Sabah Muchacho wakitumbuiza wapenzi wataraabu jijini Toronto na vitongoji vyake nchini Canada ambao kwa pamoja walipata fursa kumsikiliza msanii huyu maarufu kutoka Tanzania katika fani ya Taraabu wikiendi iliyopita.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2010

    Michuzi wewe vipi hata kuandika hujui, sio Taraabu ni Taarab, kama huandiki wewe basi uwe unapitia pitia kabla hujarusha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2010

    we annony wa wa kwanza muhimu upate ujumbe, hii sio website rasmi kwa ajili ya habari kwa umma ambapo mwandishi anatakiwa aandike kiswahili sanifu. it is his website and he can write whatever he wishes so far haivunji sheria za nchi. so kajaribu kuomba kazi wa kiswahili and your efforts will be appreciated.
    peace.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2010

    TUNAKUBALI KUA SABAH NI MSANII MZURI LAKINI SIFA ZAKE ANAJIHARIBIA KWA KIBURI CHAKE...AMEKUA NA TABIA YA KUTUMIA LUGHA ZA UFEDHULI KUWASHAMBULIA WASHABIKI HADI KUFIKIA KITENDO CHA KUTUPA PESA CHINI ANAPOTUNZWA KITENDO AMBACHO KINATUSHANGAZA WENGI ANAPOKUJA HUKU NCHI ZA KIGENI.AKAE AKIJUA HAKUNA MMBORA KULIKO WOTE DUNIANI ILA TABIA NJEMA NI SILAHA YA MJA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2010

    kaona mambo yako kule...taarab imo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2010

    Hi Fri Jun 11, 08:17:00 AM

    Mimi siyo mpenzi wa taarabu lakini hoja yako uende tabia hiyo inasababishwa na baadhi ya watu kutaka kuwavunjia heshim aakina dada wa taarabu na wacheza shoo. Sometimes inatia kinyaa kwa vitendo vya baadhi ya washabiki. Kuwakumbatia / kuwatomasa / kuwabusu bila ridhaa ya kisa katoa Tshs 500/= ama 100/=

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2010

    Haya mambo ya MODERN TAARAB yana boa sana sie wengine tumeamua kurudi back to BASICS yaani TAARAB ASLI na siyo ASILI i repeat TAARAB ASLI

    Na hapa hiyo taarab asli nazungumzia akina EGYPTIAN MUSICAL CLUB...hivi kuna mtu anaweza kuleta mashairi yaliyokuwa yanaimbwa na akina ABBAS MZEE kwenye nyimbo kama vile fitina, unanunia nini, yatima na kadhalika! now compare that to the so called MODERN TAARAB ya akina Sabah, TOT, MELODY na wengineo.

    I guess majority ya mnaochangia humu hata IKHWAAN SAFAA hamjui ni akina nani...lakini more interestingly ni kuwa leo CULTURE wakipiga na wakaweka kiingilio 50,000 ticket zinatununuliwa na zitaisha within minutes kwa sababu mume,mke,watoto wataenda kuwasikiliza kwani hakutokuwa na mashairi au nyimbo zilizojaa matusi na taarab inayopigwa kama MAYENU if anything this country has gone to Dogs, na culturally tumekuwa ma SLAVES and its despicable...systematically kila kilichochetu tumeamua kwa kususdi kua, kuanzia kipindi cha MALENGA wetu mpaka NYIMBO zetu!!!


    http://www.wazalendoforums.com

    ReplyDelete
  7. Mzee wa KidukuJune 11, 2010

    Bi Hadija Kopa amethibitisha kuwa uzee dawa na kitu chake murua cha "Timbwili timbwili la Asha Ngedere"

    Kwenye chati za taarab hapa Dar mambo yako hivi:

    1. Timbwili timbwili la Asha Ngedere (aka Top in Town), by Hadija Kopa
    2. Mashetani (aka Mama nipe radhi), by Isha Ramadhan
    3. Undugu Kufaana (aka, Wasomeshe a,e,i,o,u) ya Omari Tego na Dadaake
    4. Roho Mbaya si Mtaji, by nani vile nimesahau
    5. Walimwengu (aka Fitna za nini), kipande cha sebene, na Melody
    6, na kuendelea wengineo.

    Rusha Roho ndio taarab ya kisasa. Taarab za kukaa chini na kusikiza muda wake ulishakwisha.

    Hata Zanzibar siku hizi wanapenda Rusha Roho.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2010

    MZEE WA KIDUKU'

    hujaulizwa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2010

    Mzee wa Kiduku sikatai rusha roho ndio muziki wa kisasa lakini sikubaliani pale unapoitwa taab.

    rusha roho haina hata characteristic moja ya kuitwa taarab. Taarab kama ulivyosema wewe mwenyewe ni ya kukaa chini na kusiliza ala za muziki zikienda sambaba na muziki na mashairiya nyimbo.

    Taarab ni ustaarabu na hata panapoimbwa jambo lolote huimbwa kwa mafumbo na kwa ufundi maridai tu.

    Sijui una umri gani lakini kama umewahi kusikia nyimbo hizi zifuatazo utajua kuwa taarab ni ufundi na kinachoimbwa kina maana mbili mbili na bila ya mtu kutukana. zitafute hizi na uzisikilize.

    mshumaa
    tufaa la kiunguja
    nanasi
    chumvi
    naona ajabu mno
    kioo
    kiu
    n.k

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2010

    Mzee wa Kiduku hujui nini taarab na hujawahi kuona taarab na wala hujui raha ya taarab.

    KAA KIMYA

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 12, 2010

    I dont know if you have chance to meet Bi Sabah but i had ni mtu mzuri sana na anawasalimia na kuwashukuru fans wake for all there support ive been her fan for long time.I've been in her show in Seattle na toronto na leo ni mara ya kwanza kusikia accusation kama hiyo yeye bi sabah asingekua alipo bila ya fans wake and she knows how important to have great fans with you and i believe they have been supporting her since when she start singing some where in 1980's so as far as i know she is very good human being and she is a great singer.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 12, 2010

    Mdau uliyesema kuwa Sabah ni the GREAT naona umeanza kuijua Taarab yetu miaka 10 iliyopita

    If Sabah is GREAT then SITI BITI SAAD atakuwa nani?

    I still stand by what i believe kuwa the so called modern taarab ni CRAP na bora mngeeita TAAYENU kwani to my eyes naona MAYENU tuuu


    Its sad kuona hii art form yetu ikipotezwa mbele ya macho yetu hivi hivi.

    If anything hate the pomposity of the so called Modern Taarab, lyrics and music. I don't like the music, its non-melodic chords and progressions na nasema wazi kuwa siku CULTURE MUSICAL CLUB wakipiga diamond utaona sie wapenzi wa TAARAB AS-LI tutakavyojazana pale na wake zetu huku wamevalia ki kheshma na big G zao na wakti huo huo sie tuta kuwa pembeni twasikiliza...kiingilio 50,000

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...