Mbunge wa Singida Mjini Mh.Mohammed Dewji akihamasisha Wananchi uchangiaji wa ujenzi wa madarasa katika kata Mitunduruni Mkoani Singida ambapo shule ya awali ya watoto katika kata hiyo.
MO akipokea zawadi ya picha iliyochorwa taswira yake kutoka kwa watoto wa shule ya Sunday School wa kanisa la pentekoste katika kata ya Mitunduruni Mkoani Singida
Mgeni rasmi Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini akihutubia katika harambee ya uchangiaji wa Ujenzi wa shule ya awali ya kompasheni ya kanisa la pentekoste ya kata ya Mitunduruni mkoani humo,MO alichangisha jumla ya shilingi Milioni 10 ikiwemo na yeye binafsi kama mbunge na kwa ajili ya kuwahamasisha alichangia shilingi milioni 5 kutoka mfukoni mwake pamoja na mifuko ya cement 30.



Huu ni mfano mzuri kwa wabunge makini. Badala ya kuitisha harambee ya kuchangia campaign za uchaguzi ni muhimu kuchangia maendeleo ya majimbo.
ReplyDeleteThe next President of Tanzania
ReplyDeleteMbona kampeni zimeanza alfajiri wakati uchaguzi ni alasiri.Just kidding:)
ReplyDeleteMheshimiwa asante kwa kusaidia wananchi.
(US Blogger)
Acheni majungu,haijalishi kuwa anapiga kampeni au laa,suala ni kwamba amesaidia wananchi wake.nampa big up,hii si sawa na wale wanao fanya kampeni kwakuwapa wananchi pea za khanga au kuapikia pilau.No pilau no fulana,changia maendeleo.
ReplyDeleteMhina