hawa ni watoto wadogo sana tena wengine hata umri wa kwenda shule bado hawajafikia.lakini leo hii ndio wamejazana katika kila kona ya jiji hili la Dar kwa kuomba omba hela kama walivyotumwa na wazazi wao,kitu ambacho pia kinaweza kuhatarisha maisha yao kutokana na sehemu wanazisimama kwa ajili ya kazi yao hiyo.kitu gani kifanyike ili watoto hawa waweze kupata haki zao za msingi???.hapa ni kwenye mataa ya magomeni mapipa asubuhi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Sijui kama wazazi wao wana hali nzuri ya kimaisha wangewatuma watoto wao wakaombe tena barabarani nakuhatarisha usalama wao.

    Hayo ndio matunda ya ahadi za maisha bora kwa kila mtanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    ok yuko wapi yule alojidai humu kuwa hali ya maisha bongo ni bora kuliko kuishi na kuoiga boksi nje ya nchi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Miaka ya 70 na 80 nikiwa mtoto na kukua ndani ya DSM sikuona wingi huu wa watoto ombaomba na hata miaka ya 1990 sikuona hivyo, Je Swali Kuu ni Nini Kimetokea Kupelekea hali Hii Ya kusikitisha?

    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    swali la msingi:-
    1.ni kwanini amtoto awe aombaomba? kama ataanza kuomba kwakuwa amepoteza wazazi au mzazi hajiwezi kiafya hilo ni jambo moja,na kama anaomba wakati wazazi/mzazi yuko mzima nyumbani kwa madai eti ni maskini hilo ni jambo jingine.
    kuna sababu nyingi zinazopelekea watu kushindwa kumudu maisha na kuzalisha ombaomba.nianze na zile zinazoweza kuzuilika;-
    1. ujinga
    -hiki ndicho chanzo namba moja,pale binadamu anaposhindwa kuwa na mipango(plan)ya jinsi gani anataka maisha yake yawe na awe na familia ya namna gani kama mungu atamjalia.%kubwa ya waafrika kitu plan ya maisha haipo kichwani,na hii inasababishwa na ujinga(kukosa ufahamu wa nini kinawezekana na kinaweza kufanyikaje ili kuwa na maisha flani katika mazingira flani)hii inapelekea kukosa dira ya kimaisha na kujenga barabara inayoelekea matatizo mengine kama nitakayo taja hapa chini:-
    a)kushindwa kupanga uzazi na kuwahudumia watoto wako ipasanyo
    b}kuwa na mawazo tegemezi kuwa kunamtu atakuletea muujiza wa maisha mazuri bila kuwa na mipango,hasa kudhania kuwa miujiza hiyo italetwa na mataifa ya nje
    c)kuanza kufikiria njia mbadala za kujipatia mahitaji zisizo halali kijamii na kisheria

    2.maradhi
    -kuugua hudhoofisha uwezo wa kuzalisha,na kupelekea kwenye umaskini,na kutumia kilekidogo kilichopo ktk kujibu.hapa kuna maradhi yanayo weza kuzuilika kuanzia kwenye chanjo,kuweka mazingira safi,maji safi na salama,njia za kupika na kuhifadhi vyakula,na ulaji bora. kuna magonjwa ya kurithi yanayoweza kuepukika kama utafanywa uchunguzi wa vinasaba(genetical analysis)mapema kwa wanandoa watarajiwa na kuepuka kuoana/kuzaa mtoto mwenye matatizo hayo,na kuna magonjwa yanayo tokana na majanga ya kiasili na kimaisha ambayo yanaweza kukabiliwa kwa njia tofauti ili kurudisha uwezo wa kufanya kazi na kujihudumia.
    sitaki kueleza sana maana walengwa wengi hawapo hapa kusoma maoni,labda tuangalie suluhisho
    SULUHISHO: NIkuanza kuiandaa jamii tangu wangali watoto wadogo chekechea,shule ya msingi nk kuwa na mawazo chanya ya kuuepuka umaskini na kuuchukia,
    kuwatumia watu wa sayansi ya jamii kuuelimisha umma kwa kuwafikia walipo jinsi ya kuwa na mipango bora kwa kuzingatia mazingira waliyomo,kupitia makanisani,misikitini,vikundi mbalimbali.
    kuweka sheria na kitengo kinachoshughulikia na kutoa adhabu endelevu kwa wazazi wanaoshindwa kuwajibika kwa familia zao bila sababu za kimsingi zenye uzito unaotambulika,na kutoa huduma kwa wahanga wanao toka ktk familia za jinsi hiyo.
    kufikisha upashaji wa habari kwa njia ya TV ktk maeneo ya vijijini,ktk vituo maalum ambapo watu watajionea sehemu zingine zikoje na hii itatia changamoto na ku induce nia ya kuiga maendeleo baada ya kuona.maana wengi hukimbilia mijini kutokea vijijini. hivyo basi kuwe na kipindi cha documentary ambacho set up yake inakuwa ni maeneo ya vijijini na kiwe kinarushwa pia wanafunzi wanakiona mashuleni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    ona maisha yalivyokua magumu bongo halafu viongozi wetu wanaenda kupandikiza miti ya kichina mlimani city ili mradi tu kuwafurahisha wageni wanaokuja kukaa for 3 days ili waone wambo yetu safi kumbe hamna kitu.

    i hate bongo

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    TUSIWASEME MAOMBAOMBA SANA TUNATAKIWA KUWAPA KAMA UNACHO. SERIKARINI WAKUNA PESA KWA HIVYO WATU WASIOJIWEZA HAWAPATI MISAADA KUTOKA KWENYE SERIKARI. FEDHA ZOTE ZIMETUMIWA NA WATU KAMA LIYUMBA NA KUFANYA SERIKARI KUWA HAKUNA FEDHA ZA MISAADA KWA WASIO JIWEZA KWA KIFUPI WATU HAO WANAITAJI MISAADA. MBINU NA MAHARIFA JINSI GANI KUWEZA KUWASIDIA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    wasaidieni mpate manyoya, THE MORE YOU GIVE THE MORE MANYOYA !!!

    tena hawa omba omba watoto wanajua ku act , yaani wakikusogelea wanaonyesha sura za huzuni tena wasema "" saidiaaa saidia babaaaa ,njaa inaumaaaaa!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    Tanzania inabidi iige nchi nyingine zinavofanya:
    Mtoto asipoenda shule mzazi awekwe ndani..basi, as simple as that.
    Kwa kuwa wazazi watakuwa na ouga wa kwenda jela, hawata waachia watoto waka ombe ombe au kuzagaa mitaani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    umasikini kila sehemu upo,omba omba india ndio inongoza mpaka sasa duniani na wao wako mbele sana kisayansi lakini kwa ujinga pia wanaongoza kwa sababU ya kutowajali walala hoi na huduma tele haziwalengi wao mambo yote town kwa wajanja.
    sasa bongo kwa kiasi fulani tunafanana sana na hawa jamaa wa udosini, town mambo mswano kama anavyosema unle humu mimi sielewi maana yake hasa ndio mambo poa au moto.
    anyway mikoani mambo magumu sana sana huduma zinazidi kupungua huko vijiji vya ujamaa vimefariki kwa muda kama alivyofariki muanzilishi wake sasa hawa wazee wanahamia mijini na kuazaa bila muelekeo kwa vile kwenye umasikini ngono haiko mbali matokeo yake ujinga unazidi na maradhi kuongezeka na jamii inaonekana kuzidiwa na mpasuko huu wa umati usiojulikana umetokea wapi, jibu mikoani ambako utawala wa nchi umeipa kipa umbele mikoa si zaidi ya mitano tu tanzania nzima mtanisaidia kuitaja iliyobaki kazi kwao sasa haya ndio matunda ya mikakati mibovu ya hawa wavaa mashati kijani mchana.
    mola tusaidie sisi viumbe wako tusio na pa kwenda.
    AMIN.
    KAKA KUONA SAN DIEGO.
    MWENGE GENGENI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    Mdau wa 02:26 kula gwala baabu kubwa nakubaliana na wewe asilimia mia moja BONGO mweh tutafika tu MUNGU tusaidie!!!
    Mdau-Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    Si hao tu watoto, kuna watu wazima wanaopokea mishahara midogo serikalini kutwa kuwabomu wenziwao wanaokula rushwa serikali, ila tu tunawaona maofisini lakini hapo barabarani hatuwaoni.

    Hiyo Tshs 105,000 kwa mwezi si siku nyingi na wao wafanyakazi watatia timu barabarani kuomba au kuandamana.

    Mdau
    Wa-Kubomu Ofisini.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    Mi nafikiri ni tatizo la serikari yetu kutowachukulia hatua yoyote, kwa kweli ni kero, nafikiri sheria zetu zinazuia kuombaomba maana linaangukia katika makosa ya uzurulaji. Wiki iliyopita nilikuwa foleni nikaona omba*2 wakilizonga gari la balozi wa Japan hapa Bongo. Hivi polisi wako wapi, uongozi wa jiji, Mh. Lukuvi mbona umelala!!!!!!!!!!!!!! Kulikoni????.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2010

    siku izi wana mpya wameazisha
    ukiwa wasubiri mataa mara mtoto anatokea anaaza futa vioo vya gari adi ananyanyua wipers nk afu anaomba sh 100,na hawa watoto dawa SI kuwakusanya tu na kuwaweka ndani hawawezi ilo life maana weshaathirika yabidi waangaliwe kitaalam zaidi (psycho-analysis)na watunzwe kisaikolojia zaidi na wavumiliwe!!

    haya maisha acheni tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...