Familia ya Mzee Gembe wa Upanga Dar-es-salaam na Tabora,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu,jamaa,majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu mtoto wetu,mdogo wetu,dada yetu, Evaline Gembe ambaye alifariki huko Toronto nchini Canada katika hospitali ya Mtakatifu Michael tarehe 30/March/2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 13/Aprili/2010 kijijini Inyonga Mkoa wa Tabora.
Shukrani za pekee tunaomba ziwafikie Jumuiya yote ya watanzania wanaoishi nchini Canada hususani katika Jiji la Toronto na vitongoji vyake. Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili hadi kuusafirisha kwa gharama kubwa kutoka Toronto hadi Dar-es-salaam mnamo tarehe 8/April/2010.Asanteni kwa sala,maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu.Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Evaline kuja Tanzania.
Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani Dar-es-salaam na Tabora katika kutufariji,mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu.Asanteni sana.
Shukrani pia ziuendee Ubalozi wa Tanzania nchini Canada na Jumuiya mbalimbali za ki-Tanzania nchini Marekani na wanablogu wote waliolitoa tangazo la kifo kwenye Blogu zao.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee,tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa ndugu yetu Evaline.Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.
Sisi tulimpenda sana Evaline lakini
Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,
Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen

Nafuu ningekufaga mimi.mweee!
ReplyDeleteKifo chake kimetugusa wengi hapa Toronto.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya marehemu ndugu yetu, dada yetu, rafiki yetu Evaline mahali pema peponi Amen.
Mdau
Toronto
Canada
Mungu ampumzishe kwa amani, Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe, Amen
ReplyDeletemdau vancouver
Marafiki zangu akina Gembe poleni. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!
ReplyDeleteAnony 10:14:00Am naona hukumwelewa anony.. namba moja, inawezekana anaumwa sana mpaka amekata tamaa.. inawezekana anashangaa jinsi marehemu alivyo mzuri and yet amefariki... kwa kuwa na sehemu ya maoni ya amani na faraja basi tupeane amani na faraja badala ya kutoa maneno mazito hayo wapendwa.. Evaline RIP umetangulia tuu wote tupo njia hiyo hiyo mmoja
ReplyDeleteBeatrice
asante sana anoni wa hapo juu wewe ndio umenielewa. huyo anoni aliyesema eti alinikataa ana lake naona anataka kutueleza ya moyoni mwake. Mimi nimesikitika tu na kusema ingefaa nife mimi badala yake.
ReplyDeletewewe anonni wa 10:44am wewe ndio ushike adabu yako. Anoni wa #1 hajasema lolote baya hapo. wewe ndio unabifu na marehemu. sijui kibuti kakukataa,sema ukweli kama ndio ilikuwa jaja yako ya kutoa dukuduku. apumzike kwa amani
ReplyDelete