Mtangazaji mahiri wa TBC Elisha Eliya
Ankal salamaleko,
Siku nyingi niko kimya, ila leo naingia tena hapa kutoa pongezi za dhati kwa TV yetu ya taifa ya TBC kwa kazi nzuri waifanyayo tokea kumekucha hadi kumekuchwa.
Hakika TBC imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwa njia ya TV, kiasi si ajabu kukuta ikiangaliwa kila kona hata kabla ya kombe la dunia. Pia nampenda sana kijana huyu Elisha Eliya anayejilawa kila asubuhi nakina Marin Hassan na wengine katika kipindi cha Jambo.
Ombi Elisha naomba abadilishiwe hiyo suti...
maana kila siku namwonaga nayo hiyo hiyo tu.
Kwani hana ingine ama ni jezi ya kazi?
Mdau wa Mafia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    Naungana na mdau kuwa TBC1 inavuma sana. mimi pia ni mdau wa hiki chombo haswaa nisikiapo sauti ya Marin Hassan Marine ahhh naburudika sana, wnginge ni Gasto Msigwa anaripoti kutoka Mbeya na maeneo ya jirani na Mbeya, na Emmanuel Amasi wa Musoma na Tarime, kuna somebody Paul huwa anaripoti toka Mwanza na kwingineko kanda ya ziwa. Agnes Mbapu na yeye ni hodari sana ila naomba ratiba ya kusoma taarifa ya habari iangaliwe upya manake mtu mmoja anakuwa anasoma habari kila siku kwa muda hata wa wiki mbili, wabadilishe ratiba kuwe na shift ya hapa na pale, salamu za dhati kwa Jaffary haniu, na Neema Mhando

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    Yebooooo, jamani suti ni ya kazi hahahahahahahahahahaha :D

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    mdau wa mafia nimekukubali katika kufikisha ujumbe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    Hongera Tido Mhando TBCI kwa sasa ipo juu sana. kwa kweli mnaongoza na wengine wanajikongoja.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    hongera TBC, lakini bado mna changamoto hasa wakati wa taarifa ya habari mara nyingi mitambo yenu huwa inakwamakwama na kumuacha Msami au Dyauli wakiomba radhi,ajirini mafundi wenye viwango

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2010

    Hee kwani kununua suti nako taabu? kwakweli ukinzingatia hii ni television ya taifa lazima mtu uonekani tofauti. na TBC inaonekana pande nyingi sana. na uongozi wa TBC unatakiwa kuweka watu ambao wanakuwa makini hasa kwenye mavazi na mtu anayefuatilia kuona mtangazaji yuko smart na tofauti. sio anakuwa na jezi moja kama timu ya mpira

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2010

    Huyu kijana anapendeza sana kwenye luninga na sauti yake ni nzuri tatizo hajipendi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2010

    wamafia naona mmecharuka na ankal

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2010

    Mdau wa mafia nami nakuunga mkono kwa yote , ila tumshauri ndugu yetu Elisha achanganye suti yaani asiwe anavaa suti za mistari tu, ikiwezekana achanganye na plain suit. Yaonekana anapenda sana suti za mistari sana! Hongera sana Elisha. Keep it up!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2010

    Hakika Anony wa Wed Jun 30, 09:40:00 AM umesema kweli hata mimi namkubali sana Gaston Msigwa, Jamaa yuko vizuri sana japo hatajwi tajwi, lakini habari zake kama bbc, cnn. Hongera sana Msigwa.
    Ila yupo Songea sio Mbeya.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 30, 2010

    haters stop hating.....elisha go, go ,go

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 30, 2010

    Msimlaumu mtangazaji, yawezekana watangazaji wa TBC hupewa nguo ndani ya studio kabla habari hazijarushwa.

    Hivyo mtangazaji anakwenda kazini amepanda daladala na mavazi yake ya kawaida. Ila akiingia mjengoni TBC ktk 'locker ya TBC' kuna suti moja tu ya mistari, hivyo kama ndo hivyo basi TBC waongeze bajeti ya 'locker ' za nguo za wafanyakazi wake.

    Mdau
    MpigaBoksi
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 30, 2010

    Ubunifu wa Tido Mhando ni mkubwa sana. jamaa tangu achukue shirika, linatisha. Mimi nilikuwa mvinu wa kuamka asubuhi lakini jambo inanikosha hadi imekuwa jadi kuangalia vipindi vya asubuhi. taarifa yao ya habari kama CNN, BBC nk. Ila waandishi wao wa Mikoa mingi hawasikiki. Wanahabari wao wanaotisha ni Gaston Msigwa, Songea, Emanuel Amasi, kwa warianchari na warianchoki, Ben mwaipaja anatisha manyara, kwa habari moto moto-nakumbuka sekeseke la shekifu na sendeka nilichwa mbavu sina, kuna huyu richard leo mwanza, na mwanadad mtenzi tanga. Hawa wanajituma ila wengine mmh! wafanyiwe screening kwakweli. Big up Tido, moto uwe huo huo na endeleeni kuongeza vipindi vingi vya hapa nyumbani kama vile kipindi cha makala za nyumbani tufurahie kuona changamoto na maendeleo ya nchi yetu.

    Mdau Morogoro

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 30, 2010

    kazi ya utangazaji ni lazima uwe smart uvutie watazamaji sio muuze sura na kauka nikuvae nunua suti nyingineeeeeeeeee hiyo ishaeksipaya na macho yanaboreka new suti pliiiizo

    ReplyDelete
  15. Jamani huenda anazosuti nyingi ila za aina moja!nitumie vipimo Elisha nikakushonee pale tandale,isiwe shida!Gerson is the best,anajua anachofanya na fikiria he is reporting from Songea si dar labda angepata exposure kubwa!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 01, 2010

    Kwakweli tunamshukuru sana mdau wa mafia leo kijana elisha amebadilisha suti!! ila nadhani suti yenyewe kafanya kuanzimwa maana inaonekana kubwa!! sasa kijana elisha unakipaji saaana cha kutangaza changamoto uliyonayo ni kujipenda na kuwa na mvuto kwenye luninga. watu unaowahoji wanakuwa smart kuliko wewe. Hata leo jamaa walipendeza na suti zao ila wewe umevaa suti kubwa sijui umechukua ya nani? Hongea TBC ila mna changamoto mbele yenu ya kuhakikisha watangazaji wenu wanakuwa smart.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 01, 2010

    Susan na Tido TBC iko juu sana na imepata wapenzi wengi saana. Hebu wekeni mchakato kwenye mavazi ya watangazaji wenu. Kwanini kina Msami, Haniu, Marine wanabadilisha suti then kijana Elisha anabaki na suti moja? Hebu wekeni iwe ni moja ya kigezo cha ajira yenu kuwa mtangazaji wa luninga lazima awe na suti za kutosha.
    Au kama suti ni gharama! basi wavae tu shati na tai itapendeza zaidi kuliko mtangazaji kuonekana kavaa jezi moja kama timu ya mpira tena ya mchangani ambayo bado haijapata mfadhili ikawa na uwezo wa kununua jezi za kubadilisha. Jitahidini saana viongozi wa TBC

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 01, 2010

    Hongera TBC kwa kuwa na vipindi vinavyotuvutia, ila Elisha jifunze kujipenda kwani mshahara wako haukutoshi kubadilisha suti na mashati? kama uwezo wa suti ni mdogo vaa tu suruali na shati na tai. au ni lazima kuvaa suti?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 01, 2010

    TBC mpeni nafasi zaidi Gaston Msigwa wa Songea, huyu kijana anauwezo mkubwa sana kuliko mnavyomchukulia.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2010

    hata kama anayo hiyo suti moja so what... yanawahusu? muacheni afanye kazi yake!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2010

    Kuna watangazaji waliopo mikoani lakini kwa kweli wanapaswa kuwepo makao makuu Dar es salaam ili kuongeza uhai hapo studio za TBC1.Grason Msigwa na Emmanuel Amasi waje mikocheni kusoma taarifa ya habari.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2010

    Bila shaka maoni ya watanzania yatakufanya ujirekebishe kijana elisha. na kaka michuzi hongera kwa mtandao wako, maana kwa mambo kama haya utasaidia kurekebisha tabia za watu wengi

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 02, 2010

    Yote tisa kumi Kijana Pendaeli Omary, Michezo habari yeye yumo sana... TBC1 ehh!

    Madau Ahaz

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 02, 2010

    jamani jamani watanzania !!!! suti ni nini? mi nafikiri mnahitaji zaidi anachokisema pale na si suti aliyovaa akivaa suti nzuri na akawa anaboronga si mtasema afukuzwe kazi kabisa ? mind you ! nafikiri mnahitaji zaidi anachokisema pale na si suti iwe moja au ngapi haihu ! anaonekana msafi na anachokisema mnakielewa full stop !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...