Pichani ni jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwenye eneo hilo na kuhusisha magari hayo mawili ambayo yalikuwa yakitokea kwenye kampeni za kuwania ubunge Singida mjini. MO yuko salama na anaendelea vizuri.
Dereva Mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Hawa Ngulume mwenye traki suti nyeusi ambaye hata hivyo jina lake bado halijafahamika akihojiwa na polisi kwenye eneo la tukio hilo Manispaa ya Singida leo. Chini wakazi wa Singida wakiangalia ajali hiyo. Habari na picha na
Hillary Shoo, Singida.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini CCM, Mohammed Dewji(MO) jana amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka katika kampeni kugongwa kwa nyuma na gari alilokuwa akitumia mgombea mwenzake Hawa Ngulume kuligonga kwa nyuma basi hilo dogo.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 10 jioni katika eneo la ofisi za Manispaa ya Singida muda mfupi baada ya wagombea hao kutoka katika kata ya majengo kunadi sera zao kwa wanachama kwa ajili ya kuwania kuteuliwa kuwa mbuunge wa jimbo hilo ambalo MO alikuwa mbunge aloiyemaliza muda wake.


Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kuona dreva wa gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 425 AMK ambaye jina lake bado halijahafahamika kugonga HIACE hiyo yenye namba za usajili T 655 BEB iliyokuwa ikitumiwa na Dewji pamoja na mwenzake aitwae Mariam Mhuwila.

Habari zaidi zinasema kuwa juzi wagombea wote Dewji, Mariam na Ngulume walipanda gari moja lakini jana Ngulume alikataa kupanda gari hilo maalumu kwa ajili ya wagombea na kuamua kutumia gari lake binafsi.

Katika ajali hiyo Dewji alipata mshituko sehemu ya shingo baada ya gari hilo kugomga kwa nyuma Hiace hiyo ambapo MO alikuwa amekaa nyuma na kusababisha kupata majeraha na mshituko sehemu ya shingo na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa vipimo vya X ray ilibainika kuwa MO amepata mshituko sehemu ya shingo na kupatiwa dawa za kuchua kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbania na hali yake inaendelea vizuri.


Kufuatia ajali hiyo dereva wa Mgombe hawa Ngulume anahojiwa na polisi kwa tuhuma ya kuendesha gari kizembe na kusababisha ajali.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa Celina Kaluba amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba uchunguzi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa leo ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Juhudi za kumpata Katibu wa CCM Manispaa ya Singida Mary Maziku ili kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2010

    KWANI KAMPENI ZIMEANZA? AU NDANI YA CCM, NA IWEJE AJALI ITOKEE INAYOHUSISHA GARI MBILI ZA WAGOMBEA, HAPA KUNA MASWALI MENGI YA KUULIZA ZAIDI YA MAJIBU

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2010

    dewji anakubalika singida mjini na ndio kipenzi chao huko, wewe mama utagaragazwa hadi ujiju mmwenzako huwa hawatelekezi wananchi wake anatembelea jimbo lake mara kwa mara, leo hii waje wachague mtu amabye atakuwa anaonekana jimboni wakati wa uchaguzi tuu kama ilivyo kwa baadhi ya wabunge, sidhani kama itawezekana hii lazima itakula kwako, muache kijana afanye kazi wewe bla bla mingi kuliko kasi, michu hizi ni zama za ukweli na uwazi hapana minya minya inaumisa atii

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2010

    What a coincidence siku amekataa kupanda gari ya wagombea ndio siku gari ya wagombea inapata ajali. Mh! Haya taratibu tutajua tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...