Maelezo ya Dr ni sahihi kwa kwa sehemu na si sahihi kwa sehemu. Ni kweli kimeo kama kimeo (Uvula) hakihusiani na kukohoa wala hakihitajiki kukatwa.
Lakini kimeo kiko very vulnerable kwa infection na hivyo hupelekea ku swell, kiki swell sababu ya infection huweza hata kupelekea kufanya usaha (pus) wakati mwengine kina fanya kioteo sababu ya hiyo infection, hicho kioteo ndicho kinacho pelekea kikohozi sababu kina habour virus na bacteria kama vile streptococcus pneumoniae na wengine wanaopelekea kikohozi, hichi kioteo huwa mara nyingi hakipotei kwa treatment za kawaida, hadi kikatwe (uvulectomy)!
Ukataji huo wa kimeo tumezoea kuufanya kienyeji (sishauri iwe inafanyika hivyo, kwa kuzingatia mazingira hatarishi ya HIV, pia uwezekano wa kupelekea magonjwa mengine ya infectio kutokana na mazingira husika), ningeshauri wagonjwa wa vimeo wapelekwe hospital wakapate matibabu katika mazingira mazuri.
Lakini mara nyingi ugonjwa wa kimeo huchanganywa na epiglotittis ambayo nayo pia treatment yake ni sugery na dalili zake ni kama hizo za kimeo, ila hii epiglotittis ni hatari zaidi kwani hu grow hadi kuzuia upumuaji wa kawaida hivyo mgonjwa kukosa hewa na hatimae kufa!
Mdau Scientist (microbiologist)
Mdau Scientist (microbiologist)
Ni maelezo yalioenda shule,thanks,lakini mwisho umeniacha kidogo kwamba kimeo kikipata hao virus lazima kikatwe lakini ila kwenye mazingira makini(hospitalini).Swali ni, hospitali wanaweza kukata kimeo hata kama kina tatizo pia kuna madhara gani kukata kimeo?
ReplyDeleteankal, mie nauliza tu swali, hivi john mashaka alienda wapi? yule jamaa ndiye anayechangamsha hii blog kusema kweli, au umektaa kumplia akasusa blogu, au ndo kampeni zimeanza huko tarime. niliona watu wake wakitembea na magunia ya bangi
ReplyDeleteAnkal ee, unakimeo nini? Mbona hii ,ada imekuwa haiishi humu ndani?
ReplyDeleteThe uvula is a little bag of of fleshy tissue at the back of the throat. A uvulectomy, or the removal of someone's uvula, is a treatment sometimes applied in more or less crude fashion by African witch doctors and tribal medicine men. They believe that illnesses and evil spirits and other terrible things hide at the back of the throat, and to cut away the uvula is their answer to quite a few illnesses; especially those illnesses they have not succeeded in removing in a more regular fashion. It is often done to small children as a precautional measure, similar to having one's adenoids cut.
ReplyDeleteA lot of blood runns through the uvula. To cut it without proper precautions means to cause serious bleeding. If the patient survives the bleeding, infections may occur because of the unclean environment the procedure takes place in. In short, the uvulectomy is something modern medicine in Africa tries hard to stamp out a traditional medical treatment, because it only causes pain and mortal danger.
In the West, uvulectomy (under more sterile and safe conditions) is sometimes suggested to alleviate sleep apnea and/or heavy snoring.
Mdau mwana-microbiologist,
ReplyDeleteUkataji wa kimeo kama uliovyokutaja hapo juu kwa kimombo uvulectomy.. hutumika katika kusaidia kutibu kukoroma (snoring) au kupata matatizo ya kupumua wakati wa kulala (sleep apnea). Katika kutibu matatizo hayo wakati mwingine sio tu kimeo (uvula) hutolewa bali pia tonsils, adenoids hutolewa katika oparesheni ambayo hufanywa baada ya ushauri wa otolaryngologist. Ikumbukwe kuwa kutolewa kimeo sio tiba pekee ya kutibu apnea na snoring. Na pia kimeo hicho hutolewa sio kwa kuwa kimevimba.
Nakubaliana na wewe mdau kwamba kuvimba kimeo kunaweza kukawa kumesababishwa na sababu kadhaa kama kuwepo vijidudu katika mfumo wa kupumua kama vile virus na bakteria uliowataja hapo juu. Lakini kuvimba kimeo kunaweza pia kukawa kunasababishwa na allergy, chemical trauma, Gastroesophagel reflux disease (GERD), Nasal Congestion na mengineyo mengi.
Lakini la muhimu ni kuwa, mdau ameuliza kwamba mtoto wake anakohoa na yeye anashauriwa kukata kimeo, mimi nashauri kuwa, kukata kimeo sio tiba ya kikohozi, na la muhimu ni kuwa hata mdau hakusema kwamba kimeo cha mwanae kimevimba, ninalosisitiza hapa ni pengine hakuna uhusiano wa kikohozi na kimeo cha mwanae, hasa kama ikiwa hakijavimba na hata kikivimba pia. Vijidudu ulivyovitaja hapo juu vinaweza kutibiwa kwa kula dawa za antibiotics ambazo ziko nyingi tu na za kawaida. La muhimu ni kuwa daktari ndio ana uwezo wa kutambua iwapo hao infection wako au hawapo baada ya kufanya vipimo. Katika medicine kukata kilimi kama tunavyokata afrika kwa sababu ya kikohozi kunaonekana kama mila na mazoea yasiyo na msingi na suala lenye hatari kubwa.
Kimeo si ni kale kakitu pale kati au? Nyie mnamaanisha nini?
ReplyDeleteWadau mmempa maelezo mengi ya kitaalam mhusika na sie wengine tumejifunza. Lakini hamjamwambia aende wapi tatizo la mwanae liishe, shida yake mwanae apone.(sio yeye awe dakitari wa vimeo)
ReplyDeleteMwelekeze wataalamu wapo wapi aende uko.
Jamani kinachokatwa ni kile "KIOTEO" kama alivyoelezea mleta mada hapo! Ukweli ni kwamba lazima kikatwe na Hospital nyingi hawafanyi hiyo sijasikia, kwa hiyo watu wote ndo tuliponea pale UDOWE miaka mingi nyuma na mpaka sasa tunadunda na vimeo vyetu tunavyo,labda kesho tutarudisha namba who knows?! Hakikatwi chote ni kile kincha tu na baada ya siku tatu unapona mzima! Na unatizamwa kwanza kama huhitaji kutolewa kitu wanakwambia huna nenda hospitali.
ReplyDeleteNa miaka ya nyuma nasikia walitembelewa na mabwana afya wakatakiwa waboreshe baadhi ya mambo ikiwemo usafi wa vyombo wanavyotumia na wakafanya hivyo.
Kwa hiyo ushauri wangu yule jamaa ampeleke tu UDOWE mtoto wake akakatwe hamna madhara woga tuuu!