WAPENZI NA WANACHAMA WA KLABU YA MICHEZO YA ROSE GARDEN YA JIJINI DAR, PAMOJA NA CHAMA CHA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED NCHINI, WAKO KATIKA SIMANZI KUBWA KWA KUONDOKEWA NA MWENYEKITI WAO, BERNARD MBWAMBO, ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA GARI MJINI TANGA BAADA YA GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUGONGA KWA NYUMA GARI ILIYOKUWA IMESIMAMA.
MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU SEHEMU ZA KIJITONYAMA KWA ALI MAUA JIJINI DAR, NA KWA MUJIBU WA KAMATI YA MAZISHI MAREHEMU MBWAMBO ATAPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE SAA KUMI JIONI KESHO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KUTOA MKONO WA POLE KWA WANACHAMA WA KLABU YA ROSE GARDEN NA WANA MANCHESTER UNITED POPOTE WALIPO. MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI - AMINA
Very Sad Indeed, RIP Ben
ReplyDeleteRIP kaka Ben, utuombee na msalimie baba yetu. We already miss you so much and can't even begin to think how life will be without you. But I'm sure you'll be watching over us, lala salama kaka. Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
ReplyDeleteRIP Ben, Pole nyingi na salamu za rambirambi kwa mkewe, Kay na familia nzima
ReplyDeleteRIP Mbwambo, ulinipokea Arusha, tukafanya biashara Dar, sana tu, asante sana.
ReplyDeleteTutakutana uko Ben.
Too soon to go but all in all Glory be to God, Rest in Peace Brother Ben.
ReplyDeleteVery sad indeed! RIP Ben our Chairman....!!! We will always remember you!
ReplyDeleteeeh Mungu wangu wee nimeshtuka sana kaka wewe enzi zilee ulinipa ride nikitoka kupombeka pale rg kweli dunia hii sie ni wapitaji tuu,rest in peace kaka
ReplyDeletemdau canada
What a nice guy leaving us like that. Its hard but we are trying to come up with terms that ur not with us. RIP Bro Benny !!! Also Wishing Bro Mussa a fast recovery from the injuries you had sustained from the same accident !!! Get well soon Mussa !!
ReplyDelete