Kamanda wa FFU ughaibuni
Ras Makunja na dogo Prince Thabit


Dogo aliyejitambulisha kwa jina la Prince Thabit wa Amsterdam,akiwa na Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makunja wa Ngoma Africa band. Dogo alifanikiwa kumuweka chiini ya ulinzi kamanda huyo baada ya Ras Makunja kuvamia mitaa ya Amsterdam,Uholanzi bila ya taarifa!

Baada ya kufumwa na Dogo huyo, Ras Makunja alijitetea kuwa alikwenda mjini hapo kupangusa matongo tongo a.ka. mchanga wa uso. Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na dogo huyo na kupigishwa kwata kwa masaa kadhaa Ras Makunja alijitetea kuwa kosa ni kurudia kosa hivyo baada ya kusamehewa aliasaidiwa lift kwa msaada wa Punda ulaya na kuambiwa arudi maskani kwake Ujeurimani huku akionywa kuwa siku ingine lazima aote taarifa iwapo ataingia katika jiji kubwa kama hilo. Kamanda alisalimu amri ya Dogo na kurudi mbio mbio katika kambi ya FFU wa ngoma Africa huko Ujerumani

Wakati huo huo habari zinasema FFU wa Ngoma Africa band watatumbuiza katika onyesho kubwa la World Music Festival,Loshausen,kando kidogo ya mji wa Kassel,Ujerumani,siku ya Ijumaa 23 Julai 2010,ambako washabiki wanasubiri kwa hamu kujimwaga uwanjani.
Taarifa hizo zimedatisha kwamba wazee hao wa kukaanga mbuyu mwaka huu hawataki mchezo. Wakiwa wameanza libeneke mwaka 1993 na kujizolea umaarufu kila kona duniani hivi sasa wanatamba na singo CD mpya iliyobeba jina "Jakaya Kikwete 2010".

jipendelee mwenye kwa kujipa raha at www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kujumika nao katika baraza la
www.facebook.com/ngomaafrica
pia usikose kubofya
www.world-music-festival.de

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    sasa kamanda si unaona faida ya kuvamia vamia onyo? almanusura umepewa adhabu ya kupiga kwata,kuliko kurudi kwenu kariakoo kwa mguu.najua ulikwenda kuwinda njiwa Amsterdam kama ilivyo watoto wa uswahilini

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    Michu ulipotaja jina la Ras Makunja, umenikumbusha na Askari moja mkwara sana alikuwa kijulikana kama "MKAMA SHAP" yupo wapi huyu siku hizi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    sasa kamanda inakuaje tena?unavamia miji bila mwaliko?
    je kama wewe ungekuwa umepata ugeni nyumbani kwako bila taarifa ungekubali?
    unajua siku nyingine kamanda lazima tupeane taarifa vinginevyo
    unaanza sooo !

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    kamanda mkuu wa ffu,unaniacha hoi na miwani yako wewe mchana miwani,usiku miwani sasa hii heshima gani?ndio maana baba wa kambo kakuvukuzeni na kelele zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...