hapo unaponunua ni kiwira ndio kuna vindizi vya kuiva vingi

    nimemiss tukuyu na vitongoji vyake vya bulyaga,mabonde, ushirika,ndaga ,kiwira hali ya hewa nzuri sana

    ReplyDelete
  15. Mdogo wangu michuzi usifikiri kila kitu basi kinachekesha, mbona majina yetu mazuri tuu. kwa nini uite tokyo, ili iweje kama sio ushamba tu. Mara ukaenda reading UK unadai mji wa kusoma? tafuta vitu vya kuchekesha maana kwa mwendo huu utaharibu sifa kubwa ulioijengea blog yako. Binafsi naipenda kazi yako ila hizi lugha ulizokuja nazo hazivutii, Tukuyu ni tukuyu sio tokyo, who cares abot tokyo anyway? Jirekebishe Michuzi sometimes unabore.

    ReplyDelete
  16. What a beatifull contry, wangekuwa wazungu ndio wanaishi kwenye mandhari nzuri hivyo mbona mngependa? waafrika kweli tuna vitu vizuri basi tu hatujui namna ya kuvitumia

    ReplyDelete
  17. Uncle Michuzi leo umenifurahisha kweli. Kukaja kutukuju ndio moyo uliko. Asante kwa picha nzuri za nyumbani. Ndaga fijo malafyale.

    ReplyDelete
  18. mtoa maoni unayelalamika kuhusu tokyo mbona hata dar es salaam ni jina la mji huko united arab emirate?acha chuki za kijinga

    ReplyDelete
  19. Picha murua hizi kaka, umenikumbusha TKY!
    Ahsante sana!
    Maggid

    ReplyDelete
  20. TUKUYU NI KATI YA WILAYA CHACHE KABISA HAPA TZ AMBAZO MAZINGIRA YAKE NI KAMA ULAYA ULAYA

    ReplyDelete
  21. du kweli tukuyu kuna neema ya vyakula

    ReplyDelete
  22. UGONILE ANKAL!

    ReplyDelete
  23. nimetamani ndizi na katapela

    ReplyDelete
  24. jamani kumbe michuzi ni mny"akyusa nilijua ni mzaramo

    ReplyDelete
  25. nilifikiri tukuyu ni jangwa kama mikoa ya kati du kumbe kijani mtupu asante kwa picha nzuri

    ReplyDelete
  26. unkal kwenye limo la babu! jamamni hiyo fulana si uliiuza ukerewe kwa paund 1000? Vipi tena mbona bado unaivaa?

    ReplyDelete
  27. Ankal,ze fulanazi si uliiuza kule kwenye Diaspora? au mie kuna habari ilinipita hapa kati?

    ReplyDelete
  28. HAHAHAHAHAHAH Miwa haingolewi inakatwa Comment nimecheka kweli sababu ni ukweli Kazoea Mihogo sio hahahaahaha Mbayaaaaaaaaaaaaaaa lol! Hayajawa Baba Ubaya.

    ReplyDelete
  29. ANKAL MICHUZI HUYO ANKAL MOSES HAPO ANACHUMA AU ANANG'OWA ANATUMIA NGUVU ZOTE HAKUNA PANGA KARIBU? AU NDIO MMEKUTA PALE YA MWANAKIJIJI MNAAMUWA KWENDA KINYUME HAHAH MNABAHATI AFANDE KOVA HAYUPO SEHEMU HIZO. ANKO WA MWANZA.

    ReplyDelete
  30. Swali la kizushi Kwani Ankal Michuzi we ni Mnyakyusa?

    ReplyDelete
  31. fulanazzzzzzzz ilitolewa kule mji wa kusoma na hapa umeivaa naomba ufafanuzi zaidi

    ReplyDelete
  32. Hamna uwazi wowote hapo. Wewe kama huna maadili nyamaza uache watu wafanye mambo yao. Kwani hiyo ndege iliyoanguka Poland ni kwa sababu walikuwa wanasheherekea wafu au kwa sababu pilot anashukiwa hakusikiliza amri ya air traffic control? Hamna utamaduni wowote duniani usioheshimu wahenga wao, wawe Wazungu au Waafrika. Ndio maana ukienda makaburini kama Ubungo Dar unakuta manyasi kila sehemu.

    Mimi nashauri uache kubwiya unga, kwa sababu inaleta madhara makubwa

    ReplyDelete
  33. Ankal inakuwaje tena the Fulanas si uliiacha mji wa Kusoma ipigwe mnada?mbona tuna iona huko Tokyo kwenye Limo la babu?

    ReplyDelete
  34. Mdau wa Tue Apr 13, 02:11:00 PM umetoa maoni yako na ninayaheshimu kama maoni yako. Umetoa wito tuwe wazi hivyo nawa wazi.
    Ukumbuke kwamba wapo wengi ambao hawaoni umuhimu wa kukumbatia kitu cha kigeni kutoka mashariki ya kati ulichokiita maandiko wakati wana imani zao ambazo zimekuwa zikiwafaa siku zote. Si sahihi kuita imani zao 'mila potofu' bila kuwa na njia ya kisayansi ya kudhihirisha kwamba njia unayoiamini wewe ni sahihi kuliko anayoiamini mwenzio. Mambo kwa mifano, mfano kama ingekuwa ni suala la mtu asiyetaka kunawa mikono kabla ya kula kwa sababu ya imani fulani unaweza kusema hiyo ni mila potofu kwa sababu unaweza kuonyesha kisayansi madhara ya kutonawa mikono.
    Watu wanakufa kwa ajali wakitokea kila sehemu. Ni rahisi zaidi kukumbuka inapokuwa wametokea makaburini kwa sababu zinaripotiwa zaidi. Kuna watu wanafariki wakiwa njiani kwenda kuwaona wagonjwa wao hospitalini, wakiwa njiani kwenda kazini, wakiwa kazini, wakiwa wamelala, wakiwa wanananihii nk. Huwezi kusema kwa kuwa mtu alifariki wakati anananihii basi watu waache kunanihii.

    ReplyDelete
  35. HUO NDO UWANJA WA NYUMBANI WA WANYAMBALA? [TUKUYU STAR] WALIWAHI KUWA MABINGWA WA TAIFA MWEEE MJI UNATOWABINGWA TAIFA NA UWANJA NDO KAMA HIVYO. ANKAL WEWE MIMI NILIDHANI NI MMATUMBI/MNDENGELEKO/MKWERE!!! KUMBE MNYAMBALA!!! KWANI TOKA NIKUJUWA NA MAPICHA YAKO DAILY NEWS, UHURU NA MZALENDO MIAKA HIYO YA 80 HADI LEO. NILIJUWA NI MPWANI

    ReplyDelete
  36. ANKAL KACHEMSHA LELOOOOO LELOOOOOOOOOOO WATU WANATAKAK UJUWAK UHUSU FULANAAAAAAAAAAAZ KUMBE ILIKUWA CHANGA LAM ACHOOOOOOOOOOO DUH KUMBE MPAKA ANKO ANATURUSHA ILIKUWA APRIL FOOL NINI.

    ReplyDelete
  37. Tanzania tunatakiwa tujivunie majina ya mikoa ua miji yetu hii mambo ya kubadilisha majina na kuita nchi za watu ki ukweli tunajivunjia heshima yetu.Nafikiri nchi zingine zinashindwa kuelewa tuna matatizo gani.Majina ya miji na mikoa yetu ni mazuri kabisa sioni ni kwa nini tusitumie hayo majina.Na mwenye barber shop kwa nini asitumie jina la rais wake nakuwekabendera yetu.Vitu vingine tunapenda kuharibu.Wenyewe marekani wanaheshimu sana Rais wao hawaruhusiwi kutumia jina lake kwenye biashara la sivyo wenyeji watakupa shida.

    ReplyDelete
  38. Asajile MwaijumbaApril 13, 2010

    Mdau hapo juu uliyetoa hoja eti kwanini tusifungue saluni na kuiita jina la rais wetu badala ya kuita jina la Obama.... Jaribu wewe kufungua saluni uiite jina la Rais uone kama utanyoa hata vichwa viwili kabla hujakamatwa.
    Na wadau mnaoulizia ze-fulana nyie ndio watu mliopatwa leo na April foool ya tarehe moja?!! Ile ilikuwa siku ya wajinga.

    Asajile

    ReplyDelete
  39. Wewe Richard acha kupayuka. Kwanza Wazungu wenyewe huwa wanatunza makaburi yao na kuyapamba mpaka yanapendeza. Ingawa hawatambiki, u huwa wanakwenda na kuongea na wafu wao kama bado wako hai, kwa sababu inawafariji. Wewe kama marehemu hawakuhusu, uendelee na mambo yako. Hao wenyewe unaojifanya kuwaiga wataona you are very rude to bad mouth the dead, or at least people who are grieving. Sijawahi kusikia mtu hapa akisemwa kwa kuomboleza marehemu. Hapa Marekani kuna sherehe nyingi tu za kukumbuka maraisi wao waliokufa, askari waliokufa vitani na kadhalika. Wacha nikupe another Western tip, "Mind your our own business!" We unajua Michuzi anaamini nini? Au huamini kuwa mtu mzima ana uhuru wa kufanya anachotaka mradi asivunje sheria. Mila potofu..negative..my foot!

    ReplyDelete
  40. Watu wanapiga kelele wee hata hawaelewi Michuzi kwanini anapaita Tukuyu (Tokyo) hili jina hajatoa Michuzi limekuwepo miaka nenda rudi kama huelewi kitu ni bora ukae kimya kuliko kurukia mambo na kuonekana wakuja tuuu. Unaandika ili nawe uonekane umo pia. Unavuma lakini hausikiki......

    ReplyDelete
  41. ANKAL NAKUSHAURI NEXTIME UNAPOTAKA KULA MUA BASI USIUNGOE WOTE MPAKA SHINA

    UNAPOTAKA KULA MUA UKATE KWA PANGA AU KITU CHOCHOTE KWA CHINI NA SIO KUUTOA NA MIZIZI YAKE

    UKIUKATA INA MAANA KILE KISHINA KITAMEA TENA NA MAANKAL WENGINE WATAKUJA KUFAIDIKA NA MUA

    ILA UKIUNGOA YANI KUUVUTA NA SHINA LAKE INA MAANA PALE HAPATOWEZA KUMEA MUA MWINGINE

    ASANTE SANA KWA TWASIRA NA POLE SANA KWA KUONDOKEWA NA BIBI

    MAY GOD BLESS HER

    mdau wa mahaka kuu ya dunia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...