Na Maggid Mjengwa
PENYE urasimu ni mahala pia pa machinjio ya fikra huru, kuu na njema. Ndiyo. Mara nyingi fikra huru, kuu na njema hufia kwenye meza za warasimu. Huwa hazifiki kwa wahusika wenye kuzihitaji wazifanyie kazi.

Nimesoma mahojiano ya kuvutia na kuamsha fikra kwenye Raia Mwema wiki iliyopita yanayohusu Mwandishi wa Raia Mwema na Dk. Ramadhani Dau, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii, NSSF ( Daraja la Kigamboni si ndoto, tutalijenga- Dau. Raia Mwema Na.129)
Hakika, Dk. Dau ni kiongozi wa kupigiwa mfano kwa kuonyesha ujasiri na utayari wa kufanya maamuzi mazito. Maamuzi yenye kuweza kuwa na athari mbaya hata kwake binafsi, lakini, ameyafanya na anaendelea kufanya maamuzi hayo kwa kuamini kuwa yana maslahi mapana kwa nchi yake.

Kupitia mahojiano yale, Dk. Dau anaonyesha kuwa ni mtu ‘anayetembea kwenye maneno yake’ ( walking his talk) kwa maana ya kusema anachomaanisha. Nilichosoma juma lililopita ni aina ya mazungumzo ya kiuchumi yenye vielelezo ( evidence based economic related discussions).

Kwa mfano, Dk. Dau amezungumza kuhusu lengo la kuondoa urasimu. Tumeona mifano ya kauli yake hiyo. Amezungumzia umuhimu wa kuwashirikisha wengine katika mipango na maamuzi, tumeona kwa mifano pia, kuwa hilo linafanyika NSSF
Habari Kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. ndio huyo ni kamanda wa kweli,alikuwa kiungo muhimu kwa serikali ya awamu ya tatu,alisaidia sana serikali ya mkapa kwenye uwekezani wenye manufaa,na hata serikali ya sasa yeye amekuwa tegemeo kubwa chini ya nssf,kuanzia ubungo plaza,mafuta house(benjamin mkapa tower),mabibo hostel,nyumba za polisi,bunge jipya dodoma,chuo kikuu dodoma,machinga complex, na mengine mengi mno,hongera baba tunasubiri kigamboni daraja.

    ReplyDelete
  2. kwa mashirika ya umma bongo,ni mawili tu yaliopata mafanikio kupindukia.nssf na crdb.ndo maana nawakubali watu 2tu bongo, dr ramadhan dau na charles kimeo.tukipata kama hawa tanesco,n.h.c,posta,ttcl,air tz,bandari,reli mbona tutakimbia kimaendeleo.

    ReplyDelete
  3. Tukiwa na viongozi wengi kama hawa mbona tutafika mbali. Na mimi natoa pongezi.Jamani tupongezane watu wanapofanya mazuri. Lakini tukumbuke fedha zinazotumika ni michango ya watu, mimi na wewe. Bado mafao ya uzeeni hayatoshi na mfumo wa'social security' inabidi kuboreshwa. Wengine wanajitoa kwenye NSSF. Mchango wangu ni kwamba vile vile Dr Dau na wahusika wengine wangeangalia njia za kuboresha zaidi mafao ya wachangiaji wanapofikia kwenye fainali, uzeeni. Lengo la mfuko ni 'social security.' Mambo hayo mawili yaende pamoja: Kutimiza ndoto za wachangiaji liwe lengo kuu na Uwekezaji mzuri kama wa Dr Dau ufuate.

    ReplyDelete
  4. Hapana...jamaaa ana udini sanaaa... si kiongozi bora wa kuigwa hata kidogo... uliza wanafanyakazi wa Nssf.... kama wewe si asha, mohamed, ramdhani, rukia, said, osama etc hupandi cheo au huajiriwi..

    ReplyDelete
  5. Wewe Anony wa Fri Apr 23, 10:05:00 AM tatizo lako ni mazoea kwamba majina fulani ndio yanastahili vyeo au kupata ajira na sio hayo yaliyotajwa hapo. Kupanda cheo kama unastahili huwezi kuzuiwa sababu kuna sheria na wala huyo dau sio HR Manager, kama huna vigezo ata ungekuwa na jina la Mtume vyeo utavisikia hivyo hivyo.Soma Mchungaji then fanya kazi vizuri ndio moja ya vigezo. Acha UDINI wako humu.

    ReplyDelete
  6. Anony wa 10:05 unaonesha ni jinsi gani we ndo ulivyo mdini, huyu jamaa hana udini ila ni muislamu safi, ukweli ni kwamba watu wakigundua we unafuata dini basi huwa wanakuchukia, na najua dini ndo inamuongoza kuleta maendeleo, unaongea bila ushahidi, yaan iunayosikia ndo unayaropoka, c kweli kwamba nssf inaajiri waislamu tu, nenda kaangalie data za new recruitment utaona waislamu wangapi na wasio waislamu wangapi. HUYU MTU NI MTENDAJI SANA

    ReplyDelete
  7. Mdau hapo juu hivi udini ni kuwepo kwa akina Asha na "Osama" wakiwepo akina John, Ernest nk unakuwa ni uzalendo sio?

    Mkikosa kuchafua watu wenye utendaji mzuri wa kazi na mnakimbilia kwenye hoja za udini, ukabila nk.

    Angalia perfomance ya kazi yake dont be ahead of yourself. Huko PPF 90% wakristo shirika linafanya miradi 2 au 3 kwa mwaka tena kwa mbinde!
    Kama Dau ni mdini basi neno udini limepoteza maana na pengine mdini mkubwa ni yule alie mpa nafasi hiyo Benjamin William Mkapa.

    ReplyDelete
  8. Ni binadam kama mwingine awezi kua asilimia miamoja ila wacha tuyafunike ma baya yake kwani mazuri ni mengi zaidi ya mabayake

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Fri Apr 23, 10:05:00 AM Inaelekea hujui muongozo mzima wa kuajiri na kufukuza watu kazi, Hiyo si KAZI ya Mkurugenzi mtendaji ndugu yangu, HR wanahusika. Usilete chuki binafsi kwenye maendeleo... Ndio nyie nyie mnatamani wezi kama kina MATAKA na wenzake waendelee serekalini. Au ndio nyie fulani akipata kazi kwenye kitengo fulani mnaropoka KAPATA ULAJI. DR. DAU CHAPA KAZI. Wewe ni mfano mkubwa wa kuigwa Na wasomi wetu wa Africa.

    ReplyDelete
  10. Kweli watanzania ni watu wa majungu sana. huoni utendaji ulitukuka wa DR.Dau na kwa vile umeshindwa kusema thanks kwake? sasa mmeamua kumpaka matope ya udini.

    kama nilivyosema hapo awali kuwa Magori alikuwa karani wa kawaida sana NSSF.ame rise from the Bottom kwenye kipindi hiki cha DR.Dau,na kuwa Mkurugenzi wa kitengo muhimu.

    kuna Alfred Ngotezi naye kapanda.

    ukitizama wakurugenzi kwenye website yao kuna mama Bandawe ambaye ndio mkurugenzi Msaidizi wa karibu wa dr Dau, mama Bandawe ni mkristu.

    naomba jamani tutembelee menejimenti ya PPF Tuone wakurugenzi wa vitengo,tutembelee CRDB,TRA,Bandari,BOT tuone ni waislam wangapi na wakristu wangapi.Nssf wako fair sana.


    naomba majibu ya maswali yangu.
    Mdau Mswahili-ughaibuni.

    ReplyDelete
  11. africa hatutaendelea daima kwa sababu ya ubinafsi,yani mdau kamuona jamaa hafai kisa muislam,kuna wanaopinga viongozi wa tbl kisa wachaga,yani hamna kitu waafrica wanajua zaidi ya majungu.nasema tena watanzania tuna safari refu kifikia maendeleo,maaana ata ukiwa uchapa kazi,watu watakuangalia kwa dini ama kabila.sijutii kuhama tz,bali inaniuma kuona nchi yangu bado watu mambumbubu

    ReplyDelete
  12. Kitu kimoja ninachompendea Dr Dau kuwa, yuko simple, na karibu sana na watu. Na amesaidia watu wengi sana, tena sana. Na mbali na kuwa yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF ni mwanaharakati wa kupambana na umasikini kwa kupitia elimu, anafahamu kuwa ni elimu ni inayoweza kubadilisha maisha ya mtanzania. Waulizeni watu wa Mafia.

    Pili hatishwi na udaku wa mnagazeti wala wale wanaomuandama kuwa yeye ni mdini, kwani anafahamu kwa Tanzania kama wewe unafuata dini yako, huhongi, huendi kwenye vilabu vyao kuwahonga pombe, basi utapigwa CHAPA YA UDINI. Ni ugonjwa ambao umeota mizizi nchini mwetu wa kuwaona watu wengine kwa misingi ya udini au ukabila.

    Hongera sana Dr. Dau, kazi uliyoifanya inaonekana na itaendelea kuonekana hata siku za usoni. Umeweka legacy!

    ReplyDelete
  13. Hili lijamaa linaloleta udini ni jinga sana. Ningelijua lazima ningelipiga viboko kama toto jinga darasani. Lina akili ndogo sana maada hapa ni kuwa Dr. Dau yuko juu kwa ma CEO hapo bongo, lenyewe limeona dini ya Dr. Dau ndio isu. Sasa hili jamaa linyewe linaona bora nchi iteketee mradi kina kristofa, kristina, josefu, wiliamu wanaongoza hata kama ni wabovu. Hii ndio sumu ya huu ujinga wa kujihisi kuwa dini fulani ina haki zaidi katika kuongaza mashirika yetu hata kama kuna udhaifu miaka nenda miaka rudi.

    ReplyDelete
  14. Nimewapenda sana watanzania kwa kulipinga hilo pumbavu linalotaka kutuletea udini wake katika masuala ya msingi na ya kimaendeleo ya watanzania na sio huyu tu, na mwingine akitaka kuleta zengwe linalofanana na hilo liwe la ukabila ,ukanda ,na aina nyingine ya ubaguzi pale tunapoona ni uongo ila hisia zake tu, tuwapinge kwani ni masikini wa fikra na hoja hawatufai watu kama hao.sisi tunataka maendeleo hatutaki upuuzi wa hisia awe mkristo,muislamu,mpagani au nani sijui wote sawa tu,ili mradi anatekeleza yale yalioainishwa kwenye utratibu wa kazi poa tu. hatutaki ubaguzi wa aina yoyote ,tunataka amani na upendo kwa maendeleo ya wote..

    ReplyDelete
  15. HUYO JAMAA ALIYEULETA UDINI SITOSHANGAA NDIO WALIOMVAMIAAAA....AKAMATWEEEE

    ReplyDelete
  16. Unapozungumzia Tanesco nafikiri lazima u-acknowledge uwepo wa wazungu pale...hahaha...fanya utafiti kwanza!

    ReplyDelete
  17. Samahanini. Mimi ndiye niliyeleta suala la udini.

    Sirudii tena nimetubu sana na sintosema tena.

    Actually niko under medication kutokana na mambo ya brain so nahitaji sana msamaha wenu.

    Najua nimewahudhi sana hasa wewe unayesoma hapo kwenye computer yako.

    Nina madepresheni ya kukosa mchumba na kuwa singo kwa miaka 12 sasa. Labda nitafutiwe mchumba mrembo sana mwenye rangi ya njano ntaanza kuwa na mijibusara kama ninyi

    Funny enheeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  18. MSI PANIC SANA NA KUKASIRIKA BURE HII NI KAWAIDA HATA KWENYE COMMENTS ZA OMG WEB SITE. KAMA DEBATE INAHUSU MAFANIKIO AU MATATIZO YA BLACK KAMA OBAMA, ASHLEY COLE, TIGER WOODS, HUWA INAISHIA KWA KUTUPIANA MADONGO YA MIVUTANO YA 'BLACK' NA 'WHITE' NA MADA HUWA INASAHAULIKA. LAKINI KAMA MAFANIKIO AU MATATIZO NI YA WHITE BASI NI JAMBO LA KAWAIDA! WATU FULANI, DINI AU MAKABILA FULANI TANZANIA WAKIFANIKIWA INAONEKANA WAMEBEBWA AU UTENDAJI WAO UNA UTATA, WENGINE NI SAWA. KWA HIYO MTOA MADA WA UDINI SI KICHAA, ANA ASHIRIA TASWIRA YA JAMII SI TANZANIA TU HATA DUNIANI KWA UJUMLA. MTAKE, MSITAKE HII NDIO REALITY NA NDIO MAANA KUNA NENO STEREOTYPES. LAKINI KAMA MADAI YA UDINI NI YA KWELI, DR DAU AJIREKEMISHE!! TEHE, TEHE...!!

    ReplyDelete
  19. ni kweli kabisa wanakitumia chuo kikuu cha Dar-es-salaam kukandamizia watu!!imagine mtu unaomba kujiunga na chuo, ktk form wanakuulizia wewe ni dini gani!!mambo haya ndiyo maana Hayati Kigoma malima alianzisha namba badala ya majina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...