Mdau January Makamba akitangaza nia yake leo ya
kugombea ubunge katika jimbo la Bumbuli, wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga

January akizindua kitabu kuhusu Bumbuli

Nimewaiteni kwa mambo mawili. Kwanza, kuzindua kitabu nilichokiandika. Pili, kuzungumzia uvumi na minong’no kwamba natarajia kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bumbuli.

Nianze na jambo la pili. Baada ya kutafakari kwa kina, na kuzungumza na wana-Bumbuli wenzangu, nimeamua niombe fursa ya kuwa sauti yao, kuwawakilisha na kuwasemea Bungeni, kuwatumikia na kushirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jimboni kwetu.
Kuendelea hadi mwisho wa tamko hili la January BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Dada Mlay Mary ( Arusha)July 05, 2010

    haya mambo yamewadia. Nimefurahishwa sana kuona January kaaza safu kwa ajili ya Kujikita katika kinyanganyiro cha Ubunge.
    Hii inanipa faraja kwani sasa tutegee akina Dr Shayo, John Mashaka nao wako mbioni. Hii itaongezea chachu ya vijana wetu bungeni.
    Dr Shayo wewe unaweka sera bayana Lini? Jimbo yako la Vunjo ninakuhitaji.
    usiwaangushe wazee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2010

    KWELI SIASA NI MCHEZO MBAYA HASA KATIKA NCHI ZETU HIZI ZA WATU WENYE NJAA ZA DUNIA YA TATU NA HASA AFRIKA, WATU WANALILIA VYEO KUGANGA NJAA ZAO TU SI KUINUWA MAENDELEO YA WATU NA HII IMEONESHWA NA JANUARY MAKAMBA MWENYEWE KATIKA KITABU CHAKE JINSI ILIVYOKOSOWA HALI HALISI YA BUMBULI NA HIYO NI BUMBULI TU, NA SEHEMU KUBWA YA TANZANIA IKO HIVYO, HAMNA SHULE WALA MABENKI, HATUTOFIKA KOKOTE KULE KAMA HATUTOKUWA WAKWELI WA DHAMIRA ZETU, SOMA KITABU CHA JANUARY UTAONA JINSI TULIVYOOZA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2010

    Haya watanzania umefikia wakati wa kupokezana uongozi, kila kiongozi ampigie debe mtoto au ndugu yake apate kula, Ridhwani nawe gombea, sisi walala hoi tukale wapi. Hivi kuna mtu anategemea akichuana na Januari au Ridhwani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2010

    hongera baba!!waondoeni hao wazee,tunataka vijana zaidi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2010

    michuzi na mie natangaza nia kugombea uwanja wa fisi.

    ReplyDelete
  6. Ni haki yake kikatiba...lakini mhhh!!!! it tells the direction we're. Siku moja tusishangae tukiwa kwenye serekali za kifalme kwa staili nyengine, Gabon imeshatokea, DRC ndo hivyo tena, Znz imeshatokea, USA ndo walisha-nusa hili, anyways yato haya hayajalisi as long as he's a good leader,but tuwe macho yanakuja!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2010

    Ankal sikukuona kwenye kashuguli haka au ulipigwa chini,mimi leo nilivyosikia huyu jamaa anaenda kutangaza nia nikasema ngoja nikamuone kwasababu nimemsikia sana hasa kwenye mitandao kuna mtandao mmoja kila siku kuna topic mpya juu yake,nikasema ngoja nikamuone ingawa sikupangiwa huu mzigo mimi hapa newsroom sasa kwanza nimeshangaa kukuta ukumbi umejaa,yaani wahariri mabosi wetu pekee walikuwa zaidi ya ishirini, nikasema ya leo kali anaumbuka mtu,jamaa kachelewa kama dakika kumi,kukatokea mkangayiko kwanza. Shuguli hii kaandaa nani kwasababu mc alikuwa nevile meena halafu tena walikuwepo kinadada wengine sijui wa kampuni gani,sasa bwana mdogo kaingia na suti yake na tai ya ki-obama obama.katumbulishwa akaanza kuzungumza ndipo nikashangazwa.hakuwa anasoma popote kazungumza kwa dakika kama 25 bila kusoma karatasi na kwa ufasaha nikashangaa kwamba huyu sio yule wanayesema kilaza kule jf?sisi tumezoea hapa press conference mtu anakusomea statement yake mwenyewe katazama chini,lakini huyu bwana mdogo alionyesha kujiamini sana na kuzungumza kwa kutulia,mimi kwa hili pekee amenivutia,jambo la pili ni kwenye maswali na majibu,kaulizwa maswali ya kizushi kayapangua yote bila shaka tena mengine kwa utani na hadi watu wakaishiwa na maswali,nimetoka pale nimebadilika sana mawazo kuhusu bwana mdogo.ana safari ndefu kwenye nchi hii

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2010

    Ndugu Kalwalwa,

    sio "nyengine" ni "nyingine" hahahaha nakutania tu ndugu yangu ni umetoa wazo la kweli.

    mdau, massachussets

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2010

    Yale yale Namimi nibadirishe last name yangu. SIJUI NIJIITE MICHUZI?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2010

    Bosi nakuona na suti kubwa ndugu yako wa Galanos aka Nguvumali Sec, bweni la Pamba. Big up bosi ila usitusahau kwenye ufalme, toka zamani ulionekana kiongozi. Tulikuchagua Depurty Head Boy nakumbuka baada ya muda ukataka kujiuzulu baada ya Mama Msemo kutulazimisha kulima kwenye saa za kipindi cha darasani na ukagoma kusimamia zoezi lile na ukamwambia mama wa kipare yule achukue cheo cheo tangu siku ile nilijua utakuja kuwa kiongozi wa watu.Nakumbuka ulikuwa huli na wanoko wengine viongozi kwenye ofisi ya uongozi ile iliyokuwa kwenye njia ya mabanda ya kuku ulikuwa unakula na sisi bwaloni,labda hukumbuki.Songa mbele songa mbele bosi

    ReplyDelete
  11. Ng'wanafunyoJuly 05, 2010

    Jamani wadau huyu bwana ana uwezo wake binafsi acheni ushamba wa kumgasi kwasababu tu ya ubini wake. Mumuhukumu kwa dhambi zake sio kwa ubini wake kama baba yake yumo kwenye siasa yeye anakosa haki ya kuingia kwenye siasa mimi nimeshangazwa kwasababu ni mmoja wa watu waliokuwa wanaamini kwamba anabebwa sasa nimemuona mwenyewe nimesoma maelezo yake nimesoma blogu ana uwezo mkubwa kuliko asilimia tisini ya watu humo serikalini.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2010

    Love him or hate him January ni mmoja wa very few smart Tanzanians. Watu wengi watasema ooh sijui baba yake or sijui nini lakini kwa tunaomjua jamaa tunakubali ni very smart.

    Eniwei, I will bet you guys $ 100 jamaa atagombani urais 2015.

    ReplyDelete
  13. baraka wa sinzaJuly 06, 2010

    Ankal zote siasa hizi na wanasiasa kwa changa la macho ndio wenyewe lakini angalau huyu hata kama ni changa la macho lakini lina akili kidogo,kajitahidi kaonyesha njiaTunasubiri utekelezaji. GodBless!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2010

    Lookin' good future prezzo! Usitusahau na wala usianze kula rushwa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2010

    Mimi nashindwa kuelewa hawa watu wanaishi mjini, wamekulia mijini shida za watu huko utazijuaje?

    Ina maana ukipata ubunge utahamia huko Bumbuli au ndio itakua safari moja kwa mwaka...We need to be serous... na watu wenye majimbo yenu muwe makini. Mumpe kura mtu anaye waelewa na atakayewatete haki zenu sio muwape kura watu kwa popularity zao...

    Na utupe hii kapuni pia...

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 06, 2010

    WAPAMBE WENGI DAH , KWELI WAPAMBE NOMA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 06, 2010

    Someni historia yake kwenye blogu za mitaani. Alipomaliza shule ya msingi alikwenda shule ya kulipia. Alipomaliza sekondari ikabidi tena aende shule ya kulipia. Alipomaliza high school, ikabidi afanye kazi kule alikokuwa baba yake Kigoma. Kwa nini? Tuseme tu kwamba tunamuunga mkono lakini kwamba ana sijui akili, wala hakuna kitu kama hicho. Kasoma Marekani kwa pesa za baba yake tena baada ya kusota miaka Kigoma, kwa nini hakutinga mlimani pale penye waliofaulu form six?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 06, 2010

    ushatangaza sasa jiandae kwa wenye chuki kuanza kukuonea wivu na kukutukana.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 06, 2010

    BUMBULI - Yesterday, Today and tomorrow! ndivyo kinavyoitwa kitabu hicho.

    Mimi nina asili ya Bumbuli natamani sana kukisoma kitabu hicho, ila lugha inanipiga chenga, kipo cha kiswahili chake??

    Mnyarugusu

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 06, 2010

    Mkuu Jan Makamba sasa jiandae na chuki sasa za waosha vinywa ambao hata hawakujui na hawajui uwezo wako. nimeona wengine washaanza humu eti oh anakaa mjini oh...ujuha mtupu! viongozi siku zote ni elites huo ndio ukweli, hata wanamapinduzi wote walikuwa elites wamesoma zaidi na wanakaa mijini. Nenda mbele kaza buti mkuu! tunasubiri matokeo.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 06, 2010

    Mdau wa july 06, 05:47:00, Kama humjui Januari Makamba kaa kimya. Kasoma Galanos, shule ya Serikali. Kasoma Forest Hill Moro na kwa mujibu wa hoja yako anapungukiwa na sifa ya uongozi kwa sababu eti kasoma high school ya kulipia. Ujuha mtupu! Na kwasababu hakusoma Mlimani basi hafai kuwa kiongozi? Ujuha mtupu! Tatizo lako umelisema mwenyewe kwamba unasoma blog za mitaani. Get the facts!

    ReplyDelete
  22. The London RedJuly 06, 2010

    Guys this is the courage we need among our young people. I am very proud of the future of our country. A young has decided to do something. There are two type of people: - those who roll their sleeves and go to work, and those who are there to comment on what is happening or has happened. This young man has rolled his sleeves. Let us join him! I don't care where he went to school or who his father is, I am judging him for what he has done and as far as I am concerned this is admirable. No one can argue that this is not admirable.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 06, 2010

    Shule ni Shule tu iwe ya kulipia ama Goverment la muhimu ni mwisho wa siku utoke na Elimu bora kwa manufaa yako na Jamii inayo kuzunguka kwa ujumla. Sisi hayatuhusu kama amesoma USA ama Kigoma kama amesoma kwa fedha za baba yake ama Goverment na vile vile kusoma Mlimani siyo ndio kufaulu form six wangapi tunaona wanapewa nafasi Mlimani kwa Rushwa?
    Hukumu ya huyo mgombea ni October kama Raia watamkubali awatumikie ama vinginevyo. Kila la kheri Watanzania wenzangu ktk Uchaguzi Mkuu.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 06, 2010

    Leo headlines magazeti yote Bongo ni Bumbuli funika mbaya. Hata sheni hajawahi kupata hii.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 06, 2010

    SWALI LANGU BADO LIKO PALE PALE. HIVI MTU HAWEZI KUSHIRIKI KATIKA KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII YAKE BILA KUWA MBUNGE?

    UBUNGE NI KWA FAIDA YA MGOMBEA AU YA WANANCHI?

    HOFU YANGU NI PALE WATU WANAPOFANYA UBUNGE KUWA AJIRA YA KUENDESHA MAISHA YAO.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 06, 2010

    umeula uuu,rudi kwenu kijijini.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 06, 2010

    JAMANI UKIPERNDA CHONGO UAITA MAKENGEZA, AKILI KILA MTU ANAZO, NA KAMA UMEJIANDAA NA KITU HAKUNA HAJA YAKUSOMA TOKA KWENYE KARATASI, SI MTU MWENYE KICHWA HIVYO KAMA WATU MNAVYOSEMA MBONA AMEKUWA AKISOMA KWA KUUNGA UNGA HIVYO NGAZI ZOTE ZA HUKU CHINI ZA MSINGI ALIFELI ALIFELI DARASA LA SABA, ALIFELI DARASA LA KUMI NA MBILI NI PESA TU NDIZO ZILIZOMELEKA HAPO ALIPO SO MTU YOYOTE KAMA AMESOMA HADI ALIPOFIKIA YEYE ANAWEZAKUCHAMBUA MAMBO KAMA ALIVYOCHAMBUWA YEYE. KILA MTU AKIPATA NAFASI ANAWEZA KUONYESHA UWEZO WAKE NI KWAMBA WATOTO WA MASIKINI HAWANA NAFASI NA HAWAJAPEWA NAFASI YA KUONYESHA UWEZO WAO

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 06, 2010

    maswali mengine yamekaa kiushuzz tu, ati mtu anauliza utakuwa unakaa bumbuli au mjini, ina maana wabunge woote bongo wanaishi kwenye majimbo yao walikochguliwa??? mfano mzuri tu mbunge mo' dewji wa singida mjini, anaishi dar lakini kila mara yuko jimboni kwake akishirikiana na wananchi wake bega kwa bega, na asilimia 90 ya wabunge hawaishi majimboni kwao huwa wanakwendaga kwa msimu tu!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 06, 2010

    Copies za hiki kitabu ‘BUMBULI’ zisije zikawa ‘sold out’, maana huko Beijing wa-chinese na wanafunzi wao walivyo wacheshi watamsoma ‘BUMBULI’ mapema mapema tu - ‘sold out’

    ReplyDelete
  30. Mimi narudi tena kuchangia suala hili, napingana na hoja nyingi hapo juu, huyu jamaa simjui ila nasikia tu kama baba yake ni katibu mkuu wa ccm na yeye ni msaidizi wa rais japo sijui katika eneo gani, ila tusimuhukumu kwa ubini wake kwa kuwa ni haki yake kikatiba, na suala la kama kasoma kigoma ama USA iwe kwa kulipiwa na pesa za baba yake ama la. Jamani wote tunajua mazingira ya Tanzania kufaulu ama kuto faulu kwa mtu kunatokana na factors nyingi mno, suala la UDSM kuwa ni sehemu ioneshayo uwezo wa mtu kichwani nakubaliana nalo, japo wapo watu wengi tu waliokatiza hapo na bado ufanisi wao na fikra zao zinakuwa na walakini, hebu tujiulize kwenye Bunge letu wangapi wamepita pale UDSM, je ni wote wenye kufanya mambo ya msingi? so scientifically hatuwezi ku-conclude kwamba UDSM ni suluhisho la viongozi bora! najua mnanielewa. Sasa nije kwenye hoja yangu ya msingi, ningekuwa mimi ndo January nisinge tangaza kugombea ubunge sasa, ningekuwa mimi mzee makamba nisingeruhusu mwanangu agombee ubunge sasa, ningekuwa mwana ccm nisinge ruhusu huyo kijana agombee sasa, kwa mwanasiasa makini,chama makini, na "mtu makini kama January," maana sina uhakika ni watu tu ndo wanatoa sifa kedekede, nisingegombea wakati huu, katika hali hii hamna mtu atakaye amini ni uwezo wake bali ni kubebwa na baba mwenye wadhifa mkubwa ndani ya chama,hii ni kuzidi kuondoa imani kwa baba yake, chama na yeye mwenyewe, maana nasikia amesomea conflict resolution ameshindwaje kuliona hili, ni kwa namna gani baba ata acha kutumia mabavu yake kuhakikisha mwanae anapita, maana wote twamjua mzee makamba,sipingi kwa yeye kugombea ila anataka ubunge kipindi ambacho tunaamini kuna "conflict of interest," kitu ambacho kinanitoa imani ya yeye mwenyewe kama mtu makini, nadhani ange concentrate na kumshauri Rais, ama angesubiri mpaka baba aondoke madarakani, hii inaonesha namna baadhi ya viongozi wasivyo waadilifu, narudia tena KWA WATU MAKINI HAWAWEZI KUFANYA HIVI, na kwa kujua sisi Watanzania huwa tunalalamika kwa kunong'ona tu ndo wanakandamiza, tusubiri tuone hii filamu ya UCHAGUZI 2010.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 08, 2010

    Mimi ni mwandishi wa habari na mara kibao nimekuwa kwenye misafara ya rais ndani na nje ya rais. January nimekuwa nikikutana naye mara kwa mara na nadiriki kusema HE IS A LEADER. Kweli sitashangaa kumwona siku moja anakuwa rais wa nchi hii. Ni mtu mwema asiyependa makuu. Kwa baba yake naye kuwa mwanasiasa, that is just accidental. Go January go.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...