Katibu mkuu wa jumuia ya Afrika ya mashariki, Balozi Juma Mwapachu, na naibu katibu mkuu wa jumuia hiyo, Alloysi Mutabingwa, wakitangaza kwa waandishi wa habari mjini Arusha leo kuanza rasmi kwa utekelezaji wa soko la pamoja la jumuia ya Afrika ya mashariki unaoanza rasmi kesho Julai 1, 2010 ambalo litalegeza masharti ya ajira,mitaji kuhamishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine,huduma kuzunguka katika nchi zote pamoja na wananchi wa nchi hizo kuweka makazi. Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika ya mashariki, Balozi Juma Mwapachu, na Spika wa Bunge la Afrika ya mashariki Mh. Abdirahin Abdi, wakitangaza rasmi kuanza kwa utekelezaji kamili wa soko la pamoja la Afrika ya mashariki kuanzia kesho. Picha na habari na Novatus Makunga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    Sasa watanzania na kuppenda starehe bila kufanya kazi...mambo kwishney..!!! wneye uchungu na nchi yetu wanakuja sasa!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    Mimi nadhani umefika wakati serikali kuchukua rai ya wananchi katika masuala makubwa kama haya, inaeleweka wazi jinsi watanzania tulivyo na tatizo la ajira sasa je tutapoanza kuvamiwa na wafanyakazi toka nje. Wananchi mpaka sasa hatuelelewi mpango wenyewe utakavyokua ni wazi mpango huu utafeli kama ule wa jumuiya ya Africa mashariki.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    Let the game bagin!mchakamchaka unaanza na baada ya miaka miwili utaona mkataba unavunjika maana kazi zote wageni wamekomba,na biashara kubwa wanazo wao,mtanzania kabaki ancheza bao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    Kwani watanzania wanaobeba box ugaibuni wanachukua kazi za akina nani? Tuwache mawazo yaliyopitwa na wakati... tusipojiendeleza na kuwa tayari kushindana tusilaumu wageni wanaoajiriwa nchini... Watanzania wengi wanaweza kushindana na si ajabu kwamba wanaweza kuajiriwa popote pale siyo to Afrika Mashariki...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Soko la pamoja la Afrika mashariki je Watanzania kweli wanataarifa za kutosha na jambo hili (Awareness)au ni baadhi tu ya watu.Tunahitaji kupigwa somo bado tupo gizani totoro.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Mjomba mtukanaji toka hapo Nakuru naye aja????

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    We subiri kuelimishwa - wenzako wanaanza kazi!!! Hao wanaoanza walielimishwa na nani??

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    Hiki ni kimbelembele cha viongozi wetu kujipendekeza sijui kwa nani. Majority ya wananchi wa tanzania hawaungi mkono jambo hili hata kidogo wanaburuzwa tu. Hatuhitaji wanyarwanda wala wakenya kuja kupora ardhi na bidhaa katika vijiji vyetu hapa! Tusidanganyike kwamba suala la ardhi halimo-ukishamruhusu mtu kuingia bila control wakati hata kitambulisho cha uraia watanzania hawana utamjuaje mgeni akinunua ardhi kinyemela hasa kwa uchu wa rushwa na vihela mbuzi uliotawala hapa bongo.Watakomba ajira na biashara zote hasa za mazao na hata zile ndogo ndogo na watajazana kwa gia ya kuoa dada zetu ambao huzuzukia wageni kufumba na kufumbua watoto wetu hawana chao.Ndio yale aliyosema Nyerere kubadili Almasi kwa kipande cha chupa...kama mazuzu vile. Na huu kwa wa-tz wanaoona mbali ni uzuzu kweli! Faida zake kwetu zinazidiwa na hasara na ugumu wa maisha tutakaoshuhudia and very soon! na huu si woga ...it is just plain facts lets get real!
    Hata hiyo Euopean Union tunayoiga imeshawaboa wazungu wanakumbukia walipokuwa kivyao ilhali wao wlijiandaa kwa miongo kama minne hivi seuze sie tunaoiga bila maandalizi?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2010

    Mnaongelea biashara na ajira tu ..ujambazi je? mmejiandaaje kiusalama? Sio kila mtu aja kununua na kuuza kuna majambazi nao watajaa kwa gia mbalimbali!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...