

Wasanii nyota ambao wamejitolea kuwa mabalozi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria Prof Jay, Lady Jay Dee, Banana Zoro na Mwasiti leo wamepimwa damu kwa uwazi na madaktari kutoka hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ili kujua kama wana ugonjwa wa malaria ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Zinduka Malaria Haikubaliki – inayohamasisha watu kupima malaria hospitalini mapema pale wanapoona dalili.
Zoezi hili za upimaji damu wasanii kwa uwazi limefanyika katika hospitali ya matibabu ya Moyo Jijini Dar es Salaam, (Tanzania Heart Institute) na imeandaliwa kama baadhi ya matukio ya kuadhimisha Siku ya Malaria Dunia ambayo itaadhimishwa kwa hapa Tanzania Jumapili Aprili 25 kwenye viwanja vya Mnazi Mmmoja na mgeni rasmi akiwa Rais Jakaya Kikwete.
Kipimo cha Malaria kinachofahamika kama Rapid Diagnostic Tests (au RDTs) ni nyenzo muhimu katika kupambana na Malaria nchini Tanzania. Siku za nyuma madaktari walikuwa wanadhania kwamba kila homa ni malaria na kutoa matibabu ya malaria kwa watu wenye homa- na hasa wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Lakini kadri nyezo mbali mbali za kuzuia malaria zinavyoongezeka homa zinazosababishwa na malaria zinapungua maradufu.
Katika tafiti za hivi karibuni imebainika kwamba asilimi 25 au chini wa watoto chini ya umri wa miaka mitano wenye homa hasa katika maeneo ya vijijini wana malaria.
‘’Ni muhimu sana kuthibitisha kwamba homa ni malaria kabla ya kuanza matibabu kwa sababu dawa za malaria zina gharama na zinakuwa zimetumikabure kama mtu hana malaria na pia matumizi holela ya dawa yawaweza kusababisha dawa zikashindwa kutibu malaria. Yote haya yanaweza kuepukika iwapo mtu atapima malaria kwa kipimo cha haraka cha kutolewa damu kwenye kidole,’ alisema daktari kutoka Muhimbili Shadrack Sikiko ambaye alishiriki zoezi la kuwapima malaria wasanii.
Professor Jay alisema ‘’ mimi kama balozi wa kampeni hii za Zinduka Malaria haikubaliki leo nimejitolea kupima malaria. Ni muhimu kwa sisi mabalozi kuelewa umuhimu wa kutumia nyezo za kuzuia malaria ili tuweze kujikinga. Leo nimepima hapa hospitalini na nawaasa watanzania wote wapime ili wajilinde na malaria kila wanapoona dalili ya malaria.’’
Kwa upande wake Lady Jay Dee alisema zoezi la kupima malaria linafanyika kwa kasi kubwa. ‘’Mimi zamani nilikuwa nanunua tu dawa kila nilipokuwa na dalili ya homa na nawasihi watanzania wapime malaria vizuri badala ya kudhania kwamba wanamalaria ili dawa zisije zikawazoea na kushindwa kuwatibu,’’
Mwasiti yeye alisema yeye anaogopa sindano lakini akasema anashukuru kipimo cha RTD ambacho ni cha haraka na hakina maumivu.
‘’Nikionyesha dalili ya malaria nitaenda hospitali siogopi tena,’’ alisema Mwasiti.
Banana Zoro kwa upande wake jumapili hii ni siku ya Malaria Duniani, na dunia nzima itaungana kupambana na ugongwa huu, Lengo letu ni kufanya kila siku iwe siku ya kutambua madhara ya Malaria hapa Tanzania. Ikifanikiwa kama Rais Kikwete alivyosema tutakuwa kizazi cha mwisho kuuawa na malaria.
Kampeni ya Malaria Haikubaliki inaongozwa na serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, na inaugwa mkono na wafadhili mbalimbali ikiwemo Malaria No More, Tanzania House of Talent (THT), Johns Hopkins University, Population Services International na United Against Malaria. Lengo la programu hii ni kuhakikisha watu wote wanatumia chandarua na kutokomeza malaria kwa kuwashawishi watanzania wote Kuzinduka na kukabiliana na malaria na kujilinda na ugongwa huu hatari.
Kampeni ya Malaria Haikubaliki inaongozwa na serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, na inaugwa mkono na wafadhili mbalimbali ikiwemo Malaria No More, Tanzania House of Talent (THT), Johns Hopkins University, Population Services International na United Against Malaria. Lengo la programu hii ni kuhakikisha watu wote wanatumia chandarua na kutokomeza malaria kwa kuwashawishi watanzania wote Kuzinduka na kukabiliana na malaria na kujilinda na ugongwa huu hatari.
Ukimwi nao jamani pimeni hazarani, sio malaria tu nyie "masupa staa" wetu.
ReplyDeleteHivi vichwa lakini mpaka lini? Malaria "HAITOKOMEZWI" kwa "kupima" malaria au kutumia "chandarua". Maji machafu, mitaro isiyoenda, mazingira machafu kwa ujumla ndio furaha ya umbu. Hapo pimeni malaria mpaka Yesu anarudi, malaria mtindo mmoja!
ReplyDeletekwani kupimwa malaria ni tatizo hata wenye ngoma wanaweza kupima malaria, but kupimwa sio kutokomeza malaria jamani huyo ni ujinga tuu , wakati maji machafu bado yapo, na sio wote wa bongo wana uwezo wa kununua chandarua, so nikama mnatwanga maji kwenye kino.
ReplyDeletejamani kweli malaria itatokomezwa kwa kutumia chandarua na kupima malaria?????? sidhani!! hii imekaa kisanii zaidi mradi wa kigogo fulani mwenye kampuni ya kutengeneza vyandarua. hivyo watu wanahamsishwa ki aina. kwanza tungepambana na vyanzo vya mazalia ya mmbu jamani, mbona suala hili liko wazi.
ReplyDeleteWewe Thu Apr 22, 11:22:00 AM kuwa flexible kidogo. Ndiyo hayo maji machafu na mitaro yapo; lakini watu wanazungumzia kitu ambacho unaweza kicontrol mtu binafsi. Watu wangapi wana uwezo wa kwenda kukausha maji machafu au wasafishe na kuchimba mitaro maji yapite? Lakini kununua chandarua ni kitu ambacho mtu binafsi anaweza akafanya. Unless huyo mtengeneza vyandarua akafukie maji machafu kabla hajauza vyandarua vyake.....Siyo kila kitu mpaka serikali ifanye kwanza. Kwa hio endelea kufanya ngono kwa sababu serikali haina madawa ya kutosha ya kurefusha maisha.....
ReplyDeleteLeo nimepima hapa hospitalini na nawaasa watanzania wote wapime ili wajilinde na malaria kila wanapoona dalili ya malaria.’’
ReplyDeleteHii ni kauli ya Prof. Jay. Itafakarini kauli yenyewe!! Eti "....wapime ili wajilinde na malaria kila wanapoona dalili ya malaria". Pamoja na umatumbi wangu lakini siipati kauli yenyewe sambamba na malaria. Sasa kutokomezwa hapa kunafananaje? Msingi wa kupima ni ili kupata tiba sahihi ya ugonjwa na si kutokomeza.
Bora basi angesema tulale ndani ya chandarua ili kujikinga na maambukizi ya malaria. Huku ndiyo kujikinga. Kupima siyo kujikinga.
Lakini yote kwa yote, jamani MUHIMU KATIKA KUTOKOMEZA MALARIA NI KUHARIBU MAFICHO NA MAZALIA YA MBU. HAPA NDIPO TUTFANIKIWA KUTOKOMEZA MALARIA. VINGINEVYO, HUU NI USANII MTUPU.
Kwenye UKIMWI tunasema tuache ngono zembe, tusishikiane vifaa vya kutogea, nyembe, nk. Huku ndiko chanzo cha kutokomeza maana hakutakuwa na maambukizi mapya.
Nyinyi wa malaria siwaelewi kabisa!!!