Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameteua Naibu Makatibu Wakuu tisa (9) wa Wizara mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 20 Julai, 2010 Jijini Dares Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo inaonyesha kuwa uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu hao unaanziatarehe 15 Julai, 2010 na wataapishwa rasmi siku ya Alhamisi tarehe29 Julai, 2010 saa 4.00 asubuhi.
Taarifa hiyo imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na BwanaNgosi C.X. Mwihava, Kamishna Msaidizi (Nishati Mbadala) katikaWizara ya Nishati na Madini kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Bwana Luhanjo, Rais Kikwete amewateua Balozi Herbert E. Mrango ambaye ni Mkurugenzi waIdara ya Ushirikiano wa Kanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Miundombinu; Balozi Rajab Gamaha ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Bwana Mbogo Futakamba,Mkurugenzi wa Umwagiliaji na Ufundi ambaye sasa anakuwa NaibuKatibu Mkuu katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Katika Uteuzi huo, Rais Kikwete pia amewateua Dk. Yohana L. Budeba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti waUvuvi (TAFIRI) kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, na Bibi Maria H. Bilia ambaye ni Katibu Tawala waMkoa wa Kagera kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha, Rais Kikwete amewateua Bibi Nuru H.M. Mlao ambayekwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii; Bwana Hussein A. Katanga ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, na Bwana Job D.Masima ambaye ni Mkurugenzi katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2010

    Good job JK, this is a training ground. To make them familiar with what's going on in the ministries before promoting them into the full rank after forming the new Gov later this year. The issue here is simple the existing ones have dekivered very little to the ministries and so we need changes. They'll need to be retired now

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2010

    Tunarudi kule kule ukubwa wa serikali hauleti tija katika maendeleo tunazidi kuwapa wananchi mzigo. Huyo anony hapo amenichekesha kweli hv huwa anafuatilia hotuba za JK kweli...yeye mwenye alisha sema hakuna shule za kutrain watu katika nafasi hizo...Hongereni mliopatiwa ulaji...maumivu kwa wananchi wa chini.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2010

    haya mambo ya naibu, naibu kwa serikali nchi maskini ni taabu tupu jama manaibu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    Good Speech Makala, unafaa sana, saana tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2010

    Hivi nyie mnaojiita watanzania ni lini mtakuwa na akili ya kuappreciate au kuridhika na kile kidogo kinachopataikana. Kila kinachofanyika nyie mnalalamika tu. Sasa mlitaka Rais amchague nani? Nina uhakika hata hao waliochaguliwa hamuwafahamu hata kidogo lakini mshaanza oohwamechaguliwa ili waweze kuwa familiar na serikali ...jamani hebu jaribuni kubadilika. Nyie mmefanya nini kuisaidia nchi yenu, au kazi kufunua midomo tu ili isinuke...

    ReplyDelete
  6. Haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu; wizara ya maendeleo ya wanawake na watoto ina waziri, naibu waziri, katibu mkuu na sasa naibu katibu mkuu!! kwa kazi zipi hasa zinazohitaji all these people?? hospitali sasa zinalaza wajawazito 3 kitanda kimoja waliotoka theatre na hatuoni jitihada zozote za serikali kutatua tatizo hili.. inauma sana sana. M

    ReplyDelete
  7. Michuzi mbona comment zangu unazibana huzitoi humu? M

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2010

    hizi ni fadhila kwa wanamtandao km hamjui ule uchaguzi wa mwaka 2005 ulimuacha na madeni haya megi sana na sasa anajitahidi kujikosha ili wamsupport mwaka huu.
    hii comment ya mwisho leo km usipoweka na hii we michuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...