Familia ya Nyenzi ya Dar es salaam inatoa shukrani za dhati kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kukamilisha safari ya mdogo wetu mpendwa Hassan Habib Nyenzi aliyetangulia mbele ya haki kufuatia ajali ya gari iliyotokea tarehe 15/5/2010 majira ya saa 1.30 jioni eneo la Mlandizi karibu na daraja la Ruvu, mkoa wa Pwani.
Si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja na tunaomba hii iwe ni shukrani kwenu nyote. Tunashukuru kwa misaada yenu ya hali na mali katika wakati huo mgumu, hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombe kwa Muumba wa Vyote Mwenyezi Mungu awape uzima na afya njema na awazidishie neema na fanaka katika maisha yenu.
Mungu Ailaze mahali pema
Mungu Ailaze mahali pema
peponi roho ya merehemu
-Amina
Salehe Habib Nyenzi
-Amina
Salehe Habib Nyenzi
poleni sana ndugu zangu..saleh naomba simu au email adress yako..yangu ni kckuyava@hotmail.com
ReplyDeleteahsante sana MAX KUYAVA U.K
poleni sana wafiwa..inasikitisha sana. His life was cut too short.
ReplyDeleteHizi ajali kila siku zinaleta majonzi mengi sana..
RIP
Poleni sana wafiwa. Jamani jamani hizi ajali mpaka lini? ni madereva au ni barabara. Tafadhali tusihongane leseni.Mafunzo ni muhimu.
ReplyDelete