Tanzania House of Talent (THT) imetangaza kuungana kwake na taasisi ya Malaria No More. Kuungana huko kulitangazwa kwenye makao makuu mapya ya kikundi hicho yaliyopo karibu na viwanja vya Leaders Club, Kindondoni jijini Dar es Salaam na kwamba THT itashirikiana na Wizara ya Afya na wadau wengine wa afya kusambaza ujumbe wa malaria na kuhimiza mabadiliko ya tabia nchini kote.
THT iliungana rasmi na Malaria No More mwezi Novemba mwaka 2009 kama sehemu ya mpango wa kuwahusisha vijana wa Kitanzania kwenye vita dhidi ya malaria.
THT imeanza maandalizi ya Maigizo katika Elimu ambayo yatatumia muziki, uchezaji na maigizo maalumu kwa ajili ya vijana kuelewa mbinu za kujikinga na kutibu malaria.Sadaka Gandi, Afisa Mawasiliano ya Afya wa THT alisema, “THT imeombwa kuandaamaigizo katika elimu ambayo yatafungua macho ya vijana kuhusiana na ujumbe wa malaria.
Maigizo ni chombo chenye nguvu na hamasa kubwa katika kuwaelimisha vijana kupitia burudani na THT inafahamika nchi nzima.
Tulimaliza maigizo yanayohusu ukimwi mwezi Machi mwaka jana pamoja na maigizo yanayohusu ugomvi wa majumbani; vijana 12 wamechaguliwa kuwa mabalozi wa malaria miongoni mwa wenzao mashuleni.
”Z!NDUKA Malaria Haikubaliki ni sehemu ya kampeni ya taifa ya Malaria Haikubaliki ambayo itafanya shughuli kadhaa zinazohusu malaria zitakazolenga vijana. “Vijana wa THT wameanza mafunzo yatakayowasaidia kuelewa njia za kujikinga na kutibu malaria na watatembelea vituo kadhaa vya afya, hospitali na kliniki kama sehemu ya utafiti wao wa malaria.
”Msami, mmojawapo wa vijana wa THT alisema, “Mwaka jana tulikwenda Arusha kutembelea kiwanda cha vyandarua ziara ambayo ilitusaidia kuelewa utengenezaji na usambazaji wa vyandarua nchini Tanzania.
Kikubwa ni kwamba Tanzania ina kiwanda kikubwa cha vyandarua kuliko vyote barani Afrika lakini bado hatulali kwenye vitanda vyenye vyandarua vilivyowekwa dawa. Kama sehemu ya maigizo yetu katika elimu tutajumuisha suala la kulalia vitanda vyenye vyandarua, kwenda hospitali mapema kupima malaria na kuelezea kwa nini ni muhimu kwa vijana kumaliza dozi zao za dawa.
”THT itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya na mradi wa taifa wa kudhibiti malaria kabla ya kwenda Morogoro na Tanga mwezi Julai mwaka huu. Sadaka Gandi alisema, “THT inajisikia vizuri kuwa sehemu ya kampeni ya taifa dhidi ya malaria na itakuwepo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja siku ya Jumapili Aprili 25 katika Siku ya Malaria Duniani pamoja na Mheshimiwa Rais Kikwete na mabalozi wa Z!NDUKA.
Kampeni ya Malaria Haikubaliki inaongozwa na Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Inasaidiana na wadau mbalimbali wakiwemo Malaria No More, Tanzania House of Talent(THT), Johns Hopkins University, Population Services International na United Against Malaria. Lengo la mpango ni kuhakikisha vyandarua vinapatikana nchini kote na kutokomeza vifo vitokanavyo na malaria kwa kuwahimiza Watanzania kuZ!NDUKA dhidi ya malaria na kujikinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huku nikupoteza pesa tu na kumpigia mbuzi gitaa. Mimi naenda kulala saa 5 usiku unaniimbia nitumie chandarua chenye dawa, hao mbu wanaripoti kazini kuanzia saa 5 au 12 jioni? Bush alikuwa anazungumzia pre-emptive strike, mtokomeze mbu kwenye mazalia yake. Cubans wamewaletea bacteria wanaokula mayai ya mbu na hivyo kuzuia mbu kuzaliwa, nyinyi mko bize kutafuna pesa za "watu wa marekani" with zero results!!Zungumzeni vitu watanzania wanaweza kufanya, kuziba madimbwi ya maji, kusafisha mitaro, kukata majani karibu na makazi ya watu, kuweka nyavu za kuzuia mbu dirishani (ndani na nje ikiwezekana), kuwa na mlango wa wavu ukiwa mlango mkuu unawachwa wazi, kupulizia dawa majumbani na mitaani n,k

    ReplyDelete
  2. hizi kampeni za kutokomeza malaria zitaweza kufanikiwa endapo tu mataifa yote yaliyo karibu na tanzania mfano kenya,uganda,rwanda,burundi,kongo,nk wataweza kushiriki pia katika kampeni hizi kwa pamoja ili kumaliza/kupunguza vyanzo vya malaria(wadudu-plasmodium), na hii inaweza kufikiwa kama itafanywa kampeni ya kutoa tiba kwa wakazi wote wa maeneo hayo bilakujali wana malaria au hawana tena kwa kipindi kimoja, kisha wananchi wote kwa kipindi cha miezi takribani 6 watumie neti za mbu zenye dawa na pia wajipake mosquto repellants kuepukwa kung'atwa na mbu na kupunguza uwezekano wa maambukizi mapya. na kwa kipindi hicho hata mbu waliobeba plasmodium muda wao wa kuishi na kufa utatimia na watakufa na kutoweka.
    kisha watu wote wanaongia katika maeneo hayo tokea nje ya maeneo hayo wapimwe mara tu ktk maeneo ya kuingilia nchini kuhakikisha hawaingizi vyanzo vipya,na kama kuna magari yanayoingia yafanyiwe furmigation. hii inaweza kama sio kuondoa basi kupunguza malaria kwa kiwango kikubwa sana karibia na kuimaliza. vinginevyo zitakuwa ni kampeni za kujifurahisha na kula tu zenyematokeo hafifu sawa na kuchapa miguu hapohapo ukdai unatembea.
    mdau.

    ReplyDelete
  3. HUU NI UPUMBAVU MTUPU.....TATIZO KAMA KAWAIDA NI SIASA...TUMECHOKA NA MAKELELE YA KAMPENI,KAMPENI...KAMA KWELI MNATAKA KUPAMABANA NA MALARIA...ANZENI NA VYANZO SIYO HAYO MANETI YENU...MIMI UKINILETEA HILO LINETI NAKUNYONGA NALO

    ReplyDelete
  4. ankal michuzi nilikutumia habari moja kuhusu VVU na jinsi ya kuzuia maambukizi mapya ili wadau wajadili huo mtazamo lakini naona hukuitoa,kwa mtizamo wangu ilikuwa na uzito wake na haikuwa ina offend mtu yeyote,sasa sijui kama uliibana maksudi au iliingia kwenye junk mail,naomba uitoe nitakutumia tena draft nyingine,nadhani haya ndiyo mambo yamsingi kujadili pamoja na mengine yanayotuburudisha pia.lakini pia sikulazimishi maana hii ni blog unayoimiliki kama hutaki kuiweka hewani ni uhuru wako pia.japo mimi nadhani sisi waafrika na watanzania tunapaswa kufikia jinsi ya kujiokoa wenyewe zaidi kuliko kutegema hadi tuletewe idea kutoka nje zikiambatana na kufadhiliwa na masharti.we have got potentials to do beyond our imaginations,but we under utilise our potential by not thinking beyond our vicinity!
    ni mimi mdau niliye toa maoni no.2 hapojuu.

    ReplyDelete
  5. Wizi mtupu! Mambo yanaendeshwa kiwizi wizi tu

    ReplyDelete
  6. Uchuro Mtupu!

    Ni ulafi tu wa fedha za wafadhili. Mnafanya Ma 'dili' ya kutafuna fedha kwa mgongo wa maisha ya watu? Serikali vipi mnapelekwa pelekwa tu na wajasiliamali wasiojali maisha ya akina mama na watoto? Hivi miaka nenda rudi bado tu hatujapata njia thabiti ya kutokomeza malaria ila kwa maigizo na sarakasi?

    ReplyDelete
  7. Anon wa hapo kwanza asante sana. Na kwa kuongezea tuu kuna kitu kinaitwa DDT, kingeweza kabisa kutikomeza hii kitu. Pia ni vigumu kupaambana na malaria kama hauna sewer line katika miji. Malaria inaweza kutomezwa kama watu wataamua kuyaweka mazingira yao safi....

    Tuache kuwa shallow minded, hata mtu utapimwa Malaria aitasaidia kitu kama mazingira yako yanaendelea kuwa incubator ya mbu.

    ReplyDelete
  8. HII MISAADA YA WAFADHILI ITUMIKE KWA NIDHAMU.WANANCHI WASAIDIWE KUBORESHA MAKAZI YAO NA MAZINGIRA YAO NA SIYO WACHACHE KUJINUIFAISHA KUPITIA MGONGO WA KAMPENI.HIZO PESA ZIWAFIKIE WALENGWA KWENYE MAENEO HUSIKA NA TUMUOGOPE MUNGU KATIKA JAMBO HILI.SI VEMA NA HAKI KUJENGA MAHEKALU NA KUNUNUA MABALOON KWA FEDHA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MALARIA WANAOISHI KWA MLO MMOJA.

    ReplyDelete
  9. Mkuu Hapo Juu..DDT ilishapigwa marufuku na Serikali siku nyingi kwa sababu inaleta Canser kwa Binadamu..kwa kifupi DDT ni sumu mbaya sana. Wazee wetu wengi tu wamepoteza Maisha hasa Kilimanjaro kwa sababu walikuwa wanatumia DDT kuua vijidudu vya kwenye Kahawa.

    ReplyDelete
  10. Watu tusichanganye issues. Hata hapa Texas, kila ikifika summer magari ya halmashauri za jiji zinatembea mitaa yote na kupulizia dawa sehemu za maji yaliyosimama. Lakini na watu mnashauriwa kuwa mjipulizie dawa za kufukuza wadudu, kuvaa nguo za mikono mirefu au suruali, kuhakikisha hamna maji yasiyotembea au kuyaweka madawa, (kama mabwawa ya kuogelea), weka wavu madirishani, nk. Hivyo ni vitu ambavyo familia au mtu binafsi anaweza kufanya. Lakini watu mnang'ang'ania serikali ifanye hivi au serikali ifanye vile. Take charge of your destiny! Nunua chandarua kama itasaidia! Kujikinga ni combination of factors, siyo choice between one thing or another. Watanzania tuache culture ya helplessness na kulalamika tu.

    ReplyDelete
  11. TUNATAKIWA TUACHE WIZI WAKISIASA/UFISADI WA FEDHA ZA WANANCHI KUPITIA SABABU/UTARATIBU WA MAKONGAMANO/WARSHA/MIKUTANO/SIKU YA KILELE CHA/ N.K/ MWANACHI WA KIJIJINI ANAFAIDIKA VIPI ? NANI ANAYEKUWA PROMOTED/FAIDIKA HAPA ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...