Kikosi cha Simba

Mabingwa wa ligi kuu na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba leo watakuwa na kibarua dhidi ya Haras El Hadoud ya Misri katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba inaingia uwanjani kwenye kibarua hicho huku Ligi ya Tanzania Bara ikiwa imeshamalizika na timu hiyo kutwaa Ubingwa.

Mabingwa hao wa Bara ambao wamecheza mechi 22 za Ligi Kuu bila kupoteza mchezo hata mmoja, leo wataongozwa na kocha wao Patrick Phiri aliyerejea kutoka Zambia baada ya kukosekana katika mechi mbili za mwisho za ligi dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. All the best.
    Score many goals so that when you go to their home you have no much pressure.
    Daudi
    Arsenal Fun and Prisons Fun

    ReplyDelete
  2. hao sio yanga leo mtakula kichapo tuu piga ua ni kichapo dot com leoooooooo!

    ReplyDelete
  3. Mi naombea kama Simba wafungwe vile. Wallahi.

    ReplyDelete
  4. mungu ibariki SSC ushindi ni kwa watanzani sote

    ReplyDelete
  5. Haras El Hadoud ya Misri. hilo ni jina la kiarabu lenye maana tafsiri WALINZI WA MIPAKA. sasa nauliza simba wanaweza kuvuka hiyo mipaka inayolindwa na mashujaa hawo?

    ReplyDelete
  6. Mpaka sasa Simba anaongoza 2-1

    ReplyDelete
  7. Simba 2 Hadoud 1

    ReplyDelete
  8. Hello Michuzi saa mbili usiku ya hapo Bongo sasa hivi, mbona hautupi matokeo jamani au mnyama kalipuliwa nini.....???????!!!!!

    ReplyDelete
  9. We kundu wa msimbazi vepe?waonyeshe utundu wao tuone,wameonyesha huko nyuma majambooz,sasa leo twausubiri kwa hamu ati!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...