GLOBU YA JAMII IMEKUWA IKIPATA SIMU NA EMAIL NYINGI ZA MALALAMIKO KWAMBA INAPENDELEA AMA INALALIA AIDHA CHAMA FULANI CHA SIASA AMA DINI FULANI FULANI NA KWAMBA VYAMA AMA DINI FULANI FULANI HAZIPEWI KIPAUMBELE AU HAZICHAPISHIWI HABARI ZAO.

TIMU YA LIBENEKE LA GLOBU YA JAMII INAPENDA KUKANUSHA KWA NGUVU ZOTE HABARI HIZO NA KUSISITIZA KWAMBA SERA YAKE NI ILE ILE YA 'SIBAGUI, SICHAGUI, ATAKAYENIZIKA SIMJUI'

HIVYO KATIKA KUWEKANA SAWA MUONEKANO HUO HUENDA UNATOKANA NA MOJA YA SABABU ZIFUATAZO KAMA SIO ZOTE:

1. HAVILETI HABARI ZAO KUPITIA issamichuzi@gmail.com
AMBAYO IKO WAZI KWA WOTE KULETA HABARI NA PICHA

2. HAVITOI TAARIFA MAPEMA YA KUWEPO KWA SHUGHULI ZAO ZINAZOHITAJI COVERAGE

3. HAVINA IMANI NA TEKNOLIJIA HII YA HABARI

4. HAVIJUI NJIA GANI VITUMIE KULETA AMA KUFANYA HABARI ZAO ZITOKE (kama namba 1 ilivyoainisha)

5. HAVINA HABARI

KWA HESHIMA NA TAADHIMA TUNASISITIZA TENA KWAMBA SI KWELI KWAMBA GLOBU YA JAMII INA UBAGUZI WA AINA YOYOTE ILE.

HIVYO BASI, ENDAPO KAMA UNA TAARIFA, HABARI AMA PICHA AMBAZO HAZICHAFUI HALI YA HEWA JISIKIE HURU KUUTUMIA MTANDAO HUU WAKATI WOWOTE NA KWA LOLOTE LILILO NDANI YA MIPAKA YA SHERIA NA MISINGI YA HABARI INAYOZINGATIA DEMOKRASIA YA UHURU WA KUPATA NA KUPASHA HABARI.

MSISITIZO: MAONI YENYE KASHFA KWA MTU AMA KUNDI YAKIWA NDANI YA USHUNGI WA 'KUKOSOANA' AMA 'KUPEANA UKWELI' AMA 'UHURU WA HABARI' HAYANA NAFASI. FURSA NI KWA YALIYO NDANI YA MIPAKA KAMA ILIVYOAINISHWA HAPO JUU.
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2010

    MICHUZI USITUZINUE, UMENUNULIWA NA CCM, KWANI NI SIRI???????????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2010

    michuzi ni ccm, bania tu comenti yangu. poa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2010

    wanaopendelewa ni wana CCM na watoto wao. ila michuzi tunaomba ubadilishe kidogo ili wakulima nao wapewe nafasi, sasa wewe unanadi tu CCM, mara ridhwani yuko wapi, mara january anagombea ubunge? wapo wakulima kibao wenye uwezo kama hao watoto wa wakubwa wanaorithishwa nchi yetu na hata kuwaliko. habari ndo hiyo

    ReplyDelete
  4. US BloggerJuly 20, 2010

    us blogger)

    ankal siyo siri, nimekutumia ma atiko kibao lakini unabania tu, sasa sijui nikutetee au vipi, ila wapo ambao wakituma maatiko hata zisizofaa unarusha hewani mara moja, mfano wa nabii nanihiii

    US blogger

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2010

    Acha noma kaka yangu. You are better than that and lets keep that way...Unafanya tukuone kama fulani vile...Kaa kimya tu kwasababau comments zetu unavyozitupia kapuni kila siku na sisi utatuambiaje "wanaotuma comments tu humu ni wale wanaoitetea CCM" WAKATI Wenye comments za "VYAMA FULANI NA FULANI HAWAFANYI HIVYO" Ehe puleaaseee...Kaka yangy kaa kimya tu ......wengine wala hatuna mambo ya pilitics lakini tunaongea ukweli panapo stahili lakini inakatisha tamaa kuona unavyotupa comments humu....

    Maendeleo hayapatikani bila ukweli kuelezwa

    Sijui na hii utaitupia kapuni

    ReplyDelete
  6. Mzee wa TitizzzJuly 20, 2010

    @us blogger mzee wa mapointi.

    hii blog ni ya CCM, Vodacom, na TBL. Wengine zaidi ni Yohanna Mashaka, Ridhiwani Kikwete na January Makamba

    Mzee wa Titizzzz

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2010

    Ukisikia kujikosha ndiyo huku sasa. Kama kweli wewe hujanunuliwa na wanaotumia sana blog hii kama campaign bilboard yao ni kwa nini tukitoa maoni ya kuhoji sera zao huyatoi?

    Mi hata kuchangia niliisha acha maana naona unazingua tu, watu tunaacha kuandika thesis zetu na kuchukua muda kutoa maoni wewe unachukulia kama tumefanya tukiwa kwenye vibanda vya kahawa eenh!.

    Maoni ya mtu yana thamani kubwa sana kwani mimi binafsi kinachonifanya kila wakati nitembelee mji huu ni kusoma maoni ya watu, mbona kuna blog nyingi tu zinatoa picha ila zinatuboa?, why hakuna michango ya wadau. Michu usidhani hii goodwill ya blog hii inatokana na wewe kuitwa "Issa Michuzi" no ni kwa sababu humu kuna maonia ya watu mbalimbali.

    As long as no inflamatory language why not publishing comments which tries to question the motives of these contestants?,

    Acha kabisa kujiosha wakati sisi tumeshajua kuwa wewe unakudriven na idiology yako ya ki-CCM. For your information hata mimi ni CCM ila tofauti yangu ni kwamba sipigii kura chama kinachonidanganya kila uchaguzi ndiyo maana nataka kujua wataifanyia nini nchi yangu?, na je bungeni wangekuwa wanalipiwa malazi, usafiri na chakula kwa hundi bila kupewa pesa mkononi na kulipwa mshahara wa laki mbili wangegombea?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2010

    ni heri wamekuambia weneyewe
    hapa kuna upendeleo mkubwa sana
    wenye nazo wanapewa
    makabwela kapuni
    ndio jamii ya kitanzania

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 20, 2010

    @anony Tue Jul 20, 08:12:00 PM,
    nazania unabwia sana,blogu ni ya michuzi kwa hiyo anaweza kufanya lile anachotaka yeye. kwanza data zako siyo sahihi, mashaka siyo mtoto wa kigogo, yule ni mbeba boxi huko wichita kansas ambaye anatumia juhudi zake. january ni mtoto wa katibu mkuu wa CCM mzee wa kuropoka makamba, na ridhiwani ni mtoto wa munene, na wote wako bongo. nazani umenielewa

    @us blogger.
    mkuu wewe tuliza boli umeishiwa sera, na digrri yako ya oxford nayo imeoza wee nyambaff
    peace

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 20, 2010

    Kuna binaadamu wanapenda sana kulaumu kwa cho chote kile alimradi hakimridhi yeye.

    Sasa si muanzishe zenu kama rahisi??????????

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 20, 2010

    michuzi kubali unapendelea wana ccm, kwa nini kila mtu akuambie? nilituma habari za chadema, mpaka leo hii wiki ya nne hazijatupwa heani. ya januari makamba ni jana lakini limetokea

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 20, 2010

    Michuzi eeh,

    unabana habari kede mwanangu, unatumiwa unabana! Za wengine kama unarusha vile anony, anaesema hapo.

    But the blog.is yours fanya utakaloona sawa.
    Hata ukiendelea kubana, Mwaikusa alitetea wana Rwanda, nakifo chake kinatuachia kiulizo! Hasa ukifananisha na ile iliyotokea South kipindi fulani.
    Bana tena! Pyeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 20, 2010

    nyie wajinga wa chadema si mpeleke habari zenu kula jamii forum na ze utamu.sindio site zenu,kule ukipeleka habari ya ccm wanabania vile vile,na kila siku kumkandia january kisa wao hwana uwezo wa kumfikia dogo.michuzi kamua baba achana nao hawa.kwanza ccm si ndo wenye nchi.hebu kwendeni zenu huko na vyaa vyenu vya ukoo flani flani.ccm ndo ya wote

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 20, 2010

    Mimi ni mdau mpya wa blog yako kaka na sitetei upande mmoja au mwingine. Lakini kila nikifungua tovuti yako chama ni kile kile, watu wale wale nk. Labda ni coincidence lakini blog ni ya kwako kwa hiyo una haki ya kupendelea. Vinginevyo bado tupo wote..hii blog inatoa habari na matukio muhimu ambayo huwezi kupata kwenye tovuti nyingine.
    Mr. X

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 20, 2010

    MR. MICHUZI/MODERATOR JAMII BLOG.LABDA KUNA UKWELI KUWA UNAPENDELEA KWANI SI MARA YA KWANZA UNASEMA UMEPOKEA MALALAMIKO.HEBU ANGALIA HAO WATOA MAONI WOTE INAKUWAJE WAKULALAMIKIE?MIMI NISHATUMA MAONI MENGI YA KUKOSOA NA KUSEMA UKWELI KUHUSU BAADHI YA WATU/IDARA/VYAMA HUJAWAHI KUYAWEKA KWASABABU HAO WATU/IDARA/VYAMA VINAKUHUSU,ILA NIKIWEKA POST YA KUTUKUZA/KUSIFIA UNAIRUSHA MARA MOJA.JE UNAFIKIRI KILA KITU TUTASIFIA??KUTUKANA SIO VIZURI COMMENT KAMA HIZO LAZIMA ZITUPWE KAPUNI,KAMA UMEAMUA KUITA HII BLOG YA JAMII ACHA JAMII ITOE MAONI +VE AU -VE USIBAGUE.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 20, 2010

    Michuzi acha longo longo za kipolitiki, kataa kubali wewe unabase upande mmoja hasa kama alivyosema mdau mmoja hapo juu wewe na CCM , TBL, VODAFONE kina dada Mwamvita makamba(kama unavyomuita wewe ijapokuwa anaweza kuwa mjukuu wako)Kaka Mafuru na wengineo ambao wana vilaki laki vya kununua mchicha na kula mishikaki hao ni kuwatoa kila siku na kuwasifia bila mpango. (2)wewe kukosolewa hutaki hata kama umekosea na comments zote ambazo zitakugusa au zitawakugusa watu wako ambazo zina ukweli unazibania kumbuka Michuzi a.k.a Muhidin Issa waweza kuchoma vitabu vyote lakini Historia itabaki pale pale na unaweza kubania comments zote lakini Ukweli utabaki pale pale na msg itakuwa imeshakufikia.. zidumu fikra zako Mheshimiwa /kijana wa zamani/ ex player wa jugnu mehu el-paso/mbunge mtarajiwa wa kuteuliwa Dr Michuzi.
    mdau Pakacha la siri.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 20, 2010

    wapizani awanaposho kwa nini asifagilie ccm yenye pesa za kuonga !!1

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 20, 2010

    SIO UWONGO KAKA MCHUZI.CCM IMEKUNUNUA.LAKINI NAKATAA KUHUSU UDINI HUNA UDINI.NAOMBA KAKA TUWAANGALIE HAWA WALALA HOI ,AMBAO HAWANA SAUTI.ULIANZA VIZURI SANA.KWANZA NAKUSIFU KAKA.HATA KAMA SASA UTABORONGA LAKINI UMEJITAHIDI.NA TUNAKUOMBEA KWA MUNGU UWE JASIRI.TUNATAKA KUJENGA NCHI SIO KUBOMOA.WALE WATAKAO LETA MAMBO YA KUBOMOA HUSWARUHUSU.LAKINI FIKIRA SAFI NA ZENYE UPENDO WEKA.LAKINI SASA TUNA ANGALIA TUBOMOE UFISADI .KULETA MAISHA BORA YA MTANZANIA.
    MDAU
    USA

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 20, 2010

    Sioni tatizo, hii ni blog yako, una hiari yako ni nini unachoandika na nini huandiki. Kuiita blog ya jamii haifanyi kuwa ni miliki ya watanzania.

    kila mtu anaweza kuanzisha blog yake na kuweka anachotaka.

    Tuwache malalamiko, kama michuzi haweki habari za vyama fulani au dini fulani haina maana kuwa watu wengine hawawezi kuanzisha blog zao na kuweka yale ambayo michuzi asiyoyaandika.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 20, 2010

    Mbona hii habari waandishi wa habari wa Tanzania leo MMEIGWAYA?
    "Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema kwamba Dk. Slaa ndiye mgombea urais wa Chadema mwaka 2010." Tangu asubuhi iko kwa jamaa zako wa Jamiiforums. Tulitegemea habari na picha kwa jambo muhimu kama hili kwa Tanzania. Labda mtaandika ukipita mwezi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 21, 2010

    Habari za chadema si mpeleke huko JF?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 21, 2010

    Hii coinncidence ya kujisafisha ni kali sana. Leo CHADEMA wameteua mgombea wao wa kiti cha Urais, lakini blog yako haina hata fununu. Utasingizia kwamba hujui ama hujapata news, lakini ukweli ni kwamba taarifa unazo, lakini kwa sababu zako binafsi ambazo ni za ki-CCM zaidi wala hujaandika. Ajabu nyingine ni kwamba akina Makala na Makamba wanaenda huko maporini utashangaa unakuta mapicha ya kijani yamejaa kwenye blog, lakini matukio yaliyo Dar kama hilo la CHADEMA sijaona.

    Hili haliishi hapa, maana hata mwajiri wako TSN na kule kwingine kwa Tido Mhando, wote wamekaa kimya. Halafu wanadai kwamba eti TSN na TBC ni vyombo vya habari vya umma. Na wewe unadai hii ni globu ya jamii, sema wazi kwamba hii ni globu ya CCM. Maana hapa hata kama ni tukio la kusimika kamanda wa vijana wa CCM wa Kata, lazima utakuta news na mipicha ya kijani.

    Badilika ndugu yangu, ama weka wazi kwamba hii globu ni news outlet ya CCM, wapinzani hawana.

    Pale juu unasema Bongo Celebrity blog inataka sera za TLP na CUF, mbona hurushi matukio yao, sasa sera wazitakia nini? Watu tukiuliza sera za watu wako, unabana comment, ila wewe unataka sera za wapinzani. Haya bana, lakini tutafika tu. Hata kwa Mugabe ilikuwa hivi hivi, na Baba Moi nae ilikuwa hivi hivi, iko siku kitaeleweka.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 21, 2010

    Ah..Bwana wee.Michuzi Fisadi tu wa CCM.Tunatuma comment kibao unazibania na hamna chochote.Umekava mkutano wa CCM utazani ndio uchaguzi mkuu wa TZ.Acha uzushi kaka tushakuchoka.Alafu pia mi nashangaa unajina la Kiislam lkn humu kny Glob yako kumejaa Ukatoliki,simaanishi uwapendelee waislam lkn uwe fair.Sijawahi kuona habari ya mahakama ya kadhi hapa lkn akina Pengo na Rwakatare kl siku,au usharitadi nini? NA HII PIA IBANIE TU:

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 21, 2010

    Maoni yote ya wadau yanaonyesha kuwa wewe Balozi Michuzi unatupa katika kapu maoni ambayo hupendi yachapishwe. Nitakuelewa kama yana matusi, lakini wadau wengi wanaamini kuwa una self-censorship katika blogi hii na unapeleka nyuma maendeleo ya tanzania kama huheshimu haki ya mwananchi kutoa maoni bila ya kutukana.

    Ulishasema sana kwamba unaheshimu lakini kama CCM, wewe pia upo katika udanga'anyivu wa wananchi kama wanavyotuambia kuwa Tanzania imeendelea wakati wananchi wengi bado wanakufa njaa kila siku vijijini.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 21, 2010

    Wee Anonymous wa Wed Jul 21, 02:55:00 AM na wengine wenye mawazo hasi na roho mbaya kama wewe mnachefua. Michuzi pointi zake hapa sio kutoa maoni bali kutuma habari. Na hata hayo maoni kaweka bayana kwamba hayatoona mwanga wa jua kama yanakwenda kinyume na sera za blogi yake. Sasa mbona mnakuwa wagumu kuelewa nyie Wamatumbi????

    Amesema KULETA HABARI NA PICHA na swala hapa si KUTOA MAONI. Hamuoni tofauti hiyo. Ndio maana kina Kamau wanatucheka waswahili kwa umbumbumbu na ujuaji wa kijinga. waambieni hao wakubwa zenu wapeleke HABARI NA PICHA kwa email hiyo iliyotajwa muone kama hatotoa ndio muanze kubwabwaja EBO!

    Michuzi achana nao hao bwana. Kwanza inaonesha hao ni adui zako wa maendeleo. wanakuona unaongoza kwa wingi wa wasomaji kiasi hata wafahili rundo (tofauti na blogi yoyote) kwa ufanisi na wingi wa wasomaji. Achana nao hao wenye vijiba vya roho. Tena wakikuona kila kukicha uko vekesheni ndio matumbo yanawauma. Achana nao wala wasikukoseshe usingizi. Maji moto hayachomi nyumba, yanalowanisha tu.

    Pia kumbuka huwezi kumridhisha kila mtu. Hao watasema mchana usiku watalala. Ila nawakumbusha tena. Hoja hapa sio kutuma MAONI ni kutuma HABARI NA PICHAAAAAAA!

    Mdau Sydney

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 21, 2010

    Brother Michuzi asilaumiwe kabisa,Blog ni kitu cha bure na kila mtu anaweza kutumia na kuwa na maamuzi, pia blog zipo nyingi.Huu ni wakati muafaka kuanza kutumia blog nyingine kama ya Michuzi jr, Father kidevu,Amani Masue na nyinginezo nyingi ,tuamke kutumia vyombo vingine.....tusimlazimishe brother mnayotaka nyie.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 21, 2010

    @ 4:31 wee ndio hujui kabisa ..Upotee tu...Wenzako hatuingii kwenye hii blog kuangalia mapicha huku. Yaani kuna sijui watoto wasio na kazi humu..Mimi muda wangu niingie kuangalia picha for what. I know habari au tukio linaambatanishwa na picha ili lieleweke zaidi lakini sio kuwa nafuata picha huku. Tunafuata habari na comments za watu baada ya habari...Wee vipi wee ungejua kila gazeti siku hizi katika nchi zilizoendelea kila habari wanaachia watu wacomment ili wajue ni nini wanachi wanafikiria kuhusu jambo fulani. Na hiyo inawasaidia hata viongozi wakiamua mambo kuhusu nchi wanakua wanaenda na majority of the people kwa vile wanaona sehemu nyingi katika maoni watu wanasema hivi. Hivyo ujue wenzetu maendeleo yao mengi yanatokana na wananchi wenyewe wanavyoamua. Siye kwetu kuelezea jambo ni mwiko. Baba akisema hivi hakuna wakumchallenge au kumweleza other option. Na Serikali na nchi ndio hivyo hivyo kuburutwa tu bila kujali wananchi wanasemaje au kitu hiki kitawasaidia vipi...Mfano kama serikali ingesikiliza maoni ya wananchi sasa hivi tungekua bado hatujajoin the whatever union. Lakini kwa vile sauti ya watu hazina kazi nchini tuko wapi humo humo bila kujua gari linaelekea wapi. .

    We don't want to be treated as kings but we want fairness. Nyie ndio wale waswahili mkikosolewa mnasema ni wivu. Mkiambiwa ukweli mnaita upinzani wa watu wenye chuki. Hamna mtu mwenye chuki na chama chochote...I am not a politician but I do love my country..

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 21, 2010

    Michuzi, Iko poa sana hao wanaochonga ameamua kukuchafua tu, na Binadamu hakamiliki na pia huwezi kumrizisha kila Mtu. Michu iko JUU, JUU JUU ZAIDI.

    MICHUZI OYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 21, 2010

    Kama kweli Michuzi haupost habari za vyama vingine ukitumia(na hazichafui hali ya hewa) basi utakuwa unaupendeleo fulani.
    Anyways mimi nimetuma habari kwako mara kama 4(hazihusu siasa ila moja ni kukosoa mahala), ukapost tatu na moja ulinitumia email(ilikuwa inahusu tigo).

    Naona ambazo zinahusu sirikali na chama tawala zinapewa kipaumbele..
    Kwenye politics simooo,

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 21, 2010

    Katika mablogger wa TZ uko juu ukifuatiwa na Dina Marios, Mjengwa na Lady Jay Dee for entertainment news. Mara kwa mara nawacheki na kufurahia maisha...sina tofauti na mtu ambaye yuko Dar japokuwa nipo kijijini. Sasa Michu kidogo kuna kaukweli ni watu wenye majina tu ndo unaelekea kuwacover. What Tznians want is fresh new names in politics on the arena-alot happens it's a challenge upanue wigo ukave Mwanza, Mbeya, Zenj, Moro other cities etc. Au? USIBANIE KAKOMENT KANGU

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 21, 2010

    kumbuka ulipotoka mwakaleli sijui tukuyu na jamaa na marafiki zako uliowaacha wanavyotaabika na maisha magumu sana na endelea kukipigia debe ccm.blog ni yako tunajua ila bila sisi itakua sawa na bure.jiheshimu uheshimiwa kama ulivyoanza na ukweli ni msumemo na ngoma ikivuma sana upasuka.hii comment yako uweke usiweke shauri yako

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 21, 2010

    msimuonee....MICHUZI mtu smati sana hata siku moja hajawahi kunibania maoni yangu hata iwe maoni ya kumkosoa yeye(MICHUZI MWENYEWE)anarusha,labda kweli maoni ya watu wengine hayana msingi ndio maana anakukuchunieni.MICHUZI upo juu MPWA.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 21, 2010

    Ni tabia ya Kitanzania kuharibu kitu kizuri kinachomsaidia yeye mwenyewe. Blogu ya Michuzi imefanikiwa sana katika kuhabarisha, kuendesha mijadala bila kujali itikadi. Lakini wa Tz wanaona sifa kumkatisha tamaa mtu. mijitu mingine bwana. Na si ajabu hizi stupid comments zote zimetumwa na mtu mmoja.

    ReplyDelete
  34. Candid ScopeJuly 21, 2010

    MHESHIMIWA MICHUZI, NAKUPONGEZA KWA KAZI NZURI. HUWEZI KWEPA MALALAMIKO KWA VILE HUWEZI MRIDHISHA KILA BINADAMU. LAKINI LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA.

    KUNA WADHAMINI WA WA BLOG YAKO KAMA VODACOM, HIVYO HATUWEZI KUKWEPA KUWAONA AKINA MWAMVITA MAKAMBA KILA KUKICHA VINGINEVYO BLOG ITAPATA KWIKWI NA KISHA KUDHOOFIKA.

    MIMI NI MOJAWAPO KUBANIWA BAADHI YA COMMENTS LABDA SABABU ZIMEKUWA ZINAFUNUA UKWELI FULANI AMBAO UNALENGA TAASISI AU IDARA FULANI NA HIVYO UKAMAANISHA INAMLENGA FULANI AU KUNDI FULANI. HUU NI MTAZAMO WAKO NA WALA HAIKUWA FALSAFA YANGU.

    BLOG YAKO INAZIDI KUKUA NA HIVYO KUPATA UMAARUFU ZAIDI. JARIBU KUFUNGUKA ZAIDI. NA UJUE KUKUA NA KUENDELEA KWA BLOG HII NI WADAU SI WEWE. WEWE NI MODERATOR. JARIBU KUANGALIA KWA MAKINI COMMENTS ZA WATU NA FALSAFA YAKE BILA KUFIKIRIA KWAMBA INA MLENGA MTU AU KUNDI FULANI. LAKINI KWA ZINAZOCHAFUA HALI YA HEWA NAKUFAGILIA JITAHIDI KUONGEZA KAPU LA ZIADA ILA UWE MWANGALIFU KABLA YA KUVUTA KUTUMBUKIZA NDANI YA TRUSH.

    USHAURI WANGU MHESHIMIWA MICHUZI JARIBU KUBALANSI KIDOGO HABARI MAANA NYINGINE ZINAKIFU. MAANA SIKU UNAONA BLOG IMEJAA TU TAMASHA LA KUTAFUTA WAREMBO KANA KWAMBA HAKUNA MACHINGA WANAOHANGAIKA PALE MTAA WA KONGO AU WAMASAI WANAOKAMUA MAZIWA KULE MVOMELO MOROGORO WANAVYOPIGANA VIPEPSI NA WAKULINA KUGOMBANIANA ARDHI. HII NI MAUDHUI YANGU UNAELEWA NA MAANA GANI KWA UPEMBUZI YAKINIFU.
    ILA WAJITAHIDI NA USIRUDI NYUMA, NA JITAHIDI KUFUNGUA MACHO, JIAMINI KAMA MWANA HABARI MAHIRI AMBAYE HUBABAISHWI, KUOGOPA AU KUTISHWA NA MTU, HAPO UTAJIKUTA HURU NA KUTOBANA MAONI YA WADAU.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 21, 2010

    Michuzi nakuheshimu lakini lazima ukubali kuna double standard kwenye hii blogu. Huwezi kuifananisha na ile blogu ya Francis Godwin(Kama sijakosea) yule muandishi wakujitegemea wa Iringa. Yeye haposti mambo ya upinzani sana labda hatumiwi lakini ukituma comment ambayo haimtukani mtu ila ina question mambo ya maendeleo anaweka. Na yeye mwenyewe ni mtu makini sana ila basi tu sio popular. Ameposti mambo mengi ya ccm lakini pia anaonekana sio mtu wakuburuzwa. Kwa yeyote anayetaka kujua nazungumzia nini ingia kwenye blogu yange nafikiri unaweza ku-google Francis Godwin Iringa utampata utajua ninachokisema. Sio mtu anayeangalia sana matabaka ya juu lakini he seems to be the voice of every Tanzanian.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...