On behalf of the family of our sister Caroline Mmari, the Tanzanian Community in Southern California is sad to update everyone that police have found the body of Caroline Mmari buried in the backyard of the home that she lived prior to her disappearance. Currently the body is still with the police and will be released to the family once the investigation is completed. The husband of the deceased is already in police custody.
-
Meanwhile, the family of the victim is in the initial stages arranging to transport the body of Caroline Mmari back to Tanzania. On behalf of the family of the victim, the Tanzanian Community in Southern California is asking for your moral and financial support during this difficult time.
-
For those who are in the United States please send your financial support to Lilian Mgonja who is an aunt and a family representative of the victiom's family in Southern California: see the details below...
-
Meanwhile, the family of the victim is in the initial stages arranging to transport the body of Caroline Mmari back to Tanzania. On behalf of the family of the victim, the Tanzanian Community in Southern California is asking for your moral and financial support during this difficult time.
-
For those who are in the United States please send your financial support to Lilian Mgonja who is an aunt and a family representative of the victiom's family in Southern California: see the details below...
Bank of America
Name: Lilian Mgonja
Routing Number: 122000661
Account Number: 0475560122
-
We will provide additional updates as more information becomes available to us. Among pending issues, the family of the victim is planning for a memorial service but the date and venue will be provided once the police releases the body to the victim's family. You can reach the victim's family in the United States at:
southlandoutpatient@yahoo.com (mama Lilian Mgonja: victim's aunt)
frankray@rocketmail.com (Frank Ray: victim's uncle)
-
The Tanzanian Community in Southern California is extending prayers to the family of the victim and all those who are emotionally attached to the death of our beloved sister Caroline Mmari.
-
May her soul rest in peace, Amen...
Tanzanian Community in Southern California
Name: Lilian Mgonja
Routing Number: 122000661
Account Number: 0475560122
-
We will provide additional updates as more information becomes available to us. Among pending issues, the family of the victim is planning for a memorial service but the date and venue will be provided once the police releases the body to the victim's family. You can reach the victim's family in the United States at:
southlandoutpatient@yahoo.com (mama Lilian Mgonja: victim's aunt)
frankray@rocketmail.com (Frank Ray: victim's uncle)
-
The Tanzanian Community in Southern California is extending prayers to the family of the victim and all those who are emotionally attached to the death of our beloved sister Caroline Mmari.
-
May her soul rest in peace, Amen...
Tanzanian Community in Southern California
Mungu amlaze mahali pema. Poleni sana familia, Mungu atawapa nguvu.
ReplyDeletethis are why i left usa are not good being, why are klling us like dogs? im happy here life are goods and no bodies are killing others, Rip sisters,
ReplyDeleteOn behalf of the Ray family our true condolences go out to this family. Our son went to school with Caroline Mmari's 3 year old daughter. Our family is holding you up in praying. God will sustain you through these trying times. If my family is able to be of some assistance to the family in Southern California please email us at aray25@yahoo.com RIP Caroline
ReplyDeleteKha!!!
ReplyDeletejamani nimesikitika sana caro kama caro alikuwa ni mcheshi sana na alikuwa hana maaringo dada wa watu kwanini wamefanya ukatili wa aina hii na bado mdogo binti wa watu. otherwise wewe mbele siye nyuma, poleni wafiwa wote.
ReplyDeletePOLENI KWA MSIBA.
ReplyDeleteMIMI BINAFSI SIPENDI KUISHI MAREKANI KWA SABABU YA MAMBO KAMA HAYA JAPO KIFO KIPO MAHALI POPOTE. UGHAIBUNI KUZURI LKN DAH!!!!!!!
kwani mumewe mbongo au mmarekani? manake katusumbua kutafuta kwenye magugo weeee kumbe kamzika tu hapo hapo... kwanini wasitusogezee huyu kaka tumchome kibiriti? kumwondoshea mwenzio pumzi bila tu ya sababu yoyote au huwezi kujua mambo ya nyumba siajabu alimwambia sikutaki tena jamaa hasira kamuua.... dada zangu huku ulaya hakuna uganga mtu ukimuudhi tu anachukua bunduki na watu wengine hawataki mambo ya kuachana. Kifo cha dacaro kwa kweli kimesikitisha poleni sana familia nzima ya mmari.
ReplyDeleteRIP - Da'caro
RIP - Gary Coleman
RIP - Mwalimu JK Nyerere
da caro RIP
ReplyDeletepoleni wadau, huyo mumewe wamfanye apate death penalty na yeye
ReplyDeleteWhat ????
ReplyDeleteMi nilijua Caroline hajatoroka sababu sisi wanawake mara nyingi haswa tukiwa na watoto huwa tunakimbia nao, huyu bwana siajabu ana matatizo ya kisaikolojia. Siajabu kichwani kashavurugikiwa lakini hadi kumzika hapo nyumbani usiku alilalaje huyu jamaa?
ReplyDeletepoleni sana familia ya mmary
Mme wake alikuwa munugu, si unajua hawa jamaa, bangi bangi kwa sana. poleni sana.
ReplyDeletehawa si watu, wabongo huwa tuna kimbia tu, lakini hawa jamaa hawafanyi hivyo.
Ughaibuniiiiiii!!
ReplyDeleteHawa watu wana roho mbaya sana, mimi siwapende hata kidogo, nawashangaa wanawake wanzangu kukimbilia wazungu, eti maisha ndio yatakua poa. Wakati ukishapelekwa huko unaenda kua mtumwa wao. Tutabanana hapa hapa na wabongo wenzetu na kitaeleweka tu, hatakama uchumi unayumbu, iko day tutatoboza.
Poleni sana Familia ya da Caro.
Mungu ampumzishe kwa amani. Amen.
Mike Ngura kwani ni lazima uandike kwa kiingilishi ndugu yangu wewe? duh unatutia aibu bwana!!!
ReplyDeletePoleni ndugu na jamaa wa marehemu.
ReplyDeleteMichuzi nadhani ushachoka na maombi yangu lakini kwa kupata taarifa ya mauaji haya, narudia tena. Una uhakika kama yule dada aliepotea ujerumani yuko hai? au mumewe ndio kafanikiwa kututia changa macho?
jamani dada wa watu mbona ameuwawa kikatili namna hiyo?ni kosa gani alilolifanya kubwa kiasi cha kustahili adhabu kubwa kiasi hicho tena kutoka kwa mumewe?nimekuwa nikisoma tangazo la kumtafuta mda mrefu kumbe mume mshenzi amemfanyia ukatili.jamani kuna usemi usemao alieuwa kwa upanga atakufa kwa upanga.mi nadhani nayeye anastahili adhabu ya kifo.mtoto arudi tanzania atatunzwa na familia ya marehemu.huyo mwanamme sio mtu hata jamii inatakiwa kuwa nae makini sana.nimeumia sana kwa kweli.R.I.P.kuna na katoto pia kalikuwa kanatafutwa kaka michuzi tunaomba taarifa zake kama kapatikana au vipi?
ReplyDeleteHuyo 'mumewe' ndie aliyemuua! Period! I can bet my head on that!
ReplyDelete*Je, alichukua hatua gani za kumtafuta baada ya kugundua kuwa 'mkewe' 'katoweka'?
Kama hakuchukua hatua zozote ni kwa vile alikuwa anajua ALIPO! Si alimfukia mwenyewe bwana, baada ya kum-kosovo?
* Ameniudhi sana huyo 'mume' wa Carol! Ndio nini kukaa kimya na kutuchora sisi wote hapa tukiumiza vichwa kujaribu ku-take wild guesses kuwa ni wapi Carol anawezekana akawa yupo, wakati yeye alikuwa kabisa anajua kuwa Carol kamfukia nyuma ya nyumba yao!
* Huyo jamaa kauka KWA KUKUSUDIA, ndio maana hata hakwenda kujisalimisha polisi wala nini. Aisee inaelekea ana akili ndogo kama za panzi! Hivi alikuwa anafikiria nini? Kwamba haitakaa ijulikane kuwa yeye ndio aliyemuua Carol? Wakati mwili uko nyuma ya nyumba tu? IMBECILE!
* To all men (na baadhi ya wanawake - hasa wale ndugu zake wa Palestina wa kule Moshi), jamani, kama 'umemchoka' partner wako, labda kachuja au nini (si unajua tena sisi wanawake wengine tukijifungua - sio wote tunaoweza kurudia hali zetu za 'usichana', please MWAMBIE! "Honey, my love for you is not the same - so IT IS OVER!". Au mwambie, sikupendi tena, au tafuta namna ya kumyeyusha, au ondoka wewe mwanaume muachie mwamanke nyumba, or something like that! Nafikiri hiyo ni bora kuliko kufikia uamuzi wa kumuua 'mkeo', kisa - umemchoka! Kwa wale wenye upendo wa kweli, huwa wanawatafutia wake zao personal trainers au wanawaandikisha gym. Please don't kill me atlest! Kwani watoto huwa mnawataka wenyewe (wanaume), na kwa bahati mbaya, watoto wengi huja kwa cost ya u-chabby!
* Huyo baba anyang'anywe huyo mtoto mara moja, kwani hastahili kuwa mlezi wa watoto, na wala si wa kuruhusiwa kukaa karibu na watoto. Kaweza kumuua mtu mzima, sembuse mtoto ndio atamfanya nini?
* Samahani kwa hili, lakini nilifikiri kuwa nyie huko marekani hamuombi michango ya misiba? Au nilisoma vibaya humu kwenye Blog?
*Marekani sintakaa nikanyage n'goo!
MAY CAROL REST IN PEACE, AMEN.
Poleni kwa 'Gazeti'.
I did suspect her husband from the beginning.May god rest her soul in peace. What a sad news to hear poleni wafiwa
ReplyDeleteMungu wa upendo, wa Rehema, Bwana uliye juu Wewe mweza yote Pale ambapo hatuwezi tena Wewe upo. Kaa karibu na familia hasa watoto na wazazi wa Caro.
ReplyDeleteJaribu ni kubwa, pigo halina kipimo, Bila WEWE Bwana hatuwezi!Waape nguvu wafiwa,Tunaomba ulinzi wako kwa watoto wetu wote walioko ughaibuni Bwana. Roho wako Mtakatifu aliye ndani yao wote awafungue macho ya kiroho kusudi waone kwa mbali kabla majanga hayajawapata. Mungu wa majeshi, watoto ni baraka kutoka kwako na kawaida wao ndio watuzike sisi wazazi. Uchungu mkubwa sana, jeraha miyoyoni halina Daktari mwingine ila Wewe Mokozi.
Poleni, family, watazania wa southern California, wa wanyumbani na wote pale mlipo
RIP Caro "Ati twonane mtoni.......
Grandma
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Pema Peponi, Mumewe alikuwa MMAREKANI.
ReplyDeleteKaka Michuzi Vipi suala la Michuzi Youth Social Initiative??Nakukumbushia ni vizuri ukalianza suala hili wadau tupo kukupa Nondo
ReplyDeletenimetuma hapa najua utasoma kwani hujibu email tukikutumia
Mdau
Khamis Hassan Batanyaga
Ukerewe
daaah,RIP Caro..
ReplyDeleteWhoever posted this announcement, please do as favor of revealing the identity of the husband!!!!
ReplyDeleteIn any case he does not deserve to called a human being, he is just an animal only that he walks on two legs!!!!!!!!!!!!!!!!!
Oooh God, imenisikitisha sana.Poleni sana wafiwa Mwenyezi Mungu awape nguvu na amani katika kipindi hiki kigumu. May God Rest her in Peace.
ReplyDeleteAmina.
oooh my dearest caro jamani Mungu akulaze mahala pema peponi dear,nasi twaja we umetangulia tu..Mungu ni mwema damu yako haitopotea tu bali maajabu yatafanyika na muuaji atapelekwa mbele za haki..
ReplyDeleteJamani nimesikitika sana na taarifa za kifo cha huyu Dada Caro simfahamu lakini nilikuwa nafuatilia sana kujua kama alipatikana kupitia blog ya jamii. Kweli ubinadamu umekwisha kabisa, yaani mtu anathubutu kukatili uhai wa mwenzake kisa nini? Poleni sana familia ya Caro, inauma sana kuondokewa na mpendwa wenu lakini ndo hivyo tena imetokea. Mungu awape nguvu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kipenzi chenu. RIP Caro.
ReplyDeletemdau wa blog ya jamii
poleni sana watanzania wote. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu.
ReplyDeletepili naomba kuwakumbusha dada zetu mlioolewa na wazungu na mpo majuu. jaribu kuwa karibu sana na kaka zenu pamoja na dada zenu walio karibu na nyie. amini usiamini itasaidia.
Mungu ilaze roho ya marehemu CARO mahali pema pemoni. Nilikuwa mfuatiliaji mzuri kutaka kujua ndugu yetu amepatikana lakini ndio hivyo tena. Mungu awajalie faraja na uvumilivu familia ya marehemu. AMEN
ReplyDeleteman that is born of woman hath but a short time to live, and is full of miseries.
ReplyDeletehe cometh up, and is cut down, like a flower.he fleeth as it were a shadow, and never continueth in one stay.in the midst of life, we are in death.of whom may we seek succor but of thee, O Lord, who for our sins art justly displeased.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
kwa akina dada wa kibongo, WANAMME WA HUKU SIYO MCHEZO, HAWANA UTU HATA SIKU MOJA...AKIKUKAMATA UNACHITI AU UKITAKA KUMUACHA AU KAMA MAISHA NI MAGUMU NA UNA LIFE INSURANCE KUBWA, MARA MOJA ANAKUUWA...MSIWAONE WANANG'AA KWENYE MAGAZETI, HAWANA KITU HAWA...BORA WAKINA KAKA WA KIBONGO, AKIKUMATA UNACHITI ANAKURAMBA VIBAO TU, BASI MAPENZI YANARUDI....POLENI SANA WANA NDUGU na RIP dada yetu
ReplyDeletePoleni sana ndugu kwa matatizo yaliyowapata,
ReplyDeleteHiyo ya Mike Ngura inaitwa LUGHA BAMIZA manake huwezi jua ni ung'eng'e wa asubuhi, mchana, au jioni, Aibu bro
jkl
jamani hata mie nimeguswa na hili RIP Caroline. Nilikuwa nimeona kwenye fb kuna dada mwingine nafikiri wa west africa alipost kumtafuta
ReplyDeletehttp://www.facebook.com/pages/Missing-Persons-Unit/107453225943786?v=stream
na akasema kuwa alikuwa 3monts pregnant? kama ni kweli ina maana huyo mume kamuua mama na mtoto asiyehata zaliwa. Kwa mnaotaka kuona kuona picha hii habari pia ilikuwa kwenye habari kwenye kituo unaweza kuiona kupitita hapa
http://www.cbs2.com/video/?id=135871@kcbs.dayport.com
yaani dada wa watu alikuwa anaonekana mpole sana sasa huyo baba siajabu tu frusturation na maisha maana hii economy depression imewafanya watu wachanganyikiwe. Mungu awalinde watoto wake.
jamani caro, siamini, ulikua social leader wetu ngarenaro sec school arusha, truly i can not believe this has happen to u, the way i knew caroline back to school, very social, hakuendekeza majungu, mungu alimjalia akili ya kufaulu, na kikubwa zaidi ni jinsi alivokua hana ushoga,
ReplyDeletemay ur soul rest in peace CAROLINE, i curse who did this to u....
Jamani mbona watanzania wanauana jamani . Msigeneralise namna hivyo . Hayo ndio maisha na sisi wanawake kunakitu kinaitwa uvumilivu . Hayo ya zamani ukimwona mwanaume anadrama usijing'ang'anikize maana yatakukuta . Be careful with the sighs of abuse .
ReplyDeleteNasikitika kusema kuwa polisi wa magharibi Mara nyingine ni wabaguzi sana, walijua bibi ni foreigner na chief suspect ambaye ni mume ni raia!! Matukio ya wake au ndugu kuuliwa na kutupwa mtoni au kufukiwa kwenye back yard ya nyumba ni mengi sana huku nchiza magharibi! Yaani suala la kuchukua hatua ya kuchunguza house backyard lilitakiwa kuwa la kwanza walischa makusudi coz walijua kabisa mazingira ya kupotea dada yetu huyu chief suspect alikuwa ni mumewe ikizingatia mtoto yupo!! Haiingii akilini after three months of the disappearence ya dada yetu eti ndo wanapata akili ya kwamba houseback yard ichinguzwe!!! Tunaishi nao tu lakini hawapendi tujaze nafasi kwao!!! Hawajui kuwa na sisi bongo ingekuwa green pasture wao wangejazana kwetu!!! Imeniuma sana!!sasa tunaambulia mifupa tu!!!! Dada zetu hawaii watu achaneni nao wanawatumia lakini upendo hamna na haya ndi matokeo!!!! Sisi kaka zenu Tupo timejaaaa huku kwa niño tusipeane wenyewe kwa wenyewe Tena sisi tuko natural sana!!!!
ReplyDeleteJAMANI WATANZANINA TUWE NA UFAHAMU MPANA SANA, KWANI TUJUE HAWA TUNAOISHI NAO TUNATOFAUTIANA SANA UTAMADUNI. PILI THAMANI YA UTU NA UHAI WA MTU KWA MTAZAMO WAO NI TOFAUTI SANA NA MWONO WETU SISI.
ReplyDeleteWENGI WANAOAMUA KUISHI PAMOJA WENYE ASILI MOJA NA UTAMADUNI UNAOFANANA WANAJUA NAMNA YA KUCHUKULIANA KATIKA MATATIZO, LAKINI UTAMADUNI WA WENZETU HAWANA USTAHIMILIVU NA NI WEPESI SANA WA KUCHUKUA HATUA NA KUBONYEZA TRIGER KWANI HAWAJALI UHAI WA MTU.
POLENI WANAFAMILIA NA WATANZANIA WOTE. MATOKEAO HAYA NI FUNZO LA MAISHA KWETU WENGINE.
poleni wafiwa such a sad news really, haya wadada mnaotaka kuolewa na wthungu, angalieni hayo, aka mie bora kufa kwa ukimwi kuliko kuwawa kinyama hivyo, haya kina mk etc semoni hapo
ReplyDeletewewe anon wa Fri Jun 11, 10:39:00 AM una akili finyu namna gani? unadhani wabongo hawaui? unadhani hapa tanzania wabongo wangapi wameua wake zao? kuna mbongo pia ameua binamu yake huko usa. so shut up usiruke tu na kulaumu jambo usilolijua.
ReplyDeleteTanzania asubuhi unasikia tu fulani amelala usiku asubuhi hakuamka, hapapiti uchunguzi wowote mtu anazikwa. Jee unajua ni wangapi kati ya hao wanakuwa wameuliwa na wapenzi wao? mtu anamziba pumzi mwenzake halafu asubuhi anapiga mlio basi mambo yamekwisha.
Kwa nini asilimia ya vifo vya tanzania ni vya mtu kufa akiwa amelala? jiulize hilo! jawabu ni kwa sababu hakuna post morten kwa kila anaefariki nyumbani (kitandani)
RIP Carol,
ReplyDeleteIts so touching, Carol alikuwa jirani yangu oyesterbay na tulisoma wote Bunge Primary School.Inasikitisha sana, Pole sana Manka kwa kumpoteza Dada yako nakumbuka mlikuwa wawili tu katika familia na mlisha poteza wazazi wenu baba na mama...Tunawaombe Mungu awape nguvu wafiwa...Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe..
mdau wa Fri Jun 11, 11:06:00 AM shairi refu unachoeleza kiko obvious kama unafikiri huyu mumewe ataachiliwa vipi akae na mwanawe? tumia bongo ndugu!
ReplyDeleteWadau we are talking about home violence, home violence haina kabila, utakuta mtu mstaraabu nje lakini nyumbani ana punching bag. And when it gets out of hand this is what happens. It has nothing to do na mzungu, mchina, mwaafrika, etc.Intervention should have been done along time ago. Poleni waafiwa
ReplyDeleteRIP Caroline. Ingawaje simfahamu lakini roho imeniuma sana...Ameacha mtoto mdogo hivi kweli na mimi nilisema toka mwanzo waanze na huyo mume wake. Siku zote hizo alikua wapi hakuripoti mkewe amepotea mpaka ndugu zake waanze kutafuta....Duh maisha haya!!!!!! I hope she died quickly and she didn't suffer at all...May God rest her soul in peace....
ReplyDeleteNakumbuka kuna mtu alisema hapa kwenye blog wao ni yatima ni kweli? Inasikitisha sana kama ni kweli wadogo zake nyumbani dada naye anauliwa hivi....
Watu wanaosema marekani hukai au sijui watu wa namna hii ni vile au ni vipi...Ukweli ni kuwa kila nchi ina mashetani wake. Uwe unaishi Tanzania au nchi yeyote ile. Ukipata bahati mbaya kukutana na shetani ni bahati yako mbaya tu. Yule mtanzania aliua binamu yake huku naye tutasemaje? Na huyo mwanaume ni mzungu au black American it real doesn't matter kawa vile shetani hachagui color.
Tushukuru Police wametafuta mapema na kumpata ingekua cold case au another statistic tu. Mwanamke kapotea...I wonder kwa nini haikumfikia Nancy Grace hii story...
Tunatakiwa kuwa caution tu na kujua culture za watu na mtu unayehusiana naye kabla ya kujiingiza kwenye watu wa nchi nyingine...It is sad nikiona mtu anaingia USA within a months anapata mtu na kukubali kuoa/kuolewa naye. The more ninaishi huku the more ninaelewa tuko tofauti kwa culture sana tu.
Wao wanategemea professional cousiling a lot. Na wasipokua na hela za kwenda kutafuta psychologist, therapists ndio hivyo hawajui kusolve matatizo yao kidiplomasia. Ni kuua tu...na pia kuna wengine ni schizophrenia na bipola wanatumia dawa tu ukiwaona njiani ni kama watu wakaida tu lakini siku asahau kuchukua dawa zake ndio utajua yeye ni nani. Afathali kwetu tukiwa wadogo tukimwona Hamisi Nyalo tunajua yuleee kichana tunakimbia. Huku wengi vichaa wanatumia tu dawa sasa unawaza kudate huyo mtu usijue lakini siku baada ya siku ndio unaanza kuona mambo ya ajabu na hapo uamue kuondoka na yeye ameinvest emotion so much utakoma....
Na ufisadi wao ni kuwa Wazungu watakuua kwa life insurance na black Americans atakuua akijua unataka kumuacha mkiwa naye wakati wewe ndio unamtunza na kumlisha...
Na wote hao watakuua once mna watoto na unaanza kudai kuachana na kutaka kudai child support.
Ni bahati mbaya kwa Caroline alikutana na huyu mtu ....Poleni wafiwa
kama Michuzi hebu tupe updates za Sheryl naye ni vipi?
JAMANI CAROOO mimi hata ciamini. MUNGU akulaze mahali pema mamii u will alwayz b remembered jamani hata c amini kabisaaa. pole sana cathy n bro for all these....
ReplyDeleteKuna watu wamedata humu ndani! LOL! Eti mtu anamziba mwenzie pumzi, halafu asubuhi anapiga mlio!
ReplyDeleteLisemwalo lipo, kama halipo litatokez (God Frobid).
Tutabanana na wabongo tu kwa kweli, na sina maana ya kumlaumu yeyote, kwani kila mtu na preference yake. Wengine Rangi za Maji ya Kunde, Damu! Au vikizidi sana ..,,
Rest in Peace Carol.
Poleni Sana Wafiwa.
KIKUBWA HAPA WADAU NA WANANCHI WENZANGU NI KUWAPA POLE NA SUPPORT FAMILIA YA MMARI.
ReplyDeleteTOA MCHANGO WA HALI NA MALI NA SIYO KUJARIBU KUELEZEA UNAVYOWAFAHAMU WATU WA UKEREWE/KISHUMUNDU.
RIP BELOVED DADA CARO.
lol mdau umenikumbusha hamisi nyaloo kwa kweli acha tuu nusu atutoage roho lol. ila kweli wenzetu wako sana tofauti na sie swala la kuachwa hawataki kusikia hata kama ndoa ni ya makaratasi wanageuka ving'ang'anizi mwishowe wanakutoa roho kama yale mauaji mengine ya mtoto wa mazula na mchumba wake sijui iliishiaga wapi nayo mtu ukiona hakieleweki ni bora urudi kwenu kwa mda kwanza manake hata ukiamia state nyingine mtu kukupata pia ni rahisi hasa foreigners hivyo ni bora utafite libabu la miaka 60 huko hayanaga shida, poleni sana wafiwa
ReplyDeleteMimi nasema ni muhimu ku-muuliza Mungu na kupata ishauri kabla ya ndoa.
ReplyDeleteSiku hizi ukiwaonya watu kuhusu mchumba wanakimbilia kufikiri ni wivu badala ya kuchunguza.
Ukiwa makini watu wenye kasoro zilizovuka mpaka huwa zinaonekana. Jambo la Pili ni kuwa karibu na watu wa msaada kama kanisa hivi.
Poleni sana wafiwa.
Poleni sana wafiwa, inatia uchungu sana.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awapeni subra.
(US Blogger)
sijawahi kumjua huyu dada but sijui kwanini roho yangu ilikua haina amani frm day one limewekwa tangazo la kupotea kwake.jamani kama ni mume wake kweli kamuua ndugu na marafiki mlioko huko fuatilieni suala la mtoto aliyebaki maana huwezi jua huyo mume maybe alikuwa anawaabuse wote either violently au emotional au physical.hivi vitu si vya kuchukulia ju juu,tuanyoyaona ktk movies and tv series yanatendeka duniani,Mungu ni mwema na mwaminifu haki itatendeka na roho yake itapumzika kwa amani.na kwa wale familia yake Mungu atawatia nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.jamani tuzidi kuombeana na kupendana maana tunakoenda huko sasa ni kubaya ,binadamu wamegeuka wanyama,na tulioko nchi za watu ndio inatisha zaidi,tuombeane jamani n kama ikiwezekana tutafute hela then turudi kwetu kwenye amani na upendo though kila sehemu kuna mashetani wake na wale wanaopenda kuharibu kazi za Mungu LAKINI TRUST ME NYUMBANI NI NYUMBANI HATA KAMA MAISHA YANAKATISHA TAMAA BUT WHEN IT COMES TO THSI THINGS I MISS HOME.mUNGU AMAJLIE MTOTO WAKE ALIYEBAKI FARAJA,AFYA NA UZIMA KTK MAISHA YAKE MAANA DUNIA YA SASA KTK UMRI HUO KUISHI BILA MAMA JAMANI NA KAMA KWELI NA BABU NA BIBI HAWAPO BASI NI ANAHITAJI MAOMBI YENU ZAIDI NA MTOTO ATAKAVYOISHI KWA AMANI NA ROHO YA cAROL ITAPUMZIKA KWA AMANI.UYAANI MACHOZI YANAITOKA HAPA JUST CANT IMAGINE NDIO DUNIA TULIYOPO SASA.May her soul rest in eternal peace .AMEN
ReplyDeletePoleni wafiwa tumesikia upande mmoja wa matokeo sasa tusubiri upande wa Mume nini ataeleza
ReplyDeletePatric
Msiba mkubwa sana. Poleni wafiwa. Sista wangu mmoja hapa arusha aliyesoma naye ngarenaro kwa father babu anasema kuwa mumewe alikuwa ni mmarekani mweusi. Lakini pamoja na uchungu tusi-generalize na kusema kuwa watu fulani ni wabaya. Katika kila jamii kuna wema na wabaya. Mola amlaze Carroline pema peponi. Amin.
ReplyDeletejamani mimi nimeshukuru nimerudi toka ughaibuni kwa salama,maana wazungu na hao raia wa nje ni makatili, siwapendi sijui kwa nini wabongo tunaona ndio watu wa maana ,watu ambao hawana imani,enyi wanawake wenzangu mliobakia huko msibabaike na makaratasi msibabaike na wazungu hao watu ni makatili hili liwe somo kwetu jamani,dada wa watu alikuwa anatafuta tuu maisha yake na kufanya kazi kama mtu mwengine sasa ona ameacha mtoto mdogo maskini,RIP dada Caro sikujui ila kifo chako kimenistua na kunihuzunisha,this is why namshukuru mungu niko bongo hata kama ina malaria,maji machafu lakini niko kwetuuu!!!
ReplyDeleteMIKE NGURA ULIISHI U.S.A YA WAPI NA HICHO KIZUNGU NI CHA NTWARA NINI NJOMBA?
ReplyDeleteKWANZA NAPENDA KUTOA POLE KWA WAFIWA WOTE,MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI DADA YETU BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA.
ReplyDeletePIA NAOMBA NITUMIE WAKATI HUU MGUMU KUTOA USHAURI TU KWA KUWA MIMI NAISHI HAPA UNYAMWEZINI KWA MUDA SASA MAUAJI KAMA HAYA TUMEYAZOEA KUYAONA NA KUYASIKIA KATIKA REDIO KILICHO KIGUMU KWETU KILA BAADA YA MUDA NASI HUTUKUTA MASHAKA HAYA KWA WATANZANIA WENZETU AU WAAFRIKA KWA UJUMLA HAPA SIKUSUDII KUWAHESABU HAWA WAMAREKANI WEUSI KWANI WAO NDIO WAUAJI WENYEWE.
USHAURI WANGU NI KUWA DADA ZETU WAWE MAKINI SANA NA HAWA JAMAA WAKATI WAKITAKA URAFIKI NA HATIMAE UCHUMBA NA NDOA HUVAA NGOZI YA KONDOO BAADA YA MUDA HUITOA ILE YA CHUI AMBAYO NDIO "ORIGINO"
SISI TUPO TELE HAPA JITAHIDINI NA SISI MTUPE NAFASI YA UPENDELEO KATIKA MAPENZI KWANI HAWA SI WATU HAWAJUI MSALIE MTUME WAO KUUWA KAMA KUVUTA SIGARA HAWAONI TABU NDIO MAANA HUKO JELA WEZI NI KIDOGO KULIKO WAUAJI.
MUNGU ATAMLIPA HAPA HAPA DUNIANI HUYU BWANA ALIYEMUUWA DADA YETU.
AMIN.
KAKA KUONA SAN DIEGO.
May the almighty help the family of Caro.
ReplyDeleteRIP Caro
Mike Ngura!!! Duuuuhhh!!!
ReplyDeleteKiinglishi gani hicho hata chekechea pale tabata hawezi ongea mchapo huo? Wewe umeondoka kwa kuwa watu wanauwana au huna makaratasi? Na kwa kiinglish hicho, makaratasi yangekuwa hayawezekani. Ebu nambie, unaanzaje kumtokea demu kwa kiinglish kwa style hiyo?
Poleni wafiwa.
Michuzi, Da Sherry mpaka tumuone kwa macho, simu si kitu, utapeli mtupu. Zingatia hilo michuzi, anaweza akawa hai lakini ni mfungwa basement na anashikiwa mtutu kujibu simu zenu.
Tumeomba sana, awasiliane na wabongo wanaoishi huko mbona hajafanya hivyo na hajaonana na hata mmoja hadi sasa?
Mimi naona haya ni mazinguzi tu. Hii kesi haijaisha, hata ung'ang'anize namna gani, shery aonekane kwa macho kwa wadau na wajue anaishi wapi na anaishije. wahakikishe kuwa ni mzima na si mfungwa
du inatisha kweli yaani hata hakufikiri kuwa ana mtoto wa miaka miwili pia alikuwa na ujauzito kwa mujibu wa tangazo la kupotea kwake
ReplyDeletehatari nashindwa hata kuelewa alikuwa jambazi nini. poleni wafiwa ila iwe funzo kwa ndugu zetu wanaotaka uraia wa marekani kwa njia ya kujilazimisha kuolewa na watu ambao hawajuani vizuri
caro jamani alikuwa mcheshi anaongea na kila mtu,nakumbuka from mazinde juu...RIP dada!!
ReplyDeletepole sana cathy
NEY-Birmingham.
jamani?ee Jehova nini hiki?uyu dada kaniuma,simjui ila nilikua nafatilia hii newz kwa ukaribu nijue hatma,nilimwombea sana na wabongo wote waishio nje
ReplyDeletesina hamu
KILO hujatulia wewe,umenifanya nicheke
ReplyDeletepoleni sana wafiwa jamani,Mungu wa upendo na awatie nguvu sana
Mike Ngura umeanza lini kuichukia USA? Unakumbuka ulipokuwa ukitukana watu kwa kumpinga rais wako Bush?
ReplyDeleteNgoja nikukumbushe, fuata link hii:
http://issamichuzi.blogspot.com/2006/09/benabue.html
Jamani wafiwa, poleni sana, huyu alikuwa dada yetu sote, yaliyompata yanasikitisha na yanaweza tokea kwa yeyote yule. Tuwe makini tu na watu tunaohusiana nao.
Poleni wafiwa
ReplyDeleteHii blog komesha.. Mtu unapewa na references ...Haa!!!! nimesoma hiyoo issue ya Mike Ngura nikafuata niangalie ilikuaje huko nyuma mweeee jamani Michuzi weee babu kubwa na blog yako I am speechless...
Mike Ngura weeee....Wanasema usinyie kambi miaka 9 ukakimbia na kithungu hicho???...box ulilokua unapiga lilikua mute mute no communication at all??? Umeniangusha
mungu akulaze mahali pema peponi carol.
ReplyDeleteulikuwa rafiki yangu bunge primary tulimaliza wote 1999.
hii inasikitisha.