Ndugu wana Blogu ya Jamii,
Namtafuta Bwana mmoja anaitwa kwa jina la Ukoo Mshauri. Huyu bwana alikuwa University of Dar es Salaam miaka ya 1999. Alikuwa anachukua BCom. Nadhani alikuwa anaishi Magomeni. Na kama sikosei aliacha chuo na kwenda USA, ama alienda USA baada ya kumaliza chuo.
Yeyote anayemjua naomba contacts zake kwa kupitia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. !!!!!????? Alikuwa anachukua Bcom??? Au alikuwa anasomea shahada ya Bcom???

    Aliyekuwa anachukuwa Bcom sijui kupeleka wapi!!!, Labda yule aliyekuwa anasomea shahada ya Bcom, pengine ndiye unamtafuta?

    ReplyDelete
  2. Una maana aliyekuwa anasomea shahada ya Bcom??????

    ReplyDelete
  3. Vyovyote vile si mmeelewa lakini?awe anabeba, anachukua, anaburuza, au ananyanyua. Ni usemi ambao tumezoea mwenzenu yuou serious kama humjui anaetafutwa si lazima uccoment jamani, maana wengine mna mwiko wa kutocomment. Aaggghhh, lets be serious, mwaya mek, taratibu utampata mtu wako

    ReplyDelete
  4. Huyo anaweza akawa ni Ramadhani mshauri alisoma A-level pale Alharamain

    ReplyDelete
  5. Nyie watoa maini wawili wa kwanza hapo juu mnaboa. Hebu tokeni hapa nendeni globu ya BAKITA.

    ReplyDelete
  6. Haya sasa mmeelewa sasa mnajifanya hamjui. kama huja jibu kaa kimya au umeambiwa au kulazimishwa ujibu chochote pambavu jibu majibu kama wasomi

    ReplyDelete
  7. Ananymous wa tatu, this is also seriousness. Huo ni uchafuzi wa lugha na matumizi mabaya ya lugha. Hahuna kuzoea katika makosa. Yakionekana lazima yarekebishwe. Waswahili wanasema mwanzo kokochi mwisho nazi. Tuepuke makosa ya mazoea. Pamoja na ujumbe kufika au kueleweka, pia ni wakati wa kurekebishana.
    Tutawaelekeza na mutaelimika tu? Na mwanao, wajukuu wafahamu hivyo hivyo kuwa wanachukuwa? Tumia lugha sanifu ionekane kuna kitu kinafanyike chuoni!! Tuwe wepesi kukubali makosa.
    Ndiyo maana Ankal Michuzi anatoa humu ili kusudi tujifunze na kuelimika. Jamani, kuna wababe wa kubeza humu, na kutetea makosa!!!!!!!!!! Aibu tupu.

    Haya.

    ReplyDelete
  8. He-he-hee!
    Yaani WaTZ kwa domo!Yaani watu kumi wamechangia, hakuna hata mmoja mwenye jibu.

    ReplyDelete
  9. HAJAKOSEA CHOCHOTE HIVYO NDIVYO INAVYOKUWA KATIKA KIINGILISHI WANATUMIA NENO "TAKE" KWA NINI WASITUMIE NENO AMA "READ" AU "STUDY" YUKO SAHIHI KABISA NENO CHUKUWA HALINA MAANA MOJA TU ILE AMBAYO IMO KICHWANI MWENU LINA MAANA NYINGI MOJAWAPO NI PAMOJA NA HIYO MUULIZAJI ALIYOITUMIA.

    ReplyDelete
  10. Kweli ni makosa kusema kuwa alikuwa nachukua Bcom.Kitendo cha kuchukua kitu kinatokea kwa muda mfupi,huwezi kusema mtu anachukua kitu kwa miaka mitatu,yaani siku zote hizo za miaka mitatu huyo mtu anachukua Bcom,hilo ni kosa(kwenye sayansi tunaita blunder).
    Sahihi ni kusema alikuwa akisoma kozi ya Bcom, sio lazima uwe mtu wa BAKITA ndio uongee au uandike kiswahili fasaha chenye kueleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...