Ankal salamaleko,
Siku nyingi niko kimya, ila leo naingia tena hapa kutoa pongezi za dhati kwa TV yetu ya taifa ya TBC kwa kazi nzuri waifanyayo tokea kumekucha hadi kumekuchwa.
Hakika TBC imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwa njia ya TV, kiasi si ajabu kukuta ikiangaliwa kila kona hata kabla ya kombe la dunia. Pia nampenda sana kijana huyu Elisha Eliya anayejilawa kila asubuhi nakina Marin Hassan na wengine katika kipindi cha Jambo.
Ombi Elisha naomba abadilishiwe hiyo suti...
maana kila siku namwonaga nayo hiyo hiyo tu.
Kwani hana ingine ama ni jezi ya kazi?
Mdau wa Mafia
Naungana na mdau kuwa TBC1 inavuma sana. mimi pia ni mdau wa hiki chombo haswaa nisikiapo sauti ya Marin Hassan Marine ahhh naburudika sana, wnginge ni Gasto Msigwa anaripoti kutoka Mbeya na maeneo ya jirani na Mbeya, na Emmanuel Amasi wa Musoma na Tarime, kuna somebody Paul huwa anaripoti toka Mwanza na kwingineko kanda ya ziwa. Agnes Mbapu na yeye ni hodari sana ila naomba ratiba ya kusoma taarifa ya habari iangaliwe upya manake mtu mmoja anakuwa anasoma habari kila siku kwa muda hata wa wiki mbili, wabadilishe ratiba kuwe na shift ya hapa na pale, salamu za dhati kwa Jaffary haniu, na Neema Mhando
ReplyDeleteYebooooo, jamani suti ni ya kazi hahahahahahahahahahaha :D
ReplyDeletemdau wa mafia nimekukubali katika kufikisha ujumbe.
ReplyDeleteHongera Tido Mhando TBCI kwa sasa ipo juu sana. kwa kweli mnaongoza na wengine wanajikongoja.
ReplyDeletehongera TBC, lakini bado mna changamoto hasa wakati wa taarifa ya habari mara nyingi mitambo yenu huwa inakwamakwama na kumuacha Msami au Dyauli wakiomba radhi,ajirini mafundi wenye viwango
ReplyDeleteHee kwani kununua suti nako taabu? kwakweli ukinzingatia hii ni television ya taifa lazima mtu uonekani tofauti. na TBC inaonekana pande nyingi sana. na uongozi wa TBC unatakiwa kuweka watu ambao wanakuwa makini hasa kwenye mavazi na mtu anayefuatilia kuona mtangazaji yuko smart na tofauti. sio anakuwa na jezi moja kama timu ya mpira
ReplyDeleteHuyu kijana anapendeza sana kwenye luninga na sauti yake ni nzuri tatizo hajipendi.
ReplyDeletewamafia naona mmecharuka na ankal
ReplyDeleteMdau wa mafia nami nakuunga mkono kwa yote , ila tumshauri ndugu yetu Elisha achanganye suti yaani asiwe anavaa suti za mistari tu, ikiwezekana achanganye na plain suit. Yaonekana anapenda sana suti za mistari sana! Hongera sana Elisha. Keep it up!!
ReplyDeleteHakika Anony wa Wed Jun 30, 09:40:00 AM umesema kweli hata mimi namkubali sana Gaston Msigwa, Jamaa yuko vizuri sana japo hatajwi tajwi, lakini habari zake kama bbc, cnn. Hongera sana Msigwa.
ReplyDeleteIla yupo Songea sio Mbeya.
haters stop hating.....elisha go, go ,go
ReplyDeleteMsimlaumu mtangazaji, yawezekana watangazaji wa TBC hupewa nguo ndani ya studio kabla habari hazijarushwa.
ReplyDeleteHivyo mtangazaji anakwenda kazini amepanda daladala na mavazi yake ya kawaida. Ila akiingia mjengoni TBC ktk 'locker ya TBC' kuna suti moja tu ya mistari, hivyo kama ndo hivyo basi TBC waongeze bajeti ya 'locker ' za nguo za wafanyakazi wake.
Mdau
MpigaBoksi
Ughaibuni
Ubunifu wa Tido Mhando ni mkubwa sana. jamaa tangu achukue shirika, linatisha. Mimi nilikuwa mvinu wa kuamka asubuhi lakini jambo inanikosha hadi imekuwa jadi kuangalia vipindi vya asubuhi. taarifa yao ya habari kama CNN, BBC nk. Ila waandishi wao wa Mikoa mingi hawasikiki. Wanahabari wao wanaotisha ni Gaston Msigwa, Songea, Emanuel Amasi, kwa warianchari na warianchoki, Ben mwaipaja anatisha manyara, kwa habari moto moto-nakumbuka sekeseke la shekifu na sendeka nilichwa mbavu sina, kuna huyu richard leo mwanza, na mwanadad mtenzi tanga. Hawa wanajituma ila wengine mmh! wafanyiwe screening kwakweli. Big up Tido, moto uwe huo huo na endeleeni kuongeza vipindi vingi vya hapa nyumbani kama vile kipindi cha makala za nyumbani tufurahie kuona changamoto na maendeleo ya nchi yetu.
ReplyDeleteMdau Morogoro
kazi ya utangazaji ni lazima uwe smart uvutie watazamaji sio muuze sura na kauka nikuvae nunua suti nyingineeeeeeeeee hiyo ishaeksipaya na macho yanaboreka new suti pliiiizo
ReplyDeleteJamani huenda anazosuti nyingi ila za aina moja!nitumie vipimo Elisha nikakushonee pale tandale,isiwe shida!Gerson is the best,anajua anachofanya na fikiria he is reporting from Songea si dar labda angepata exposure kubwa!
ReplyDeleteKwakweli tunamshukuru sana mdau wa mafia leo kijana elisha amebadilisha suti!! ila nadhani suti yenyewe kafanya kuanzimwa maana inaonekana kubwa!! sasa kijana elisha unakipaji saaana cha kutangaza changamoto uliyonayo ni kujipenda na kuwa na mvuto kwenye luninga. watu unaowahoji wanakuwa smart kuliko wewe. Hata leo jamaa walipendeza na suti zao ila wewe umevaa suti kubwa sijui umechukua ya nani? Hongea TBC ila mna changamoto mbele yenu ya kuhakikisha watangazaji wenu wanakuwa smart.
ReplyDeleteSusan na Tido TBC iko juu sana na imepata wapenzi wengi saana. Hebu wekeni mchakato kwenye mavazi ya watangazaji wenu. Kwanini kina Msami, Haniu, Marine wanabadilisha suti then kijana Elisha anabaki na suti moja? Hebu wekeni iwe ni moja ya kigezo cha ajira yenu kuwa mtangazaji wa luninga lazima awe na suti za kutosha.
ReplyDeleteAu kama suti ni gharama! basi wavae tu shati na tai itapendeza zaidi kuliko mtangazaji kuonekana kavaa jezi moja kama timu ya mpira tena ya mchangani ambayo bado haijapata mfadhili ikawa na uwezo wa kununua jezi za kubadilisha. Jitahidini saana viongozi wa TBC
Hongera TBC kwa kuwa na vipindi vinavyotuvutia, ila Elisha jifunze kujipenda kwani mshahara wako haukutoshi kubadilisha suti na mashati? kama uwezo wa suti ni mdogo vaa tu suruali na shati na tai. au ni lazima kuvaa suti?
ReplyDeleteTBC mpeni nafasi zaidi Gaston Msigwa wa Songea, huyu kijana anauwezo mkubwa sana kuliko mnavyomchukulia.
ReplyDeletehata kama anayo hiyo suti moja so what... yanawahusu? muacheni afanye kazi yake!
ReplyDeleteKuna watangazaji waliopo mikoani lakini kwa kweli wanapaswa kuwepo makao makuu Dar es salaam ili kuongeza uhai hapo studio za TBC1.Grason Msigwa na Emmanuel Amasi waje mikocheni kusoma taarifa ya habari.
ReplyDeleteBila shaka maoni ya watanzania yatakufanya ujirekebishe kijana elisha. na kaka michuzi hongera kwa mtandao wako, maana kwa mambo kama haya utasaidia kurekebisha tabia za watu wengi
ReplyDeleteYote tisa kumi Kijana Pendaeli Omary, Michezo habari yeye yumo sana... TBC1 ehh!
ReplyDeleteMadau Ahaz
jamani jamani watanzania !!!! suti ni nini? mi nafikiri mnahitaji zaidi anachokisema pale na si suti aliyovaa akivaa suti nzuri na akawa anaboronga si mtasema afukuzwe kazi kabisa ? mind you ! nafikiri mnahitaji zaidi anachokisema pale na si suti iwe moja au ngapi haihu ! anaonekana msafi na anachokisema mnakielewa full stop !
ReplyDelete